SAMAHANI!! SAMAHANI!! SAMAHANI!!

Ningependa kutoa samahani zangu za dhati kwa wasomaji wote wa blogu hii pamoja na ye yote aliyeguswa na posting inayosema "MAAJABU 7 YA WAKRISTU".
Nia yangu haikuwa kukashifu dini au Wakristu kwa namna yoyote ile. Mimi naheshimu sana imani ya kuabudu ya kila mwanadamu na kuziheshimu dini zote. Mimi si mdini na sijalelewa hivyo, na labda tu ningeongezea kwa kutaarifu kwamba mama yangu pamoja na upande mzima wa ndugu wa mama ni Wakristu. Mke wangu pia ni mkristu.

Nimepokea malalamiko mengi kuhusiana na uchapishaji wa utani huo, ambao ulitoka kwa ndugu yangu ambaye ni Mkristu sana, na sikutegemea kabisa kama ingeleta kutokueleweka kulikotokea.
Nimeamua kuyaondoa mara moja maandishi hayo katika blogu hii na kutoa ahadi ya kuwa mwangalifu sana siku za mbeleni. Madhumuni na nia ya kuanzisha blogu hii si kukashifu, kutukanana au kuvunjiana heshima bali ni kuchangia matukio na kuelimishana ili kuendeleza jamii.
FUNDI K.R.

BOFYA HAPA UTEMBELEE GLOBU YAKE


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 34 mpaka sasa

  1. Itachukua muda kusamehewa kwani wewe ndio walewale "akutukanae hakwambii tusi"au wale "Ukipata mkundu hulia mbwata"sawa broo Mungu akubariki. by msufini

    ReplyDelete
  2. Ukisikia bahati mbaya ndiyo hiyooooo.....jamaa kaingia bloguni tu na kasheshe zimeanza kumuandama! kaweka picha za wafanyakzi wenzake sijui kama walimruhusu azitumie kutangaza blog yake na sasa wale kina dada wakisikia hiyo blog imeingia kwenye kasheshe na picha zao ziko front page sijui kama patakalika pale ofisini!! 2009 imemuanzia vibaya technician Kombo!!! duh

    ReplyDelete
  3. watu wengine bwana, sasa si uombe msamaha tu, bila kujitapa ooh,sijui mke wangu pia ni mkiristo, si na awe, owa hata kanisa baba. Dunia yako kwa mungu zenda hesabu.

    ReplyDelete
  4. Mzee umetuangusha bwana!!!wachana na dini ongea kila kitu but not religion.

    ReplyDelete
  5. mambo ya didi ni mambo sensitive sana maana ni imani ya mtu. sasa wewe utakapoanza kuoffend imani ya mtu tena na unatumia blog yanaweza yakakukuta makubwa zaidi unavyofikiri.
    Usimess na imani ya mtu kabisaaaaaaaaaaaa. Michuzi ameanzisha hii blogu siku nyingi umeshawahi kuona mambo ya dini humu ? hakuna . hakuna mambo hayo na nchi yetu sisi haina mambo ya dini kabisa wala ukabila uache tena uache . Fuata mifano ya wakongwe wa blogu kama TMZ wa tanzania MICHUZI .

    ReplyDelete
  6. Mie nilisikitiswa mno na hiyo posting, na nilimwandikia vikali ingawa hakuiweka haradhari. Nafikiri kuwa iwapo mtu anaomba radhi hadharani, inabidi tukubali hoja zake. Wengi tunafanya makosa na kubakia vichwa ngumu hata wakati jumuia nzima iko against. Nasifia kitendo cha kuomba radhi, na ninachukulia hiyo kuwa ni jinsi gani mtu ni 'mzima' ki umri na kiafya.
    blackmpingo

    ReplyDelete
  7. Mtu akiomba radhi husamehewa. Ni mangapi tunayafanya mabaya kwa Mungu na kwa binadamu wenzetu yanasamehewa na ni makubwa kuzidi hili. Huo amesema ni utani.Kama mtu unaona ni mbaya basi msamehe halafu hatua ya pili mpige injili.Patrick.

    ReplyDelete
  8. Ninavyowafahamu wakristo wa kweli watakusamehe hara na washabiki watakusotesha. Wasomi watakuelewa haraka na washangiliaji watataka kurefusha mada.

    Mi ngekuwa wewe nsigefuta kwa sababu ya koments. Maana koments zeweza kuwa positive tuu, au negative tuu au mchanganyiko. Sasa wewe unalenga positive peke yake? Basi hiyo haitokuwa blog ya jamii!!!

    ReplyDelete
  9. Hebu kuwa strong wewe. Kutowa kwako kichekesho hicho kwa kuogopa siasa kali kunaweza kuonyesha makusudi ya kuwakosea. Rudisha sisi tuvunje mbavu.

    ReplyDelete
  10. kaka michuzi,mbona unaruhusu watu watuchafulie hali ya hewaa?wengine tunaosoma comment ni ma ustadh kaka,inabidi watuwie radhi!

    ReplyDelete
  11. Tushakusamehe kaka, kuwa na amani . It takes a strong man to apologise publicly.tuendeleze libeneke.

    ReplyDelete
  12. posting yangu ya jana nilisema "blog haina hata wiki ameshaanza udini...."

    maadamu ameomba radhi, na amerekebisha kule kwenye blog yake, basi mimi kwa moyo wa dhati kabisa nimemsamehe na naomba wengine mumsamehe pia.

    ReplyDelete
  13. Wala wakristu tuna noma basi sema waislamu ndo hawana mambo ya kutaniana inapokuja kwenye dini na wala usijaribu.

    ReplyDelete
  14. MIMI NI MMOJA WA HAO WALIOMPAKA SANA NINAMSAMEHE, M IMI NILIMSHANGA SANA PAMOJA NA USOMI WAKE KATUNDIKA MAMBO KAMA YALE, ILI HALI AKIJUWA KUWA ANA DAMU YA HAO ALIOKUWA AKIWAKASHIFU.

    ReplyDelete
  15. kaka ...
    sisi ndo wakristu, waislam na watanzania wenzio..na ndio wasomaji wa blogu ...blog yako imenyampa...
    em revamp blog yako...sidhani kama utapata wageni ..we are happy with michuzi ..we get everything from all over the world !!...umeyata mwenyewe ..umeyaona mwenyewe ...

    ReplyDelete
  16. hizo komenti za kidini za awatu waliochukia ni siasa kali. Wanamshambulia kwa udini nao pia ni wadini wala hawana uvumilivu.

    Pia hii inaonyesha Tz udini umo kwa sababu mtu kuandika joke watu waja juu.

    huwa nasikia wakristo unaweza kuwatania kumbe uongo. siasa kali siku hizi dini zoote.

    ReplyDelete
  17. Huyu mtu anajua marketing kweli.

    Blog nyingi Michuzi anazozitangaza humu wala siendagi kuangalia. Hii nimesikia watu wanavyosema kuhusu hiyo topic nikabidi na mimi niende kuangalia. Controversial topics,au pictures zinauza sana.

    Shukuru umeweka umewatania wakristo siye hatuna neno wa la kinyongo ingekua vice versa sasa hivi sijui ingekuaje.

    Halafu ukumbuke dini haina mtani wa jadi.

    Cha mwisho blog yako sijui unablog na rafiki zako au........Mkiona blog ya Michuzi inapata watu mnazania tunakuja humu kila siku kuangalia cake za mwaka mpya au nyama choma tu humu?

    Tafuta agenda na nyama choma iwe mambo ya ziada. Halafu uwe na mpangilio. Picha na habari zimepandiana kishenzi. Rangi ya Halloween haifai kabisa ukiangalia umri wako na personality yako.

    Ni hayo tu mkuu

    ReplyDelete
  18. UTANI NI UTANI....UWE WA DINI, KABILA, RANGI, SHEPU HAIJALISHI...KAMA UMEWEKWA KWA MALENGO YA UTANI; UCHUKULIWE KUWA NI UTANI.

    HIVI WATANZANIA NYIE MAMBO YOTE YA KUWA NA HASIRA NAYO KATIKA NCHI YETU, NDIO MMEONA MUWE NA HASIRA NA KOMBO, KWA KUWEKA UTANI..!!??

    ReplyDelete
  19. Sikiliza hutuba ya nyerere ya 95 kuhusu udini labda utaelimika sisi tulio huku ughaibuni tueshazoe watu kamanyiyi haswa wazungu wanpokubaua wakipelekwa mahakamani hujitetea kama wewe ohh mimi nina mjoba mweusi au sahangazi kaolewa na mtu mweusi mbona jirani yangu mweusi na kadharika kwahiyo wewe hata ukiomba msamaha wala usiwe na wasi wasi ni Mungu tu ndio atakayekusamehe umesha chemka na utabaki na ujinga wako na wajinga wenzio wanokupa kichwa kuwa ilikuwa joke mungu hayo hapa kwa ajili ya joke zako

    ReplyDelete
  20. Kaka Fundi pole sana.Jana nililalama sana na kukwambia nawaachia waungwana waosha vinywa wa blog yetu tukufu WAKUFUNDE,bilashaka wamekupasha inavyo stahili.Utani huo ungewafanyia waumini wa kiislamu,nadhani Ijumaa wangekuwa Jangwani/Biafra wakiandamana.Pamoja na shule walokupa,mie bado blog yako siifagilii hata kidogo,nakwambia tena iite "BLOG YA FAMILIA YANGU" vile umefanya coverage ya familia yako + wafanyakazi wenzako tu.Kwa ujumla kaka "umetoka vibaya",ila nimekusamehe.God bless you!

    ReplyDelete
  21. Yap namoba nami niseme kidogo kwenye hili. Sajaona hiyo joke bali nataka tu kusema kuwa kwanza hukutakiwa kuiondoa lakini pia ukishasema kitu ni utani hupaswi kutoa maelezo yoote hayo oo ati nami nimeoa mkristu, oo ati mama kwao wote ni wakristu. Sidhani kama hii inasaidia sana. umeshaomba radhi just ends there, sawa kaka. Next time ujifunze usikurupuke.

    ReplyDelete
  22. Kwanza kabisa nakupa Hongera kwa kuanzisha blog yenye akili, rangi, mpangilio umetulia.

    Usivunjike moyo ndugu yangu, hao wanaokulaumu wote wanastress za maisha na ndio maana wanashindwa kung'amua joke na ukweli.

    Hivyo ni vitu vya kawaida sana na tunatumiana kila kukicha kwa sms/emails.Kama mtu ameguswa basi abadili tabia kwani nikweli wengi tunakumbuka kusali wakati wakula tu.LETS BE REAL

    ReplyDelete
  23. Tena ana bahati kawakuta wakristu sio washari ingekuwa ni wale wengine wale wangemsomea albadil huyu.ila kaonyesha uungwana kwa kuomba msamaha TUMSAMEHE

    ReplyDelete
  24. pole mr kombo kwa upande wangu mi ni mrokole nilijiona kweli vitu vingine navifanya ikabidi nijilekebishe . unajua ktk jamii watu tunatofautiana uelewa ukisema hivi mwingine atatafsili vile .usijali mwanzo mgumu sana mbona hata BWANA YESU alipo waambia ukweli mafalisayo walichukia na kumtafutia visa vya kumuua. binadamu ndivyo tulivyo isikukatishe tamaa .naamini umewasoma sasa hautaludia .makosa hayajalishi mkubwa wala mdogo endeleza blog yako kaka .JAMANI WAKRISTO MBONA MMEKUWA HIVI NI NANI KAWAROGA DAA!!!! MMEKUWA WAKALI SANA.

    ReplyDelete
  25. We dont need to know that your mamma and all in your mamma`s family are christians.Thats childish,immature and irrelevant. You need help.
    Mdau, Kimanzichana safarini kuelekea unyamwezini.

    ReplyDelete
  26. wacha wacha waseme watasema mchana usiku watalala haya na tumuongelee ticks siyo kombo acheni ujima nyie na ntima nyongo mwe tumuongelee karamagiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete
  27. Hayo jamani hayakuwa utani hayo ni mahubiri kabisa yaliyoletwa hapo, ila kila mtu anapokea kwa mtazamo wake. Nilichojifunza hapa ni unyenyekevu, jamaalipoambiwa amekosea amekuwa rahisi kujishusha na kutaka radhi, hivyo ndugu enenda zako kwa amani, imani yako imekuokoa, umesamehewa

    ReplyDelete
  28. UTANI NI UTANI , LAKINI UTANI WA KIDINI NI HATARI NA HUWEZI KUJUA MWISHO WAKE.HTA HIVYO MIMI NAMSAMEHE NDUGU HUYU KWA KUONYESHA UADILIFU WA KUOMBA RADHI KWA UTANI USIO WA KITANZANIA, NA KWA KWELI NAMHESHIMU KWA HILO.INAONYESHA DHAMIRA YAKE HAIKUWA MBAYA NA WATU WASIICHUKULIE HIVYO .MIMI NNI MKRISTO NA MTU AKIKUOMBA RADHI NIVYEMA KUMSAMEHE ILI MIOYO YENU WOTE IWE HURU.INGEKUWA NCHI NYINGINE KAMA NIGERIA ,PAKISTAN, INDIA N.K INGEKUWA KASHESHE

    ReplyDelete
  29. naudia tena, michuzi sikuelewi kuruhusu maoni ya kwanza kabisa.
    mbona kina mamvi hawajaomba radhi popote?

    ReplyDelete
  30. Komenti nyingi zilizomo humu zinampa hongera fundi kwa kuomba msamaha na kuitika wito wao.

    Hii inaonyesha wakristu wengi waliguswa saana na wakashindwa uvumilivu. Hii pia inaonyesha wakristu wa sasa si wale wapole tulowazoea wa "mpende adui" au "mpe shavu jingine".

    Wakristu wa sasa wanaacha utamaduni wao wanaingia kwenye hasira, kufoka na visasi. Wanapoteza nafasi yao waliokuwa wakijidaia ya mfano bora wa jamii.

    Na hii inaonyesha jinsi mivutano ya kidini na udini vinavyozidi kushamiri nchini.

    Ni kweli ingekuwa ni mkristu au mwislamu katania waislamu hasa katika utani wa mtume au maandiko ingekuwa balaa kwa sababu globaly imeshajulikana tania dini zoote siyo uislamu. Tumewazoea na tunajuwa kucheza nao na hawajabadilika wako vilevile, na huenda hawatobadilika.

    Japo katka jamii mchanganyiko nimekuta waislamu hutaniwa na kukubali matani ilimradi hayamhusu mtume wao wala kitabu. Matani haya ni kama, waislamu wanapenda chakula, wanapenda sherehe, waswahili, vilemba, mzee kidevu, wazee wa njiwa, maninja, nk. na wao pia hutaniana hivyo.

    Mengine ni mashambulizi (hasa myths na stereotypes) ya kawaida yaliyozoeleka kama vile waislamu hawakusoma, waislamu wajinga, waislamu hawapendi shule, waislamu wazembe, wasilamu wamejaa magereza, waislamu wachafu, nk.

    Kuhusu usafi au uchafu, waislamu huonekana wachafu kwa utamaduni wa kuchamba. Lakini mi nimeishi uswahilini amabko watu wa dini zoote ni wakipato kidogo, watu wa dini zoote wanachamba. Suala la toilet paper ni la kitajiri zaidi kuliko la kidini. We hela ya dagaa huna utanunua wapi toilet paper?

    Na Je haitokei mtu yeyote asiyechamba akashika sehemu chafu za siri hata wakati wa kuoga?

    Mbona mapenzi tunayoiga kwenye filamu za magharibi ni hatari zaidi, maana ulimi wachukua nafasi ya vidole, sihisi kama hapa kuna usafi pia kwa watu wa dini zoote.

    ReplyDelete
  31. Anon wa January 07, 2009 11:12 AM, inaonekana wewe unagwaya albaidili, we mkosea watu saana nini. Jiamini, kama huna kosa haikupati, Teh h tih toh.

    Mwingine anasema eti wakristo wapole hujenga mashule na kunyanganywa kisha hukaa kimya, Hivi mnapinga zimio la arusha au? Mtkumbuke serikali ilitaifisha mashule ili kuleta usawa katika utoaji wa elimu nchi na kuuwa matabaka ya dini moja kuwa yenye elimu na wengine wajinga, kama ilivyokuwa wakati wa ukoloni wa mwingereza.

    ReplyDelete
  32. Mi sipokeai msamaha wako wala sikuwii radhi kwa sababu sioni kosa ulilokosea.

    ReplyDelete
  33. Hapo ujue kuna tofauti za kijiographia. Kwa wazungu au wabongo walioenda shule ya jumapili majuu si neno.

    Ila kwa wale waliohudhuria shule ya jumapili bongo, shughuli kubwa, hawako liberal, nk.

    ReplyDelete
  34. Ninasikia saana watu wanasema udini, hivi maana yake ni ipi? Na dalili zake ni zipi? Michuzi tafuta mada watu tusiojua tuelimike!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...