makao makuu ya tanesco ubungo,k dar

Naomba mtusaidie kudadisi hao jamaa na kupata jibu juu ya huduma muhimu ya umeme katika maeneo ya kwetu (SEGEREA ,KINYEREZI NK. )kwingine sina taarifa zao.


kwani kwa kipindi kisichopungua majuma mawili umeme umekuwa ukikatika kila siku kwa muda usiopungua masaa manne mfululizo .


Kama ni mgao si waseme tujue kabisa maana si jambo la ajabu kwa wabongo la sivyo tatizo ni nini?nina wasiwasi hata jana tukashindwa kushuhudia tukio muhimu la kihistoria la kuapishwa kwa mh Obama, mweusi wa kwanza ndani ya white house ...Sijui itaitwa black house

Mdau wa myblog yako

J.MBWAMBO(Baba Jordan)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Sehemu ya jengo la tanesco kubwaaaaaa! sasa sijui humo wamepangisha office zengine au wao tu? Jengo kubwa hakuna kinachoendelea sijui wanafanyakazi gani humo ndani Ufisadi mtupu kutuharibia vitu vyetu vya umeme mnatuumizaaaaaaaaaaaaa. Ndosi.

    ReplyDelete
  2. Ni sababu kubwa ya kuondoka Bongo. Kuna wasomi wengi tu Bongo sasa, lakini hamna mtu anaweza kutatua matatizo yoyote. Tangu nilipoondoka miaka 20 hivi mpaka leo, sijaona maendeleo yoyote, na kama yapo naomba nikosolewe: majo machafu, dawa hamna, wizi serikalini, barabara mbovu, elimu duni, hamna usalama katika kona nyingi za nchi, ujambazi, haki za binadamu haziheshimiwi, sheria inaendeshwa na serikali sio majaji wa mahakama na kadhalika.

    Tunaambiwa sana hapa sijui turudi nyumbani kuendeleza maendeleo. sasa nyinyi wasomi huko mbona hatuoni mnaendeleza maendeleo yoyote? Nilikuja kuangalia hali ya kazi, naambiwa elimu yangu ya biashara ya marekani (MBA, UCLA) ina thamani ya dola mia tano tu. Tusichuzane hapa, Bongo haina kitu mbele. Wenzetu miaka 20 wanatengeneza magari yao wenyewe, akina Malaysia, Korea Kusini na kadhalika.

    Mwisho, Kabla ya wachovu kufungua midomo yao, nimeondoka kihalali na bado natesa na pasi zote mbili.

    ReplyDelete
  3. WEWE OBAMA ANAKUHUSU NINI? UTUMWA TU

    ReplyDelete
  4. obama sio mweusi,,,ana rangi-rangi (chotara)so aitwa mchanganyiko, mkewe ndo mweusi.
    kwanini wamwite mweusi?wazungu wana lugha "chafu" sana juu yetu sijui tuliwafanya nini jamani!!!
    afu awataki kutamka HUSSEIN hahahaaaa lilitamkwa pale alipokua anaapa basi,yule MC na wengineo ata kidogo!!!tamka jina la mtu kikamilifu na kwa roho nyeupe if manelomango poa tu
    "muslim world itawezekana kweli?"nao wanaakili na wanaona

    ReplyDelete
  5. Ndosi wafanyakazi ndani ya jengo ni zaidi ya 700 na jengo halitoshi.. tehe tehe ! bitter pill but swallow it !!!
    na ili usiharibiwe vitu vyako vya umeme ni shurti uviwekee protection na fundi umeme utakayemchagua kukufungia awe certified usichague wa mtaani....ngoja nisiendelee sana...

    ReplyDelete
  6. Nji yoyote makini haifanyi mzaha hata kidogo na swala nyeti la ENERGY.... UMEME, MAJI MAFUTA yaani bidhaa za petroli.... Hapa kwetu jambo hili ni jepese kwa serikali yetu na hamna anayelitazama kwa makini. TANESCO ni moja ya mashirika nyeti sana hapa njini ila kama Ndosi anavyoshangaa.... huko ni wizi mtupu Hmna lolote... wamejaa humo wababaishaji na mafisadi watupu!! Tanesco na Muwasa mpo!! Moshi ndio vinara!! wizi mtupu!!

    ReplyDelete
  7. Nji yoyote makini haifanyi mzaha hata kidogo na swala nyeti la ENERGY.... UMEME, MAJI MAFUTA yaani bidhaa za petroli.... Hapa kwetu jambo hili ni jepese kwa serikali yetu na hamna anayelitazama kwa makini. TANESCO ni moja ya mashirika nyeti sana hapa njini ila kama Ndosi anavyoshangaa.... huko ni wizi mtupu Hmna lolote... wamejaa humo wababaishaji na mafisadi watupu!! Tanesco na Muwasa mpo!! Moshi ndio vinara!! wizi mtupu!!

    ReplyDelete
  8. We anon wa pili hapo juu unayejisifia kwa kuwa mtumwa wa hiari mbona unashangaza , unadhani kukimbia tatizo ndio dawa ya kutatua tatizo? sasa wote wangekuwa na mawazo kama yako kungekuwa na Tanzania au hata Afrika? Au unadhani kwamba tayari umeshakuwa mzungu? na hata kama umekuwa raia wa huko uliko basi ni wa daraja la chini ( Unanikumbusha wimbo wa CHAKUBANGA wa Marehemu MARIJANI RAJBU )
    Tunakubali kwamba tuna matatizo ila lazima tuelewe kwamba ni sisi wenyewe ndio wenye jukumu la kuyatatua ili siku moja tufikie hali kama hiyo inayokuzuzua wewe huko uliko au unafikiri hiyo hali uliyoikuta huko imeshuka tu toka mbinguni? soma historia yao wazee wao hawakuyakimbia matatizo badala yake walikomaa nao ndio wakafanikiwe, ACHA MAWAZO YA KITUMWA MSOMI MZIMA

    ReplyDelete
  9. Nimepitia kwenye website ya TANESCO,, ukisoma vision na mission yao utalia... NAOMBA WABADILISHE au wawe wanasoma na kuifanyia kazi(VITENDO)

    VISION OF THE COMPANY

    To be an efficient and commercially focused utility supporting the development of Tanzania.

    MISSION STATEMENT

    To generate, transmit and supply electricity in the most effective, competitive and sustainable manner possible.

    IMPORTANT VALUES

    * Ethical business conduct.
    * Respect.
    * Integrity.
    * Service excellence.
    * Stakeholder Opinions.
    * Environmentally responsible.

    To realise the vision and mission, TANESCO business imperatives are to :

    * Ensure financial viability through revenue improvement and reduction of energy losses.
    * Increase customer satisfaction by putting in place processes that meet customer care needs.
    * Employee satisfaction through competitive employment package and good working environment.
    * Support the National Energy Policy through appropriate company policies.
    * Accelerate the pace of electrification for economic growth.
    * To increase generation capacity so as to avoid load shedding.

    ReplyDelete
  10. Anony 8:29, kukaa nje kwangu sio maana ya kuwa nina mawazo ya kiutumwa. Hamna uraia wa daraja la chini haoa, acha wifu wa kike. Nataka sana kuja nyumbani kuishi lakini sioni faida yoyote. Sina muda wa kukusubiri wewe msomi ulete maendeleo. kama mpaka leo hamna maji masafi wala umeme, unafikiri maendeleo yatakuja katika uhao wako au wangu (tunaishi zaidi hapa)? Naomba unipe muda gani, ili niweze kuanza kujitayarisha nirudi nyumbani. Mimi sitaki zaidi ya elimu bora ya watoto,maji safi, umeme, usalama, na haki yangu kama binadamu itaheshimika.

    kwa taarifa yako, naishi maisha bora sana hapa, mwaka jana kampuni yangu imefanya biashara ya dola milioni nne. Kazi kwako.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...