
Ajali hiyo iliyotokea jana usiku haikuleta madhara kwa abiria waliokuwemo ndani ya basi hilo.
Chini mafundi umeme wa Shirika la Ugavi wa Umeme Nchini(tanesco) wakiondoka eneo la tukio baada ya kuangalia uharibifu uliotokea.Eneo la Banana litaendelea kuwa gizani kwa kipindi kisichojulikana mpaka itakapofungwa transfoma nyingine kutokana na Transfoma iliyokuwa ikifanya kazi kuungua .
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
Sijui kwa huko nyumbani inakuwaje, lakini kama ingekuwa ni hapa ninapoishi Japan, huyo dereva angelipa hiyo transformer pamoja na hizo siku watu watazokakosa umeme. Hata kama ni lofa hana kitu, angefanyishwa kazi jela hata kama ni maisha yake yote, na pesa inayopatikana kutokana na kazi anayofanyishwa akiwa jela ndiyo ingelipa deni.
ReplyDeleteLakini kwetu si ajabu ukamuona jamaa anadunda barabarani kama kawa na hakulipa chochote.
Hiyo daladala ina insurance. nani atagharamikia kutengeneza hiyo transformer.
ReplyDeleteBongo tambarare
Kaka michuzi hiyo daladala si kwamba ilikuwa ikitembea ndio ikagonga hilo Transfoma, ukweli ni kwamba lilikuwa likisumkumwa ili liwekwe kando maeneo ya hapo banana, kwa vile trasfoma nyingi za tanesco zipo ajili ya kuzalisha umeme tu! bila ya hadhari yoyote ya hatari,likagusa nyaya ambazo zikapiga shoti, na kusababisha huo moto. Hali iliyowanya waliokuwa wakilisukuma watoke nduki na kuliacha likiteketea. Hakika pia nikiri raia wengi wa nchi hii hatuna elimu ya kuepuka majanga sababu huo moto mwanzoni haukuonekana kuwa na madhara na bahati njema Tanesco waliwhi kuzima umeme eneo lote hata baadhi ya vitongiji vya jirani viliathirika. Still tukabaki tukiutaza moto huo ukifanya vitu vyake.
ReplyDelete