MAOFISA wa ngazi za juu katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba na Deogratius Kweka, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam, wakikabiliwa na mashitaka matatu ya kutumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh bilioni 200.
Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo Hadija Msongo jana, Wakili wa Serikali John Lwabuhanga alidai kuwa Liyumba ambaye ni Mkurugenzi wa Utumishi na Utawala wa BoT na Kweka ambaye ni Meneja Miradi wa BoT, wanakabiliwa na mashtaka ya kutumia vibaya madaraka wakiwa watumishi wa umma.
Akiwasomea mashitaka, wakili huyo alidai katika mashitaka ya kwanza dhidi ya Liyumba kuwa, katika siku tofauti kati ya mwaka 2001 na 2006, akiwa mtumishi wa umma BoT, alitumia madaraka yake vibaya kwa kuchukua uamuzi wa kuandaa ujenzi wa jengo la BoT bila kufanya makubaliano na Bodi ya Uongozi wa BoT.
Soma stori nzima kwa



hivi jamani nchi yetu ni tajiri kiasi gani mpaka hela nyingi mno kiasi hiki kinapotea na bila watu kuwajibika wakati huo huo? Tanzania ni masikini kwa kujitakia thats it.
ReplyDeletemda "cha mtu mavi"
Hii haijakaa vizuri, mkurugenzi wa utumishi na utawala atachukuwa vipi maamuzi ya ujenzi huu mkubwa hivi bila kuidhinishwa na bodi?waendesha mashitaka fanyeni kazi vizuri.
ReplyDeleteNakumbuka kuna gazeti lilitoa habari kuhusu ufisadi mnamo 2001 ikaundwa tume na matokeo ni kwamba hakuna ufisadi, sasa mheshimiwa wa wakati huo kabla ya JK ndio alioitoa hiyo statimenti basi inabidi aitwe mahakamani akaidefend statement yake.
Thumbs up JK, kumbuka Rome ilijengwa baada ya kufagia mafisadi kwa kaisari kuwapeleka kwenye gullotine kukatwa vichwa pindi wanapobainika, hao inabidi walindwe kweli kesi iishe, wananchi wana hasira nao, viva JK!
MWALIMU KASEMA "IT CAN BE DONE, PLAY YOUR PART". Oh My God I loved that song. Chears JK and your people. these are the type of people we were waiting for. Na wale mabinti aliokuwa anawapa vi 'red saloon cars nyekundu' wote wanyang'anywe mara moja.
ReplyDeleteMdau
Cardiff
How on earth just one office of the Central Bank - a GOVERNMENT BANK can have such a power of doing things alone! I don't blame him, it is the entire govern is rotten and need to be taken into task. PEKE YAKE NI KUMUONEA SERIKALI NZIMA HAINA AKILI ITAWEZEKANAJI CHOMBO CHA UMMA KIKUBWA KAMA HICHO OFISA MMOJA TU AWE NA UWEZO KAMA HUO, NI UZEMBE WA SERIKALI YOTE, JAMAA HAKIMU AMWACHIE TU. NCHI ZENYE UTAWALA WA HAKI NA SHERIA ANGEACHIWA HURU NA MAHAKAMA HURU
ReplyDeletei don't believe mtu mmoja anaweza kutoa uamuzi wa kujenga benki kubwa kama hiyo bila ya kushirikiana na wakuu wake. nina shangaa kwamba serikali ilikua kimya mpaka jengo likaisha kujengwa ndio ikatambua mambo hayakuwa sawa. mbona hawakusimamisha ujenzi wa hilo jengo? ninafikiri ujenzi mkubwa kama huo lazima bodi ya benki ilikubali na serikali ilikubali pia. sasa kwanini watu wawili tu wapelekwe kotini. hizi kesi za ufisadi zimetungwa in such ni vigumu kuwashinda. sisi tungojee mwisho wake. i hope walipa kodi hatutaishia kulipa pesa za kuendesha hizi kesi na kuambulia ZERO.
ReplyDeleteMwee! we Anony wa January 28, 2009 3:59 AM usitake kutuchanganya vichwa... yaani vyombo husika vya dola vimefuatilia kwa kina tena kwa muda mrefu na hatimaye vimegundua kuwa huyo/hao jamaa wana issue ya kujibu wewe unasema aachiwe huru??!! Mheshimiwa mkuu wa wilaya ya nanihii, sampuli hii ya mtoa maoni hayo ndio wanazidi kututia hasira na uchungu. Acha wenyewe wajitetee huko kwa pilato, acha kuchongachonga hapa kujifanya unajua kuongea kama huna cha kuongea tulia tu. Mbona hujashangaa mtu huyo kuwanunulia mabinti kibao magari mekundu kila mmoja? yaani wewe umemaindi kufikishwa mahakamani kwani hela alizokuwa anazitawanya ulimkopesha? Big up JK nimekuelewa kwani ulisema wewe huwa ni mtu wa kutabasamu muda wote lakini kwenye issue za muhimu upo serious, nimekupata; kwangua wote mmoja baada ya mwingine mpaka watie fahamu.
ReplyDeleteKwa kweli haya mashtaka yanaacha maswali mengi kuliko majibu! Ninajikuta nina maswali na mtazamo kama wa annon wa Jan 28, 2009 8.11 AM. Hivi kweli limsingi linachimbwa uwanjani kwenu hiyo bodi ilikuwa wapi kuona? Ilikuwa safari za nje? Au kwenye ule usingizi wao wa kawaida? Vinginevyo na bodi nayo iwajibishwe kwa kujitia upofu! Na serikali wala haiwezi kukwepa lawama kwani nayo haiko makini vile vile!
ReplyDeleteTena nianze kwa kuilaumu kutuongezea hali ngumu ya maisha, huduma duni za afya, elimu misukosuko, miundombinu balaa...wakati kuna mabilioni ya fedha yanafujwa kihivyo! Na nchi yenyewe ikijifedhehesha kwa kukesha ikiomba omba misaada nje.
Michuzi kawape ujumbe wetu kuwa, kwa kweli wanatuudhi mno.....na kama inawezekana basi tuuze nchi yote kwa yeyote mwenye dau, hizo pesa tugawane kila mtu ajue lake. Manake tumewapa dhamana ya kututunzia amana zetu na wanashindwa kufanya hivyo...
ilo kabila mboni huwa halikosekani kwenye izi kesi za ufisadi Tz??
ReplyDeletedah!!jamaa wana akili za chap-chap
tih tih tih
wanaonewa tu,,wawapange msururu wale wooote ofisi kuu apo then tutaelewa
Namtafuta rafiki/dada yangu anaitwa MARY MWIWA SHELUKINDO KIEGEZO. Yeyote mwenye contact zake naomba anifahmishe tafadhali.
ReplyDeleteBENKI KUU NI CHOMBO KIKUBWA SANA CHA SERIKALI SIAMINI MTU MMOJA TU ANAWEZA KUFANYA MAAMUZI MAKUBWA KAMA HAYO NA KITU KIKAENDELEA BILA YA WAHUSIKA KUKISHTUKIA, HAPA KUNA JAMBO WANATAFUTA WA KUMTUPIA LAWAMA TU NA KUTAFUTA MTAJI WAKISIASA WA KUSHINDA TENA 2010. UKWELI MNAWAONEA TU WANAPASHWA KUACHIWA HURU KAMA WATU WALIVYOSEMA HAPO JUU NA KAMA KUNA HAKIMU ANAYEJUWA HAKI NINA AMINI WATAACHIWA. NA KIUTENDAJI SIDHANI HUMAN RESOURCE DIRECTOR NI KAZI YAKE MASWALA YA UJENZI? HIYO HUMAN RESOURCE GANI? THE GOVERNMENT INATAKA KUWAFANYA HAO SCAPEGOAT KUFICHA MAOVU YAO, HAPO IKULU INAHUSIKA, WIZARA YA PESA INAHUSIKA, WIZARA YA UJENZI INAHUSIKA, OFISI YA WAZIRI MKUU INAHUSIKA. NITAELEWA KAMA ALIAGIZA KITU KIFANYIKE KINYUME CHA MAKUBALIANO YA BORAD NA SERIKASLI, AU ALI-INFLAT PRICES ZA VITU NA KUONGEZA TEN PERCENT YAKE LAKINI MAAMUZI YOTE YA JENGO PEKE YAKE.
ReplyDeleteWEWE MGOSI HUYO MARY NI MKE WANGU WEWE UNAMTAFUTIA NINI TUTATIANA ZAMBI MGOSI
ReplyDeleteDAH HIVI KWEKA BADO ALIKUWA MENEJA WA MRADI HUU?. JAMAA NAMKUMBUYKA ENZI ZA NAFCO KAPUNGA RICE FARM PROJECT ALINUNULIWA GARI MPYA AINA YA NISSAN PATROL ROOF TOP WAKATI ZINATOKA KAMA ZAWADI KUTOKA KWA WADE ADAMS WALIOKUWA WAJENZI WA MRADI HUO.
ReplyDeleteKIMSINGI HAIKUWA ZAWADI MAANA JAMAA WALIJUMUISHA KATIKA MALIPO KUPITIA MALIPO YA UJENZI WA KILA MWEZI. CERTIFICATE ZIKITENGENEZWA JAMAA WANAWEKA NA MALIPO YA NISSAN.
ALIJENGEWA PIA NA NYUMBA. AMA KWELI ALIYE NACHO HUONGEZEWA. MWAKA 2001 TENDER ILITANGAZWA TENA SKANSKA WAKAOMBA KUIJENGA KWA DOLA MILION 36 , WACHINA DOLA MILION 18, NA KAMPUNI YA AFRICA KUSINI MILIONI 45, BODI IKAZIKATAA TENDA ZOTE IKATANGAZA UPYA. SASA NASHANGAA KUONA MAJENGO YALE YALE KUGHARIMU POUND MILIONI 300.
LAZIMA KUNA SIRI ITATOKA BAADAE SIAMINI KAMA NI HAO WAWILI TU.
ALAFU DHAMANA NI BILLIONI 55 UNAAMBIWA LYUMBA ANAYO YAKE TAYARI PALE PALE KATAKA KUTOA SEMA MAHAKAMA IKASITISHA IMESEMA INAHITAJI MDA KUAKIKISHA NYARAKA.HA HA HA BONGO KWELI TAMBARARE.
ReplyDeleteACHENI UTANI...NAVYOELEWA MKURUGENZI WA UTAWALA NA UTUMISHI ANAHUSIKA NA MAMBO YANAYOHUSU MASLAHI YA WAFANYAKAZI.SASA INAKUWAJE NDIO APANGE MIPANGO YOTE YA FEDHA..KWELI WATANZANIA NA SERIKALI YETU NI VIHIYO!!!SIJAWAHI KUSIKIA POPOTE DUNIANI KUWA MKURUGENZI WA UTAWALA NA UTUMISHI ANAHUSIKA KATIKA KUPITISHA NA KUIDHINISHA MIRADI..NI HUKO TANZANIA TU.JE TUTAJIFUNZA LINI?TUTAENDELEA KUDHARAULIKA SIKU ZOTE KAMA HATUTABADILI OUR MINDSET.UPUUZI MTUPU SERIKALI YETU INAFANYA.
ReplyDeletewatu wengine wanasema eti one of those people aliwanunulia watu magari jee ulifanywa uchunguzi ikajulikana kweli alifanya hivyo au ni mambo ya ku guess. mimi kwakweli sikubaliani kuwa hao watu wawili peke yao walitoa uamuzi wa kujenga hiyo benki. first of all mkubwa wa benki alikuwa wapi. itakuaje waziri, gavana wa benki, serikali na bodi waachie maofisa wa chini kuliko wao watoe uamuzi. hawa watu pengine walikua wanatumiwa kuweka saini kwenye mikataba tu. hivi tanzania kila mwenye kesi ni lazima awekwe ndani? sheria zetu zimejaa siasa. sijui kama tuna koti HURU.
ReplyDeleteWEWE UNAYESEMA KABILA FULANI HALIKOSEKANI KWENYE HIZI KESI ZA UFISADI UNAMAANISHA KABILA GANI. KAMA UNASEMA NI WACHAGGA TAFADHALI UWAKOME. WACHAGGA HAWAJA MWIIBIA MTU. FUNGA MDOMO WAKO.
ReplyDeleteWadau, naona kuna confusion ya mashtaka, sio kwamba wao ndio walioamua kuhusu kuanza huo ujenzi,
ReplyDeleteNaona ripoti ya kwanza kwenye hii blog - ' uamuzi wa kuandaa ujenzi wa jengo la BOT bila kufanya makubaliano na Bodi ya uongozi BOT' sio sahihi haikunukuliwa vizuri.
Kwenye gazeti la citizen wanasema waliidhinisha 'extensions' soma
http://thecitizen.co.tz/newe.php?id=10196
'Mr Liyumba, in his capacity as the BoT's director of personnel and administration, made a decision to extend the project's contract without the approval of the central bank's board of directors.
In the second count, also against Mr Liyumba, the prosecution alleges that he authorised substantial structural changes to the BoT project without official approval and in contravention of the Public Procurement Act and the bank's regulations'
Magazeti ya daily news na ipp media
http://dailynews.habarileo.co.tz/analysis/index.php?id=9732
http://ippmedia.com/ipp/guardian/2009/01/28/130462.html
nayo yanasema- '
Liyumba abused his authority by undertaking major decisions on the extension of the construction project and implementing it without the approval of the bank`s board of directors'
Nimeamua kusafisha hewa ya mashitaka yenyewe kwamba hawa jamaa baada ya maamuzi ya kwanza ya ujenzi huo wao walipitisha kinyemela maongezeko ya bei bila kupitishwa na bodi.
kwa hiyo bado ni mafisadi na hizi tuhuma ni nzito na sio kwamba zimefanywa ili waondoke kirahisi kwenye kitanzi.
swali nauliza - raisi hawezi akatumia madaraka yake akawapa kibano cha detention na kazi ngumu hata kama watatoa dhamana, manake kila fisadi anatoa dhamana ....sasa ndio nini...wakae waoze huko ...hawatakiwi kurudi kuishi na jamii...wadau mnaionaje?