Hello Brother Michuzi,
Nashukuru that unaendeleza gurudumu kama kawaida, pia nawasalimu wapenziwa blog yako kama kawaida. Kunajamaa mmoja anajiita mtoto namsalimu pia.
Sasa brother michuzi mimi napenda kuchangia maada iliyopita ya afande. siokama natetea au namuonea jamaa but, ndugu zangu nadhani hapa jamaa wawiliwote wanatatizo.
Kaka mwaka jana aliwahi kukosa leseni mwanama
/south-asia/splashing-a-pedestrian-
can-cost-you-your-driving-licence_10093920.html )
kama inavyosomeka kwenye link hiyo kwakumwagia maji mpita njia hukoduniani.
Pia kama mmeshafuatilia bongo mara nyingi kuna waendesha magari kibaoambao mchezo wa kuwamwagia maji wapita njia huwafurahisha sana, kiasi kwamba hata ukajaribu kumkwepa anaforce kukulowesha.
Labda pia wadau munaionaje suala la afande kufungua kesi na baadae achukuwe several days kufuatilia hukumu compared na adhabu ya muda mfupi?
Ni hayo tu, ----
Najua kuna kuheshimu umuhimu wa sheria,
and najua afande hakutakiwa kuadhibu lakini......(jaza mwenyewe).
Ni G7

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. Vitu Vingine Mnaongea Tu Ili Mradi mmeongea .sasa dereva ndio kanyeshesha Mvua au yeye ndio kaweka madimbwi barabarani na wewe mpita njia unaona dimbwi la maji na gari linakuja unataka gari lisimama upite? Hata Huko Kwenye Rami Mpaka chooni watu wanamwagiwa maji

    ReplyDelete
  2. you missed out the main point! human rights supposed to be put first before anything else, same as a police officer he should know better of the word "common sense". This is the problem we have with our police force, narrow minded and probably not educated! what a shame situation to see that type of behavior! he should be sacked and be a lesson to all.

    ReplyDelete
  3. huyo afande ni haki yake kumchapa na kumuogesha huyo dereva,hapa norway ukimwagia mtu maji machafu unaenda dukani kumnunulia nguo nyingine,madereva wa bongo wamezidi!!hongera afande..mkereketwa

    ReplyDelete
  4. Ukimwagiwa maji unatakiwa uende kushitaki mahakamani siyo kujidai we ni mahakama.

    Ikiwa wataachwa wanajeshi wawe juu ya sheria, hivi hiyo amani na demokrasia ya kweli na utawala wa sheria tutaufaulu lini?

    Dereva anatakiwa akashitaki mahakamani.

    Siku hizi wanajeshi wanatii sheria tangu wakati wa mboma na waitara alivyowafukuza wakipiga raia. Ila bado wachache wasioenda shule.

    Tena utakuta huyo mjeshi ni NCO (non-commission offiser), yaani hana hata mtoto wa nyota begani.

    ReplyDelete
  5. We unafikiri JK angekuwa hana nidhamu jeshini angekuwa kanali mpaka raisi? angefukuzwa au kufungwa.

    JK nyoosha tanzania.

    ReplyDelete
  6. mie wasiwasi wangu ni wakati wa adhabu, watoto walikuwa wapi (maana ni school bus).
    1.) usalama wa abiria (watoto) ulihatarishwa sababu dereva aweza kuchanganyikiwa.
    2.) watoto watakuwa na uoga wakiona wanajeshi na chuki na kazi za jeshi wakiamini kaka (dereva) kaonewa.

    ReplyDelete
  7. Anony wa tarehe January 27, 2009 9:28 PM:

    Wewe ni typical Tanzanian driver. Na kwa kuwa Tz imejaa watu kama wewe, itachukuwa miaka mingi sana kuelendelea. Kwa mawazo yako hayo, watu watazidi kufa tu barabarani. Nyie ndo mnaoshika brake mkiona ng'ombe barabarani, lakini mnakanyaga mafuta mkiona binadamu barabarani. Mvua hainyeshi Bongo tu. Na maji hayatuami Bongo tu. Hapa Japan kuna lami almost kila sehemu - isipokuwa mashambani, viwanja vya michezo...lakini maji hutuama pia (kama si kutiririka) kwenye lami km mvua ni kubwa. Pamoja na hilo madereva wanawaheshimu wenda kwa miguu. Haipunguzi chochote kutoka kwako ukipunguza mwendo unapofika sehemu ambayo maji yametuama na kuna binadamu wenzio wanaotembea kwa miguu. Ukapita kistaarabu halafu ukaendelea. Jiweke kwenye nafasi ya yule unayemrushia maji machafu. Kwa vile gari ina speed kuliko mwenda kwa miguu, mara nyingi (km si zote) wewe mwenye gari utakuwa umemkuta mwenda kwa miguu hiyo sehemu unayomrushia maji machafu. Sasa unata yeye apotee/ayeyuke tu ghafla hivi hivi ili wewe upita?

    Tubadilike jamani. Tusiishi kama wanyama - simba na nyumbu Serengeti. Tuweke ubinadamu mbele.

    ReplyDelete
  8. Wewe unayeleta mambo ya Japani humu wakati tukio hill limetokea bongo iliyojaa madimbwi kila mahali. Eti huku japani ndio kwanza umesafiri ini bwege wewe (mithupu) bwege siyo tusi acha tumweleweshe huyu fala. Anatuambia japani kuna barabara za lami halafu tena anatuambia maji sijui viwanjani sijui mashamabani. Kwa hiyo wajapani wanaendeshea viwanjani?

    ReplyDelete
  9. Mimi ninampa shavu huyo mjeshi. madereva wa bongo (sijui kwingineko) wamezidi sana. Tena kwa sisi akinadada anakurushia maji, anaendelea kucheka na kama ukilalamika anakutupia na matusi juu. Sasa immagine mtu unaenda kazini, na foleni za Dar, sijui urudi home kubadilisha au uendelee mbele kama umechanganyikiwa kidogo. wamezidi hao. Eti watu wanawatetea hapa, "haki za binadamu, haki za binadamu" ina maana wao ndo wana haki zaidi. Sasa kama barabara ina madimbwi tuache waenda kwa miguu kupita barabarani??? ama?? Tena angemchapa na vibao kabisa, upuuzi mtupu wanaoufanya hawa jamaa. Na ndo utakuta wanagonga watu kwenye Zebra, kwa ajili hii ya kutoona kama waenda kwa miguu nao ni walipa kodi ambazo zinatengeneza hizo barabara?? mfyuuuuu!!

    ReplyDelete
  10. kama alimwagia bila hiana angeomba tu samahani yaishe basi,,ila kama alimwomba msamaha na bado akamwogesha??walhali uyo askari nyambafu na wababe sana hawa sijui why???
    kama hakuomba msamaha apo fresh tu,kwani ata mie ningemsurubu tu

    ReplyDelete
  11. Wewe anony wa tarehe January 28, 2009 9:08 AM ni FARA TU. Kwani hapo Posta Dar hujaona maji yametuama siku zenye mvua nyingi? Kuna mashamba hapo posta. Pambafuuuuuuuuuuuuu! Mbuzi wewe.

    ReplyDelete
  12. kwanza asante sana "afande" kwa kumtia "adabu kidogo"huyu dereva typical wa tanzania yetu.Ningekuwepo ningekusaidia kurekebisha tabia yake zaidi!!

    kwa anony wa jan 28 2:27,
    ni swala zuri kinadharia kupeleka mambo kama haya mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake-lakini kwa mfumo wetu na mazingira ya matukio(too theoretical),hakuna hatua itakayochukuliwa na kwa kupeleka hilo utaonekana huna cha kufanya! dawa kumalizana kimtindo na hiyo ndiyo Bongoyetu.wabongo tumezoea hata itokee ajali,trafiki hajafika ama amefika watu wanamalizana wenyewe ama utabaki mwenyewe na mengi mengine ya barabarani ama mtaani.

    Mwanajeshi ni kioo ndiyo sababu kila mmoja amevutika na hili,japo wapo raia wanaofanya hayo na watu kubaki kukenua meno tu.kama hawa madereva hawatawaheshimu hawa walinda wananchi kwa kuwamwagia maji machafu nk.,wananchi hawatawaheshimu na hawataona umuhimu wao katika jamii-"dharau"

    pole sana wewe anony na wengine ambao hamna mnachojua juu ya mifumo ya jeshi letu, mnaowaletea dharau wanajeshi wetu tunaowaheshimu kwa kazi zao-unaongelea swala la elimu jeshini",umepitwa na wakati kabisa! "mjeshi ni mjeshi tu,awe na nyota ama la-heshima ni ile ile-ona unavyojifanya kutafasiri hiyo "NCO",umekwenda shule weye?-...(°°)..mbafu!

    kwako anony wa jan 28. 3:06
    1)unajiuliza wakati wa adhabu watoto walikuwa wapi! je wakati wa afande kumwagiwa maji watoto walikuwa wapi..!(piga brush akili yako-kuna vumbi jingi)
    2)watoto hawatakuwa na uoga wakiona wajeshi bali wataogopa kuendeshwa na dereva asiye na nidhamu!pia wanafundisha nidhamu mbaya hao watoto,unafikiri kwa mtindo huu hao watoto watawaheshimu wanajeshi kama watamwagiwa maji machafu na kutoheshimiwa?-"je,tunatambua wajibu/umuhimu wao hawa walinda nchi ama tunaosha vinywa tu.." hao watoto wenyewe mnawapigia "honi" wakiwa wanavuka barabara tena kwenye pundamilia na maneno juu!..mbafu!
    -pole/poleni sana walengwa.heshima kwa wote please!

    Ujumbe kwa madereva,nidhamu ya hali ya juu inatarajiwa kutoka kwenu ili muwe mfano wa kuigwa,usalama wa watu na heshima kwa jamii vipo chini yenu.

    msituongezee hasira kwa kutokuwa makini na kukosa nidhamu.
    sitawavumilia wala kuwatetea
    -"mfurukutwa"

    ReplyDelete
  13. Why are you so ..Upid! The is not who's who, but KWA NINI ACHUKUE SHERIA MIKONONI, KUTOA ADHABU TENA DHALILI KAMA HIYO.

    Mwanajeshi sio mahakama kamwe, na kazi yake sio kuhukumu. Hakuna mwenye haki ya kuhukumu isipokuwa mahakama.

    Kukosa leseni kwa huyo mwanamama ni issue isiyo kawaida ndio maana ikafanywa "NEWS." Learn how to think, and think deeply before you let others think with you.

    ReplyDelete
  14. Duuuu... mie siungi wala sikatai athabu aliyopewa Dereva. miaka ya 1997 nakumbuka dereva wa ice alinirushia maji machafu makusudi, tena mbaya zaidi ni school uniforms. Jino kwa jino eneo lenyewe karibu na dumpo nilichukua kopo chafu chota maji machafu tena yanayonuka maana kwambele kidogo atasimama kupakia nakushusha abiria. nilihakikisha abiria wa mbele hatodhurika nikamwaga usoni. maana kweu bongo kweli ukienda kumshitaki unajisubua bure. maana lazima uanzie kituo cha polisi njaa tupu, mahakamani. kesi ni nyingi hadi hawana muda wa kusikiliza. kikubwa tulichokiangalia hapa ni mtoa adhbu ni nani. kwani angekua rai wa kawaida ndo katoa je? Watembea kwa miguu wana haki ya kutumia barabara. sasa dereva kama hana nidhamu na udereva wake itafutwe njia mbadala. Sio wote wanaowavalisha wezi matairi wanapenda. Bali ni kule kujua wasi kuwa hata akipelekwa mahakamani baada ya muda utamwona mtaani anakutamia.

    ReplyDelete
  15. Sasa Marwa Chacha alitomsomea mashitaka na akahukumu mwenyewe. Mwenye wivu na ajinyonge. Tunaamini dereva atakuwa amejifunza ustaarabu. Usipofunzwa na mamako ulimwengu unakufundisha.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...