TIMU YA TAIFA YA BARA KILIMANJARO STARS IMEFUNGWA bao 2-1 na UGANDA CRANES LAKINI IMEWEZA KUTINGA NUSU FAINALI YA KOMBE LA CHALENJI IKIWA KAMA MSHINDI WA PILI TOKA KUNDI A.
HADI MAPUMZIKO VIJANA WA MAXIMO WALIKUWA WAMESHAPIGWA 2-0 NA GOLO LA KUFUTIA MACHOZI WALIPATA DAKIKA CHACHE BAADA YA MUDA WA MAPUMZIKO KWA NJIA YA TUTA.
KILI STARS SASA ITAKUMBANA NA WATANI WA JADI (KENYA) KWENYE NUSU FAINALI YA KWANZA ITAYOCHEZWA SAA SITA UNUSU MCHANA UWANJA WA NAKIVUBO, KAMPALA.
UGANDA WATACHEZA NA BURUNDI KATIKA NUSU FAINALI INGINE BAADA YA MECHI YA KILI STARS NA HARAMBEE STARS.


sasa wamekuwa wa maximo nyinyi machongo hamna maana mmeanza kumgawiya na kuwagawa mkishinda matusi kibao kama utazani mnauwezaa
ReplyDeleteHayo matokeo hayabadiliki tu? hata hivyo tunasonga mbele.
ReplyDeletewakifungwa vijana wa maximoo wakishinda vijana wetu au siooooo. Eeee ndo maana yakeeeee
ReplyDeleteHAKUNA CHA KUHOFIA WATANZANIA... HATA TUKICHAPWA BAO 10, TUMESHAFUZU... KWANI RWANDA (WALIOSHINDA LEO) WANA POINTI 6 TU, KAMA TANZANIA...NA KINACHOANGALIWA KWANZA NI HEAD-TO-HEAD (TANZANIA vs RWANDA)..KWA BAHATI NZURI TUMEWACHAPA RWANDA, KWA HIYO TANZANIA OYEEE...TUSIPOSHINDA LEO, TUTAKUTANA NA KENYA NUSU-FAINALI, WAKATI UGANDA vs BURUNDI...
ReplyDeleteMichuzi uwe na speed ya kuupdate hizi habari ambazo ni matukio yanayokuwa yanaendelea kwa wakati huo."RTD" inayoutangaza TZ haina website,CECAFA hawana website!!!!Ngoma imeisha zamani tangu 1800hrs E.A.T lakini bado umekomaa na hayo matokeo wakati ngoma imeisha na tumelala 2-1 lakini tumesonga mbele.Hongera kili stars lakini inabidi mkomae hasa manake uwezekano wa kukutana na Uganda tena Finals=90%
ReplyDeleteHuu upuuzi mkumbuke kuna Fifa Rankings huangaliwa pia kwa hiyo tunapofungwa hivi na nafasi yetu ya kupata timu ulaya kama UK inakuwa finyu maana hawasajili mchezaji kama nchi anayotokea iko chini ya nafasi ya 70
ReplyDeleteRafael Barnitez meneja wa Liverpool FC, ktk mikutano ya kawaida ya mameneja wa timu za premier league na waandishi wa habari siku ya ijumaa kuamkia mechi za ligi jumamosi na jumapili amemshutumu vikali meneja Sir Alex Ferguson wa ManUtd.
ReplyDeleteRafael Barnitez alisema Sir Alex ana tabia ya kuwatisha marefarii na viongozi wa chama cha mpira cha Uingereza FA.
Alitoa mfano mastaa wa ManUtd wakikabwa sana pale Old Trafford,wakati wa mapumziko humzonga kamisaa wa mchezo pamoja na marefa wake. Pia Sir Alex huwa anaipa presha chama cha mpira FA kupanga mechi ktk mtiririko unaoinufaisha ManUtd. Mara zote Sir Alex husema hayo waziwazi na huwa hapigwi faini kama mameneja wengine.
Rafael Barnitez alitoa ujumbe kwa Scolari asiyumbishwe kwa ugeni wa ligi ya Uingereza na mbinu za Sir Alex na awaambie vijana wake wa Chelsea kufanya kweli kati mechi hiyo na ManUtd hapo Old Trafford siku ya Jumapili.
Pia Rafael Barnitez alipinga vikali maneneo ya Sir Alex kuwa Liverpool Fc hawawezi kuhimili kupata mchecheto wa kufukuziwa na ManUtd na Chelsea, hivyo Liverpool wataishiwa na pumzi na kukosa ubingwa wa premier League mwaka huu.
kisiju natinga.
ReplyDeleteKwanza hongera kwa moja ya timu yetu kupata tiketi ya kuendelea.
Pili na kurudia Mdau wa TFF na Maximo.Kaka huyo mkenya anaetuburuza kwenye ligi yetu kwa kufunga magoli mengi alifundishwa tangia udogoni ama alipitia shule ndogondogo za soka huko kenya? mjomba ni upuuzi unaongea kwamba mchezaji lazima afunzwe tangia utotoni kufunga ama kupasiana.!! George Weah alifunzwa na nani? je akina Romario, Edmundo,Ronaldo, hawa ni wachezaji waliokua na vipaji na ambao waliokotwa barabarani mpaka wakawa masupa star. Tabia hiyo hapa hamna. Mchezaji kuchezea timu yeyote lazima awe na konection. la sivyo hata awe na kipaji gani hakitambuliki.
Mjomba hujui kwamba kocha wa timu yeyote ya nchi ilioendelea kisoka lazima atoe analisis ya mechi ilivyo kua baada ya mechi Either kwenye National Chanel or kama ni klabu basi kwenye Club Chanel? Hili hua somo kwa mdau wowote wa soka kuelewa kiegezo cha kwa nini timu imefungwaau kushinda. Maximo ana jukumu si kwangu tu ila kwa taifa maana sisi ndio tunaemlipa. kwa hiyo tuna haki ya kujua progress inavyokua.
Sasa nashangaa kuona mdau unafagilia usiri huu ambao hatu uelewi. Yaani makocha wote hawa tuliokua nao hapa nchini ni kocha mmjoa tu ndie aliopelekwa kusoma nje ya nchi. kaka huu ni msiba. swala la ufungaji kuna kitu kinaitwa coordination ambacho ndio ufunguo wa mfungaji yeyote mzuri duniani. Na hili mchezi halipati mitaani kaka ila kwa mwalimu aliebobea si Maximo maana limemshinda. Haiwezekani mtu anajaribu kupiga mpira golini mwili wote uko nje ya mpira hatoweza funga hata kama hamna kipa. Ni jambo la kusikitisha kua mwalimu halioni kwenye mechi wala mazoezini na kulirekebisha.
Sasa hilo ni tatizo la nchi kutokua na vipaji? Kama ni hivyo bora raisi alivyositisha kumlipa kocha huyu na kukimbilia kwenye fani nyingine ya michezo. Bora huko atleast tunaweza jisifu duniani kwamba tushawahi shinda medali hadi za zahabu kwenye masumbwi na mbio.Kama tunahamu yakufuatilia soka bora tuangalie watu wenye kulijua maana tunajihangaisha. Huko Ivory Coast itakua aibu Mdau wa TFF na MAximo subiria msiba.
mbona mnafungwafungwa kama yoyo la juu chini???inamaanisha hatuna uzoefu wa maadili ya dunia...bado sisi chipukizi tuu...debe tupu hupiga makelele sana...don't waste our money in Ivory Coast!!!
ReplyDeletenyie watu mnosema tutatia aibu ivory coast kabla hamjazungumza maneno hayo hamfikirii kwanza kufanikiwa tu kuenda huko nihatua amboyo miaka ishirini iliopita ilikuwa ndoto kwetu hata kama itatolewa mapema uzoefu watakao pata huko wewe mwenyewe unae ongea hivo am sure 100% hujacheza socer kama ungecheza japo mchngani usinge ongea uzushi wa kutia aiubu na ule ndo mwanzo wa kuuza wachezaji wetu ulaya am sure baada ya michezo ile kwisha tutasikia japo mmoja au wawili wamepata timu ulaya sio mnakaaa kulaumuu tu hamshukuru kiwango walichofikia japo kinatia moyo kurudisha imani na hapo ulipo wewe unaeongea kuna nchi ngani zinacheza vizuri kuliko starz toka east hazija fanikiwa kwenda huko je hutajisikia safi kuiona ni nchi yako iliyo fanikiwa kuwa huko kabla huja laumu fikiri kwanza tunatoka wapi miaka ya 80 timu yetu ikienda chanlange cup inarudi nyumbani round ya kwanza na hata wanashindwa kufunga goli moja wanatoka na magoli ya kufungwa tu unakumbuka?sasa hivi ni timu mojawapo zinazo ogopewa east africa kwanini inaogopewa jiulize kama hujui inaogopewa soma magazeti ya uganda michezo inapofanyika utajua uzuri na ubaya wa starz sio mnakalia majungu tu palipo na mafanikio hata adui yako mpe haki sawa mmenichefua sana hivi ndo vipande vangu kwa lwo ok
ReplyDeletekisiju kama kawaid
ReplyDeleteMjomba Ivory Coast tunaenda sindikiza. Kuna mdau anadai eti mara ua mwisho mashinda hayo tulishiriki mwaka 1980. Mjomba mbona una chemsha ? Mwaka 1980 mashindano haya yalikua hamna.mwaka huu ni mara ya mwanzo kufanyika.
Funzo hilo kaka. Kama mambo huyajui bora unyamaze tu.