Marehemu Mohamed Abddul Shakur aka Captain PAMA
Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Italy unasikitika kutangaza kifo cha Ndugu MOHAMED ABDUL SHAKUR (PAMA) kilichotokea jana asubuhi katika hospitali ya SAN GIOVANNI DI DIO E RUGGI D'ARAGONA" SALERNO.
Kutakuwa na Mkutano wa Watanzania wote leo jioni saa kumi na moja 17:00 pm.
Sehemu: LAGO PATRIA MABEMBEANI.
TAFADHALI TUZINGATIE WAKATI NA KUFIKA BILA KUKOSA.
Mwenyekiti wa jumuiya ya Watanzania Italy,kwa niaba ya uongozi na watanzania wote hapa Italy,anapenda kutoa salam za rambirambi kwa wazazi na ndugu wa marehemu nyumbani na popote walipo, kuwa tumepokea taarifa hizi kwa masikitiko makubwa na tunaungana nanyi katika wakati huu mgumu wa maombolezo.

Mungu ailaze roho yake mahala pema .
Amin.
Abdulrahaman A.Alli.
Mwenyekiti
*****************************************************************

WA WALE WOTE WALIO NJE YA ITALY KWA MAWASILIANO TUPIGIGIE SIMU NAMBA:
+39 3271753565(Mwenyekiti)
AU
+39 3453118431 (DULLAH)
au
+39 331 8360509 (Katibu mkuu)
au
+081 3340635 (ofisi ya jumuiya)
HABARI ZAIDI: http://www.tnzncommunity.blogspot.com

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Poleni sana ndugu zetu wa italy kwa msiba mzito wa Mpendwa wetu PAMA,namjua mshikaji vizuri sana tulikuwa nae kinondoni mkwajuni,na pia Brother wake anaitwa STIBA mshikaji wangu wa karibu mno
    MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEN
    Mdau kutoka UK

    ReplyDelete
  2. mungu amsamehe makosa yake amjalie makazi mema na poleni ndugu na jamaa wote wa karibu lkn duh jamaa ameturushia ngumi sana bila sababu za msingi ama kweli kila chenye mwanzo kina mwisho wake lkn natumaini waliopigwa ngumi na huyu kaka watamsamehe wote na kumtakia makazi mema. Amina!!

    ReplyDelete
  3. duuu si mchezo, yaani kila mara tunasikia italy mtz mmoja anafariki kunani huko, duu PAMA amefariki, hakuna mtu asiemjua PAMA ambaye anatokea tanga, tanga nzima jamaa wanajulikana PAMA STIBA NA MKUSA. MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALA PEMA PEPONI AMEN

    ReplyDelete
  4. Poleni sana kwa msiba mzito ndugu na jamaa,cpt PAMA ni kama mdogo wangu na si kweli kama jamaa hapo juu kuwa anapiga bila sababu,kwa kujitetea ndio kama kila mtu duniani,Mungu ailaze roho yake pema Amin.mdau andrew neri

    ReplyDelete
  5. Mungu ailaze roho ya marehemu wetu peponi Amen! Bwana ametoa na Bwana ametwaa.... Rest in peace brother PAMA

    ReplyDelete
  6. KAKA PAMA NAIANGALIA PICHA YAKO KWA HUZUNI. UMETULEA MIMI NA AKINA ABDALAH SHAKUR. TWASHUKURU NA HATUNA LA KUKULIPA LEO HII SISI NDIGUZO ILA KUKUOMBEA DUA MUNGU AKUPELEKE PEPONI.AMEEN.
    MDAU NA NDUGU WA KARIBU SANA WA MAREHEM. UK..DAH ALHAMDULILAH.

    ReplyDelete
  7. innalillah wainnailaih rajiuun. sote tuko njiani. mdau andrew namtafuta nduguyo R, je nitampataje?
    Mdau finland

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...