MWANAMUZIKI mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed 'TID' juzi usiku alikonga nyoyo za mashabiki alipopanda jukwaani kuimba na bendi ya muziki wa dansi ya African Stars 'Twanga Pepeta International', katika onyesho maalumu la Usiku wa Zain.
TID ambaye Desemba 9, 2008 aliachiwa huru kutoka gerezani kwa msamaha wa Rais Jakaya Kikwete, alikofungwa kwa mwaka mmoja baada ya kukutwa na hatia ya kumpiga mtu, ilikuwa mara yake ya kwanza kupanda jukwaa la Twanga Pepeta kuwasalimia mashabiki tangu atoke gerezani.
TID alipanda jukwaani kwenye ukumbi wa Mango Garden baada
ya kukaribishwa na rapa wa bendi hiyo, Saulo John 'Ferguson', na alipagawisha mashabiki waliomshangilia kwa nguvu alipoimba wimbo wa Huyu ni Wangu alioshirikishwa na rapa na mwimbaji wa Twanga Pepeta, Khalid Chuma 'Chokoraa' katika albamu yake binafsi ya Kuachwa.
Mashabiki wengi walijitokeza katika onyesho hilo la juzi usiku, ambalo ni moja ya maonyesho yanayodhaminiwa na kampuni ya simu za mkononi ya Zain.
Meneja Uhusiano wa Zain Tanzania, Beatrice Singano alisema wameamua kuidhamini Twanga Pepeta kwa vile wanaamini ni moja ya bendi bora Tanzania na zinazoongoza kwa kuwa na mashabiki wengi, na inaamini kupitia maonyesho ya Twanga Pepeta wataendelea kujitangaza zaidi hasa katika promosheni zao za Programu ya Uaminifu (Rewardz), Jirushe, Jiachie na nyinginezo nyingi.
Katika onyesho la juzi usiku, Twanga Pepeta ikiwa na wanamuziki wake mahiri wakiwamo Charles Gabriel 'Chaz Baba', Chokoraa, Kalala Junior, Luiza Mbutu, Saleh Kupaza, Ferguson, Dogo Rama, Janeth Isinika na Msafiri Diouf, ilikonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria Mango.
Twanga Pepeta hivi sasa inawachengua mashabiki kwa staili zake mpya za 'Sugua Kisigino' ya Ferguson, 'Nimeokota Kidude', Ronaldo za Chokoraa na Weka Selo, Kitumbua mbona wauza usiku, Obama, Wizi Mtupu na Mambo Maregea za Msafiri Said 'Diouf'.
Wakati huo huo, Meneja wa Twanga Pepeta, Hassan Rehani amesema bendi hiyo inatarajia 'kusugua kisigino' na mashabiki wake wa Mabibo Makuburi katika ukumbi wa Usesi Club Centre Alhamisi ya Januari 15, mwaka huu.
Rehani alisema Twanga Pepeta itaporomosha nyimbo mpya zinazotarajiwa kuwemo kwenye albamu ya 10 ya bendi hiyo itakayozinduliwa mwaka huu ikiwa ni pamoja na
Sumu ya Mapenzi ambao ni utunzi wa Chokoraa, Shida Darasa na Mwana Dar es Salaam (Chaz Baba) na Nazi Haivunji Jiwe (Thabit Abdul).

Hongera sana T.I.D!
ReplyDeleteUKISIKIA KUKOMAA KIMZIKI NDIO HIVYO!KWAMBA UWE MBUNUFU! USIWE MWOGA WA KUJIUNGA NA WENZIO WAWAPO JUKWAANI! WEWE UMEONYESHA MFANO!KWA WENZIO WA KIZAZI KIPYA!
Big Up
Msema Kweli
Ughaibuni
mabank wafanye nini kupunguza foleni?
ReplyDeleteJibu: kwa sasa Tanzania internet services zinakua kwa kasi kwahiyo naona ni vizuri mabank watoe huduma za internet banking ambazo zitasaidia kupunguza foleni kwa kiasi kikubwa
Grace - Netherlands