Mwenyekiti wa UWT Taifa Mh. Sofia Simba

Nikiri ya kwamba nimesikitishwa na kushangazwa sana na baadhi ya ukosoaji wa Mhe. Simba kufuatia mahojiano yangu naye siku chache zilizopita. Kilichonisikitisha zaidi ni jinsi gani baadhi yetu tuna angalia vitu ambavyo si vya msingi na kuviacha vya msingi; kilichonishangaza zaidi ni jinsi gani wengine wamekuwa wa kali kiasi cha wao wenyewe kuwa kile wanachomtuhumu Mhe. Simba.. arrogance!

Katika mahojiano yangu na watu mbalimbali (kama Dr. Migiro, Dr. Salim, na wengineo) sijawahi kujaribu kumtetea mtu yeyote kwa majibu yake. Hata hivyo katika hili la Mhe. Simba nimeona kilele cha kebehi na kina cha parapanda ya unafiki wa uongo. Wengi wamemhukumu Mhe. Sofia kwa ukali ambao haukustahili na umeenda zaidi ya ukosoaji wa kumjenga mtu!

Kwa hawa nina ujumbe ufuatao:
Sikiliza!
Title: KLH News Episode: Utetezi wangu wa Sofia Simba

entry/2009-01-15T21_40_42-08_00

Enjoy!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 36 mpaka sasa

  1. Mwanawane acheni kumshambulia mwenyekiti wa UWC (Umoja wa Wanawake CCM)

    ReplyDelete
  2. Mwanakijiji, sidhani kama ulipaswa kujibu ama kutetea. Watu 9 wametoa maoni kwa Michuzi (sijui sehemu nyingine) na imekugusa.

    Vipi kama wangetoa maoni watu alfu?

    Isitoshe, waliotoa maoni walikuwa wanatoa maoni kutokana na kusikiliza 'mahojiano yako na Bi Simba'

    Kama kuna tatizo katika jinsi alivyofanya mahojiano na wewe, lazima ukubali kuna tatizo, sio unatetea tu.

    Na kama ulivyosema, mambo hayana 'uzito' ama 'kina' ama 'yanapwaya' kama ulivyosema.. kwa nini umejibu kwa namna hiyo?

    Jambo sio kukatisha tamaa, wala watu wasiseme ukweli, jambo ni jinsi alivyofanya mahojiano. Period. Wewe kinakuuma nini kuwa katoa mahojiano isivyo?

    Hamna mtu anayenyenyekea uongo ama kupigia magoti unafiki, kwani hata wewe unaonekana umekwama hapo, kubali ukweli, kuwa namna aliyotoa mahojioano sio, kubali hilo mwanakijiji.

    Tena sikiliza tena hayo mahojino, yarudie tena, sikiliza
    Sio unatetea tu.

    Chaupele

    ReplyDelete
  3. Bado Mwanakijiji nashangaa kwa nini hili jambo limekugusa kiasi hichi?

    Kwa nini?

    Wakati we umefanya mahojiano, ukayaweka hadharani watu wasikilize, na kwenye kusikiliza, kila mtu anyaa maoni tofauti, sasa ulitakaje?

    Ulitaka kila mmoja afurahie kilichomo kwenye mahojiano?

    Ama hutaki watu watoe maoni yao kwa uhuru juu walichosikiliza?

    Mbona unanitia mashaka?

    Nilidhani ulipaswa kufurahi kuwa kuna watu wamechukua muda kusikiliza mahojiano, na kuamua kutoa mawazo yao?

    Unadhani watu wenye nia ya kukosoa ama kukatisha tamaa wangepoteza muda na kuanza kusikiliza mahojiano?

    Umuhimu wa kutoa maoni ni kutoa maoni kwa jinsi ulivyoelewa, na kwa uwazi kabisa watu wachache waliosikiliza na kutoa maoni wameguswa na mahojiano yale, ndio maana wakachukua muda kutoa maoni.

    Maoni yalikuwa yako juu ya mahojiano yale tu.

    Kwa mtazamo wako waliotoa maoni ni 'wajinga' kiasi hicho hadi ukaona uchukue muda kutetea?

    Mi nilidhani waliotoa maoni wamekuwa waungwana kufanya hivyo bila woga wa kinafiki wa kusifia kila kitu?

    Mi binafsi Mwanakijiji umenishangaza sana na jinsi ulivyolichukulia suala zima.

    Na kukurahisishia, mi wala si mwanasiasa, wala sikujui hivyo usijedhani kuwa nina chuki na wewe, simjui Bi Simba hivyo usijesema nina chuki na yeye, ila ni mTanzania ambaye anapenda kujua mambo mbali mbali ya nyumbani Tanzania, ndio maana nikachukua muda kusikiliza mahojiano na kutoa maoni kama haki yangu ya msingi.

    Utakapoanza kuogopeshwa na maoni ya kawaida ya watu wachache, basi una tatizo.

    Chaupele

    ReplyDelete
  4. Duuu, waswahili husema ni ajabu na kweli. Sio siri kuwa nilikuwa na imani kubwa kwa mwanakijiji na kujifariji kuwa amekuwa miongoni mwa waandishi wa habari wanaokemea uozo unaofanywa na serikali yetu tukufu lakini nilivyunjika mbavu nilipoona kwamba naye ni mmoja wao baada a kuona anapinga uozo mmoja na kutetea mwingine. Kwa kifupi mwanakijiji, huitaji kuwa "Smart" kugundua kuwa muheshiwa JK amechemsha kwa kumteua huyu mama kuwa mmoja wa mawaziri wake. Sipingi uteuzi wa wanawake bali unapofanyika basi mueshimiwa JK azingatie ni nini mteuliwa atachangia kwenye taifa. Nimeshagongana na muheshimiwa huyu akiwa mgeni rasmi kwenye baadhi ya hafla za kiserikali na kwanza nicheka, then nikamuonea huruma kabla ya kulisikitikia taifa letu tukufu kwa kuwa na viongozi wa kiwango cha chini kama huyu bibie. Tanzania ina wanawake wengi wenye elimu na ufahamu wa matatizo ya kilasiku yanayowakabili watanzania zaidi ya huyu mama. Tumeshaona watu kama marehemu Salome Mbatia (RIP) ambaye alionyesha uwezo mkubwa wa uongozi. Kuna mama Nagu, Monica Mbega nk ambao wana uwezo mkuwa tu. Lakini kwa huyu muheshimiwa, JK amechemsha. Mwanakijiji baadhi yetu tulishakuweka katika daraja la watu wanotetea kero za watanzania wa kawaida. daraja hilo lina watu kama kina Kubenea wa mwanahalisi n.k Utetezi wako kwa muheshimiwa huyu unatia wasiwasi na kutufanya tujiulize kama kweli ni wewe au faranga imefanya kazi. Namalizia kwa kukumbusha kwamba mwenye macho haambiwi ona, hivyo mtazamo wako hautamsafisha huyu mama kutoka kwenye mioyo ya watanzania wanaoathirika na uongozi wake wa kiwango cha chini sana- Ubarikiwe

    ReplyDelete
  5. KAKA MICHUZI naomba sana sana mkubwa wangu uitundike hapa hii habari ya ndege ya kimarekani iliotumbukia mtoni.kwavile mdogoako nipo huku moscow ITV zao zote na clouds fm zao ni kirusi kitupu na mimi hakipandi nisingependa hii habari inipite juu juu hivi hivi nitakuwa nimedhulumiwa.ASANTE SANA

    ReplyDelete
  6. my take:
    Mwanakijiji you dont have to take any stand if you are an ethical journalist representing majority's views, you have asked us to listen to it and we've told you we haven't heard nothing yet !! i actually listened to it after you alleged we didnt get you right, now 9 people commented and 8 said it was arrogance, what you should do or Sofia ( but maybe both of you coz you are also aggrieved ) is either put an umbrella and let shower of criticism flow through your back ; because you cant kick a dead dog ( meaning she is already a chairperson we cant change that no matter how much we will post comments on this blog )
    two: she can learn from the critisism to be a better leader and grow from it to realize her mistakes, if i were simba wa yuda i would have taken option 2
    and if i were you mwanakijiji, i would just advice you that you dont have to drag big names that you have interviewed which didnt negate your reaction... it should actually make you learn a thing or two Asha Rose Migiro whom you interviewed and sofia simba are way too different, Asha Rose is in a different league altogether she is just too big for Simba wa Yuda she can only be compared to the likes of condoleza rice etc, our Simba wa Yuda can be compared to people on her own league...

    ReplyDelete
  7. Nadhani hata wewe mwenyewe Mwanakijiji unahitaji msaada..maana maelezo yako yanakasoro kibao!!!

    ReplyDelete
  8. Nikweli Mwanakijiji kwa bahati mbaya katika jamii yetu kuna mgawanyiko.Kwani kwa baadhi ya watu akitajwa mtu au mahojiano au kauli yeyote kwa mtu kutoa CCM kwa upande ambao sio CCM watu watanza kutoa matusi na kauli ambazo sio muafaka bila kujali ni nini mhusika kakitamka na hali hiyo iko vilele vile kwa viongozi wa CCM na wanachama wa CCM ambao kauli yoyoyote kutoka katika upande mwingine (wapinzani) hata iwe ya manufaa au muhimu uipuuza.Ni madhambi mangapi yaliyoibuliwa na wapinzani Richmound,Buzwagi,EPA,ladar,Bandarin.k lakini viongozi wa CCM baadala ya kuchukulia maswala haya kwa uzito na kuyachulia maamuzi walikua wakitoa kauli za kuponda madai hayo cha kusikitisha baada ya muda baada ya kubanwa wanaanza kukubali ukweli.Mwanakiji umewahoji watu wengi kutoka CCM ambaao wanauchungu na nchi yao na wanajitahidi kutumia taaluma na uwezo wao kuisaidia nchi yetu kuwataja wachache.Dr.Salim,Rose Mingiro,Nape Mnauye,Mama Malecela,Mwakyembe,Ssophia Simba n.k.Kwa upande mwingine Zitto,Dr Slaa,Mrema,Mtikila,Kubenea n.k.Hawa watu mbali na kua wanatoka kambi tofauti wanazungumza au walizungumza mambo ambayo ni muhimu kwa taifa letu kwa hoja zao wale ambao hawakua au hawana hoja wamekua na tabia ya kukata simu au kukataa kuongea na waandishi wa habari Nguvu ya hoja ujibiwa kwa hoja mungu ibariki Tanzania

    ReplyDelete
  9. Viongozi wetu bwana, kijihotuba kidogo tu tena cha lugha ya kiswahili mpaka asome, yaani hakuna vichwa kabisa!!!

    ReplyDelete
  10. Watanzania jamani tuwasifu wasomi wetu na tusipo wafagilia watajifagilia wenyewe kama alivyofanya Mh. Simba. Sasa mnataka aseme uongo kuwa hajasoma? kama mgombea lazime atoe wasifu wake wote ili kumwongezea sifa za kugombea, Yeyote ruksa kujifagilia kama anachosema ni ukweli. Hongera Mh. Sofia tuko nyuma yako na tunaimani na wewe. Kina Mama Hoyeeee!

    ReplyDelete
  11. Mwanakijiji kaka, usipoangalia tutakuweka kwenye list ya kina John Mashaka.

    Naomba nieleze masikitiko yangu makubwa kwa wewe binafsi kutokuwa na hata chembe ya ya ethics za uandishi. Kuwa na media ya kufikisha ujumbe sio ndo utumie unavyotaka. Unaanza kuhutubia kama mwanasiasa, unafikia mahali unatukaripia... we uko timamu kweli?? Utapingaje maoni ya watu??? hivi umejisikiliza kabla hujapost hio kitu?? maoni ni maoni, ndo uhuru wa kujieleza. Wewe ni nani wa kuja kumsemea Mh Simba?? Usiogope kuwa podcast yako imemfanya watu wamseme vibaya kesho utaonekana sio a gud boy kwa wakubwa!!! Grow up.

    Umesema it watu wanaongelea vitu visivyo vya msingi. Una define vipi 'vitu visivyo vya msingi'??? we ni nani wa kutuambia nini ni vya msingi kwetu??? kile ambacho we unaona sio cha msingi mi naona ni cha msingi. Wengi wamekuwa offended na lugha iliotumika na jinsi ilivotumika, jinsi alivojieleza, bila mpangilio na kwa majidai. Tunataka viongozi wanaoamini kuwa binadamu wote ni sawa, wa kutuunganisha na kutufanya tusahau tofauti zetu na kujenga nchi.

    1. Kuchanganya lugha sio sahihi. Usitumie vigezo kuwa mbona wengine wanachanganya. Sio sahihi.
    2. Simba alielezea elimu yake bila kuulizwa. Hebu kumbuka lini uliskia kina Clinton wanaongelea elimu zao?? Kuna mdau kasema hapo juu kuwa vigezo vya kugombea vinatolewaga mwanzoni, hivo anaefikia finali ana timiza vigezo. Kuanza kutuambia alikosoma na jinsi alivokuwa anasema imefanya watu wengi tuone sio sahihi. John Major alikua na elimu gani?
    3. Kubagua watu kwa misingi ya elimu ni ubaguzi kama ulivo wa rangi, kabila au jinsia.

    Napinga sana suala la watu kuona waliosoma ni zaidi. Unajuaje historia ya mtu?? Tafadhali kaka, kama unaona kaonewa, nenda kafanye mahojiano nae tena halafu aweke maelezo sahihi, lkn safari hii apangilie hoja, asiongee kama anapiga story kijiweni. Kha!

    ReplyDelete
  12. Wapeeeee wapeeee eheeee vidonge vyao!
    Wakimeza, wakitema shauri yao!

    ReplyDelete
  13. Wewe unayemtetea Mheshimiwa Simba naona huna point na umechemsha. Umetutukana hadharani kwenye hiyo blog yako una maana gain? Je una hati milki na Sophia Simba? Unaposema angeongea mwanaume maneno hayo tusingesemaje. J eTulisema she is arrogant kwa sababu ni mwanamke? Analyst you are hopeless. Mifano yako yote ni irrelevant na nadhani ulitakiwa hata usitoe hizo hoja zako. Are real a a journalist au ni mbabaishaji tu? Aliposema amesoma Marekani, ni lawyer? Maranda mwizi, Janeth Kahama hana uwezo, na mengine mengi tu. Mimi najiuliza huyu jamaa anayetutukana sisi watazamaji ni nani? Natamani nipate namba yake ya simu nimpigie.
    Mdau

    ReplyDelete
  14. Siku hizi watu wananunuliwa kutumia kalamu zao kuwafagilia watu. Sioni sababu za wewe kuleta ujinga wako huku

    ReplyDelete
  15. NDIO Maranda mwizi na NDIO Janet Kahama hajasoma chuo kikuu, mlitaka atafune maneno kama kawaida ya ujuha wa wabongo, Mwizi umwite "mtu wa dili", asie soma umwite "mjanja", sawasawa SOFIA SIMBA, wape vidonge vyao karne ya 21 hii hakuna KUTAFUNA MANENO TENA NCHI HII. Ndio Mzee MWANAKIJIJI TUNAKUUNGA MKONO WENGI TU KWA KUKEMEA UJUHA, WIVU, MAJUNGU NA ROHO YA KWANINI. TUTAFIKA TU KWA KUITA KOLEO, KOLEO, sio kijiko kikubwa.

    ReplyDelete
  16. Huu ndiyo mjadala sasa! Huyo Anon wa 7:74PM anayetaka namba yangu au kutoa maoni apige (567) 202-0011 na anaweza kuniandikia email vile vile: mwanakijiji@mwanakijiji.com

    Na wengine wanaotaka kutoa maoni yao kuhusu mahojiano na Sofia Simba.. tutakuwa na show siku ya Jumapili saa nane ya mchana EST. Na watumie namba hiyo hiyo hapo juu kupiga tukiwa hewani.

    ReplyDelete
  17. Mimi namtetea tena Sophia Simba, unajua ninachokiona hapa ambacho wengi wanakiona ni tatizo, ni ujasiri wa Mama Sophia Simba kuita ''spade a spade'', naanza kama ifuatavyo,Swali; Sophia Simba amesoma au hakusoma? Jibu; Amesoma. Swali; Amesoma UDSM na Marekani? Jibu; ni kweli. Janeth Kahama ni Mzee au siyo Mzee? Jibu; ni Mzee. Swali; Maranda(mtuhumiwa wa EPA) ni mwizi au sio mwizi? Jibu; Ni mwizi!. Maranda amesoma au hakusoma? jibu; hakusoma! Sophia Simba ana vision yake kuhusu UWT? Jibu; aliieleza kwenye mahojiano. Sasa tatizo liko wapi???
    Narudi kwa Wabongo wenzangu, tuache unafiki, huu unafiki wa kufichaficha mambo ndio maana hata ukimwi unatumaliza! katika kueleza kitu, tunazuunguuka weee, mpaka meaning inapotea. Hata elimu ya ukimwi tunaitoa kwa kuzungukazunguka ili tusionekane arrogant, matokeo yake somo halieleweki vizuri, watu wanaendelea kufa.

    ReplyDelete
  18. Binafsi nawaunga mkona viongozi wanaoweza kumwita mwizi mwizi, mvivu mvivu, mbumbumbu mbumbumbu,fisadi fisadi, hiyo ndio sifa iliyokosekana kwa miaka mingi sana kwa watanzania, Mwalimu tu ndio aliyekua hamumunyi maneno. Ukiangalia hizo sifa zote sio kilema useme anawasimanga. Ni tabia zao au sifa zao ambazo mtu kwa jitihada zake anaweza akaziacha hizo tabia au akaondokana na hiyo sifa kama ni mbaya na inamkera. BIG UP MAMA SIMBA!

    ReplyDelete
  19. Kwanza Mwanakijiji hajaongea ukweli. Anadai kwamba criticism kubwa dhidi ya Simba ni swala la Simba kusema kasoma, au kuchanganya kuchanganya kiingereza na kiswahili.

    Sio kweli, na yeye Mwanakijiji anajua hasemi ukweli.

    Criticisms kubwa dhidi ya Mama Simba ni 1) swala la rushwa na jinsi palivyo na conflict of interest katika yeye kama bosi wa Tukukuru kusimamia uchunguzi dhidi yake. 2)swala la Simba kupigiwa debe na Rais 3) swala la Simba na CCM wenzie (Chiligati, Kikwete, Makamba) kubugia bugia na kupeana madaraka makubwa makubwa mengi kana kwamba hakuna wengine.

    Mwanakijiji hana chembe ya integrity kuyaongelea haya. Kachagua vi weak point dhidi ya Simba ndio anakuja kuvitete tetea hapa, kwa sababu tu kamchunuku, au sijui kapewa interview, ambayo Mama Simba alilia lia kwamba blogs hazijamjadili vizuri. Sasa huyu Mwanakijiji anataka kumsawazishia, kumtetea kwenye ma blogs, yeye kama the grand daddy of Tanzanian political cyberspace, you know, John Mashaka type of jazz.

    Kama alivyosema Waefeso hapo juu, asipoangalia kweli Mwanakijiji nae ata descend into the league of John Mashaka's of the world.

    ReplyDelete
  20. Jamani huyu mama Sophia LION ni ghetto dispite her education.2009 TUTAONA MAAJABU ZAIDI YA MUSSA NA FIRAUNI KWA GETTHO LEADERS KAMA HAWA.michuzi ukibana utaniudhi

    ReplyDelete
  21. You know what mwanakijiji, mimi nafikiri wewe na huyo mama wote ni arrogant.
    Wewe ni mwandishi wa habari, kazi yako ni kupresent habari na kuacha wasikilizaji au wasomaji wakachambua. Ila nashangaa u trying to have it both ways...akha (na mimi nimekasirika kama wewe unavyofoka)
    I know u did this intentionally ili uone reaction itakavyokuwa; the truth is you are crossing your fine line. I am guessing, you can't differentiate between arrogance and stupidity.
    Ukweli ni kwamba, narudia tena huyu mama Simba ni arrogant, simchukii hata kidogo ila I can read btn tell.

    ReplyDelete
  22. Mtu wa kwanza kabisa kumtunuku degree msomi mwenza yeye mwenyewe hakuwa na degree bali alitambulika kutokana na mchango wake wa kielimu au uelevu wake (experience) katika fani husika.
    Dharau za mama Simba kuwa mama Kahama hana kisomo ndio kitu watu wengi wamekishikia bango kuwa she is ignant and arrogant eventhough she is schooled.
    Nimesikiliza mahojiano yote na vilevile kumwandikia email mwanakijiji ili kama kuna uwezekano wanablog wakampelekea in advance maswali kwa ujio wa watu unaowahoji ili watu waweze kuleta maswali yao. Nadhani hili jambo litaepusha mtafaruku uliotokea na vilevile kuwawezesha wanablog kumsahili mhusika ipasavyo.
    Mkude.

    ReplyDelete
  23. Mwanakijiji kwa ujumla hauko sawa kuingilia katika maoni ya watu. Sababu zako za utetezi ni weak sana, kwa mfano utumizi wa English na Kiswahili hau make sense. Yeye Bi Simba ni kiongozi, na kiongozi anatakiwa ajue mahali pa kutumia lugha za kigeni na mahali pasipo kutumia lugha za kigen. Angalia mfano wa viongozi wa ulaya. wengi wao wana jua english na wanaongea lugha hiyo panapoitajika. Kwangu mimi kwa kiongozi ku mix lugha inaonyesha serikali isivyokuwa na nidhamu na uongozi bado unafikira za kitumwa.

    ReplyDelete
  24. MWANAKIJIJI!MWANAKIJIJI! SIJUI WEWE NI MUANDISHI WA HABARI AMA VIPI. LAKINI KAMA NI MWANDISHI WA HABARI THEN A GOOD REPORTER SHOULD KNOW BETTER THAN THIS. HUYO UNAEMTETEA KAONGEA UTUMBO MTUPU, MIMI NI MWANAMKE NA NAWAONEA HURUMA WAKINA MAMA WA CCM WANOMUITA HUYO NI MWENYEKITI WAO. KINGEREZA CHENYEWE HAKIJUI ANABAKI KUBABATIZA TU, WHEN TIME COME WHEN TIME COME! KIONGOZI KAMA UNATAKA KUTETEA WANANCHI NA UNA NIA NJEMA HUCHUKI FORM KUJARIBU. MASILAHI YA WANANCHI SIO YA KUJARIBU. ANASEMA YEYE MSOMI MSOMI GANI BWANA! KUREPORT DARASANI TU SIO USOMI HUO, VITENDO VYAKE VINAONYESHA KABISA KWAMBA KICHWANI KUTUPU AU USWAHILI UMEZIDI! I WONDER WHICH BETTER! KAMA KWELI AMEISHI USA BASI ANGALAU ANGEKUWA NA CULTURAL NZURI YA UCHAGUZI. UMESHINDA UMESHINDA UNATUKANA WENZAKO ILI NINI. NA SIJUI NI WAKINA NANI WALIOMCHAGUA, HALAFU ETI NI WAZIRI! AHHH TANZANIA SAFARI NDEFU TUNAYO! NI HAYO TU.

    ReplyDelete
  25. Mimi ni mwna CCM wa Damu, lakini kusema kweli kwa uteuzi wa mama Sofia Simba na wengine wengi JK kapiga chini. Mama Simba kichwani mtupu kabisa kajaa uswahili tu. Nimeshakutana nae sehemu kadhaa,nikija nyumbani for vacation and work.Mimi na mwanamke lakini nashindwa kabisa kujua JK kikwezo cha kumchagua SImba ni nini, kama walivyosema wengine kama unataka kuchagua wanawake ni vizuri lakini take those who are qualify not just any woman will do. Tuna wakina mama wengi wenye sifa kuchagua hawa wakina Simba ni kututia aibu sisi wengine. Simsemi mama Simba ila that's the truth.

    ReplyDelete
  26. JOHN MASHAKA KAFANYA NINI?mbona mnamzungumzia mume wangu humu???

    ReplyDelete
  27. Mwanakijiji aliwahi kusema katika Jamiiforums kuwa yupo kwa ajili tya special mission, kwa sasa amekimbia anatoa michango kimtindo na ameamua ku base kwenye KLHNews yake na sasa katika KLHNews naona ni haya mambo ndio anatuletea sasa.
    Nimeamini kweli mwanakijiji yupo kwa ajili ya special mission.
    Only few will manage to point it out.

    ReplyDelete
  28. SIWAELEWI ATI,,,
    mara sofia simba,mara john mashaka bla bla bla

    sio viongozi wote wajenga hoja,bt wapo wenye akili na vision nzuri tu
    anyway mwanakijiji lianzishe

    ReplyDelete
  29. Inaonekana kiburi na uswahili alivyonavyo Bi. Simba na mwanakijiji ni hivyohivyo. Sijui ni mtu na ndugu yake? Maana mwanakijiji anavyorespond kwa hoja za wateja wa blog utafikiri ana ugomvi nao. Bwana Mwanakijiji endelea tu na maisha yako huko Marekani. Kumbuka tu kwamba kumtukana mwenzio matusi mazito kama uliyoyatoa hadharani sio vizuri. Next time kaa kimya uangaliea tu comments za wateja wako. Kuna positives na negatives. Ndiyo utamu wa mjadala. Sasa comments za negatives zilipoonekana kuzizidi zile za positives naona ukaamua kuingilia kati kwa kuwatukana wote wenye comments za negatives. Was that real fair? Nadhani katika maadili ya uandishi wa habari it is wrong. Utatoa speech ya matusi?? who are you by the way?? Mwanakijiji hivi ni nani hasa mpaka awe na uhuru kama huo?? Anyway Michuzi yote tumwachie Mungu.
    Mdau

    ReplyDelete
  30. MwanaKJJ kuanzia leo nimeamua niwe nakutazama kwa mtazamo mwingine... Amen

    ReplyDelete
  31. jamani wa tz mbona sijaona kosala mama simba katika mahojiano yake acheni chuki jamani wa tz

    ReplyDelete
  32. Pole sana mwanakijiji. Naona hatuwezi kukulaumu wewe bali yawezekana ikawa ni upeo wako wa kuchambua masuala ndiyo tatizo. Nina wasiwasi na kiwango chako cha elimu na uzoefu wako katika fani ya uandishi wa habari. Sikutegemea mwandishi wa habari aliyeelimika awe na ufinyu wa mawazo kama ulivyojikanyaga kwenye hotuba yako iliyojaa kukemea na kutukana. Nafananisha hotuba yako na zile za enzi za Nyerere wakati wa uhujumu uchumi. Mimi nadhani kwa hotuba kama uliyoitoa kwa mwandishi wa habari anayejua kazi yake asingethubutu hata kidogo. Hotuba iliyojaa mambo ya kisiasa ambayo utafikiri ni mmbunge au kiongozi fulani wa kitaifa anayekemea jambo fulani. Lakini kwa journalist anayeelewa kazi yake asingeliweza kufanya hivyo. Umeongelea mambo mengi sana ambayo hata Bi. Sophia hakuyasema na wala hata watoa hoja hawakuyasema na hata hayahusiani. Nadhani kwa muda mrefu sana ulikuwa na usongo wa kutoa speech ili wakuone cheche zako. Bahati mbaya speech umeitoa kwenye wrong forum. Nadhani unahitaji urudi shule ukajifunze “Analytical journalism” Uwezo wako wa conceptualize na ku-articulate ideas ni mbovu sana. Ulidakia vitu vilivyo nje kabisa ya topic. Lakini pia wewe ulipotoa sehemu ya watu kutoa maoni ulitegemea nini. Kuna positive na negative opinion to the subject under discussion. Kwa hiyo wewe ulitakiwa usikilize maoni yote halafu uchukue maoni hayo kama unataka kumsaidia Bi. Simba basi ungelimpelekea. Yale mazuri angeshukuru na yale mabaya basi angeliona jinsi ya kujirekebisha. Wewe ni referee na mchezaji, itawezekana kweli? Nadhani inabidi ukasome zaidi kuongeza upeo wako wa kuelewa mambo. That is the fact. Nina wasiwasi hata diploma ya journalism kama utakuwa nayo. Maana kwa hali hiyo! Mmmmmmmmmmmm
    Mdau

    ReplyDelete
  33. Pole sana mwanakijiji. Kule kumiliki tu Blog ya Mwanakijiji basi tena hatusemi kitu. Siku ukimiliki vyombo vikubwa vya habari si utaamuru watu wote duniani wavuliwe nguo hadharani? Sikutegemea mwandishi wa habari aliyeelimika awe na ufinyu wa mawazo kama ulivyojikanyaga kwenye hotuba yako iliyojaa kukemea na kutukana. Mimi nadhani kwa hotuba kama uliyoitoa kwa mwandishi wa habari anayejua kazi yake asingethubutu hata kidogo. Lakini kwa journalist anayeelewa kazi yake asingeliweza kufanya hivyo. Umeongelea mambo mengi sana ambayo hata Bi. Sophia hakuyasema na wala hata watoa hoja hawakuyasema na hata hayahusiani. Nadhani kwa muda mrefu sana ulikuwa na usongo wa kutoa speech kali kwenye society ili wakuone cheche zako. Bahati mbaya speech umeitoa kwenye wrong forum. Nadhani unahitaji urudi shule ukajifunze “Analytical journalism” Uwezo wako wa conceptualize na ku-articulate ideas ni duni sana. Hii inatupa wasiwasi kuhusu kiwango chako cha elimu. Nadhani inabidi ukasome zaidi kuongeza upeo wako wa kuelewa mambo. That is the fact. Nina wasiwasi hata tu diploma ya journalism yawezekana huna. Maana kwa hali hiyo inatia huruma! Mwandishi wa habari aliyejaa ubabaishaji kama wewe nadhani hata hatakiwi kwenye society. Hivi wanaofeli form four Tanzania si ndio wanaoenda kusomea kozi kama ualimu wa primary, journalism, hotel management, upolisi, magereza, n.k. Pole sana mzee
    Mdau

    ReplyDelete
  34. Wewe anonymous wa 7:58 PM ndiyo kusema unataka kutuambia kwamba Mwanakijiji aliferi mtihani wa form four na ndiyo maana uwezo wake wa kuchambua masuala unakuwa mdogo? Basi kama ni hivyo inabidi aka-resit mitihani yake ili aweze kupata nafasi ya kuendelea na masomo. Maana kwa hali hiyo kwa kweli inatia aibu. Hajachelewa maana hata Bi. Simba alikuwa katibu muhtasi na leo hii ni lawyer na ana master. Hii inaweza kumsaidia sana kuwa anafanya upembuzi yakinifu wa mambo kabla ya kukurupuka.

    ReplyDelete
  35. Tatizo la Mwanakijiji sidhani kama ni shule. Sijui ana formal education kiasi gani lakini hata Sophia Simba na madigrii yake si nae ameongea kama ngingi mmoja wa Buguruni Malapa?

    Na kugomba kwake pia sioni kama ni tatizo sana, hata ma pundits wa maredio ya US, kina Sean Hannity na Bill O'Reilly nao wanatoka mapovu kwenye mic, wenyewe wanasema - na Mwanakijiji naye anatumia hili neno - wanaita ni "passion."

    Tatizo ni kwamba huwa ana agenda katika kila kitu. Anasema ana "mission," kama alivyosema mchangiaji mmoja hapo juu. Hapa agenda yake ni kumsafisha Simba. Simba kalalamika kwamba blogs hazijamchambua vizuri, sasa Mwanakijiji anataka kumwonyesha Simba kwamba "I can sway the direction of this discourse in the blogs." Anadai criticims dhidi ya Simba ni kuchanganya lugha, au kusema kasoma. Si kweli na anajua. Hasemi kuhusu rushwa, kujilimbikizia madaraka, na conflict of interest ya kujichunguza mwenyewe. Anarukia ku address hoja dhaifu dhaifu za kuchanganya lugha. Mwanakijiji sio mkweli, ndio tatizo, sio shule yake.

    Bongo imejaa wanahabari waliosoma vizuri lakini vilaza watupu, na kuna wasiosoma, Kubenea kwa mfano nasikia hajasoma, lakini eti ndio top journalist wa Bongo. Shule hapa haihusiani na hawa journalists vilaza wa Bongo. Ni vilaza tu, elimu au bila elimu.

    ReplyDelete
  36. eti .. ''mbona hata chumbani watu wanachanganya kiswahili''!!!!!!!!!!!!!!

    duh!!!! kweli mwanakijiji... umenipa, goose bumps..................

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...