Home
Unlabelled
muonekano mpya wa forodhani, zenji
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Safi sana. Inapendeza namna hii na naamini patatunzwa maana hilo ndio lililo gumu. Si kujenga, si kupendezesha bali kupaweka pawe kama palivyokusudiwa. Inapendeza sana na asante mdau kwa taswira mwanana
ReplyDeletePanavutia. Ila je, mimi mlalahoi niliokuwa nauza urojo hapo kabla ukarabati haujaanza ntapata nafasi?, au watapata kina nanihii tu?(wanajijua)
ReplyDeleteDuh, pamependeza sana hapo forodhani. cant wait kupaona. ila watu wasianze kuleta uchafu wao kutupatupa ovyo na kukanyaga majani halafu ikawa kazi bure.
ReplyDeleteTatizo la huku kwetu hata tukitengenezewa vitu tambarare lazima tuvisambaratishe. Haichelewi hiyo bustani mara utaona chupa za maji, mifuko ya rambo, vifuu na takataka lukuki za masalia ya vyakula!! usishangae kugeuzwa kijiwe cha wavuta bangi, vibaka nk!! Yetu macho! Ila nawasifu Zenj kukataa kuwekewa Baa kwenye makazi ya watu!! HONGERENI YAKHEEEEE!
ReplyDeleteoo yees - haya ndio mambo...e bwana pametoka pina kisawa. ambaye hajawahi fika hapa aende for the w/end
ReplyDeleteYangu mengine lakini yanafanana na haya. Hapa Dar kuna Bustani nzuuri yaitwa Botanic Garden, iko mkabala na Karimjee Hall na nyuma ya Southern sun Hotel, zamani ikiitwa Holiday Inn. Bustani hiyo kwasasa imevamiwa na wanafunzi wa IFM, eti wakijidai kujisomea, cha kusikitisha pamoja na matangazo ya kuchimba mkwara watu wasichafue mazingira katika bustani hiyo, wanafunzi hao wamekuwa wakichafua mazingira saana kwa makaratasi na chupa tupu za maji, kiasi cha kwamba bustani imepoteza TASWIRA. Mamlaka ichukue hatua kuzuia hili. Nawakilisha.
ReplyDeletekama wananchi ni wakorofi bassi tutumie staili ya mwanza maana huko baadhi ya bustani zinalindwa na kutunzwa masaa 24 kwa hiyo siku zote ni safi na zinapendeza. kwa hiyo dawa ni kuweka walinzi
ReplyDeleteCha Muhimu hizi bustani lazima ziwekewe wasafishaji, kila asubuhi wasafishe, pia liwekwe tangazo kwa herufi kubwa kabisa "KUNYA_BUSTANINI_HAIRUHUSIWI"
ReplyDeletemkuu nimependa taswira ya foro naomba kama unazo picha zaidi tuwekee tafadhali
ReplyDeleteIwe mfano kwa nchi nzima. Imependeza saaaaaaana
ReplyDeletehiyo bustani ni nzuri sana. wananchi tuwe wastaarabu tusitupe taka hapo. panatakiwa pia kuwe na vitu vya kutupia takataka. wekeni matangazo kueleza watu wasitupe takataka hapo. pongezi kwa waliotengeneza hiyo bustani.
ReplyDeleteanyway tanzania we have a long way to go.. havent seen anything fantastic.. then again HAYA NI MAWAZO YANGU NA NAOMBA YAHESHIMIWE
ReplyDeleteBustani inahitaji maji, mimea kumwagiliwa ili iwe imenawiri. Matumizi ya mboji na kuwe na kamashine kakunyolea ukoka (mower) sio kufyeka kwa makwanja.
ReplyDeleteMiti (shrubs, bushes and trees) inahitaji kupunguzwa (trimming)
uwekaji bustani nayo ni fani, sio ajira kwa itikadi ya chama au Manispaa kutoa tenda kifisadi