Baadhi ya wacheza sarakasi wa kikundi cha Zain Sarakasi Mama Afrika, wakionesha umahiri wao wakati wa maonesho yao.
MAONYESHO kabambe ya sarakasi ya kwanza ya aina yake barani Afrika yanayojulikana kama Zain Sarakasi Mama Afrika, yanayoendelea kuoneshwa jijini Dar es Salaam, yataendelea kurindima hadi Machi, mwaka huu.
Maonesho hayo ya sarakasi ya kusisimua yanayoonyeshwa kwa muda wa saa mbili na nusu katika eneo la Uwanja wa Jeshi Masaki, Dar es Salaam, sasa yanatarajiwa kuhamishiwa kwenye viwanja vya Biafra, Kinondoni mwishoni mwa mwezi huu.
Meneja Masoko wa Zain, Costantine Magavilla alisema Dar es Salaam juzi kuwa wameamua kuyahamishia Biafra ili kuleta hamasa zaidi miongoni mwa mashabiki wa madaraja yote.
Magavilla alisema hayo baada ya baadhi ya wasanii wa muziki wa kizazi kipya wakiwamo Selemani Msindi 'Afande Sele' na Farid Kubanda 'Fid Q' kuwa miongoni mwa wasanii waliojitokeza kwenda kushuhudia maonyesho hayo.
Alisema maonyesho hayo yaliyofunguliwa Novemba 26, 2008 na Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya, yataendelea kufanyika kila siku za katikati ya wiki isipokuwa Jumanne, na pia yanarindima kila Jumamosi na Jumapili.
Mkurugenzi na mwandaaji wa maonyesho hayo, Winston Ruddle kutoka Zimbabwe, alisema kuwa maonesho hayo ya sarakasi ya aina yake yaliyodhaminiwa na Zain Tanzania, yataendelea kuoneshwa hadi Machi au Aprili, mwaka huu tofauti na awali ambapo yalitarajiwa kufikia tamati Januari 18, mwaka huu Dar es Salaam.
Magavilla alisema Zain inaona fahari kusaidia kuleta shoo hiyo Tanzania, na baada ya kumalizika Dar es Salaam, yatahamia katika miji ya Mwanza na Arusha.
Ruddle alisema vijana hao 65 wanaounda kundi la Zain Sarakasi Mama Afrika, ambao wengi wao wanatoka Tanzania, wamepata mafunzo ya kutosha ya kuonesha vipaji vyao, ambavyo Watanzania wengi wanavyo.
“Ni shoo ya sarakasi ya aina yake. Tulijiandaa kwa miaka sita na tunawasisimua watazamaji wa rika zote kuanzia watoto hadi watu wazima. Ni maonyesho yenye utajiri wa utamaduni wa Afrika," alisema Ruddle.
Kikundi hicho kilichoundwa mwaka 2001 kina wasanii kutoka Afrika Kusini, Kenya na Ethiopia ambao huonyesha vionjo mbalimbali na vikaragosi, mazingaombwe na mavazi zaidi ya 500 ya kitamaduni kutoka nchi mbalimbali za Afrika.

Wadau vipi? mbona sioni comments kwenye issue ya sarakasi?
ReplyDeletekwa kweli hicho kikundi kinafanya kazi nzuri sana.Wasanii wengine hapa nchini wanatakiwa kubuni na kufanya vitu vyenye akili kama hivyo. hayo ni mazoezi ya shoka,wanaonyesha jinsi walivyo mahiri wa fani ya sarakasi.ushauri wangu ningeomba wadau wa masuala ya michezo hata wizara husika wawaone na kuwasaidia wafike mbali zaidi. Wanafanya kazi nzuri tena ya kujituma na wanaipenda kazi yao.
ReplyDeleteWATAZAA KWELI HAWA???
ReplyDeleteWAKISHA KOMAA, MIAKA ITAPITA WATAWEZA KWELI KUNANIHII??