RAIS Jakaya Mrisho Kikwete Alhamisi, Januari 15, 2009, ameanza awamu ya pili ya mikutano muhimu na wizara mbalimbali kufuatilia utendaji wa wizara hizo, utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, pamoja na maagizo aliyoyatoa kwa wizara hizo wakati anaingia madarakani.

Katika mikutano ya mwanzo, Rais Kikwete ataanza na wizara zinazohusika na masuala ya uchumi, ambayo ni sekta kuu lengwa katika utekelezaji wa Serikali ya Rais Kikwete kwa mwaka huu, 2009.

Jana katika mkutano wake wa kwanza ameanza na Wizara ya Miundombinu pamoja na uongozi wa Bandari ya Dar es Salaam na Kampuni ya Ndege ya Tanzania (ATCL).

Leo, Ijumaa, Januari 16, 2009, ataendelea na Wizara ya Miundombinu kwa kukutana na viongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL), Wizara yenyewe, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, Wakala wa Majengo ya Serikali, TANROADS na SUMATRA.

Jumatatu ijayo, Januari 19, 2009, Rais atakutana na viongozi wa Mamlaka ya Kodi Tanzania (TRA), Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Wizara ya Fedha na Uchumi pamoja na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG).

Jumatatu ya Februari 9, 2009, Rais atakutana na viongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko; Shirika la Viwanda Vidogo (SIDO) pamoja na Bodi ya Biashara ya Nje (BET).

Jumanne, Februari 10, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Nishati na Madini, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Shirika la Kusambaza Umeme Vijijini (REA), Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), na Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (EWURA).

Februari 11, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika. Siku hiyo hiyo mchana, Rais atakutana na Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia; Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano (TCRA) na Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL).

Alhamisi ya Februari 12, 2009, Rais atafanya kikao na Wizara ya Elimu, Mafunzo na Ufundi; Baraza la Mitihani, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu, TAHLISO na viongozi wa vyuo vikuu vya umma nchini.

Ijumaa ya Februari 13, 2009, Rais atakutana na uongozi wa Wizara ya Maliasili na Utalii pamoja na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Ngorongoro Conservation Area Authority (NCAA).

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Mwelekeo uliokuwanao, ndani ya msimamo wako ni mzuri sana.
    Sisi tunakuombea pia katika suala la kuzifuatilia wizara!!
    Mdau kutoka canada!

    ReplyDelete
  2. mbona hamna wizara ya afya?
    ndio mana ubovu wa huduma ya afya unazidi au kwakua hamna uchumi unopatikana?

    JK unahitajika kukutana nayo ili kuboresha huduma zake pia

    ReplyDelete
  3. Nampongeza Mh JK kwa jitihada bila kuchoka katika kuiongoza nji yetu. Niuombe uratibu wa shughuli zake umpatie wakati pia atembelee manispaa zetu na kujionea uozo uliopo humo na itakapobidi wahusika wabanwe kwa mtindo wa wenzao walio na vya kujibu kisutu..... tafadhali aanzie manispaa ya Moshi. Hapa pana uozo na wizi mtupu .... sokoni, barabara, maji, umeme, uchafu na wizi wa huduma ya parking... ne mengineyo mengi.

    ReplyDelete
  4. Raisi wetu pia atembelee manispaa zetu kwani kuna wizi uliokithiri .... taarifa feki zenye udhaifu mkubwa wa ukweli halisi.... wananchi walipa kodi wanadhulumiwa huduma muhimu wanzolipia kwa gharama ya vikao visikvyokiwsha wala vyenye tija ofisi za kurugenzi za manispaa na majiji. Moshi sokoni pameoza na watu wanalipa kodi... fedha hii inakwenda wapi?? Mh Mkurugenzi wetu tunaomba jibu>>> Jamani tumwogope Mungu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...