
Idhaa ya Kiswahili ya Sauti ya Amerika – VOA Swahili – itakuwa na matangazo ya masaa mawili mfululizo kuanzia saa moja jioni hadi saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki.VOA Swahili itakuwa na watangazaji mbele ya jengo la bunge - Capitol - atakapoapishwa Obama na pia kutoka Freedom Plaza ambapo Obama atapita kuelekea White House.
Utasikia pia viongozi wa Afrika Mashariki na Kati wakitoa salamu zao kwa Rais mpya wa Marekani Barack Obama.
VOA Swahili, Utajua Mapema.


Usijali tutakua Ireporter for you. Tutakutumia picha.
ReplyDeleteTunamuombea kwa Mungu Heri na Baraka!!!!!!!!!!!! Katika kazi inayomkabili ya kuibadilisha Marekani, na hasa katika suala linalozungumziwa sana Duniani (Uchumi!!!)
ReplyDeleteMdau kutoka canada!!
Ni Rais peke yake wa kuweza kuwapatia Weusi "voting rights, permanently", kama walivyo Wazungu, kuliko kila baada ya mika fulani Rais kuridhia upya "the right to vote" kwa Weusi!
ReplyDelete"Voting rights" mpaka sasa hivi is never a federal law; it is determined by state laws...ndio maana Bush kamshinda Al Gore kule Florida!