Habari zako mpendwa mwanamapambano ya fikra;
Tumepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Sofia Simba kufuatia ushindi wake siku ya Ijumaa ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Wanawake wa CCM (T) Ngazi ya Taifa.
Tumepata nafasi ya kuzungumza kwa kirefu na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Mhe. Sofia Simba kufuatia ushindi wake siku ya Ijumaa ambapo alichaguliwa kuwa Mwenyekiti Mpya wa Umoja wa Wanawake wa CCM (T) Ngazi ya Taifa.
Hiyo ndiyo habari inayopamba toleo hili na habari nyingine kem kem. Usisite kuendelea kuwakaribisha watu wengi zaidi kujiandikisha kupata nakala ya kijarida chenu hiki bure kabisa kikiwa na habari ambazo huwezi kuzipata kwa uchambuzi na kina cha kijarida hiki. Lengo letu ni kuwa inapokuja suala la habari za Tanzania, sisi tunataka kuweka kiwango!
Tunawashukuru wasambazaji wetu ambao wamekuwa wakifanya kazi ya ziada. Siku chache zijazo tutaonesha shukrani kwa wale wanne ambao wamekuwa waaminifu muda huu wote! Asanteni sana.
Twende na tuwe "Cheche"!
Wiki njema!
Hivi UWT nayo ina wanaume siku hizi?? Naungana na Rais kuwashangaa wanaume na baadhi ya viongozi waliokuwa mstari wa mbele kwenye kampeni za uchaguzi wa UWT.
ReplyDeleteShibuda, Dewji, Makongoro Mahanga walikuwa wanafanya nini kwenye kampeni hizo?? Ama ni ktk hatua za kulinda maslahi yao kwenye kamati nyeti za CCM! WIIIIZI MTUPU!!!!!!
M/Kijiji mimi interest yangu ni kujua kule magomeni walikuwa wameenda kufanya nini. Je hilo swali limo kwenye mahojiano haya? Nikijua hilo itanisaidia kuongeza speed yangu kulitafuta cheche mitaanai
ReplyDeleteMdau
Cardiff
Gazeti ni zuri sana, bali wengine kila tuki login in web inakata ku-download pdf file.
ReplyDeleteHili suala linatunyima sana hu-hondo wa kulisoma gazeti letu tulipendalo.
Mwanakijiji fanya utaalamu watu waweze kulisoma hili gazeti kirahisi.
Asante.
Yaani huyo mama nikiitazama sura yake tu namuona ni mtu mwenye uchu mkubwa sana wa madaraka yuko tayari afanye chochote ayapate hayo madaraka duh!!!!sura inamuelezea kabisa yukoje huyo mwenyekiti uwt.
ReplyDeleteMwacheni mama wa watu jamani!!
ReplyDelete