Majibu kuhusu post moja nimeona hapo kwako Bro Michu jamaa wanakata miti katika barabara ya Ocean (Ocean road).
Sijajua sababu lakini ukiwauliza wanaweza kukuambia ni kupisha mradi aidha wa upanuzi wa barabara ama sababu nyingine.
Nimekutumia hii post na hizo picha wadau waone tofauti nyingine kati ya nchi zilizoendelea na zinazoendelea.

Jamaa wana magari maalum kwa ajili ya kuhamisha miti mikubwa endapo itahitajika kutoka mahali ilipo na kwenda kupandikizwa sehemu nyingine.
Sababu zinaweza kuwa ni kama hizi za kwetu tu.. kupisha eneo kwa ajili ya mradi ama sababu nyingine kama hizo.

Kazi kwenu Wadau...
Mdau,
Gongo la mboto Mzarambarauni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Mdau umewa-provoke vizuri hawa wenzetu walioshikilia mpini Tanzania.

    Lakini kwa mtizamo wangu, wenzetu wanakosa vision kutokana na kuvimbiwa madaraka - kwa maneno mengine hata wakihaibu hawapati criticism usoni.

    Ukijaribu kuangalia miji yetu inavyoendeshwa ni worse kuliko miaka 20 iliyopita.

    Bw Charles Keenja aliwahi kuibadilisha vizuri Dar Es Salaam kunako miaka ya 90 kutokana na vision aliyokuwa nayo.

    Siku hizi jiji linaongozwa na watu wenye maneno mengi lakini hawajui wanachotakiwa kufanya.Inasikitisha sana, lakini ndiyo Tanzania ya kisasa hiyo.

    ReplyDelete
  2. Dah! A subject guys or call it a period

    ReplyDelete
  3. Aina hii ya project hata mimi niliiona mitaa ya mzambarauni nikiwa kwenye daladala kuelekea Gezaulole.
    Mdau, Kibaha picha ya ndege.

    ReplyDelete
  4. Tanzania sijui kama tutafika kwa kweli. Juzi JK anazungumzia panda miti na kuweka mandhali ya Dar vizuri. Leo miti inakatwa! miti hiii ilipandwa miaka na miaka, hivi tutaendelea sisi. basi kwa nini tusiiamishe tu kama wenzetu! Badala ya kuikata. kama kwa ajili ya kupanua barabara basi ihamishwe the same kama kwa kuweka parking lot! Hivi watanzania jamani hawaoni nchi nyingine au ndio hivyo tena kichwa cha mkichaa ni kichwa cha mkichaa tu. Naungana na wengine kuwa Tanzania ilikuwa bora miaka 20 kuliko sasa. Sasa hivi serikali imejaa Wezi, na kama sio wezi basi hawana point yeyote. Acha wengine tujilipue tuwaachie BOngo yenu kama Bongo ndio hiyo.

    ReplyDelete
  5. Kuhamisha miti ni wazo zuru lakini miti hiyo kuendelea kukua tena chances ni ndogo sana kwani kuna miti yenye mizizi mirefu sana.

    Dawa ni kata mti mmoja (1) otesha / panda kumi (10), baada ya miaka kadhaa angalau 50% ya miti hiyo itakuwa imeshamiri tena.

    JK - Toronto

    ReplyDelete
  6. Hii ya kuhamisha haijaniingia akilini na hiki kiangazi chetu huyo mmwagiliaji mwenyewe ni nani hivi utaweza kuungòa mu40 temeke uje kuupandikiza sinza kweli?labda maua hayo unaweza kuyahimisha kwenye bustani ukayapandia ndani.HAPA TUNAZUNGUMZIA MITI SIO MAUA MAANAKE KUNA MAUA YANAREFUKA KAMA MITI LKN YANA MIZIZI MICHACHE SISI TUNATAKA MITI SIO MAUA.IT SOUNDS LIKE U CAN KILL A HUMANBEING AND MAKE HIM LIVE AGAIN IN ANOTHER PLACE.. LOL

    ReplyDelete
  7. Chambilecho wahenga "akili ni nywele kila mtu ana zake".

    ReplyDelete
  8. Nyie wengine mnaongea tu hajui chochote. Yes miti inawezwa kupandwa sehemu nyingine na ikawa mikubwa na kuhamishiwa sehemu nyingine. Tembeeni muone au kama hamuwezi kutembea basi at least someni mlichokuwa nacho muone. Sio maua tu hata miti. Nchi za baridi na nchi za majangwa kuna kitu kinaitwa green house miti inapandwa humo for years iwe mi 40 au miti ya aina nyingine baadae inahamishwa na kupandwa sehemu nyingine, na vile vile kama sehemu inatakiwa kuwekwa kitu kingine miti huamishwa, Tanzania bado hatujafikia huko basi badala ya kubisha angalau tujifunze hiyo miti inahamishwa vipi. Na kubaliana na msemaji hapo juu tatizo kwa Tanzania ni utunzaji. mti ukishwa hamishwa utahitaji maji 24 hr na matengenezo mengine ili mizizi iweze kushika shini. Maji ya kunywa watu hatuna tutapata ya kumwagilia miti kweli? Kwahiyo hilo ndio tatizo kubwa linalotukabili.

    ReplyDelete
  9. Kuhamisha miti ni wazo endelevu,Tanzania inao uwezo wa kunua japo mashine kama hizi 10,na zitatosha.
    eg.Raisi Jk,alipoingia aliagiza BMW mpya kama 7 hivi,wakati kuna Ma Benz kibao left behind by Mkapa!!!
    so we can afford it.swala ni jinsi ya kuishinikiza serikali kupanga na kuweka matumizi yake bayana-online ili tuweze kutoa maaoini etc.
    Michuzi bado hatuna jibu la Kukata miti ikulu,tueleze or sidia kupata jibu

    Mdau
    aka Mkereketwa na umasikini wa taifa

    ReplyDelete
  10. tutafika tu
    me ni mfano wa kuigwa,,karibuni kwangu pia ata ushauri

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...