Toka kwa


Pichani ni mrembo Miss Brazil, Mariana Bridi (20) ambaye amefariki dunia leo asubuhi huko Brazili baada ya kuugua ugonjwa wa bacteria usio na tiba.

Hivi karibuni alikatwa sehemu ya tumbo na mikono na miguu yake kusudi bacteria usisambae zaidi mwilini mwake. Jitihada za kumwoka hazikufanikiwa.

Awali madkatari walidhani ana ugonjwa kwenye njia ya kupitisha mkojo. Bridi aliwahi kushiriki katika mashindano ya urembo wa Miss World. Alikuwa mmoja wa warembo watano bora.
Mungu ailaze roho yake mahala pema mbinguni.
Amen.

Kwa habari zaidi someni:
http://timworstall.typepad.com/timwor
stall/2009/01/mariana-bridi-da-costa.html

http://www.thesun.co.uk/sol/
homepage/news/article2160372.ece

http://www.theaustralian.news.com.au
/story/0,25197,24960178-12377,00.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Vipi ndugu yangu? Huyo mrembo amefariki karibu siku tatu zilizopita na si leo kama ulivyomnukuu dada yetu Chemponda.Vipi mambo lakini?Wanasemaje lango la jiji.Karibu tena Pumbu Dr. hapa Kinshasa.

    ReplyDelete
  2. Huyu mbona kafariki toka tarehe 23 Jan 2009 baada ya kufanyiwa operation ya kukatwa miguu na mikono yote kufail.

    ReplyDelete
  3. Mungu amlaze mahali anapostahiki pia hali hiyo itatowa elimu hapa kwetu kutokana na dhana tulizonazo na kama ingekuwa hapa BONGO basi hakuna shaka watu wangeweza kusema ni uchawi tuwacheni haya mambo ya kuamini uchawi kuwa ndiomaendeleo au kinga ya maradhi

    ReplyDelete
  4. ivi wanadamu tuna nini cha kujivuna??yani leo uko mzima kesho ndo kama uyo dada eti ugonjwa wa bacteria usiopona!!why walimfanyia operesheni ilhali walijua hauponi?wamemtia mwezao maumivu ya bure tu,ata ivo yan kwa urembo woote huo angeweza kweli kuishi no miguu,no mikono,tumbo limekatwa
    aisee Mungu atuhurumie

    ReplyDelete
  5. Dr. Remmy alisema kifo ni kiboko yao. Kifo hajali wewe ni mzuri,mrembo,Waziri,Rais. Demu alikuwa mzuri kinoma lakini mbele ya kifo alikuwa sawa na taahira fulani.Rest in peace

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...