E bwana mheshimiwa mkuu wa wilaya ya nanihii mbona Stars ikichapwa huwa hautupi habari zilizovunjika? We uwe unatujulisha tuu maana kufungwa ni sehemu ya mchezo. Au umeshakua mzee wa sisi mbili wao bila?
``Kwa ufupi ni wale mapirates`` (Wasomali) leo wametufunga moja bila! ni hayo tuu.
Mdau wa Sao Paulo
HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Maximo nae anakuwa kama Arsene Wenger...kushinda pale msipotarajia na kufungwa pale mnapokuwa na uhakika kabisa wa ushindi!Naamini kwa kiwango cha hivi karibuni cha Stars,sie ni bora zaid ya hao "pirates" wa Somalia (kumkuu mdau aliyeposti news hizi).

    ReplyDelete
  2. Mdau wa Sao Paulo, tunashukuru kwa taarifa hiyo ya kuvunjika. Ila napenda kukusahihisha, timu iliyofungwa sio Taifa Stars, bali ni Kilimanjaro Stars (Timu ya Bara), maana unaposema Taifa Stars fahamu unazungumzia timu ya Tanzania, na si ya Bara.

    Japo wachezaji wengi sana wa Kilimanjaro Stars kuwa ndio hao hao wa Taifa Stars, haina maana maana timu hiyo kuitwa Taifa Stars.Hiyo ni sawaswa na Barcelona ya miaka ile ambayo ambayo first eleven ilikua na wachezaji kama nane hivi waholanzi, enzi za akina Overmars, Zenden, Kulvert, Davids, Debore etc, na kocha wao akawa ni Mholanzi pia, haikumaanisha Barcelona ilikua timu ya Taifa ya Uholanzi, tusichanganye hapo wandugu.

    Maana kufungwa au kushinda kwa Kilimanjaro Stars hakuna athari ktk rekodi za FIFA, sema kimazoezi na maandalizi ya kwenda kuwafunga Ivory Coast na Senegeal.

    Poa
    MDAU

    ReplyDelete
  3. Brother Michuzi; tunaitegemea blog yako sana from latest breaking news from Home; good example is NAM championship we did not get any info from you; now Challange Cup Stars (kilimanjaro) lost I had to go through New Vision to follow up the game -- NO TZ newspapers has posted the loss as of yet... it is painful... we bank on your blog to give what is missing from our poor service tz newspapers online --- we still appreciate you

    YOUR BLOG FOLLOWER IN US

    ReplyDelete
  4. Anko michuzi iliyofungwa ni timu ya Taifa Tanzania Bara(Kilimanjaro stars) na siyo Taifa stars,ingawa Kili stars imesheheni wachezaji wa Taifa stars.Bado najiuliza kwa nini Maximo(Coach) anafundisha Kilimanjaro stars??Kwa nini hii timu asipewe local coach,yeye Maximo afundishe tu wachezaji wa Taifa stars(Bara na visiwani),sioni logic, kwa sababu Taifa Stars coach=Maximo OK,lakini Taifa stars bila wachezaji wa Zanzibar=Kilimanjaro stars.Sasa hapa maximo anaingiaje?,anyway sifahamu mkataba wake.

    ReplyDelete
  5. Anko michuzi iliyofungwa ni timu ya Taifa Tanzania Bara(Kilimanjaro stars) na siyo Taifa stars,ingawa Kili stars imesheheni wachezaji wa Taifa stars.Bado najiuliza kwa nini Maximo(Coach) anafundisha Kilimanjaro stars??Kwa nini hii timu asipewe local coach,yeye Maximo afundishe tu wachezaji wa Taifa stars(Bara na visiwani),sioni logic, kwa sababu Taifa Stars coach=Maximo OK,lakini Taifa stars bila wachezaji wa Zanzibar=Kilimanjaro stars.Sasa hapa maximo anaingiaje?,anyway sifahamu mkataba wake.

    ReplyDelete
  6. HIVI NYIE MNAO MLALAMIKIA MICHUZI KUWA HAWAPI NEWS HARAKAHARAKA KAMA MANAVYOTEGEMEA? MNANISHANGAZA SANA NA SIJUI MNA MAANA GANI. MANAZANIA MICHUZI NI tmz NA ANALIPWA HAPA AU ANA AGENT KILA KONA YA NCHI WA KUMPA NEWS? AU MANAZANIA MAISHA YAKE YAKO BORED KAMA YENU? MICHUZI ANA MKE, WATOTO NA KAZI YAKE SIJUI MNAKUMBUKA HAYO????????

    MUACHENI KAKA WA WATU NA MSHUKURU KWA HATA HICHI MNACHOKIPATA

    SORRY NIMEUSE ALL UPPER CASES SIO KUWA NASHOUT TO ANYBODY BUT I REALLY WANT TO VENT. KUNA WATU HAWANA SHUKURANI KABISA HUMU WENGI TU.BADALA YA KUSHUKURU MNACHOPATA MNAMCONTROL MICHUZI WA WATU.AGRRRRRRR

    ReplyDelete
  7. Matokeo mengine ni kwamba Zanzibar imetoka droo na wenyeji Uganda 0-0,na huku mechi ya kwanza ikiwakandamiza hao hao ma-pirates ya Somalia 2-0,
    teh teh teh

    ReplyDelete
  8. ETI mnadhania michuzi maisha yake yako BORED kama maisha yenu..lol

    ReplyDelete
  9. Wapemba bwana!
    Angalia wanavyoleta ubaguzi wao hapa.... hahahaha mko chini daima mpaka mtakapoacha kujiona waarabu.... hahaha LMAO.....
    ukitaka kuwajua kapose kwao uone sheghuli yake....! bora mitoto yao iolewe na viziwi wa kiarabu kuliko mbara!.....

    ReplyDelete
  10. Jamani waTanzania tujifunze kusoma vitu kwa makini kabla ya kutoa maoni maana kukosa userious ndio kunatufanya tuchemke ktk mambo mengi. Mathalani ktk habari hii Kichwa cha habari kinasema ``Kilimanjaro Stars yalala``sijaona sehemu iliyoandikwa ``Taifa Stars``. Na hata mdau wa Sao Paulo yeye kasema Stars hajasema Taifa stars! Sasa watu bila kusoma kwa makini wanaanza Ubarcelona wao! hii kasumba ya uzungu itaisha lini? Tuwe makini ndugu zangu.

    ReplyDelete
  11. Sasa ni wakati wa Mwanakijiji kuongea.

    ReplyDelete
  12. Kisiju naingia.
    kwanza kabisa mdau wa juu Barcelona haina Uholanzi iko Spain.
    kuhusu Maximo nilisema sana last week kuwa sio kocha ni TEKNISHENI TU NA MUHAMASISHAJI TU.mwaka jana kwenye chalenji wasomali hawa tuliwafunga kwa msaada wa refa. timu iliyocheza ina wachezaji wote wa stars isipokuwa Haroub Canavalo.hatuna kocha acheni kutetea ujinga na kesho tunatoka draw ya ZNZ au kufungwa.
    Maximo sio kocha hilo ndiyo jibu.acheni ushabiki wa kijinga.

    ReplyDelete
  13. timu kufungwa na Somalia ni aibu kubwa. Somalia yenyewe haina serekali,haikua na maandalizi hata ya siku tatu. kabla ya mechi hii imecheza mechi mbili in two years.ukikompea na timu yetu ina wachezaji ambao kila timu ikitwa asilimia 95 wanakueko.sasa mnatetea ninini?ama tufuate kauli ya mgema ukimsifia tembo hulitia maji ndio maximo!!KACHEMSHA

    ReplyDelete
  14. Mdau Kisiju..unajitokeza timu inapofungwa..wala huongei kisayansi zaidi ya kuendekeza ushabiki wa mitaani...katika soka linatokea lolote lile tena wakati wowote ule..inawezekana wachezaji baada ya kucheza mechi ngumu sana dhidi ya Sydan, Uganda na Kenya , wameanza kuchoka..Kisiju kuna kitu kinaitwa Fatigue..yaani ni uchovu mkubwa wanaokuwanao wachezaji wetu baada ya kucheza mechi nyingi na ngumu ndani ya muda mfupi.

    Michuano hii ya chellenge ni michuano ya ukanda huu..kwa maneno mengine haina ubora kama ile ya CAN na CHAN..Ndio maana BBC walisema Tanzania has qualified for major tournaments after 28 years..hawakusema kuwa Challenge Cup ni mashindano makubwa!!!..ndio maana hata zenji wamepeleka timu ya wachezaji wenye miaka 23..wakongwe ni Abdi Kassim na Cannavaro...watanzania ukiwemo Kisiju tumezoea kuishi kwa mazoea ndio maana mpaka leo hii challenge cup tunaiona ya maana sana..siwezi kumtukana wala kumdhalilisha maximo eti kwa sababu tumefungwa na somalia..tuliwahi kuwafunga Burkina Faso na Sudan wakiwa kwao..Kisiju hukuzungumza lolote!!..unasubiri timu ifungwe ndio uongee..mawazo yale yale ya wanachama wa simba na yanga..akili zile zile za kuwapangia makocha timu ya kucheza uwanjani!!..kwa sababu maximo ana msimamo na hasikilizi upuuzi wa wale wanaojiita wadau basi kisiju umeamua kumchukia!!?..usimba na uyanga upeleke huko huko kwenye vilabu vyenu visivyokuwa hata na viwanja vya kufanya mazoezi!!...Tangu aje maximo tumeshinda mechi 13 tumefungwa mechi 7..ni mechi moja tu dhidi ya Senegal ambayo tulifungwa zaidi ya magoli 3..ukumbuke kuwa enzi za makocha wako wa kibongo tulishawahi kufungwa bao 5-0 na kenya tena hapa hapa bongo!!..kisiju mbona hatukukusikia ukimponda kocha..acha kasumba zilizopitwa na wakati..na mpaka leo unasema teknisheni..unaelewa maana ya hilo neno?.
    Patrik Phiri karudi simba na watu watakao pima utendaji wake ni aina yako wewe kisiju..ataweza kweli kutekeleza mipango yake ya muda mrefu?..badilika ndugu yangu achana na huo ushabiki wa kizamani.

    ReplyDelete
  15. Kosa kubwa alilolifanya Maximo ni kuendelea kuwatumia wachezaji wale wale wa taifa stars kwenye hii challenge.

    Miaka ya karibuni challenge imekuwa ikitumiwa kama mashindano ya kuwapa uzoefu wachezaji vijana ndio maana nchi nyingi zinazoshiriki mashindano haya zimekuwa hazileti nyota wao bali zimekuwa zikileta wachezaji wanaochipukia.

    Ungekuwa ni uamuzi sahihi kabisa kama Maximo angeamua kuwapeleka akina Jabir Azizi , Adam Kingwande , Bunu Abdallah na baadhi ya vijana waliong`ara kwenye copa coca cola ya mwaka juzi, wachezaji hao angewaongezea na wachezaji wachache wazoefu kama akina Kelvin Yondani , Shaban Dihile, Jerry Tegete na Kigi Makasi ili aweze kuweka balance kwenye timu.

    Haina maana yoyote ile kutwaa kombe la challenge halafu timu hiyo hiyo ikawa inatolewa kila mara kwenye mashindano ya kutafuta nafasi za kwenda CAN au World Cup.
    Wadau wa soka la bongo akiwemo kisiju wanatakiwa kuelewa kuwa sifa za kijinga kwenye soka zimeshapitwa na wakati.
    Maximo alitakiwa kufanya kama tulivyofanya mwaka juzi kwenye challenge iliyofanyika Ethiopia kwani matunda ya challenge ile ndio hawa akina Tegete na Makasi.
    tunahitaji kama taifa kuwa na nia ya kuwa na wachezaji wengi ambao wanaweza kuchezea timu yetu ya taifa kwa wakati moja yaani muda wowote ule watakapohitajika, na mashindano haya ya challenge ndio nafasi ya dhahabu ya kuandaa kundi kubwa la wachezaji ambao wanaweza kutusaidia kwa muda mrefu.
    Mara ya kwanza tumetwaa challenge mwaka 1974 mara ya pili mwaka 1994, baada ya miaka ishirini kupita, kama sisi kweli tunastahili na ni bora kuweza kutwaa challenge kwanini tusubiri mpaka miaka 20 ipite ndipo tutwae kombe hili?.
    Tuanze kufikiri mbali zaidi ya challenge kwa sababu mashindano haya ni ya ukanda huu pekee, tuanze kuwa na ndoto kubwa ili tuweze kufika mbali, kutwaa challenge na kuanza siasa nyiiiingi za kujisifu kwenye radio na magazetini hakutusaidii katika karne hii, tunatakiwa tuanze kutamani kuwa na wachezaji wenye uwezo wa kuchezea barcelona, madrid , ac milan na timu kubwa kama hizo.
    Hatutaweza kuwa na wachezaji wa kuchezea timu hizo kama ndoto zetu ni zile zile za kutwaa kombe la challenge ambalo ni kombe la ukanda huu pekee.
    Kisiju jiulize kama Tunisia , Nigeria , Cameroon wakiamua na wao kushiriki challenge, je kuna timu ya ukanda huu itakayoweza kulibeba kombe?.

    ReplyDelete
  16. kisiju una mjombaako nae anausikilizia ukocha wa stars nini?nakuona kama unaempigia mtu chapuo vile aje kumriplsesi maximo

    ReplyDelete
  17. Ndugu yangu Kisiju pamoja na wadau wengi wa soka la bongo..tuna ugonjwa wa kujiona sisi sio watu wa mafanikio..ndani ya vichwa vyetu kila siku tunajenga taswira ya mtu wa kushindwa tu, tunajiona sisi ni losers na sio winners!!!

    Kisiju alisema kuwa timu ya Zanzibar itashinda au itatoa droo na kilimanjaro boys..matokeo yamekuwa kinyume na matarajio yake..na sababu kubwa ni ile ile hali ya unyonge inayotutesa wabongo weengi sana..kabla hatujacheza na Cameroon baadhi ya wadau waliamini kabisa eti tutafungwa mabao matano hapa hapa kwetu..lakini tuliwapeleka puta akina Eto`o na tukapata droo..bado wadau hawa wakaamini eti tutakwenda kupigwa goli kumi kule Yaounde , lakini tukafungwa 2-1 tena dakika kumi za mwisho!!.

    Tufike wakati wabongo tuachane kabisa na hii hali ya unyonge kama aliyonayo bwana Kisiju ..na tuanze kujiona sisi pia tunaweza tena sana tu.

    Pia wabongo tupunguze hii aina fulani ya ujuaji ambayo inawafanya makocha weengi washindwa kufundisha hizi timu zetu kwa muda mrefu..tunawaleta makocha wa viwango vya juu sana halafu tunaanza eti kuwapangia wachezaji wa kucheza uwanjani!!..kama tuna utaalamu kuliko hawa makocha waliosomea kazi yao , kwanini tusiombe kazi ya kuzifundisha hizi timu zetu kama tunajiamini tunaujua mpira?..simba ilimleta aliyekuwa kocha msaidizi wa timu ya taifa ya Bulgaria halafu hawa wahuni wa mjini wakasema eti hajui kufundisha!!!..amewafundisha akina Berbatov atashindwa kuwafundisha akina Henry Joseph!!?..sasa hivi kaletwa Patrik Phiri kocha anayeheshimiwa sana Zambia..lakini kuna wapuuzi fulani watasema eti na yeye hafai!!..makocha wataalamu wanakuwa hawafai wakija bongo tu, mbona wakienda kwingineko wanafanya mambo makubwa?...alikuwepo Trott Moloto kocha wa zamani wa timu ya taifa ya afrika ya kusini nae aliambiwa eti hafai!!..hao wanaodai kuwa makocha wote hawa hawafai hawajui lolote kuhusiana na soka na ndio hawa wanaosema eti Mximo hafai..fikra zile zile za kwenye vilabu vyao wanazihamishia kwenye timu ya taifa..tuwaepuke sana watu wa namna hii kama na sisi tunataka kupata maendeleo ya kweli ya soka.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...