Habari uncle Michu,

natumai umzima wa afya na wadau wengine wote wa blog hii ya jamii. Kheri ya mwaka mpya kwenu wote. Napenda kushare na waTz wenzangu kote ulimwenguni hii habari kwa picha yenye kusisimua niliyoipata katika gazeti moja hapa Odessa ikionesha taswira ya mfano wa wajihi wa kibinadamu hasa sehemu za MACHO pia na pua kwa mbali katika ukanda wa anga!


Tukio hili la kihalisia (natural phenomenon) lilitengeneza taswira hiyo angani kutokana na muunnganiko wa mawingu ya mvua na thunder storm “mmweko wa radi” (samahani kama nitakuwa nimekosea Kiswahili fasaha) Taswira hii ilinaswa magharibi mwa Ukraine wakati wa kiangazi uliopita ambapo kulikuwa na mvua kubwa na radi zilizosababisha mafuriko yasiyo ya kawaida nchini humu.

Hayo maandishi chini ya picha husika ni ya kirusi yanayotafsirika ifuatavyo kwa kiingereza:

«The eyes in the sky» or «The Eyes of God» - a natural phenomenon that has occurred in western Ukraine last summer, during a thunder storm, the day before famous floods.

Mdau Meddy,

Odessa UA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Scary.......... u never know who is watching when u think no one is watching.......its time to pray... LOL..

    ReplyDelete
  2. Hakika huyo ndiye aliyeahidi kuwa Atakuja tena...lakini kwanini aanzie kule Ukraine? Tusali jamani.

    ReplyDelete
  3. photoshop inafanya kazi.

    ReplyDelete
  4. GOD IS WATCHING YOU.

    ReplyDelete
  5. Mdau hapo juu si photoshop hiyo!Ulimwengu umekwisha, kuna kila dalili, kwanza tu tuaangalie na mabadiliko ya sio ya kawaida ya hali ya hewa, another good example ni mwaka jana Antarctic kuyeyuka barafu isivyo kawaida cause of global warming haya leo tena twaona vitu vya ajabu mawinguni mbona hatari, tutubuni jamani lol!

    ReplyDelete
  6. whaaaaaaaat??
    hey yu acheni izo zenu "tom &jerry"

    ReplyDelete
  7. wewew ngozi vichwa vp moscow wanachinja balaaaaaaa kaaaa makiniiiiiiiiiiiiiiiiiiii

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...