Wakati hali ya upatikanaji wa mafuta ya petroli kuwa tete kwa vituo vingi Dar jana na leo, hali hiyo imekuwa tofauti kwa kituo cha Big Bon cha Mtaa wa Msimbazi kuendelea na huduma hiyo kama inavyoonekana pichani

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imesema kuwa hakuna uhaba wa mafuta nchini licha ya baadhi ya vituo vinavyouza nishati hiyo kufungwa.

Akizungumza kwa niaba ya Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji EWURA) Bw. Michael Mshighwa alisema kuwa mamlaka imefikia hatua ya kuzungumzia hali hiyo baada ya kuwasiliana na wadau (wasambazaji) wakuu wa Mafuta ambao kimsingi wana takwimu sahihi zinazoonyesha kutokuwepo kwa tatizo la ukosefu wa nishati ya mafuta nchini .

“Leo asubuhi tulikuwa na mkutano na wafanyabiashara wakubwa wa mafuta nchini (wholesalers) ambao wamekanusha taarifa za kuwepo kwa tatizo la uhaba wa mafuta na kusisitiza kuwa vituo vyao vya kusambazia bado vina mafuta”Alisema Mshinghwa.

Kuhusu hali inayoendelea hivi sasa ya ukosefu wa mafuta katika baadhi ya vituo jijini Dar es salaam na ile iliyotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, alisema EWURA imeliona hilo na kwa sasa inatathimini mwenendo wa utekelezaji wa bei mpya za uuzaji wa mafuta zilizotolewa na mamlaka hiyo zilizoanza kutumika jana.

Ameongeza kuwa baada ya hapo hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote yule atakayekaidi agizo hilo la kuuza nishati ya mafuta kinyume na bei elekezi kama ilivyotolewa na EWURA.

“Tumetoa bei mpya za mafuta zitakazofutwa hivyo tunategemea ushirikiano kutoka kwa wauzaji katika vituo vya mafuta, baada ya hapo tutajua kama hali ya ukosefu wa mafuta wikiendi hii ulikuwa ni mgomo wa wauzaji au walikuwa wanasubiria bei mpya tulizozitoa, kinyume na hapo sheria itachukua mkondo wake” Alisisitiza

Bw. Mshighwa aliendelea kusisitiza kuwa wadau wote wanaouza mafuta wamekwisha sambaziwa waraka huo unaoonyesha bei mpya za mafuta zinazotakiwa kutumiwa.

Pia alisema wadau wengi wamekuwa wagumu kutekeleza matakwa ya serikali kutokana na mazoea waliyokuwa nayo ya kutoingiliwa katika uuzaji wa mafuta na kutokana na soko huria kwa muda mrefu na kuongeza kuwa wengi huwa hawapendi kudhibitiwa.

Hali ya ukosefu wa mafuta katika baadhi ya vituo vya mafuta hapa nchini kutokana na kutolewa kwa bei mpya zinazotakiwa kufuatwa na wafanyabiashara wa mafuta umeleta adha kubwa kwa wamiliki wa magari, wasafiri na watumiaji wa vyombo mbalimbali vinavyotumia nishati hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Serikali ikague vituo vya mafuta kama kweli wanaosema hawana mafuta wanasema kweli. ikibainika wafungiwe hawa ni wahujumu uchumi, wasio na huruma.
    Walizoea sana kutukamua yaani masikini tunamuliwa mpaka ngama ya mwisho huku wanafurahi kwa kicheko.

    Mhe Ngeleja na Malima na Katibu Mkuu wenu vita mnayopigana eleweni kuwa hatua iliyofikia ni of no return. its NOW OR NEVER.

    ReplyDelete
  2. WANA-CREATE UHABA ILI WAPANDISHE BEI, THAT IS JUST SIMPLE ELEMENTARY ECONOMICS YA DEMAND NA SUPPLY, SUPPLY IKIWA NDOGO NA DEMAND KUBWA BEI JUU. HUO NI WIZI NA KUKAIDI MAAGIZO YA SERIKALI

    ReplyDelete
  3. Tusidanganyane bwana, hao EWURA wanajua fika kinachoendelea. Hapa ndio utajuam serikali ya muungano inaongozwa na watu au watu ndo wanaongoza serikali. Huu ni uhujumu uchumi wa hali ya juu.

    ReplyDelete
  4. aya ayayayaa mpangilio gani huu gasi station? Afrika kweli tuko nyuma

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...