JK akimjulia hali mpiga picha wa magazeti ya Serikali ya Daily News na HabariLeo, Mpiganaji Athuman Hamisi Msengi, wakati alipomtembelea kwenye Hospitali ya Milpark (pichani chini) ya mjini Johannesburg, Afrika Kusini jana baada ya kikao cha wakuu wa nchi za SADC. Mpiganaji Hamisi amelazwa baada ya kupata ajali ya gari huko Kibiti, Mkoa wa Pwani, takriban miezi mitatu ilopita na kupata majeraha kwenye shingo na uti wa mgongo. Hali yake inaendelea vizuri japo maungo bado hayafanyi kazi sawasawa. Picha na mdau Juma Kengele wa Ikulu



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 16 mpaka sasa

  1. Watanzania , nadhani wakati umefika wa kuwa na hospital zenye kiwango cha kimataifa Tanzania na sio watu kwenda kutibiwa nje. Kama nchi hio itakuwa na proper priorities haya mambo yanawezekana.sio mambo ya twin towers,rada na upuuzi mwingine ..

    ReplyDelete
  2. neno mpiganaji linakera. kuwapa kichwa waandishi.

    ReplyDelete
  3. Rais mtu wa watu rafiki wa walala hoi. Ila mzee JK hapo jifunze. Huyo Mpiganaji ana insurance ya kumlipia matibabu. Weka mambo sawa hiyo itakupa heshima zaidi. Watu wamezidi kwenda nje kutibiwa, wanalazimika kufanya hivyo na pia kuwe na insurance za kulipia matibabu hiyo itaongeza kipatao cha madkta wa muhimbili na hospitali zingine. Unasemaje?

    ReplyDelete
  4. SASA HAPO KUNA TOFAUTI GANI NA MIKOCHENI HOSPITAL, HATA MUHIMBILI NI BABU KUBWA, SOMESHENI WATAALAMU JAMANI ACHANENI KUTUMIA MAPESA KWA MAMBO YASIYO YA MAANA, SEMINA ZISIZO NA MATUNDA NA WIZI WA EPA AMBAO UNGEWEZA KUSOMESHA MADAKITARI MAMILIONI KWA MAMILIONI.

    ReplyDelete
  5. Pamoja na kwamba huduma za matibabu zinaweza kuboreshwa na ninaamini huo uwezo tunao kama mdau hapo juu alivyosema kama tunaweza kujenga mitwini tawas ukijumulisha na epas, nk, lakini katika zama hizi za kujenga matabaka makuu mawili kutibiwa nje ya nchi ni kitambulisho cha tabaka, tabaka la walionacho (kwa viwango tofauti) na ni hao hao wanaofanya maamuzi kuhusu maisha ya wabongo!!!!!

    ReplyDelete
  6. we unaesema eti hiyo hospitali kama muhimbli acha uongo.hata hiyo 1st track waliojenga haijafiia hivyo usiwape vichwa viongozi wetu mafisadi hawana muda wa kutujengea hosptali kama hiyowaoni matumbo yao tu..kwa maana wao wakiumwa wanauwezo wa kwenda popote wanatusahau sisi tuliowachagua.

    ReplyDelete
  7. annon apo juu ungemalizia kusema....na kujenga miundombinu ya maana Tz shule,vyuo vikuu,hostel za wanafunzi ona chuo wanavopata shida,madawati,maji safi,hopsitals,madawa mana MSD ni EPA ingine.

    ReplyDelete
  8. Wewe unaesema somesheni madaktari sasa tukiwa na madaktari milioni mbili wataajiriwa na nani? Unafahamu kuwa Cuba ni nchi ya kwanza duniani kuwa na high level of literacy na katika kila wanachi kumi wana daktari mmoja lakini hakuna mtu wa kuwaajiri. Cha maani hapo ni kuboresha huduma za jamii in general ikiwa ni pamoja na mishahara, hospitali bora, sera bora za elimu ya juu nk.

    LK

    ReplyDelete
  9. Ama kweli kila mtu na mawazo yake, wengine pumba wengine point.... hahahha We LK wa January 28, 2009 7:49 PM Unaakili tumamu kweli?? cuba kuwa na madaktari sio issue, tatizo wamejifanya wajima mno mpaka wanashindwa kutoka na kufanya kazi nchi nyingine dunaini, Kusoma Muhimu sana, Ajira sio lazima taifa ulilozaliwa, Kama kwenu hakuna Ajira toka nje katafute ajira nchi za jirani au Nyingine kabisa, Kuna wabongo kibao Botswana wana Maisha mazuri sana na wana mchango mkubwa kwa familia zao, ni Madr kama hao wa cuba na waajiriwa wa nchi nyingi tu sisi ni wabongo, Tuna elimu na inatusaidia kutokomeza umasikini nchini kwasababu tunapata uwezo wa kuwasaidia walio Home, Ni kweli kabisa miundo mbinu inabidi kuboreshwa lakini sio kila kitu kifanywe na serekali, nakumbuka Kwetu Mbezi beach tulipitisha muswada wa kuchanga pesa na kujenga barabara ambayo ilikuwa ni kero kwetu sote lakini wachache WAMIMI walikataa na kurudisha nyuma maendeleo, kwahiyo mpaka sasa tope kama kawaida na inatuathiri wenyewe, Swala la serekali za Africa kubadilika na kuleta maendeleo kwa Raia Sahauni, ni kama Ngamia kupita kwenye tundu la sindano... Fanya Makeke usaidie wanaokuhusu, ndugu jamaa na marafiki, sio kusubiri serekali ya mafisadi, wala rushwa wapenda matumbo yao iwaletee maendeleo...Ukweli ni kwamba haitakiwi kuwa hivi lakini kwasababu hakuna ujanja wa kuwabadilisha walio juu na kuleta maendeleo ya wote kwa pamoja, basi Jitahidi uwe na maendeleo binafsi... Hebu angalia toka uhuru uanze africa serekali ngapi zimeweza kuleta mabadiliko kwa raia wake...?! lakini Ni Raia wangapi wameweza kujikwamua na kusaidia Ndugu zao, jamaa na marafiki??? Jibu lipo wazi, UKISUBIRI MAENDELEO HAYAKUFATI MLANGONI... Get out and work Hard for real change...Kabla HUJAFIKIRIA MABADILIKO YA WOTE, BADILIKA MWENYEWE KWANZA.
    India na china ni Moja ya nchi zenye kutoa Mifano hai kabisa duniani... KUna mabilionea Wengi sana wa Doller na wanafanya mabadiliko ya uhakika kwa raia wao na watu wanaowazunguka... Wangetegemea serekali zao, ingekuwa mzozo mpaka leo... emagine Tata inanunua makampuni makubwa yanayoshindikana Ulaya na Kufanya real change, china wanatujengea Africa nzima kwa wingi na kampuni zao za uhandisi... na wakandarasi..
    THINK BiG MZEE, Halaf kuna Anon anadai health Insurance!!! WE UNA AKILI TIMAMU KWELI??? Marekani inawashinda raia robo ya population, na ndio mama wa dunia kwa uchumi, JE Tanzania yenye asilimia tisini na tano ya wananchi wasio na bank account??
    Sio kila mnachoona Ulaya kinawork mnadhani na kwenu itawezekana, hawa jamaa walitutangulia toka karne ya 15... Kwahiyo waangalieni kama mifano tu, sio kila kitu mtake kifanyike nchini kwenu... Ili uendelee inabidi ufikirie kutokana na mazingira uliyopo..ni sawa na kutaka bongo kuwe na treni za umeme wakati barabara za matope hakuna..!

    Mdau UK

    ReplyDelete
  10. Washamba Health Insurance imewashinda Marekani umesikia wapi? Acha Kupayuka. Free health care ni tofauti na health insurance, Free healthcare inakuwa funded na Govt. Health insurance inakuwa funded na employees and employers. Sasa kama unafanya kazi nzuri kama mwandishi wa Daily News kwa nini usiwe na health insurance ya kuweza kukulipia matibabu?
    MDau Wa UK, unabisha mambo bila kuyaelewa inaeekea huko UK umepelekwa na baba wee ni kula kulala tu. Kasome magazeti ya Play Boy ulale.

    ReplyDelete
  11. Mdau UK, una degree ya Pumba na ubishi usiokuwa na maana.

    ReplyDelete
  12. 3.7tn/- CIS debtors now for court - Mkulo

    2009-01-28 10:39:02
    By Joyce Kisaka


    The government has vowed to haul to court individuals, companies and institutions that obtained credit under the Commodity Import Support (CIS) scheme yet to repay the money.

    Finance and Economic Affairs minister Mustafa Mkulo revealed this during an exclusive interview with The Guardian in Dar es Salaam early this week.

    A total of 26bn Japanese Yen (equivalent to 3.7tn/- at current exchange rate) was dished out under the scheme in the 1990s, but the government had from 1993 to December 2008 managed to collect a paltry 10bn yen (equivalent to 1.4tn/-).

    The minister said the government has now hired Msolopa Investment Company Ltd, an independent debt collector, to recover the funds.

    He warned that the agency was observing a strict deadline, adding: ``Some people are not willing to pay, while others have paid only part of the debt. Our intention is to recover the whole amount,`` he said.

    Mkulo said the government hired the agency to collect the pending amount, part of which was owed by government institutions, necessitating an independent body to do the work.

    He said his ministry gave Msolopa a deadline to collect the money and all those who would not have paid by then will face legal action, adding that he would issue more details about the import support scheme in the on-going sessions of the National Assembly in Dodoma.

    ``The government knows clearly that those who got money under CIS met the set requirements and signed agreements to pay back, so there is no argument about repayment,`` explained the minister.

    He said some of the debtors are highly respected people and institutions and the government was not out to embarrass or shame anyone, ``only to speed up the repayment process which has dragged on for too long``.

    Reached for comment, Msolopa Investment Company Limited executive director Ibrahimu Msolopa said: ``Some of the big debtors are telling us that they will not pay and are ready to be taken to court. The government plan is not to take them to court, but what if they insist they wouldn`t pay?``

    Explaining the mode of payment, he said there are those paying through banks and submitting receipts to his office while others make payments through the Tanzania Revenue Authority (TRA) and notify him on the amounts collected.

    Asked to clarify the involvement of TRA, he said the authority had been collecting the debts before he was appointed and he relied on it ``for some of the relevant information``.

    Msolopa said his company expected to submit a report on the exercise to the Finance ministry soon, adding that submission of regular reports on the exercise was one of the conditions of the contract.

    He said some of the debtor companies had since ceased operating ``but our company had managed to trace the names of their directors and the records``.

    SOURCE: Guardian

    ReplyDelete
  13. AHA, KUMBE MOI FEKI.

    ReplyDelete
  14. Ni kitendo kizuri na chakutia moja viongozi wetu wanapowatembelea wagojwa na kuwajulia hali wakati wakiwa katika ziaara zao za nje.Lakini kuna kitu kimoja najiuliza .Gavana wa zamani wa BOT Balali alipokua anaumwa mpaka kifo chake alipokua amelazwa hospitalini huko Marekani mbali na kua alikua kiongozi muhimu wa serikali na ukizingatia katika kipindi kile kabala ya kuvuliwa madaraka alikua ni mfanyakazi wa serikali.Viongozi wengi wa serikali skiwemo Rais JK walikuwepo katika nchi hiyo mara kadhaa lakini hatukusikia hata siku moja ya kua kiongozi Rais,Waziri hata balozi kwamba amemtembelea na kumjulia hali marehemu Balali.Au kunasababu.MUNGU IBARIKI TANZANIA

    ReplyDelete
  15. ETI DEFINITION YA HEALTH INSURANCE NI KUWA INALIPIWA NA MWAJIRIWA NA MWAJIRI, HIYO SI DEFINITION YA HEALTH INSURANCE NA SI SAHIHI, JE NA WALE AMBAO HAWAJAARIWA? HEALTH INSURANCE NI KUWA INALIPWA NA MTU AMBAYE AKIPATA MATATIZO YA KIAFYA ATATIBIWA KUTOKANA NA HEALTH INSURANCE YAKE UWE UMEAJIRIWA AMA LA. TUSICHANGANYE VITU HAPA, MWAJIRI HUWA ANASAADIA TU MFANYAKAZI WAKE KUMCHANGIA GHARAMA YA HIYO HEALTH INSURANCEB NI KAMA MOJA YA FRINGE BENEFITS ZA KUAJIRIWA NI SAWA NA KUNUNUWA MAFUTA YA GARI SI WALIOAJIRIWA TU NDIO WANAONUNUA MAFUTA YA GARI MAFUTA YA GARI HUNUNULIWA NA KILA MTU MWENYE GARI UWE UMEAJIRIWA AMA LA, LAKINI KUNA WAAJIRI WANAOTOA FUEL ALLOWANCE KWA WAAJIRIWA WAO. NI KWELI U.S.A WATU WENGI HAWANA HEALTH INSURANCE SIMPLY BECAUSE THEY CAN NOT AFFORD IT, IT IS VERY EXPENSIVE, NI WALE WACHACHE TU WALIOAJIRIWA NDO WANAMUDU KUNUNUWA HEALTH INSURANCE WAKISAIDIWA NA WAAJRI WAO HATA HAWA SI WOTE KWA VILE KUNA WAAJIRI WENGINE HAWAWEZI KUWALIPIA WATU WAO, U.K. HAKUNA HEALTH INSURANCE MATIBABU NI BURE YANALIPIWA NA SERIKALI.

    ReplyDelete
  16. Mdau wa UK you are real mbongo!
    In prestenting your comments you don't need to put others down, however I'm glad to hear your comments. In your view of people should deliver development strategies in their community instead of waiting for central government, sounds real great, but what will happen in those areas with less resources such as people like you who are ready to finance projects?
    You have been talking about Mbezi, I assume that is where you reside, what about your native village where you and your ancestors are coming from? Have you already organized and funded for better health services, good road servises, electricity, water supply etc?
    In Tanzania we are now moving fast in social economic and one of the reasons is having good leveal of literacy, during socialst era, the majority achieved goals of being fluent in Swahili reading and writing. Comparing to our neighbours Kenya and Uganda where by they have good level of education on few and large number of elders who are completely ilterate.

    LK.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...