JK akiweka jiwe la msingi katika majengo ya kota za polisi barabara ya Kilwa rodi leo akiwa pamoja na Mkuu wa polisi (IGP) Afande Said Mwema
Habari ya kazi Brother Issa,
Napenda kuchukua fruksa hii kwa kukujulisha kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya M. Kikwete leo tarehe 13/01/2009 anaweka jiwe la msingi katika nyumba za Polisi eneo la Kurasini jirani na Barabara ya Kilwa rodi.
Tunampongeza rais wetu kwa kutekeleza Ilani ya CCM kwa kuboresha maisha ya Mtanzania hasa askari Polisi. Juzi juzi alikwenda kufungua nyumba za wanajeshi leo Polisi. hii ni Hatua kubwa sana

TUNAMPONGEZA
Hapo nakutumia baadhi ya nyumba hizo mpya na za zamani ili wadau waweze kuziona kwani askari wetu wanapata taaabu sana. ila isiishie kwa serikali tu hata wadau wanaruhusiwa.
Kwani hapo zamani zilionekana hivyo zilivyo na sasa ni maghorofa

Regards...
masqtz@yahoo.com





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Mtuma picha naye ni askari, hongera sana kijana. Naona soon tutakualika uwe unapiga picha katika sherehe, manake mwanzo niliona ulimtoa na mkeo hapa bloguni. Kaza buti kijana.

    ReplyDelete
  2. ninyi polisi hata mpewe dunia hamtaacha kutafuta rushwa. mnanikera ninyi #$%^&*()

    ReplyDelete
  3. Halafu sijui bado mtamsubiri huyo JK aje kuwahimiza swala la usafi??manaake nishatembelea sehemu tofauti zenye makazi ya hawa jamaa wala rushwa wao wanachojua ni kupiga kiwi mabuti yao meusi tu na kunyoa denge lkn idara ya USAFI NI ZERO KABISA!!Inakuwaje jamaa wachafu sana namna hii hawa kwenye makazi yao kibaruani kwao kote wachafu hawajijali kabisa,tembeleeni kote kwenye makazi ya polisi mtakubaliana na mimi jamaa hawajipendi kabisa hawa kuanzia huko oysterbay,changòmbe kooote kwenye makazi ya polisi hadi huko mikoani.NAZIONEA HURUMA MASKINI HIZO NYUMBA ZITAKAVYOFUBAZWA NA HAWA MAKONKODI WA KUDAKA KITU KIDOGO.BADILIKENI MJIPENDE KIDOGO MMEZIDI UCHAFU NYUMBA MZIJALI HIZO HUKO KWENYE HIVYO VITUO VYAO VYA KAZI KUNATEMA HARUFU KALI UKIINGIA WENYEWE HATA HAWAJALI NAWASHANGAA SANA HAWA MABWANA UJUE

    ReplyDelete
  4. hayo majengo mapya yape mwaka mmoja tu yatakuwa na rangi tofauti na ya sasa,mavi ya bata yatakuwa kila sehemu hawa jamaa kwa uchafu nadhani wanaongoza,jamani uchafu siyo umasikini ni tabia zenu nyie manjagu.

    ReplyDelete
  5. Mimi kilicho nitoa apetite ya hizi picha ni kwamba mtuma picha ni polisi ila analeta U-CCM hivi kweli kwenye uchaguzi mtaacha upendeleo wa kuwapiga wapinzani mabomu ya machozi na virungu kwa kauli kama hizi?.

    Siasa ndizo zinafanya watu waache kutoa maamuzi ya maendeleo na badala yake watu wanafanya watakavyo hasa wafanya biashara kama ya mafuta. Hebu tuache siasa sasa tuchape kazi kujenga nchi. Hilo ni jukumu la serikali yoyote bila kujali chama kuhakikisha askari na raia wake wanakuwa na maisha bora, Tuache itikadi tujenge Tanzania yetu

    ReplyDelete
  6. Wekeni gesi kutoka huko Songa na Mkuranga ili wasipikie mkaa!

    ReplyDelete
  7. Aroo! Michusi uwe unariambia
    'Mtuma habari unatakiwa uwe makini' ukiongerea masuala ya geshi, hakuna siasa katika mageshi yetu. Ira uritakiwa kutoa pongezi kwa serikari tu na sio vyama na irani zao za ukaguzi! na maana Uchaguzi- maana nidhamu ya kijeshi iko juu.

    ReplyDelete
  8. nampongeza Jk kwa project hiyo, sijui kaileta yeye au Babu Ben? kwa kweli nyumba za polisi zilikua zinatia kinyaa. halafu mambo ya kupanga kwa polisi si mambo, mtoto wa mwenye nyumba kama kibaka polisi atasema nini?

    ReplyDelete
  9. Hallow hapo juu nakuonga mkono, hawa jamaa ni wachafu saana ndio maana wanacheza mchezo mchafu wa rushwa maana wamezoea uchafu. Sasa subiri baada ya mwaka hizo nyumba utaziona. Wapewe somo juu ya matumizi sahihi na utunzaji nyumba.

    ReplyDelete
  10. Naungana na anoun hapo juu.USAFI jamani.Nyumba za polisi ama jeshi zimezidi kwa uchafu.

    Mzitunze hizo nyumba ili na wajukuu zenu wakiwa polisi waweze kuishi.

    ReplyDelete
  11. Nyumba zinaonekana safi lakini zitachakaa ndani ya mwaka mmoja tu. Hawa jamaa na familia zao ni wachafu ajabu. Utakuta mama anayekaa floor ya juu anamwaga maji machafu chini kupitia kwenye dirisha la jikoni, anarusha uchafu na choo cha mtoto chini tokea ghorofani. Anapika kwa kuni kwenye mafiga wakati yuko ghorofani au mkaa usioiva vema na punde si punde ukuta wote ni mweusi tii, hakuna tena rangi, madirisha hayana kioo hata kimoja, milango yote vitasa na bawaba vimeng'olewa, vyoo na mfuma wa maji machafu vyote vimeziba na kila aina ya ghasia. Hayo ndiyo mambo ya nyumba za umma. Bongo tambarale
    Mdau

    ReplyDelete
  12. hongera JK lakini pia mapolisi wafundishwe usafi wa mazingira na uzazi wa majira. nakumbuka nyumba za arusha mjini zikichafuliwa sana na wake zao walikua wanazaa kila mwaka. Hawakua na uwanja wa michezo karibu basi kijijini hapo kulikua shida sana.

    Wanatakiwa wawe wanalipa association fee kwa mwezi angalau wapate watu wa kufagia au hao wake zao kwa vile wengi hawafanyagi kazi basi wapangiane zamu ya kusafisha mtaa kama sungusungu vile. Kila mtu ajue zamu yake.Bila hivyo within a year itakua balaa.

    ReplyDelete
  13. Jamani hawa jamaa si kama tunawasingizia,Ni wachafu big time.Hebu mdau mmoja ajaribu kwenda pale makao makuu ya traffic,hatua chache kabla ujafika kwenye ile reception yao kama unatoka upande wa central huku,kuna harufu kali mpaka unasikia kizunguzungu,Khaaaaap!poh!Ukiachilia mbali swala la UCHAFU,wao wenyewe ni vibaka kwelikweli,ukienda baada ya mwaka utakuta vitasa vyote hamna,si kama vimeharibika,Vitasa utakavyovikuta kwenye hizo nyumba mpya ni vitasa original kwa sababu jamaa wamefanya projections za miaka mingi mbele.Utakuta hawa jamaa wanaving'oa wanaenda kufunga kwenye nyumba zao MBAGALA anaweza akaacha hivyohivyo au kwa kuona noma akanunu kitasa cha shilingi elfu mbili na mia tano akakifunga,akiulizwa anasema kiliharibika mimi nikajitolea kununua kipya.Bastard!

    ReplyDelete
  14. Hongera NSSF chini ya uongozi wa Dr Dau naona mnazidi kufanya mavituz...juzi Arusha Leo Dar ..makes you wonder hao akina PPF na NSPF wanafanya nini?

    mdau wa MADAFU hapa juu

    ReplyDelete
  15. Majambazi yachapana risasi na polisi Dar

    2009-01-13 16:24:43
    Na Sharon Sauwa, Manzese


    Eneo la Manzese Jijini Dar es Salaam leo asubuhi limegeuka kama uwanja wa vita baada ya majambazi na Polisi kurushiana risasi, zilizofanya barabara ya Morogoro kufungwa kwa zaidi ya nusu saa huku wananchi waliokuwa katika eneo hilo wakikimbia ovyo kuokoa maisha yao.

    Katika tukio hilo, majambazi watatu walijeruhiwa na wengine wawili kutoroka kwa kutumia gari walilolipora fasta fasta katika eneo hilo.

    Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo ambalo limetokea mishale ya saa 3:00, gari lililoyabeba majambazi hayo lilikuwa linatokea Ubungo kuelekea Magomeni, na lilipofika Manzese Darajani, yakaanza kurushiana risasi na Polisi.

    ``Yaani ilikuwa kama filamu...tuliona polisi wakianza kurusha risasi kuelekea kwenye gari hilo na mara majambazi nayo yakajibu mapigo...punde si punde, yakateremka kwenye gari,`` mmoja wa mashuhuda hao amedai.

    Amesema katika mpambano huo uliodumu kwa zaidi ya nusu saa, majambazi wawili yaliyokuwa kwenye gari inayoaminika kuwa ni teksi yenye namba za usajili T680 AEN, yalijeruhiwa kwa risasi na kupelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

    Imedaiwa kuwa kama si polisi kutumia nguvu za ziada kuyalinda, basi wananchi wenye hasira wangeyamalizia mbali.

    Imedaiwa kuwa majambazi mengine mawili yalikimbilia sokoni ambapo nako yalikumbana na wafanyabiashara katika soko la Manzese.

    Habari zaidi zinadai kuwa jambazi moja lililokuwa tayari limejeruhiwa, lilidondosha bunduki moja sokoni hapo lakini jingine lililokuwa nyuma, likaibuka fasta na kuiokota na kisha yote mawili yakaanza kutimka pamoja kuelekea maeneo ya bondeni.

    ``Yakiwa njiani, yaliona gari moja lililokuwa linapaki, yakalivamia, kumpokonya swichi dereva wake na kisha yakatoweka nalo,`` kimedai chanzo hicho.

    Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakuweza kupatikana.

    SOURCE: Alasiri

    ReplyDelete
  16. nimecheka mpaka mbavu sina jinsi watu walivyo andika juu ya uchafu wa polisi wetu. kwakweli hii tabia ni lazima waibadilishe. mbona nguo zao na viatu vyao ni safi hivyo. wanatakiwa wawe na watu wa kuwafundisha usafi. i hope some of you watu wa jeshi mnasoma hii blog.

    ReplyDelete
  17. Jamani Mimi nilikuwa naishi kwenye kota za NBC Mtoni kijichi, baada ya muda zile nyumba walipewa polisi hebu nendeni mkazione mtasikitika!!! kwanza unakutana na mikaa imemwagika ngazi zote!!! mifuko ya rambo, bata wamezaliana wala hawana muelekeo, zinanuka hata ukipita karibu hiyo harufu yake sipati picha kwekweli Mapolisi wachafu sana, sana, sijui kwanini? YAANI ULE UNADHIFU WA WA AWALI KWENYE ZILE NYUMBA HAUPO TEN YARABI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...