Mheshimiwa Balozi na Mkuu wa Wilaya
Ningeshukuru sana kama ungetundika ujumbe huu kwenye hii blogu yetu ya jamii. Nimetoa mawazo yangu kuhusu suala la matawi ya CCM nje ya nchi, ili niweze kusikia mawazo ya wengine na kupata elimu juu ya suala hili.
http://hapakwetu.blogspot.com/2009
/01/matawi-ya-ccm-nje-ya-nchi.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. 1. Matawi Ya Vyama Vya Sisasa Ughaibuni - JamiiForums.com

    Soma link hiyo
    www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/11759-matawi-ya-vyama-vya-sisasa-ughaibuni.html

    2. Watu pia walitoa madukuduku yao kuhusu suala hili - Comments katika Blog hii ya Michuzi)
    http://issamichuzi.blogspot.com/2008/08/ccm-shina-la-reading.html

    3. (Maelezo mengi utayapata hapo kwenye link hiyo)
    www.jamiiforums.com/habari-hoja.../2343-jumuia-ya-watanzania-united-kingdom-uongozi-mpya-na-lawama-kibao-4.html - 96k -

    Jumuia ya watanzania UK: Uongozi Mpya na lawama kibao! - Page 4 ...

    4. Hapa chini katika link hiyo (Utaona wanachama wa vyama mbalimbali vya kisiasa wakiwa pamoja katika jumuiya - Wapi WAMECHUKIANA/KUTENGANA AMA KUBAGUANA?)
    www.tzcommunity.co.uk/tanewsletter.pdf

    Nina imani pia hata wewe Prof. Mbele ulichangia hoja hapo awali katika mitandao kuhusu hili. Anyway Nimeipitia Blog yako kuna mengi mazuri tu, ni njia mojawapo ya Kuiadvertise hususani hapa kwa Michuzi ili tuendeleze libeneke, hakutakuwa na jipya katika mdahalo wa hoja ya Matawi ya CCM Nje ya Nchi, mengi yatakuwa ni "MAZUNGUMZO BAADA YA HABARI"

    "WANACHAMA WA JUMUIYA ZA WATANZANIA NJE YA NCHI(KWA MFANO UK) NDIO HAO HAO NI WANACHAMA WA VYAMA MBALIMBALI VYA KISIASA NJE YA NCHI KWA TAARIFA YAKO (CUF, CHADEMA, TLP, CCM N.K...) WOTE WAMO KWENYE JUMUIYA"
    USHAURI" KUMUELIMISHA ZEUTAMU AMBAYE ANAVUNJA MAHUSIANO,USHIRIKIANO KATIKA JAMII, KWANI YEYE NDIYE ALIYELETA MTANDAO (WEBSITE) YENYE KUCHOCHEA CHUKI NA UHASAMA KWA WATANZANIA POPOTE WALIPO, HIVYO BASI ZEUTAMU ANA WAJIBU NA KAZI KUBWA YA KUIJENGA JAMII YENYE UPENDO ILI JAMII IFAIDI UTAMU WAKE" WATU WANAISOMA ZEUTAMU BAADA YA KUPEANA TAARIFA KWAMBA UMEANIKWA HUKO KWENYE MTANDAO TEMBELEA UONE. KUHUSU SIASA KILA MTU ANA ITIKADI YAKE KATIKA MAISHA, LAKINI SOTE NI WATANZANIA, HIVYO SIDHANI KAMA UTAKUSUMBUA KICHWA.IS IT POSSIBLE FOR THE THINGS TO FALL APART? NO LONGER AT EASY FOR THE AFRICAN CHILD TO BE IN THE RIVER BETWEEN "MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE". NI MIMI "OBI OKONKWO"

    ReplyDelete
  2. Mimi pia sioni sababu ya kuanzishwa matawi ya CCM huku ngambo kwasababu sijui lengo za matawi haya huku nje ni nini hasa.

    Lakini uzoefu wangu wa matawi haya ya CCM kwa kule Tanzania hasa Zanzibar ambako ndiko nnakotoka mimi,ni kuwa huanzishwa kwa sababu mbili kubwa.

    1.Sababu ya kihistoria: Tokea enzi za zamani hili tawi lilikuwepo na linaendelea kuwepo.Lakini pia watoto na jamaa wa wanasiasa pia huanzisha matawi ya CCM ili waonekane kuwa ni wapenzi wa CCM kama wazee wao.

    2. Sababu za kiuchumi: Kuna wakati hasa siku za nyuma watu ambao walianzisha matawi ya CCM walikuwa wakipata misaada ya kifedha na vitu mbalimbali kama baskeli,redio, kanga nk. Siku hizi wenye matawi hunufaika wakati wa pirikapirika za uchaguzi. Kwasababu matawi ndio huchannel pesa na takrima.

    Sasa mimi nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kuhusu haya matawi ya CCM nje hasa Ulaya na Mashariki ya mbali.
    Nahisi watoto wa vigogo wa CCM ambao wako nje kwasababu za masomo au kwa wale waliojifanya wakimbizi wa CUF na baadae kupata kuishi nje, ndio kundi la kwanza la wanaoanzisha matawi ya CCM.

    Watu hawa hufanya hivi kwasababu ya kuwa hutaka kujiweka karibu na siasa za nyumbani ili watakapokwenda huko baada ya kusoma waweze kupata mdomo wa kuingia katika CCM.Kwahiyo katika "resume" zao wataonesha kuwa walikuwa makatibu au wanachama wa CCM huku nje.
    Pia hufanya hivi kwasababu ya manufaa ya kupata mialiko na kupata connection za mabalozi wa Tanzania walioko nje na kujiweka mbelembele pale viongozi wa CCM wanapotembelea nje.

    Lakini kwa kweli matawi mengi ni kwa manafaa ya binafsi na wala sio manufaa ya Taifa letu au manufaa ya watu wengi.

    Kule Zanzibar kulikuwa na tawi la CCM(au kwa jina jengine Maskani) maarufu sana kwa jina la Kisonge. Ilianzishwa wakati wa utawala wa Salmini.Lakini alipokuja Amani Karume haikuchukua muda maskani ikakatika sehemu mbili. Moja ikawa inamuunga mkono Karume(walikuwa wanapata maslahi kwa kufanya hivyo) na moja ikawa inamuunga mkono Salmini na Bilali(hawa walikuwa zaidi watu Kaskazini Zanzibar) ambao waliona kama wameporwa uraisi wa Zanzibar(Na wao wanaona iko siku maslahi yatarudi tena kwao)

    Kwahiyo tuendelee kuchangia lakini as long as kuna watu wanaohisi kuwa watapata maslahi binafsi wanapofanya hivyo basi matawi yataendelea.Wakiona wanapoteza muda wao bila maslahi yoyote basi matawi yatakufa yenyewe.

    ReplyDelete
  3. Matawi ya CCM yana faida na hasara zake. Tujadili kwa mtizamo wa uanzishwaji wa kikundi chochote kile mahali pengine, kisha tuangalie aina ya vikundi, na hatimae tuone faida na hasara zake kabla ya kutamatisha ni vibaya au vizuri.

    Mimi sitaki kuchangia, ila naomba niwe muwezeshaji i.e facilitator kwa kikwao! Niwakumbushe kwa haraka haraka kwamba tunaweza kuviweka vikundi anzilishwi katika makundi makuu mawili; shindani, na vutio.

    Aksante

    S.E.M

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...