Bwana Michuzi salama?
pole na hongera kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuelimisha na kuhabarisha jamii.
Naomba msaada wako kaka yangu. Mimi ni kijana ambaye sijawahi kukutana na mzazi wangu wa kiume yaani baba mzazi. I dont know what happened between him and my mother but I know I have a father somewhere in this world. Nimebahatika kuwa na jina na anwani ya mahali alipokuwa akiishi wakati wako na mama .
Mr. Abraham Lyimoaliishi Morogoro maeneo ya Kilakala miaka ya 1970s.
Please kama kuna amjuaye huyu baba anijulishe kupitia blog yako kaka yangu.
Mdau DS.
Naomba msaada wako kaka yangu. Mimi ni kijana ambaye sijawahi kukutana na mzazi wangu wa kiume yaani baba mzazi. I dont know what happened between him and my mother but I know I have a father somewhere in this world. Nimebahatika kuwa na jina na anwani ya mahali alipokuwa akiishi wakati wako na mama .
Mr. Abraham Lyimoaliishi Morogoro maeneo ya Kilakala miaka ya 1970s.
Please kama kuna amjuaye huyu baba anijulishe kupitia blog yako kaka yangu.
Mdau DS.
Hawa ndio watu wa kusaidiwa ISsa Michuzi siku nyengine Comment zak ina Stella tunaomba waambie watafute Blog ya mambo hayo kama mtu anamjuwa mzazi wa huyu jamaa msaidieni labda anataka kumjuwa tu baba yake sio kwa kumuaribia na familia yake amjue akubali ajue ilikuwaje? yameisha. mungu atawasaidia wote wawili. James
ReplyDeletesina nia mbaya lkn nakushauri achana nae kwani kukuzaa sio tija tumeletwa duniani hapa ili tuzaliane kuwa baba kama hajakulea hamna point na kama kuna mjomba au baba mlezi mfanye huyo ndio baba yako,najua nitapingwa na wengi lkn hio ndio REALITY.kwangu mimi
ReplyDeleteAnon wa pili 9.19 umenena point ya msingi sana. Kama umelelewa na watu mpaka una umri mkubwa namna hiyo na hujawahi kukutana wala kumfahamu baba yako, haina haja kumtafuta sasa. Kama angekupenda ukiwa mdogo angekutafuta na kujenga mahusiano ya kifamilia kama baba. Kitendo cha kuwa mama yako (kama yupo hai) hajakupa taarifa mpaka leo hii ni dalili kwamba si muafaka kwako kumtafuta baba yako. Usije kuumia moyo wako pasipo sababu. Kuwa na imani. Waliokulea ndio wazazi wako. Ridhika na ulichonacho. Onyesha shukrani kwa watu waliohangaikia maisha yako hadi leo. Ondoa presha ya kutaka kumuona mtu ambaye hakuyajali maisha yako kwa muda wote huo.
ReplyDeleteBlessings.
Michuzi kuna comments unabania za kumsaidia huyu bwana....Kuna comment nimeweka hapa kuwa huyo bwana Abraham Lyimo nilikwisha fanya naye kazi, ingawa anaweza asiwe baba wa huyu jamaa lakini naona michuzi kaminya....Una nia kweli ya kumsaidia huyu bwana au?
ReplyDeleteRafiki nakushauri weka contacts zako hapa ili watu tukutafute kukusaidia, maana naona naye Mheshimiwa Muhidini naye kawa Senene
Huyo baba namfahamu sana. Ana good time na kwa sasa anaishi maeneo ya Chamwino pale Morogoro.
ReplyDeleteANON wa 11:52PM wewe unapajuwa chamwino tu basi sio zaidi ya hapo????Na kweli upo serious si ungesema hapo muwasiliane na kutoa details zako atakupata vipi.........
ReplyDeleteAnyway sijuwi inakuwaje mtu azae na mwenziwe na asimjali mtoto na kupotea moja kwa moja, ama anawezekana upatikanaji wa mototo ulikuwa wa matata matata, yaani pengine baba huwa aafaki kuwa mtoto ni wake, pengine alikuwa ana wasiwasi kuwa kuna mwenzie alikuwepo pembeni, na jingine ni kuwa baba anaweza kuwa ameshaoa na kuona kuwa na mtoto wa nje pengine mama wa ndani ataleta longolongo ndo anaona aingie mitini, au wakati mwingine wanaweza kugombana na mama akakasirika na kumwambia kama anataka aende zake na wala hana haja msaada wake atalea mtoto pekee yake, na kweli baba akaanza mbele moja kwa moja. Mimi binafsi nilikuwa na dada yangu alizaa na bwana mmoja wakati huo nasoma na dada yangu ndo amemaliza la saba tu na bwana huyu alikuja huko kwetu kuanza kazi na wala hakuoa,alipoondoka na kuhamia Dar basi alitupa jongoo na mti wake, mimi bahati nzuri nilisoma vizuri tu na kupata kibarua kizuri tu nikawa na msaidia dada kusomesha huyo mtoto, baadaye nikahamia Dar,nilimuona jamaa lakini mimi sikutaka kujitambulisha kwake siku zikapita, mara mtoto wa dada alipokuwa mkubwa na kesha maliza sekondary alikuja kunitembela Dar,katika maongezi aliniomba nimpeleke kwa baba yake akamtambue,nikasema sawa mara tu tulipofika kwa jamaa ofisini, si alitutoa nje ya ofisi kuongea naye si ndani ya ofisi na huku sura yake ikionekana ya aibu,woga na wasiwasi sana na si ya uraha, kwa vile mimi ni mtu mzima na elimu yangu nikajuwa hahutaka mtoti aende kujitambulisha au kumtafuta, mimi nikasogea pembeni nikawaacha wanaongea, mara wakaagani akaja kwangu tukaondoka, from there on hawakuonana tena hadi leo. mimi nikahisi alikuwa hataki watun pale ofisiwajuwe kuwea ana mtoti wa pembeni na pengine asingependa mkewe ajuwe, na kwa vile pia pale palikuwa na offisiyake binafs ya biashara zake na kulikuwa na wanawake kibao inawezekana mmoja wao alikuwa ni kewe wa sasa wa arusi. Mimi kwa huyu bwana namshauri afanya utafiti kwanza kabla ya kuonana naye ajuwe kama baba angependa ajitumbulishe kwake akipata jibu yes then anaweza kusonga mbele, akisema no basi aachane nae. kwani kumzaa si hoja.
ReplyDeleteAnon wa pili na wa tatu, uhusiano wa mzazi na mwana hauishii kwenye fedha tuu. Kama kuna tatizo lilitokea si kosa la mtoto ni la wazazi kama akina .......
ReplyDeleteMtu kakosa malezi ya baba, basi hata mapenzi ya ukubwani? Damu nzito kuliko maji.
Angalau hata ajue ukoo wake na watoto wa baba huyo maana ni ndugu zake.
Msijidai wazungu, sisi watanzania.
Sikubaliani na Anon mnaosema hakuna haja ya kumtafuta baba. Hilo ni jambo linaloweza kukusumbua maisha yako yote na linahitaji jibu. Inawezekana nia isiwe kuwa na relationship yoyote kubwa lakini ni kujua kwamba unatokea wapi and you want to know your other fanily. Pia kuna maswali yanahitaji majibu mfano kwanini mzee hakuwapo katika maisha yake, nk. Utaona mtu kama Obama hata kama baba yake hakuwapo lakini atajitahidi kutafuta familia yake na kuwa na mahusiano. Kujua historia yako ni kitu muhimu sana na usipojua unaweza kutokuwa na raha katika maisha yako. Wat wengine wanatumia madawa, ulevi nk. Kwahiyo saa nyingine ni hatua muhimu to find closure
ReplyDeleteNapinga kwa nguvu zote wote wanaosema hakuna haja ya kumtafuta baba. May be mama ndio alikuwa sababu ya mtoto kutomuona baba yake. Na wote wanaosema hakuna haja ya kumjua baba naweza kusema hawajawahi kuwa katika hali kama iliyomkuta ndugu yetu. Baba ni muhimu sana, watu wote wasio na baba wanaweza kunielewa. Anony wa 03:51 ana busara sana kwa ujumbe wake!
ReplyDeleteNyie mnaosema asimtafute,mnasema hivyo kwa sababu hampo kwenye position yake. Mara nyingi mtoto akikua atataka kumtafuta baba yake kwani huwezi jua huyo mtoto ameathirika kiasi gani. Hata kama baba ni jambazi au hata kama baba hakutaki,mtoto unakuwa na maswali kibao yamekuzunguka kichwani na unakuwa hu move on mpaka umuone mzazi wako.
ReplyDeleteKila jambo na wakati wake, kama huyu kijana ameamua baada ya takriban zaidi ya miaka 30 kumjua baba yake ni jambo zuri na asaidiwe. Hakuna ajuaye ni sababu gani zilipelekea wazazi watengane. Na chuki uliyoundwa hapo ilikuwa na sumu kali kiasi, mpaka wazazi wasiamue kuzungumiza matunzo ya mtoto. Lazima tujifunze kusameheana na kupendana, na ni muhimu kusahau yaliyopita. Wewe unayesema kama ulilelewa na mjomba au baba mdogo, basi huyo ndo baba yako, EBOOO, NANI KASEMA BABA MDOGO AU BABA WA KAMBO NI BABA? Tumsaidieni mwenzetu na tusimletee CHENGU.
ReplyDeletewasalaam, makuna pa kudengu
JAmani wanaosema hana haja kutafuta baba ni kosa.
ReplyDelete1. Mtafutaji anapotafuta baba si kwamba anamtafuta kwa pesa sizani muda mwengine unatakak ujuwa ilikuwaje baba akutaka mawasiliano je ni kweli baba yako au kama kweli kwanini kakuweka pembeni au pengine hataki yote anataka tu akutane na baba yake. Jamaa afurahi na nafsi yake.
2. Jamaa pengine ana watoto anataka awaoneshe wajukuu zake itamfuraisha jamaa na nafsi yake.
3. Kama alivyosema mmoja malezi sio baba tu ni yoyote atayeweza kukulea kwani hata mwenyezimungu kasema kama huwezi kumlea mwanao mtafute mtu amlee mwanao ila usimtenge mwanao. Jamaa anakila haki ya kumjuwa baba yake hata kama hatotaka tena kuhusiana naye ila amjue tu.
4. Kama mzee umeona hii stori nakushauri kama hutaki huyu mtoto uhusiane naye sababu ya kifamilia mtafute sehemu mkutane muongee mmalizane huko. Mungu atakusaidia kama kweli Baba yako akukubali mkae kwa amani. Kama sio Mungu pia atakusaidia uishi vizuri tu uwatizame wanao kama huna mtoto atakusaidia mungu kama hutopata yote uwezo wa mwenyezimungu. Si mganga wala si stella ahaahah.
Oya si kila mtu anamtafuta Baba yake sababu ya Pesa.
ReplyDeleteKijana mmoja alikuwa anaishi Marekani mama yake alitembea Nje na Mzee wa Kihindi akamzaa huyo mtoto ila hakutakak uhusiana na huyo mama tena wala mtoto sababu ya familia yake.
Kijana alikuwa akilelewa na Mama yake mkubwa mpaka anakuwa alijuwa Mama yake mkubwa ndio Mama mzazi kutokana na Mama yake alikuwa Hajatulia katika maswala ya kutumia madawa.
KIjana alivyofikisha Miaka 18 alikuwa na kazi alivyopata mshahara wake wa kwanza akataka kumpa huyo Mama yake mkubwa, Mama yake mkubwa alimwambia Kijana mpe Mama yako mzazi ushakuwa Akamuweka chini kumwambia mama yake ni Flani Kijana akasema kama Mama yangu ni flani nashukuru ni mama yangu ila wewe ndio Mama yangu ninayekujuwa je Baba yangu ni nani?
Akamfata mama yake wa kweli akamwambia yote akarudi Tanzania kumtafuta Baba yake alikuwa Tajiri na Maduka makubwa yule kijana kufika kule kwenye Duka akamkuta yule mzee ni muhindi jamaa kachanganya alivyomwambia tu Babu wa Kihindi akaenda kujificha na kumvuta pembeni Kijana utaniharibia. Yule Babu akakubali kama ni mwanae akaongea naye kumueleza hataki familia yake ivunjike Kijana akamwambia sijaja kuharibu familia yako ndomana nimekufata pembeni na wala sijaja kwajili ya pesa zako nimetaka kukujuwa basi wakamalizana bila familia ya babu kujuwa Dogo kaondoka kwenye Moja yule kijana alisema Moyo ulifurahi japo hata kama hatomuona tena baba yake ila tu kapata kumuona katikam aisha yake. Plz michuzi weka watu wasome na jamaa pengine huyo mzee atafanya hivyo.
Huyu bwana ana haki na ni jambo la busara sana kumfahamu baba yake na ndugu zake. mojawapo ya faida nyingi ni kuepusha shari. inaweza kutokea akakutana na binti wakapendana na kuamua kufunga ndoa na kwenda kuchumbia akakuta aliyepaswa kuwa baba mkwe ndiye baba!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteni lazima umjue mzazi wako kabisa,siku mtaoana ndugu wa damu.
ReplyDeletejamani acheni zinaa ndo mana mnazaa watoto hamuwajui,au nyie mnaokataa watoto mshindwe.
Jehovah atusaidie
mimi pia nakubaliana na waliosema asimtafute huyo baba maana haina haja. ikiwa mama hakuwahi kumwambia baba yake yuko wapi na sababu za kutomuona mpaka kawa mtu mzima, achana naye. nina mifano miwili ya watoto ambao walitafuta baba zao wakati wameshakua watu wazima.
ReplyDelete1. kuna mwanamziki maarufu, sitamtaja jina, alimkataa mwanae wa kiume ambaye alienda kwake wakati kushamaliza form iv, nia haikua kupewa pesa wala msaada wowote, ilikua ni afahamiane na baba yake tu. alipofika kwake, alimkuta baba ana mke tayari, na mke hakuwahi hujua kua mumewe ana mtoto wa nje maana alimkataa tangu akiwa tumboni. mtoto alijitambulisha kwa mke wa baba kua yeye ni mwanae, na kwa sura zilivyofanana wala huna cha kubisha. mke akaingia ndani kumwita mumewe lakini kukawa na mzozo huko ndani ambao mtoto aliusikia. baba alipotoka baada ya muda, alimtukana yule mtoto mitusi, kua anamvunjia nyumba yake na yote aliyoweza kusema kwa yule kijana na kukataa kua yeye sio baba yake, kijana akaomba msamaha na kuondoka. hamuwezi kuamini huyo baba nadhani ana zaidi ya miaka 15 na mkewe lakini hawajajaliwa mtoto. sasa arudije kule kwa aliyemkataa..? hivyo kijana endelea na maisha yako, baba ndio alipaswa kukutafuta, sio wewe. mfano mwingine nitawapa siku nyingine, karibu ufanane na huu.
inahuzinisha sana,,,ni kama obama-obama vile then mtoto awa rais wa dunia then mnaanza kujipendekeza (watani wa jadi)
ReplyDeletemtoto hana kosa,nyie ngojeni siku.wakati mnakula good time na mama yake hukujua hutumii zana na pills au?
kaaazi kweli kweli