Home
Unlabelled
BREKING NYUUUUZZZZZZZZZ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Mzee nakuona LIVE, Uko hapo kene ka LapTop kako unaingiza vutuz, Je hii ni leo au jana ?, Mpe huyo jamaa aliyeingia uani pole sana, namfahamu sana, cha ajabu, nimesearch name yake kene contact zangu ndani ya kaselula kangu, lakini cha ajabu nimefogeti akchuali nilivosev jina lake.unaweza kuonge anaye hapo nikubeep unipigie niongee naye, kama hautajali tafafadhali ?, usinibanie maana najua ww si unawekaga ile nini vile ?, Jirushe ?, hapana, nni tena ?, chizika ?, au nni mi i don no.
ReplyDeleteBONGO TAMBALALE ..
ReplyDeleteNingekuwa Rais wa Nchi hii, hawa wafanyi biashara wa mafuta ningewafutia leseni za biashara wote walioshindwa kutoa huduma. Hii ni kwa sababu hawa ni wanyonyaji, mafuta yameshuka kwa zaidi ya 70% huku kwenye soko la dunia, wanaambiwa washushe hawataki. Mafuta yakipanda kwenye soko la dunia siku hiyo hiyo wao hupandisha bei...huu ni wizi mtupi!!
ReplyDeleteNaishauiri serikali itafishe biashara ya mafuta. Enzi za Mwalimu hii mtu asingethubutu kufanya sabotage ya namna hii. Hawa ni sawa tu na wahujumu uchumi. Hawa ni wabaya kuliko EPA zote zilizowahi tokea nchi kwani wao wanamwumiza mwananchi papo kwa hapo.
nashindwa niseme nini ila nina chuki na hawa wahujumu au wahaini.
Ole Ndukai
Kaka Michuzi.
ReplyDeleteHappy new year. What's up with calling all the Petrol stations 'Sheli/Shell'? So then, what will you call the Petrol station with the name 'Shell'?
Naona bonny love na joseph kusaga awahamini macho yao wanaambiana michuzi jr na umaarufu wote anaendesha gari imechoka namna hiyo hata aina service yoyote break ya kupampu.
ReplyDeleteNilitarajia kitu kama hiki kingeweza kutoa. Wafanyabiashara wameachwa kujiamulia kufanya wanachotaka kiasi kuona kuwa wanaweza kuitetemesha Serikali.
ReplyDeleteKitendo hiki ni cha kuijaribu Serikali kama ulivyodai Bw Michuzi.
Nadhani ni nafasi nzuri kwa Serikali kuonyesha makucha yake.Ikidhibitika kama wafanya hujuma kwa makusudi, hatua kali zichukuliwe dhidi yao.
Mdau
Faustine
http://drfaustine.blogspot.com/
HAO DAWA YAO NDOGO WANYANG'ANYWE LICENSE,KAMA NI HUKU KWENYE NCHI ZA WENZETU WANANYANG'ANYWA NA FINE JUU MAANA WAMEKIUKA MASHARTI YA BIASHARA ZAO NA KUSABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WATEJA WAO,SASA HIVI KILA CORNER YA DUNIA MAFUTA YAMESHUKA BEI SASA WAO NI KINA NANI WANAOTAKA KUPINGANA NA SERIKALI YAO.
ReplyDeleteKWANZA WANALITIA AIBU TAIFA.
Mdau Canada.
Adha kama hizi ndizo Mwalimu alikuwa akijaribu sana kutufundisha ili tuepuke kutawaliwa na watu wenye nazo, na hapa JK lazima awabane sana tena sana kama hawataki basi wafutiwe kabisa biashara ya mafuta na leseni kupewa watu wengine... Hiki ni kipindi sasa watu waamke na nguvu ya hoja itawale kwamba kila mwananchi awaone hawa matajiri ni maadui wa taifa na maendeleo ya nchi yetu... (dRU)
ReplyDeleteKikwete hana wasiwasi ana njia mbili za kuwalima kwanza ni kuhakikisha leseni za waliogoma zinanyang'anywa halafu wawekezaji wapya waje wenye kukubaliana na masharti ya serikali pili ni kuwalima kodi zaidi wauzaji mafuta halafu kushusha VAt kwa mafuta ili sie tukilipa tunalipa kidogo watakoma wenyewe wasikubabaishe mheshimiwa sie vijana tupe meno watatutambia kuwa huu si wakati wa nyerere kutishiana mikwala mbuzi wakitaka wafuate wasipotaka wakawekeze burundi au Kenya waone
ReplyDeletewakati serikali ina-deregulate biashara ya mafuta wadau waliionya kuwa TPDC iendelee kuagiza na kurefine mafuta haikusikia,Haya ndio matokeo yake jeuri ya pesa inatikisa jamii.
ReplyDeleteSerikali ijitahidi kurudisha TPDC na Kigamboni refinery jeuri hii haitakuwepo kamwe.
hawa jamaa wenye ma-sheli wamezowea kuwakandamiza watu,kwani mara ngapi wanakuwa na stoki ndani na mara baada ya kusikia bei imepanda huku inakotoka oil mara huwa wanachekelea na kukurupuka kuongeza bei na kuwakandamiza wenye magari,lini uliwahi kusikia Tanzania bei ya mafuta imeshuka?
ReplyDeletemiaka yote bei ya oil nchini inakuwa inapanda na kupanda,na hawa jamaa wanakuwa kunanenepa milima matumbo yao, MIMI NAWAONYA WENYE OIL STATION,KAMA HAWATOFUNGUA NA KUUZA HIVI SASA,BASI WAKATI WOWOTE OIL ITAZIDI KUSHUKA NA KUSHUKA TENA KWA MUJIBU WA WACHUNGUZI WA OIL WA NJE,KAMA WANAKATAA HII BEI YA SASA,BASI BEI ITASHUKA ZAIDI NA KAMA WANOGOPA HASARA,BASI WATAPATA HASARA MARA MBILI PALE BEI ITAKAPOSHUKA TENA, NA KIKWETE KIWALAZIMISHA LAZIMA WAFUNGUE AU WAFUNGE NA KUNYANGÁNYA LESENI ZAO, hawa wajamaa hawana utu hata kidogo wanajali zaidi zaidi maslahi ya matumbo yao,wamezowea bei zipand kila siku na wao kupandisha stoki zao,kama hawauzi hivi sasa masi wajiandae kwa hasara ya kushuka zaidi oil,pia kufungiwa station zao,kwani wasione wao ndio wana rule nchi kwaajili ya kuwa na oil station zao,na hii itapelekeakama wale waliokuwa magavanor na mawaziri waliokuwa kuli rule na kuchota hera kwa kuona wao ndio mawaziri ,ndio wenye,hiisio tena time ya kujisikia wewe ndio una i rule TZ,kama wakifunga basi karibuni wataipata safi.
Maajabu hayo hayapo kwetu Nailobi!
ReplyDeleteNa kwenu kweli tambalale!!!HARAMBEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE!!!!
Hawa wana i beep siri kali ooooh watakiona kilicho mtoa nyoka pangoni we acha tu
ReplyDeleteBongo inahitaji dictator japo kwa miaka 5.
ReplyDeletekuna mtu anamuliza michuzi kwanini
ReplyDeleteanaita sheli kwani nini haiti kituo cha mafuta, kuitwa kwa sheli imetokana jina la shell,hapo zamani tanganyika au east africa ilikuwa inatawaliwa na uingereza vituo vyote vilikuwa na jina la shell hakuna hata kituo kimoja kilikuwa na jina jingine,maana kampuni ya shell ni uingereza maana wakamua kutua nafasi kwa shell . na wazee wetu kwa muda mwingi kuona jina kama hilo ndio maana wakiona kitio cha mafuta wanasema sheli kwa kujuwa kuwa hapo zamani ndio iliokuwa inatumika na sisi tumerithi kwa wazee wetu na utakuta mzee anakutuma kanunue mafuta sheli ndio maana tukachukulia kituo mafuta chochote ni sheli.
KAAAZI KWELI KWELI!!! KISWEKENI BWANA ETI "PETROL STATION" INAITWA SHELI. JE NA SHELL ITAITWA SHELI YA SHELI AMA.....?
ReplyDeleteHayo magaloni na madebe ya kubebea mafuta ni hatari...moto ukitokea!
ReplyDeleteTusije tukawa kama wa-Nigeria (wanaokufaga kwa moto kama sisimizi) wakichota mafuta, kama maji, wakati bomba lipasukapo au wakilipasua kwa makusudi!
Asante mtoa maoni uliyesema Michuzi anaharibu kuita vituo vya mafuta "sheli."
ReplyDeleteMichuzi ni ngwini, ni alwatan wa mjini, mwandishi mkongwe nchini lakini Kiswahili tabu! Bongo kila kila hatuwezi, hata lugha yetu!
duh kumbe vituo vya mafuta vyote huitwa SHELL?
ReplyDeleteKUMBE HATA BONGO??
ReplyDeleteKUANZIA J'5 LAST WEEK HADI JMOSI INDIA NAO WALIKUWA NA MGOMO PIA KAMA HUKO,SASA FIKIRIA JAMAA WALIVYOWENGI HALAFU KERO KAMA HII INATOKEA.ILIKUWA BALAA MAANA KARIBU MIJI YOTE MIKUBWA KAMA DELH,MUMBAI,BANGALORE,CHENNAI,HYDERABAD,KOLKOTA NA KWINGINEKO,SASA SIJUI NA BONGO NI NCHI NZIMA AU NI DAR PEKE YAKE.NDIO DUNIA HII JAMANI LABDA ENGINE KIUNO NDIO ITASAIDIA ILA MMMH BODY MWILI WAKO???
Hii ndio shida ya kutokuwa na National Oil Company, kwa ajili ya ubinafsi wa watu wa chache, WASIOTAKA TPDC ifanye biashara ya mafuta kisa? wana makampuni yao ya mafuta. Mi sipati picha ikitokea vita, inabidi kupeleka mizinga kwenye mzigo / ndege za vita halaf hawa jamaa wanagoma!
ReplyDeleteTPDC irudishwe jamani. Kila nchi ina shirika lake la taifa la mafuta (reliable source of oil and gas), kasoro Tanzania!
Na kwa mrindo huo viburi havitaisha! Maana hamna mshindani wa kweli, wote hao wenye "sheli", kaka na dada / dam dam.
Kinachoniogopesha mimi mwenzenu ni tabia ya hawa wafanyabiashara ya mafuta kwani siku 1 mafuta yakipenda marekani wao wanapandisha bei ya mafuta siku hiyo hiyo lakini bei ya mafuta imeshuka kutoka dola 147 mpaka dola 47 tena kwa zaidi ya mwezi wao wanakataa kushusha bei inayolingana na kushuka; kwa nini?, why?. Wakati wanapandisha bei ya mafuta wanasema mafuta yamepanda bei ya dunia na wanasahau kama wanastoki ambayo waliinunua kwa bei rahisi lakini mafuta yakishuka wanasema wanstoku ya zamani ambayo waliinunua bei kubwa hata kama wameyanunua juzi!!! Huu ni uuaji wa wananchi na pia ni dharau kwa serikali na vingozi wetu. kwa nini wafanyabiashara hao hao wanatii sheria katika nchi zingine lakini hawazitii za Tanzania? kuna watanzania wachache wanashirikiana na hawa madaidi katika kuihujumu nchi? TUMECHOKA.
ReplyDeleteOMBI langu kwa JK na EWURA ni kwamba hiki ni kipimo kwao cha kuonyesha kwamba wapo kwa ajili yetu na siyo kwa kuwalinda wahujumu uchumi naomba WASHUGHULIKIENI IPASAVYO kwani wananchi tumechoshwa nao. Pia tukumbuke bila kuwa na udhibiti bora wa bei ya mafuta, sarafu yetu itakuwa duni siku zote kwani mafuta ndicho chanzo kikubwa cha inflation na sisi hatuzalishi mafuta
Mheshimiwa JK, ungekuwa na jeshi linaotakiwa kupelekwa mstari wa mbele ungekuwa umeshashindwa tayari. Mafuta is a sensitive issue in any country. Mafisadi wa awamu ya tatu waliamua kuachia kiholela biashara ya mafuta kwa sababu zao binafsi. Matunda yake ndiyo haya yanaonekana kwenye awamu ya nne. Wasulubishwe, wasulubishwe, waliohujumu nchi na kubinafsisha biashara ya mafuta kwa visingizio vya "World Bank Pressure". Sijui kama hao "World Bank" watakuja kuisadia Tanzania sasa hivi kwenye hii crisis.
ReplyDeleteSi tulibinafsisha kila kitu. Ngoja tuone effects za ubinafsishaji. Maana kungekuwa na National Oil/Petrolium Company hawa wote wasingekuwa na hiyo jeuri ya kutuchezea kama wapendavyo. Lakini kwa kuwa wao ndiyo main importers and distributors of petroleum in the counrty basi wana uhuru wa kufanya jambo lolote na serikali inabaki kulalamika tu pasipo kufanya lolote.
ReplyDeleteMdau
Ndugu zangu mwaweza kudhani kwamba ni utani lakini si hivyo. Kuna watu watakuwa wamekufa leo huko mahospitalini kwa kuwa madaktari hawakuweza kufika makazini. Kuna watu wenye safari muhimu watakuwa wamechelewa safari zao, na wengine hawataweza kabisa kwenda. Kuna watu watalala nje wakiwa wanalinda magari yao kwenye foleni za kusubiri mafuta, na inawezekana nyumba zao zikavunjwa na vibaka kwa kuwa hazina usalama. Kuna maofisa wa ubalozi watashindwa kufanya kazi zao kwa sababu hawana mafuta. Kuna mikutano na wawekezaji ambayo haitaweza kufanyika kwa sababu maofisa au wawekezaji watashindwa kuhudhuria. Kuna biashara zitashindikana kufanyika kwa sababu hakuna mafuta, nk. Hii ni hujuma kubwa ya aina yake kwa Taifa, na kwa wananchi, na aibu kubwa kwa Taifa. Hujuma za aina hii zilidhibitiwa kikamilifu katika awamu ya kwanza, na zilikuwa haziwezi kutokea. Tunaelekea wapi?
ReplyDeleteKWA TAARIFA YAO TPDC INARUDI FULL NONDO NA KWA SASA WATAANZA KUSAMBAZA MAFUTA TOKA MALAYSIA NA WAMEYAOMBEA KIBARI CHA PUNGUZO LA KODI KWA MUJIBU WA HABARI ZA NDANI KABISA LITA YA MAFUTA HAITAZIDI 800. MTANIAMBIA NI HABARI INAKUJA HIYO.
ReplyDeleteHAHAHA HABARI NDIYO HIYOOOOOOOOO!!
Tunakiu ya Balanced news 9reporting)
ReplyDeleteNews inge-balance kama ungetupa hoja za upande wa pili ... yaani upande wa hao wauzaji (masheli yote)kwa nini wanashindwa kuwauuzia wateja mafuta?
Ungeweka ka utamu wa sheria juu ya hawa jamaa kutuweka rehani kwa kutukatalia kutuuzia mafuta, au pale DAWASCO au TANESCO wanpositisha kutoa huduma yao kwa mteja au kwa wateja? Kuna kosa? Hiyo sheria ya fair trade inatoa adhabu gani mtu akionekana anakosa la kunyima huduma?
Msomaji wa breaking views
KWELI BONGO TAMBARARE AS PER MICHUZI!!!!
ReplyDeleteWabongo kwa maneno mengi!!! Hebu tuonyeshe vitendo kuwa tumekerwa na hawa mabaradhuli wakubwa, TIA MOTO VITUO VIWILI AU VITATU mwone kama hawatafungua vilivyobakia!!!
ReplyDeleteNaomba kutoa hoja!!!
aya ndiyo yaliyotokea zimbabwe wazungu wamefunga supermarket zote.
ReplyDeleteIngekuwa nyerere angesema hawa ni waujumu uchumi kinachofuata hapo si mchezo.....
awa mabwanyenye wangeshusha bei wenyewe..
Yule mzee ametusaidia sana kitu kilichoturudisha nyuma ni vita ya UGANDA ya mwaka 1979 -1980/1.
Angetafuta njia ya amani na IDD amini, maana yake ni hela nyingi mno iltumika kupigana mwaka mmoja sio mchezo. Baada yapo tukawa tunashindia unga wa yanga
BAADA YA KUPITIA COMMENTS NYINGI HUMU NA KUWA KIMYA MUDA MREFU KUTAFAKARI KULIKONI WATU WAZIMA WANATOA COMMENTS ZA NAMNA HII, NIMEGUNDUA ASILIMIA 90 YA WATU WANAO POST COMMENTS HUMU NI MBUMBUMBU HAWAJAENDA SHULE NA KAMA WALIWAHI KWENDA BASI MAFANIKIO YAO DARASANI HAYAKUWA MAZURI, KWA KIFUPI WALI FERI MITIHANI YAO. JARIBU KUPITIA COMMENTS ZOTE HUMU UTAGUNDUA KARIBU WOTE WANAANDIKA KAMA WATOTO WA DARASA LA SABA. WACHACHE WAMENIFURAHISHA KIDOGO. SASA SIJUI NI TATIZO LA MICHUZI KUFICHA COMMENTS ZENYE MAANA AMA NI WADAU WA HII BLOG WENGI NI MBUMBUMBU? SIJUI LAKINI NAAMINI WADAU WENGI HUMU NI MBUMBUMBU.
ReplyDeleteEX MUZUMBE CHUO KIKUU!
ni shell zote!!!!, au ni gas station...mbalimbali!!!!!!!!! how about agip,total and more, zote hazina mafuta?
ReplyDeleteHawana akili. Wote wanyang'anywe leseni za biashara maana naona biashara zimewashinda. Wezi kabisa hao. Marekani kwenyewe mafuta yameshuka, sembuse TZ? ALA!!!!!
ReplyDeleteAnonymous wa 8:26 uliyozungumza ni sawa kabisa. Infact umesahau kutaja kwamba kuna kina mama wajawazito watakuwa wamepoteza maisha leo, (pamoja na vichanga) wakiwa katika dharura za kujifungua au kukimbizwa hosiptali na kushindwa kupata huduma kwa kukosekana madaktari na magari ya kuwakimbiza mahospitalini. Hili si suala la mzaha. Jamii nzima inatakiwa kulikemea kwa sauti moja.
ReplyDeleteYAANI WATU WANANUNUA GAS KWENYE OPEN CONTAINERS........THATS VERY DANGEROUS KAMA MLIPUKO UKITOKEA HAPO SI ITAKUWA HAPATOSHI WAJEMENI?
ReplyDeleteHUKU KWETU USA KUNA PLASTIC CONTAINERS MAALUMU KWA KUNUNULIA MAFUTA UKIENDA GAS STATION NA HAYO MADUMU YENU HUUZIWI MAFTA HATA KAMA LINA KIZIBO HADI UWE NA ONLY THOSE DESIGNED TO FILL THE GAS..SASA HAPO MOTO UKITOKEA NDO WATAANZA KUSEMA UCHUNGUZI UFANYIKE WAKATI BALAA NA HASARA ISHATOKEA...KUWENI MAKINI NI VITU VYA MOTO WAJEMNI..
Kuna mtu katumia msamiati wa Kikenya, eti wafanyi biashara, nenda Nairobi ukakae huko. Na huyo aliyendika Nailobi akasome shule.
ReplyDeleteHuyu anayemlaumu Michuzi kwa kuita vituo vya mafuta sheli, mbona hajalalamikia utani mwingine wa lugha kama kuita Chuo Kikuu cha University of Dar es Salaam? (siyo mambo ya wafanyi biashara na Bailobi, huu ni umbumbumbu wa lugha na kuandika). Hii ni blogu inayotumia lugha za mitaani za kawaida, siyo academic forum. Hii ni lugha inayobeba maudhui ya kijamii na utani wa kwenye lugha yenyewe na mazoea. Ni kawaida kabisa kwa watu kuita Sheli kumaanisha vituo vya mafuta. Lugha ina vionjo vyake, ndiyo maana wanawake wanaitwa mademu au mtaani watu wanawaita wanaume mamen - kwa ni Kiswahili hiki? Weka akili nyie mnaotafuta vya kuponda kila kukicha.
Kuhusu kioja hiki, si busara kurejesha kampuni ya taifa ya mafuta, itaongeza wizi, itaiminya serikali yetu maskini, na itapunguza ufanisi wa kibiashara. Kinachohitajika ni sheria kali ya kudhibiti biashara ya mafuta, duniani kote watu wanatawaliwa na sheria isipokuwa Tanzania tu.
Ama kweli tu nchi ya wajinga, we soma tu hata jinsi watu wanavyotoa maoni. Kazi kubwa ipo!
1) SERIKALI IPITIE SHERIA YA KUUZA MAFUTA NA IBADILISHE VIPENGELE FULANI (WANAVIJUA) ILI WAKILETA TABIA KAMA HII WACHUKULIWE HATUA KIRAHISI.
ReplyDelete2) SASA HIVI SERIKALI HAIWEZI KUWAFANYA KITU CHOCHOTE KWASABABU SERIKALI ITAPELEKWA MAHAKAMANI NA KULIPA FIDIA.
Anony wa 6:24 nimeipenda coment yako ni fupi na ni ya kisayansi, watu wanakata tamaa kutoa/kusoma koments maana inakuchukua mda mrefu sana kupata komenti ya ukweli na kuisoma nadhani watoa komenti wengi ni watu wasiokwenda shule na ni watu waliojiwekea utaratibu wa kila anapopitia lazima asema chochote hata kama hana analojua. Michuzi plz kwenye ishu muhimu na za kitaifa kama hizi uwe unapiga chini comments za washinda vibarazani.
ReplyDeleteBWANA PETER NALITOLELA,(WA EX MZUMBE "CHUO KIKUU") KWA SISI TULIOSOMA VIZURI NA ELIMU IKAKAA MAHALI PAKE ,COMMENT YAKO NI UTUMBO MTUPU NA HUJATOA HOJA YA MAANA.
ReplyDeleteKUMBUKA KUWA MZUMBE IS JUST AN UP GRADED INSTITUTION, NI COLLEGE NA HAINA SIFA YA UNIVERSITY.
KWA COMMENT YAKO INAELEKEA ANALYTICAL CAPACITY YAKO NI WANTING!!
MSOMI
DSM
wewe peter nalitolela hakuna mbumbumbu humu ndani wewe ndiyo mbumbumbu usiite watu humu ni mbumbumbu
ReplyDeleteKUNA MTU ANAITWA "PETER NALITOLELA" ANAYEJIHISI NI MSOMI. SIJAONA AKITOA HATA UCHAMBUZI WAKE JUU YA HILI SWALA NA WALA HATA KUWEZA KU-CONCLUDE KWENYE HII ISHU NZIMA. ZAIDI TU NAONA ANASHUTUMU WATU KUWA NI MAMBUMBU NA NI WATU WALIO"FERI" (Naamini alimaanisha kufeli) SHULE.KINGINE ANADAI YEYE NI "EX MUZUMBE" I DOUBT KAMA ALISOMA HAPO MAANA HATA KUTAJA JINA LA SEHEMU ALIYOSOMA HAJUI AU ALIKUWA NI MSINDIKIZAJI WENZAKE DARASANI.
ReplyDeleteKUTOKUJUA KUWA HUJUI NI KAAAZI KWELI KWELI.
Sijui Peter ni msomi au la, lakini naamini pia kuwa maoni ya wadau wengi hayana maana kuhusu uchumi wala biashara. Kwa kuwa kuna internet kila kona sasa na ni rahisi, ndio maana kila mtu ana haki ya kutoa sumni yake hapa lakini wengi wetu hawatuelewi dunia inaendeshwa vipi kibiashara, ila kila mhindi ni mwizi, kila myanyabiashara halipi kodi na ni mnyonya damu na kadhalika.
ReplyDeleteKifupi, Tanzania hatuna mafuta ya kutosha. hatujui wafanyabiashara wananunua kwa kiasi gani au wana contract ya aina gani na wazalishaji wa petroli. Kwa wao kufunga biashara, inamaanisha kwamba hawawezi kushindana na serikali na pia hawawezi kufanya biashara kwa hasara. Hamna mtu aliyeshinda hapa, watu wanateseka, serikali inapunguza mapato na biashara inakufa. Hamna hata serikali moja duniani iliyoweza kufanya biashara ya faida, hata Nyerere alitulazimisha kutoendesha magari jumapili kwa kuwa petroli ilikuwa shida kununua.
Kwa kung'ang'ania kuwa serikali iwatie ndani au ichukue leseni zao hawa wafanyabiashara, inaonyesha jinsi wadau tulivyo mbumbumbu hapa. Bado siasa ya Ujamaa imetujaa kifikra na hatujaelewa kabisa jinsi dunia ya leo inavyofanya biashara. Nilicheka sana mdau juzi alivyodai serikali ianze tena kudai kuona visa kabla ya kununua dola na ipitie benki kuu kwanza. Yaani, katika darasa la uchumu, ni "F" ya nguvu.
Aluta Kontinua
PETER NALITOLELA humu kuna vichwa vinaishi duniani na vimesoma duniani sio morogoro mzumbe kwenye UNIVERSITIES za ukweli zinazotambulika duniani,umechemka umeshindwa kuchangia mada ukaona uropoke tu sidhani kama unao hata huo usafiri wa kukuingiza petrol station lkn bado hio sio sababu ya kukufanya ushindwe kuchangia zaidi ya kulalama watu hawajasoma na kudai eti wameferi(wamefeli)sasa kiswahili kama kinakugonga ugokoni namna hio hayo masomo yako umeyasomea kingoni nn huko mzumbe???kaa kimya kama huna cha kuchangia.WATU HUMU WAMESOMA,WAMETEMBEA NA MAGARI PIA WANAYO NA WANACHUKIZWA NA UZEMBE KAMA HUU.WEE UMEJIDHIHIRISHA ULIVYO TOFAUTI NAO YAANI KINYUME CHAO HUNA HILO GARI WALA HIO ELIMU NA HUJATEMBEA NA UCHUNGU WA NCHI YAKO HUNA.
ReplyDeleteSULUHISHO LIPO TU 2009 NA KUENDELEA
ReplyDeleteWAHUJUMU UCHUMI LAZIMA WATALIPA TU KWA GHARAMA YOYOTE!!
kama Mungu aishivyo labda waombaji wamekufa!!
jinsi ilivo ngumu ngamia kupita ktk,,,,,
Kinachotakiwa ni kuwa na Shirika la Mafuta la Taida (sort of TPDC) ambalo litakuwa linaagiza mafuta wakati bei inaposhuka kama sasa, na kuweka stock (National Reserve) ya kutosha ili kuyauza ama wakati wa dharura au kwa ajili ya ku-control bei ya mafuta (energy) nchini.
ReplyDeleteKama wakati huu, TPDC wangekuwa na mafuta, wakaanza kuyauza kwa sh. 1000 kwa lita nani angehangaika na hao wenye "sheli"? Matokeo yake nao wangelazimika kuuza mafuta yao ili kuendenea na biashara.
Sasa hivi dunia ni ya uchumi wa soko. Serikali haiwezi kulazimisha bei. Bei zinatakiwa kuwa regulated na nguvu ya soko, lakini tatizo letu bongo wauza mafuta wote ni sponsors wa CCM, na hawategemei biashara ya mafuta kuishi! Kuna EPA na uppuzi mwingine mwingine mwingi kiasi kwamba mtu anaweza kuamua kufunga biashara wiki nzima eti ana-protest bei; au kuchangia milioni 500 kwenye mkutano wa CCM!
Kupanda kwa mafuta nchini kuna a very bad inflationary consequence, kwa uchumi wa nchi, lakini siji kama 'wataalamu' wa wizara ya uchumi wanaelewa hilo!
Kunatakiwa pia kuwa na national energy indepency strategy. Tugunguze matumizi na mafuta (hadi tutakapoanza kuchimba ya kwetu) kwa kutumia natural gas ambayo tunayo nyingi tuu.
Kuna watu wa chuo kikuu kama miaka 2 iliyopit), wali-demo conversion ya magari kutumia both fossil fuels na natura gas at the time. Serikali ingeamua kuwekeza kwenye hii technology, ili magali yote ya serikali watumie natural gas, hii technology ingekua na kuwa rahisi kwa individuals na ingeweza kupunguza matumizi ya mafuta kwa zaifi ya 50%, hence ku-save balance of payment ! na tungeweza kui-export hii technology na gas kwa majirani zetu na kusaidia kukuza uchumi.
Yako mengi ya kuongea, na ingawa mimi sio mchumi, lakini nadhani umaskini wetu unatokana na sisi wenyewe.
Mdawa.
Ndugu Mdawa,
ReplyDeleteMaoni yako yamenigusa sana. Kwa bahati mbaya hatuna mafuta ya kutosha ya kwetu wenyewe hawa hio natural gas ya kutosha. Nadhani wewe ni msomi na unaelewa kuwa nchi yetu ni masikini sana. Brazil, ambayo ina uchumi wa nane duniani kwa ukubwa imelazimisha magari yote kwao kutumia petroli na mafuta ya kupikia au yaliyochanganywa na maji ya miwa (Bio fuel). Pia Brazil wanatengeneza magari ya nchi nyingi na wana nguvu ya kiuchumi. Sisi tunaagiza magari bado Dubai na Japan bado.
Hata Marekani na Japbado hawana uwezo wa kufanya magari yao tatumie natural gas au bio-fuel kwa asilimia 100, sidhani Tanzania watakuwa na ubavu katika swala hili. Kuongelea ni vizuri lakini ni rahisi kuliko kutenda.
Kuhusu swali la siasa, kila mfanyabiashara duniani kote anakula sahani moja na serikali, Marekani wanawaita Lobbyst, lakini ni jina lingine la kumwita Mwizi,wanawapa fedha serikali au chama kinachoendesha nchi ili iwalinde na kupitisha sheria zinazowalinda. Sioni kwa nini mfanyabiashara hapa hawezi kutoa milioni 500 kwa CCM kama itamlinda.
Tanzania kama nchi masikini na isiyo na mafuta ya kutosha, haina sauti katika bei za mafuta ulimwenguni. Bei zinatokana na matukio duniani na ni nje ya uwezo wa serikali yetu.
Kama nilivyosema nyuma, hatujui mafuta walininua kwa kiasi gani na kwa lita ngapi. Kama wamenunua mafuta ghali, hawataweza kuuza kwa hasara kwa kuwa bei imeshuka sasa katika soko. Kuna namna nyingi ya kununua mafuta katika soko, sio tu kwa kulipa cash, kuna contract nyingi tu.
Tungekuwa na uwezo tungefanya kama India na Indonesia, serikali zao zinasaidia kupooza bei kwa kumlipa mfanyabiashara asilimia 30-50% ya bei ili imsaidie mwananchi wake anunue petroli bei rahisi. Lakini kama nilivyosema uchumi wetu ni mdogo sana.
Technology unayoisema ipo miaka mingi lakini sio rahisi kuianzisha, itahitaji dola bilioni nyingi tu, kama serikali inategemea wazungu ku balance bajeti yake tangu uhuru mpaka leo (2008 walisaidia dola milioni 350), Je, unafikiri watakuwa na uwezo wa kuendesha biashara hio ya conversion ya wasomi?