Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imetupilia mbali rufani iliyowasilishwa kwake na mgombea wa ubunge kwa tiketi ya Chadema katika Jimbo la Mbeya Vijijini, ambaye ni Mwanasheria wa Kujitegemea, Sambwee Shitambala na kumuengua kutokana na kukiuka taratibu za sheria katika ujazaji wa fomu za uchaguzi.
Akisoma uamuzi wa tume, Mwenyekiti wa NEC Jaji Lewis Makame alikubaliana na pingamizi zilizowekwa na mgombea wa CUF, Daud Mponzi na wa CCM, Mwanjale Luckson, kutokana na mgombea huyo kuapa kwa wakili kinyume cha Sheria Namba 1 mwaka 1985 inayotaka mgombea aape kwa hakimu.
HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Hii inaonesha ni jinsi gani baadhi ya wawakilishi wetu ambavyo awapo makini huyu mgombea tunaelezwa anafani ya sheria lakini kashindwa kuzifuata,na matokeo yake kaenguliwa na pia inaonesha jopo la viongozi wa chama chake waliweka kipaumbele zaidi ktk kelele za kampeni na kusahau jambo muhimu kwanza la kufanya mchakato husika wa kumpitisha mgombea.TUJIFUNZE KUTOKANA NA MAKOSA

    ReplyDelete
  2. Kanuni ziko wazi hata katika web ya chadema kipengele cha sifa za mgombea kipengele hiki cha kuapishwa na hakimu kimeainishwa pale kwa hiyo kelele na rufaa za chadema ilikua ni mfa maji lakini walikuwa wanalielewa hili fika.
    Walifuata haki yako ya kukata rufaa wakidhani pengine sheria itapindishwa la hasha.
    Kama kuna mapungufu yoyote au sheria hii inakandamiza demokrasia ndo wakati wa kuibadilisha sasa.Ila maamuzi yaliyo fikiwa ni sahihi na hayana budi kufuatwa

    ReplyDelete
  3. Ukimwaga MBOGA, namwaga UGALI!! Hili liwe funzo kwa Chadema kwa kujifanya wapiga kelele za kibabe bila kufuata sheria. Pia wajue kitendo cha kutoshirikiana na vyama vingine vya upinzani na kutopeleka ruzuku kwenye ngazi za chini kutafanya hiki chama kionekane ni cha kikundi fulani chenye malengo binafsi na hivyo kupoteza wanachama wake, mfano mzuri ni hivi karibuni ambapo kiongozi wa chadema wilaya huko mbeya amehama chama kwa madai kwamba chama hicho kinawakumbuka wakati wa uchaguzi na baada ya hapo RUZUKU huishia makao makuu na kulipa madeni ya Mbowe

    ReplyDelete
  4. Duh!, hapa udhaifu wa sheria umetumika kumuondoa huyu bwana ambaye ndiyo alikuwa tishio kwa CCM,yawezekana lile neno 'hakimu' linasimama tu kama kijumuisho cha wale ambao wanaruhusiwa kuapisha, mbona tunaapa kwa mawakili na viapo vinakuwa poa tu!!!!

    Ni changamoto kwa viongozi wa vyama vya siasa kuangalia upya kwanza upatikanaji wa uongozi na uundwaji wa tume ya uchaguzi na pili sheria za uchaguzi zenyewe!

    Hapa Demokrasia pia inaweza ikawa imebakwa nyuma ya ukuta wa sheria ya uchaguzi.
    Wenye akili akili wataliona hili!

    Ningeelewa kama angeenguliwa kwa kuwa baadhi ya maelezo yake yangekuwa ni ya uongo.

    Wana mbeya poleni sana, wana chadema poleni sana, lakini msikate tamaa!!

    ReplyDelete
  5. Angekuwa mgombea a ccm mngesikia tu,oo sijui ilikuwa ni kasoro ndogo ya kisheria lakini haina tatizo saaaaaaaana!!!!

    Mwakili na wanasheria hembu jitokezeni mbina kama mmedhalilishwa vile , kwani mawakili wanapoapishwa wanaapishwa wakafanye nini kama sio ni pamoja kuapisha viapo vinavyotambulika,
    Jaji Makame, je kiapo cha bwana Shitambala ni batili au halali?, kama ni halali basi hiyo sheria irekebishwe!

    ReplyDelete
  6. Sasa nafikiri ndiyo mmefahamu na kuelewa kuwa CHADEMA ina viongozi who are suffering from intellectual arrogance. Huyo Slaa anayejifanya yeye anajua sheria na huwa anajiita mwanasheria hali alichosomea ni cannon law ya kanisa katoliki. Hana lolote. Yeye ni bingwa wa kuwahonga mahakimu na makarani wa mahakama. Lakini mbele ya Jaji Lewis na akina Kiravu kashindwa. Na huyo Tundu Lissu mwanasheria uchwara alikuwa wapi kumsaidia Shitambala. Na mgombea mwenyewe Shitambala anaonekana ni mkaidi, mkorofi na ujanja ujanja wa kupanga maneno tu bila ya substance. Kiko wapi? Ama kweli ndege mjanja hunasa kwenye tundu bovu. Sasa wanakula kiburi na jeuri yao. Supporters wa CHADEMA wanajitetea oh sheria mama ya kiapo ndiyo ingetumika. That is mispalcing the argument and they are being rhetoric and vituperous. Sheria na kanuni ya uchaguzi iko very specific. NEC imetenda haki hakuna ubishi. Viongozi wa CHADEMA na hasa LIssu na Slaa wanajiona wana akili kupita hata waliotunga hiyo sheria. Ndiyo maana hata kwenye kesi ya petition dhidi ya ushindi wake karatu ushahidi ulitolewa mahakamani ulionyesha dhahiri shayiri kuwa CHADEMA kwa kushirikiana na msimamizi wa uchaguzi karatu walikiuka taratibu nyingi za kisheria. Lakini huyo anayeitwa the learned judge kwa sababu naye ni mwanaharaki akaamua kuwa nao. Sasa hali hii ndiyo imewalewesha viongozi hao wakiamini kuwa hata Mbeya mambo yangekuwa upande wao. Kudos to NEC and Judge Makame.

    ReplyDelete
  7. bongo tambarare.....

    ReplyDelete
  8. Chadema aibu maana mbona wana wabunge wengi tu ambao wanafuata kanuni, na huyu wanasema ni mwanasheria...hivi kamati yake ilikuwa wapi?

    ReplyDelete
  9. kuchamba kwingi mwishowe huondoka na kideshdesh!

    Mimi mdau wa Mchamba-wima

    ReplyDelete
  10. Jamani NEC imetenda haki. Mnajua hao CHADEMA na hasa Slaa ni mabingwa wa kushort ciircuit system. Thank God. Judge Lewis na NEC haihongeki hiyo. Nina hakika angelikuwa judge RM ambaye alimwachia huru Padre Kimaro mtuhumiwa wa kulawiti kivulana kule UDSM na pia akamsaidia Slaa akashinda kesi ya petition dhidi ya ushindi wake Karatu, CHADEMA Mbeya rufaa wangelishinda. Sasa wamekula joto la jiwe haswa. Siyo siri nimefurahi sana wameshindwa. Watz wengi hawafahamu kuwa ufisadi wa kuiba kura na kuhonga ndiyo style ya Slaa and his cohorts. Ndiyo maana documents nyingi kutoka serikalini anazipata kwa sababu anazinunua.

    ReplyDelete
  11. benson mwakyanjala (mwanakijiji)hajaandika makala kulaani tume?

    ReplyDelete
  12. wee petro uliemkana masiya mara3 kabla jogoo halijawika ulilaaniwa wewe mimi naona sio bure na huyo mwenzio Gwargwe hanikomvisi kama ni mmoja kati yetu watanzania nami pia namkana haiingii akilini eti Slaa aweze kuwahonga mahakimu na makarani wa mahakama dhidi ya mafisadi CCM,hivi Slaa na CCM MAFISADI nani mwenye uwezo wa kuhonga hapo?vione vile sijui vishahongwa tembo na pilau na khanga za india sijui?

    ReplyDelete
  13. BY THE WAY ANAYEDAI KUWA NI WAKILI SHAMBWEE WA CHADEMA HAYUPO KWENYE ORODHA YA MAWAKILI WA TANZANIA NIMEWASILIANA NA TANGANYIKA LAW SOCIETY HAWAJAWAHI KUWA NA MTU KAMA HUYO.CHADEMA NI MATAPELI.WWW.TANGANYIKALAWSOCIETY.OR.TZ WAKO MAWAKILI 1071 TOKA 1932 PITIENI ORODHA AU WASILIANENI NAO.
    NI MIMI CHINGA BIN CHINGAS KIBOKO YA CHAGGA DEVELOPMENT MANIFESTO-CHADEMA.

    ReplyDelete
  14. I can't believe this! Kweli tuna Demokrasia sisi? Yaani chama kitakosa mgombea eti kwa sababu mtu aliapa kwa wakili! Are we serious? Kwa nini walipokuwa wanahakiki makaratasi yake hawakumwambia aende kuapa mahakamani. Kwa nini isiwezekane kurekebisha hilo kabla ya uchaguzi? Wapiga kura wa Mbeya msilikubali hilo!

    Na mnaoleta ukabila, acheni hizo, vibaraka wa chama tawala!

    ReplyDelete
  15. Wewe Anon mimi ni mwanachama wa CHADEMA halafu ni mwenyeji wa Karatu. Niliyoyasema sitii chumvi. Muulize Slaa ile kesi yake ya kutaka kumtwanga bastola mtu aliekuwa rafiki na swahiba wake mwaka jana iliishia wapi? Just ask him kwa nini polisi hawajapeleka mahakamani. Narudia just ask him. Ninajua ninachkisema bwana. Acha hizo wewee!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...