Leo nilipokuwa nasafiri kuelekea jiji kubwa la Tokyo niliona kitu ambacho nikafikir kama huko nyumbani wakiiga basi kinaweza kupunguza maafa ya terrorism .
Kama unaweza kukumbuka maafa makubwa yalitokea huko Spain wakati bomu liliwekwa kwenye dustbin na kuleta mauaji kwa watu wasiukusudiwa . Baada ya kuona hivyo nchi mbali mbali zimechukuwa taadhari kukabiliana na majanga kama haya mfano mzuri ni hapa ninapoishi Japan , Train stations zoote waliamua kwa pamoja kutotumia black pastic bags kwa ajili ya kuhifadhi taka taka.
mifuko hiyo kwa sasa ni transparent na mtu ukiwa nje unaweza kuona nini kimo ndani , hapo mwanzoni dustbins ilikuwa full covered... ila kwa sasa imetobolewa tundu kubwa na unaweza kuona nini kilichomo .
Kila baada ya nusu saa taka taka huondolewa na pia kuna patrol of plain clothes guards kila baada ya muda fulani kucheck kuna nini ndani .
Mchango wangu ni huu lakini inaweza kuokoa maisha ya wengi kama viongozi wetu wanaweza kutilia maanani .
Kidumu
Mdau Japan!
...Hayo mawazo ya mdau wa Japan yanawezakana ila ni lazima wabongo nao wawe wastaarabu kwa kuangalia vizuri wenzetu wanatofautisha takataka ...yaani glasi,mbao , vitu vinavyochomeka kwa moto na vitu ambavyo havichomeki . hii itawezekana kama sheria itapitishwa mapema kuwa watu watenganishe takataka zao naweza kusema kuwa kufanya hivi tutajenga hulka kwa kizazi cha baadye nao kuendelea na ustaarabu huu .
ReplyDeleteKidumu ...
Nadhani mdau aliyetoa hili wazo ameruka step moja muhimu... kwanza angetoa wazo kuwa hiyo mifuko myeusi tuletewe sisi ili kuhifandhi hizo taka mana sio kila sehem kuna dust bins.
ReplyDeleteterrorrism Tanzania? tuna ugomvi na nani? au huo ushauri upeleke US embasy ya TZ
Anonyomous wa 12.45 .... hivi kuchukua hatua za kujihadhari ni lazima uwe na ugomvi na nchi fulani .... maafa kama haya yanaweza kutokea sehemu yeyote bila taarifa ... yale mauaji ya American Embassy pale kwenye Corner ya kinondoni ...sisi wabongo tuna ugomvi wowote na waarabu ... hizi ni hatua muhimu za kuchukua
ReplyDelete...hiyo step ya kuletewa mifuko myeusi tayari imeshapitwa na wakati.. wewe unataka kuturudisha nyuma tena na imani yako potofu namuunga mkono mdau huyo wa japan
ReplyDeleteNamuunga mkono mdau January 03, 2009 12:54 PM, Ukweli ni kwamba sisi hata hizo dust bin zenye mifuko myeusi hatuna, sasa iweje leo hii tutamani mifuko myeupe ambayo hatuwezi kuimudu wakati hata myeusi imetushinda?. Ni Bora wewe mdau wa Japan ukaikusanya hiyo myeusi wanayoitupa uitume Bongo kama msaada kwa nchi yako. Jiji la DSM chafu na umesikia juzi tu JK kawakoromea Halmashauri sasa huu ni muda muafaka wa wewe kuleta hiyo mifuko myeusi wanayo i-skip.
ReplyDeleteNakubaliana na anony wa jan 3 12:54. Tanzania hakuna ugaidi hata huyo aliyesema ubalozi wa Marekani kidplomasia ile ni ardhi yao hatujawahi kuwa na tukio la ugaidi nchi mwetu. Tuna mabo mengi mno ya maana ya kufanya kusu usafi kabla ya kurukia vitu kama mapipa special. Kwanza lazima watz waelewe maana ya usafi na mali pakutupa taka. Unaweza ukaweka yayo mapipa yakawa mapambo tu taka zinatupwa sentimeta chache kutokea pipa lilipo.
ReplyDeleteLakini kitu kingine mfuko wa pipa transparent je bomu likiwa kwenye mfuko non transparent au mfuko wa nguo hiyo transparent bag inasaidia nini? Hebu uliyeleta mada hii tueleweshe hapo.
mdau amesema hivi "niliona kitu ambacho nikafikir kama huko nyumbani wakiiga basi kinaweza kupunguza maafa ya terrorism" suali langu ni tanzania kumetokea maafa mangapi ya terrorism kiasi cha kuwa mdau anasema hivi?
ReplyDeletenaamini hawajaweka mifuko hiyo sababu ya kuona kilichotupwa, sasa kama nachukua bomu na nazungushia karatasi nyeupe kisha natupa ndani wataona ni nini kipo ndani ya hiyo karatasi?
ReplyDeleteJamani wadau mie naomba kuelezwa Bongo Train statitions zipo wapi? Reli ya kati? Tuanze kwa kusafisha jiji la Dar kwanza ni chafu sana.
ReplyDeleteMDAU kataka na yeye aonekane katuma mada jamani hapo siajabu mwenyewe ana kazi ya kuirudiarudia kila mara kuisoma hadi comments zake zote.Na je nyie watanzania mnaokiri kabisa kwamba wabongo sie usafi sio ngoma zetu sasa nyie tuwataitaje sie wabongo wenzenu wengine ambao usafi tunaufagilia????maana wakiwaita watu wasio wabongo nyie wachafu mtangàka na kuja juu kama mbogo waliojeruhiwa vile,tuambieni sie tuwaitaje nyie mlijikubali kabisa kama ni wachafu
ReplyDeleteMaafa ya Terrorism? Mmmh kaka sie tunajaribu kupambana na maafa ya njaa, magonjwa na ukame wa mvua.
ReplyDeleteNaona umekuwa brainwashed na siasa za magharibi.
LOL!! makubwa haya. Sasa hizo dustbin ziwekwe wapi? Subway?
ReplyDeleteMie mdau wa Japan ningependa pia kuchangia machache zaidi baada ya kuona kuwa wadau wenzagu wamechangia mada hii . Mtoa mada wa kwanza labda angeelimisha jamii hayo mapipa siyo taka taka zoote zinatupwa humo ukiangalia vizuri kuanzia kushoto ni vitu vikubwa , magazetti , vitu vya round shape bins , cans , glass and aluminium materials should be separated with different bins .
ReplyDeleteMfumo huu ni vyema wakaweka sehemu zenye mkusanyiko mkubwa watu mfano Bus Stands za kwenda mikoani , Ferry Stations i.e kwenda Zenji ,Mtwara ,Mafia etc na Airports vile vile .
Kumbuka kuwa hizi ni sehemu muhimu zaidi ukichukulia kama Airport ikilipuliwa pale maafa makubwa yatatokea kiuchumi pia .Idadi ya watalii itashuka kwa kiwango kikubwa ikizingatiwa kuwa pato kubwa la taifa linatokana na utalii ukiachilia mapato ya ndani .Sasa kwa nini tusichukue tahadhari kubwa wakati ni kitu ambacho kinawezekana . Mimi nimekuwa msafiri katika airport nyingi tu ..kuna airports zingine ukishuka tu unaambiwa uvue kofia , kama una sun glasses unaambiwa utoe pia hapo ni kabla hata hujafika kwenye Migration Point . Kumbuka kuwa wenzetu wanachukua tahadhari kubwa zaidi kabla maafa makubwa kutokea na pia tusisahau kuwa KINGA ni BORA KULIKO TIBA >>>>>
Wadau tuachane na sily jokes kuwa tuweke haya mapipa kwenye Subways coz..hii ni kuonyesha jinsi gani tulivyo primitives katika kutoa michango/mawazo yetu kwa jamii.
Cheers !
Mimi ni mdau wa Tokyo. Haya sio mapipa ya kuzuia mabomu. Mapipa kama hayo yapo huko Israel kwa kuwa wapalestina wanatumia mabomu mitaani kwao. Kama mdau wa 10:34 anavyosema, ni kwa ajili ya Ku-recycle takataka kama magazeti, chupa za vigae na za plastiki na za bati na kadhalika.
ReplyDeleteWauzaji wa magazeti wanabeba magazeti walioniuzia kila mwezi ili wa recycle wanapokuja kudai fedha zao nyumbani. Na wafanyabiashara wengi wanapokea mali zao za zamani kutoka kwa wateja ili wa recycle kama friji, komputa, gari na mashine ya kufulia nguo. Siruhusiwi kutupa kitu chochote bila ya kupeleka dampu ya serikali ambapo nalipa ada kutupa kitu chochote kikubwa maka mkeka au viti.
Tanzania kama wadau wanavyosema haitasaidia kuleta mapipa haya kama watu hawatabadilisha tabia za uchafu na serikali haitafungua makampuni ya ku recycle bidhaa kama chupa baada ya utumizi. Sisi hapa tunalipa dola 5 kununua mifuko kumi ya takataka, tunatupa taka kwa mara mbili tu kwa wiki, na kuna siku maalumu za kutupa chupa, magazeti na plastiki na bati ili wa recycle. Wananchi hapa hawatupi taka nje ya pipa kabisa na Japani inajulikana duniani kote kama ni nchi safi sana. Cha umuhimu hapa ni kuwa kama hamna viwanja vya ku-recycle Tanzania, haya mapipa au mabegi meusi ya plastiki hayatasaidia. Kuna faida gani ya kuweka mapipa kama hatugawanyi takataka tunazoweza ku recycle na takataka za kuchoma moto au kufukia? Wenzetu hapa wana recycle asililia 75% ya takataka kabla ya kutupa taka yoyote.