HABARI TOKA KAMPALA, UGANDA, ZINASEMA MCHEZAJI KEVIN YONDANI WA KILIMANJARO STARS ANATAFUTWA NA POLISI WA HUKO KWA TUHUMA ZA KUMJERUHI KWA CHUPA MSHABIKI WA MPIRA BAADA YA GEMU NA HARAMBEE STARS AMBAPO TIMU HIYO YA BARA ILILALA KWA BAO 2-1.
HABARI ZINASEMA VIONGOZI WA TFF WALIONGEA NA MDAI NA KUKUBALIANA WAYAMALIZE KWA WAO KUKUBALI KULIPIA GHARAMA ZOTE ZA MATIBABU ZA SHABIKI HUYO AMBAYE NI RAIA WA UGANDA AMBAYE BAADA YA KUPIGWA ALIKWENDA KULIPOTI POLISI.
sio KULIPOTI ni kuripoti!
ReplyDeleteHawa watoto wajinga, wameshaanza mambo ya Kibongo, sijui tutabadilika lini: There is no excellency in our country. Wamefungwa halafu wanaanza upuuzi.
ReplyDeleteNi matokeo ya malezi mabovu kwenye klabu anayotoka ambako mchezaji anaweza kumtukana kiongozi wake au kumpiga kocha wake tena hadharani na asichukuliwe hatua yoyote ,alijisahau alidhani yuko bongo hao jamaa bado wanakumbuka vita ya Kagera
ReplyDeletesasa kama walishakubaliana kuyamaliza wenyewe kwa wenyewe polisi wanamtafutia nini?
ReplyDeletePia hii ndio maana tuko nyuma sana kwa mambo mengi, mtu akipata umaarufu mdogo tu bichwa huwa kubwa kuliko gunia la nazi. i hope atafungiwa maisha kucheza timu ya taifa kwani kitendo chake kimeiletea timu na nchi aibu. watu lazima wakumbuke wanapowakilisha taifa letu wanatakiwa kijiheshimu na ku-behave vyema.
Hivi jamani nazisikiasikia tu hizi habari kuwa kuna mchezaji kama sikosei wa simba ambae alimpiga kocha wake je ni mchezaji gani huyo na kocha gani nae aliepigwa?na hatua zipi zikachukuliwa?ni hayo tu wadau....kingine kabla ya kuanza kulalama hapa tujiulize nini kilipelekea hadi huyo mchezaji kurusha chupa?washabiki wa soka nao wasisahau kama wachezaji sio manabii nao ni binadam pia kwahio wasizidishe ushabiki wao kupitukia kiasi cha kuanzisha fujo za kumkasirisha mtu.Binafsi nilikuwemo kwenye kikosi cha stars kilichotolewa na sudan kwenye challenge ya mwaka jana mjini daresalaam 2-1 baada ya mpira kwisha ilibidi wachezaji pamoja na mwalimu maximo tuje tusindikizwe na FFU coastal bus tulilolipanda wachezaji lilirushiwa mawe,vyupa nk mchezaji meshack abel nusura atolewe jicho na mashabiki wahuni.mi nashauri washabiki baada ya game wasiwakaribie wachezaji ambao mara nyingi wanakuwa na tempa baada ya game.
ReplyDelete