sio kweli kwamba utamaduni wa kujisomea umeyeyuka. hii ne shefu ya nyumbani kwa mmoja wa wadau kadhaa niliowahi kuwatembelea na kukuta imesheheni vitabu mbalimbali ambavyo vyote amesoma na anaendelea kusoma vingine. hongera mdau kwa kudumisha utamaduni huu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Mkuu wa Nanihii umekumbushia jambo la muhimu sana.
    Hivi lakini katika mipango miji huwa kuna maeneo ya maktaba? Sijaona maktaba jirani na uswazi napoishi, kila nikihitaji huduma za maktaba mpaka niende sentro tu.

    ReplyDelete
  2. kimekosekana cha kitabu cha Nyerere hapo.

    ReplyDelete
  3. Bado sijaona Rasputin mshauri wa Mfalme wa mwisho wa Himaya ya Urusi. Hiki kitabu kinafaa kusomwa na kila mpenda kusoma vitabu.

    The Clash of Civilizations and the remaking of world order- Samuel P. Huntington ISBN 0-684-81987-2

    The clash of fundamentalisms: crusades,jihads and modernity by Tariq Ali ISBN 1-85984-679-3

    ReplyDelete
  4. Vinasomwa ama ni mapambo tu!

    ReplyDelete
  5. siyo mbaya, lakini ni collection ndogo sana hiyo halafu iko too safe and dull. Matter of fact, kwa nini wazushi msianze kutuma collection zenu humu kama alivyofanya huyu shujaa, tuidiversify kidogo hii blog bab-kubwa ya michuzi, don't you all think it's a great idea?

    ReplyDelete
  6. Nilikuwa namaanisha kusema ipo dull and too safe. Jinsi nilivyoandika mwanzo inaweza kuonekana kuwa contradictory.

    ReplyDelete
  7. sikuiz ni mambo ya net kaka!vitabu vyote vipo kwenye net na story za watu wote mashuhuri.nafkr kwa generation ya .com itakuwa ngumu kusoma vitabu.teh!teh!

    ReplyDelete
  8. mkuu ni kweli kuna watu wanajisomea ila wastani wao ni mdogo sana. watu wengi hutumia muda mwingi kwenye mabaa, kwenye mambo ya siasa, kuangalia mipira hasa ya Uingereeza, vijiweni n.k

    kuna mambo mengi yanachangia mfano utamaduni wetu, uchumi wetu, uhamasishaji, muda, upendeleo, starehe zinazokuzunguka n.k

    yote yakifanyiwa kazi yanaweza kuleta mabadiliko

    ReplyDelete
  9. road to freedom siyo kitabu cha kusomwa na mswahili. neda amazon tafuta kitabu chchote cha steve biko ndo utajua hiyo shelf yako ina mis kitu

    ReplyDelete
  10. Hicho cha Mugabe noma angekitoa!!

    ReplyDelete
  11. Hivi kupanga vitabu kwenye shelf ndiyo kusoma? Mbona tunapotea njia katika kutoa maelezo fasaha? Ukija kwenye nyumba yangu ukakuta vitabu vimejaa kwenye shelf na vingine vimeota fungus then utanisifia kwamba ni msomaji wa vitabu mzuri kweli? Mimi naona huo ni usanii.
    Mdau

    ReplyDelete
  12. imekosekana vitabu vingi tu vya msingi jamaa inaonesha ka egemea sana marekani na south of africa. Mwenye vitabu atakuwa anataka kuelekea kwenye siasa hasa kujuwa kuwa kiongozi wa kitu fulani ni vizuri ongeza bidii, sababu hata watu unaowasoma wanamuelekeo na pia wameendana, tunajaribu kuwasomesha wenetu vitabu sana kuliko kuwaacha kutizama ma tv muda mwingi TV wawe wanatizama vipindi vya watoto na documentary zinazoendana nao tusikate tamaa. Khamis Seif.

    ReplyDelete
  13. safi sana,,,mdau
    haijalishi ana mlengo gani wa kusoma vitabu ilmradi anapanua mawazo ya how the world goes on!!
    sio mtu kakalia mipicha weee na ushabiki usiomsaidia kitu,,so negatively addicted.
    kila nyumba ingekua na wazazi wenye akili wangewahimiza watoto wasome vitabu mbalimbali vya maana na wao wawe mfano,sio mzazi kakalia ku-watch kaole,nigeria nk
    hahahahaaaaa

    ReplyDelete
  14. Jamani tuache usenene hapa.Kujisomea vitabu ni kitu kizuri sana.Watz sisi ni wavivu wa kusoma vitabu.Huyu jamaa anafanya jambo la maana.Vitabu vipo madukani vingi tu,mitaani n.k. binafsi napenda sana kusoma vitabu lakini najikuta nakosa huo muda wa kusoma vitabu kwa sababu nipo 'bize'!!lakini muda wa kukaa Bar ninao mwingi sana.Hili ni tatizo kusema kweli.Ili nisibaki nyuma sana najitahidi kusoma makala ndefu kwenye magazeti "yenye akili"(Yapo duniani yakiwemo na ya Tanzania)

    ReplyDelete
  15. magazeti ni tofauti kabisa na vitabu wee "david villa"
    mda wa bar unaoeeee??afu nyie mnaoendaga bar kutwa kuchwa,au watoka ofisin kitako bar adi liamba ivi niwaulize mnapata nini uko cha maana??cha maendeleo??msilete sababu za kipuuzi tunazozijua
    kitabu ni kitabu

    ReplyDelete
  16. Someni Dreams of my father, Obama. Ama zao ama zangu, Elvis Musiba.

    ReplyDelete
  17. Someni NIKKI TURNER, huslers wife1 au HAROLD ROBBINS! WAANDISHI WA KIBONGO WAKO WAPI?CHNUA UPO? AGORO ANDURU UPO?

    ReplyDelete
  18. Anon wa jan 28 2009 1:56 pm. Anon tunakuomba Kaanze kusoma vitabu vya kiswahili Unaoeeee? Maana ya huo msemo unamaanisha kitu gani? Ofisin adi liamba, mnaoendaga, ivi.

    Kijana kasome muombe hata mwanao kitabu cha kiswahili akufundishe sio vibaya kufundishana. Mdau Iringa.

    ReplyDelete
  19. wee wa iringa kumbe tunajuana eee??
    namaanisha "yu do have time for"dont yu?
    "to go to" and from mornign till next day"

    understood?
    kalagabaho

    ReplyDelete
  20. kaka michuzi usidanyanyike kiurahisi mimi hapa kwangu nina Book Shelf Tano kama hizo na zimejaa vitabu vya kila aina dini na vya dunia fiction na non fiction , life teachings na leisure and I can guarantee you that nimesoma kama vitatu tuu hivi mpak mwisho .......so what I am saying ni kwamba kuwa na Shelfu ya vitabu katika nyumba haimaanishi kupata time ya kuvisoma.!!! Jaza mwenyewe

    ReplyDelete
  21. Du! Jamaa ana kitabu cha End of Poverty by Jeff Sachs wa Havard. This Fellow is real!

    ReplyDelete
  22. Michuzi hii post ni ya zamani kidogo. nimeipata kwa namna namna hivi. baadhi ya wachangiaji wamemuongelea agoro anduru. huyu jamaa nimemsoma akiwa ameshafariki. unafikiri hivi kwa nini hatuwaenzi watu kama hawa? this guy was great! he could have reached the levels of the achebes and ngugis had he been alive.

    Ombi. Tutafutie na tuwekee picha yake. RTD (tbc) wanaweza kuwa nayo. hazina hizi jamani, historia isijepotea.

    Nikuchekeshe. Unajua siijui sura ya Niko Zengekala

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...