Mwenyekiti ya Bodi ya Wakurugenzi ya Tanzania Standard Media Group, Adolar Mapunda (shati jeupe) na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Profesa Amandina Lihamba pamoja na waombolezaji wengine wakitoa heshima zao za mwisho kwa hayati Cassian Malima, aliyekuwa Mhariri wa gazeti la Kiswahili la Serikali la HabariLeo, aliyefariki juzi na kuagwa leo nyumbani kwake Tabata, Dar, kabla ya kusafirishwa kuelekea kwao mkoani Mara ambako anatarajiwa kupumzishwa kesho.
Picha zaidi za msiba huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. michuzi ni mimi tena narudia mara ya pili kuandika comment yangu iwekwe humu bloguni kama wengine Je huyu mama hapo anapita amefunga ribon nyeupe kichwani aliwahi kucheza mpira wa kikapu ama ni mpenzi wa mpira wa kikapu? anaonekana amepiga ribon kichwani kama Lebron james wa lile jiji la Cleverland Columbus Ohio usa. ni hayo tu sina mengi ya kuongea asante kaka Michuzi!

    ReplyDelete
  2. Peter Nalitolela
    Huyo unayenzungumzia ni profesa na mwalimu wa Sanaa Chuo Kikuu cha DSM na anaitwa Amandina Lihamba kama Misoup alivyoandika. Kama aliwahi kucheza mpira wa kikapu, sijui ila amekaa Marekani miaka mingi sana sana

    ReplyDelete
  3. Peter Nalitolela feki, huna mpya, apa ndio pa kuulizia kilemba huku watu wanaongelea msiba! grow up

    ReplyDelete
  4. Mama Lihamba nimtaalamu wa sanaa, ndiomaana unaweza kuona yeye ni Profesa. Mara yangu ya mwisho kumuona, alikuwa ni mkuu wa kitengo cha sanaa pale chuo kikuu cha dsm (ud} na alishawahi kuishi marekani zaidi ya miaka Kuminane, kule alikuwa akifundisha chuo kikuu cha carfonia. Kwa hiyo kilemba ni moja kati ya tamaduni ya fani yake!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    mdau kutoka canada

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...