Mh. Dk. Slaa akiteta na mwenyekiti wa Chadema Mh. Freeman Mbowe (shoto) na Mh. Zitto Kabwe kwenye moja ya mikutano ya hadhara ya chama hicho


Mwishoni mwa mwaka jana nilipata nafasi ya kuzungumza na Bongoradio.com kuhusu masuala mbalimbali ya kufunga mwaka. Ninawaletea sehemu kidogo ya mahojiano hayo pamoja na mahojiano niliyoyafanya na Mhe. Dr. Wilbroad Slaa (Karatu-Chadema) kuhusu kilichosababisha mgombea wao msomi mwanasheria Bw. Sambwee Shitambala kushindwa kufuata taratibu rahisi za kuapa kabla ya kushirki uchaguzi huo mdogo.




Baada ya kusikiliza mahojiano hayo piga kura na upande wa kulia wa tovuti hii na utoe maoni yako ni nini unafikiri kilitokea Mbeya Vijijini. Unaweza kusikiliza mahojiano kwa kuingia kwenye "Podcasts" kwa kubonyeza herufi ya "M - Podcast" upande wa kulia wa ukurasa wa mbele wa tovuti yetu Kisha angalia miaka na tarehe ya onesho.



Kwa mawasiliano mengine yote tuandikie






na kwa kutaka kujiandikisha kijarida cha bure cha "Cheche za Fikra" tuandikie mhariri@klhnews.com


M. M.


Title: KLH News Episode: Exclusive: Dr. Slaa azungumzia yaliyojiri Mbeya Vijijini


/entry/2009-01-06T19_48_52-08_00Enjoy!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Nge nge nge ngeeeeeeeeeeeeee Sikia kengele kumekucha.Kilicho nishtua na kunisikitisha hapa ni USHIRIKIANO WA UPINZANI UNEKUFA TANGU ENZI ZA TARIME. Langu Jicho.

    ReplyDelete
  2. He! Mbowe vipi hapo pembeni ya jicho, mbona kuna mkwaruzo alianguka au alipata dhoruba gani?

    ReplyDelete
  3. The leaders of CHADEMA lacks the vision of bringing change to Tanzanians by being selfish and arrogant. Most Tanzanians need change rather than partisan politics practiced by CHADEMA leadership with other opposition parties. Dr Slaa has came up with the dumbness argument not to support CUF which inturn shows his arrogance.
    How would you bring CCM down while you can't accept the fact that CHADEMA screwed up in the process.
    Learn from US. The Clinton's supported Obama after loosing in the preliminaries . This helped Obama win US presidency.

    ReplyDelete
  4. Leo ni mara yangu ya mwisho kumsikiliza Slaa au kiongozi yeyote wa CHADEMA. Sitaki kusema amesema nini nyie nendeni wenyewe kwa mwanakijiji mkamsikilize. Halafu mtindo wa kuchanganya kiswahili na kiingereza hata kwa maneno ambayo yana tafsiri ya kiswahili unanichefua sana.
    Mwisho, ni swali kwa wewe mwanakijiji, najua unaweza usijibu hapa kwa kulinda maslai ya chama. Nilikuwa najua CHADEMA hawajui sheria, kumbe hata kuhesabu hawajui pia? Ni kivipi tutawaamini na kuwapa nchi? Ulipomuuliza ni mambo gani wamejifunza alitaja moja halfu tatu. Nimerudia mara kumi sehemu hiyo na sijaona kama uliikata. Kwa hiyo CHADEMA wakiingia madarakani tutakuwa tunahesabu moja,tatu,nne, tano,sita....
    KWA KWELI KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI NA CUF

    ReplyDelete
  5. madau wa tatu englishi iz not richabo andika kiswahili mimi sijaelewa kitu chochote.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...