Hello Mkuu Michuzi.
Natumaini hajambo na unaendelea na libeneke kama kawaida.
Natumia muda huu kukuomba kunitangazia blog yangu mpya hii iitwayo Wabongomeet

Nimechukuwa jukumu hili la ku-blog kama ufanyavyo ili niweze kuwasaidia watanzania wengine kupata nafasi ya kuungana katika kutafuta marafiki na hata wachumba popote duniani. Hakuna binadamu perfect, natumaini kwa nyie wazoefu wa ku-blog mtakuwa tayari kubadilishana mawazo na wale wanaoanza shughuli hii.
Ninajivunia kwa hili (ingawa mie bado mchanga katika blogging) kwa sababu mimi binafsi nili-immigrate kutoka Arusha kuja hapa nilipo baada ya kukutana na mme wangu miaka 6 iliyopita kupitia cyber-love. Na mpaka sasa hivi bado niko katika ndoa na nina mtoto moja.

Nitashukuru iwapo utafiria ombi langu. Vilevile nimeweka link ya blog yako kwenye blog yangu. Naamini hii ni njia mojawapo watu wanaweza ku-network kupitia blog mbalimbali.

Natanguliza shukrani.
Josephine M.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Big-up JOSEPHINE

    ReplyDelete
  2. Kaka Michuzi nashukuru sana kwa kusikiliza maombi ya kiwekea tangazo kwenye blog yako.
    Husijesita kunipa ushauri anytime nitakapohitaji especially kwenye blogging.
    Nashukuru sana kaka yangu.

    ReplyDelete
  3. libeneke la wachumbaaaaaaaaaaaaaa.....

    msiwe sasa mnatuzingua humu kwa michuzi...okeeeeeeeee

    mi namtaka mashaka tu!!!!

    BIG UP josephine!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...