uwanja wa karume na majengo yanayokaribia kwisha ujenzi ya machinga complex ambayo yatatumiwa na machinga wapatao 10,000 kufanyia biashara zao. kwa sasa uwanja wa karume umegeuzwa kituo cha mazoezi kwa timu za taifa za vijana, wakubwa na wanawake

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. kaka Michuzi taswiraaaz !
    Sasa hapa focus yako ilikuwa wapi?
    Ulitaka kuutoa uwanja ama majengo yaliyo nyuma ?
    Asanta kaka
    mwaka mpya mwema

    ReplyDelete
  2. Ebwana bonge la view ila tatizo linakuaj tena pale pale..!! Kwamba tukija na magari au waendao kwa magari wanapaki wapi ili kuingia ndani kufanya shopping? Narudia tena swali langu..!! Kwamba tukija na magari au waendao kwa magari wanapaki wapi ili kuingia ndani kufanya shopping?
    Hili ndio swali langu tu mwanawanee....!!

    ReplyDelete
  3. Yaani Baabkubwa kwa wale washkaji kutoka Ukerewe wanaowapa mazoezi makinda wetu au nguvu ya soda au Serenget boys na kisha kuwachukua na kuwapeleka kwenye academy zao huko Ukerewe..!! Big Up sana..!! Sasa inabidi tufanye hivyo na kwenye michezo mingine kama Basketball, Volleyball, Swimming na mingineyo...

    Baabkuubwaa..

    ReplyDelete
  4. hapo ni changamoto kwa TFF kuingia ubia na NSSF n.k kujenga majukwa upande usio na masoko yamachinga complex ili huku uwanja uwe na majukwaa ya kisasa angalau watu 15000 waliokaa kama viwanja vya FULHAM,STOKE CITY,Queens park rangers n.k maana pitch tayari ya kimataifa.

    Fanyeni hima iliTFF/NSSF/PPF, DSM iwe na viwanja viwili vyenye hadhi ya kisasa, maana ni ajabu ya kweli TFF kukalia kulia hawana fedha za ziada na vitega uchumi wanavikalia, chelewachelewa mtakuta mwana si wenu 'wawekezaji wa ndani wakakomba viwanja vyote vinavyoizunguka pitch ya Karume.

    ReplyDelete
  5. duh...umeniletea kumbukumbu kabambe hapo...nakumbuka michezo baina ya Simba na Cosmo pamoja na timu mbalimbali za hapo Dar!!!enzi hizo niliwahi kuichezea timu iliyokuwa ikiitwa Shetani wekundu!!!asili haswa

    ReplyDelete
  6. duh...umeniletea kumbukumbu kabambe hapo...nakumbuka michezo baina ya Simba na Cosmo pamoja na timu mbalimbali za hapo Dar!!!enzi hizo niliwahi kuichezea timu iliyokuwa ikiitwa Shetani wekundu!!!asili haswa

    ReplyDelete
  7. Ngoja nigeuke Michuzi..''Mbona picha haina uhai? Ungesubiri watu, ndege au mijusi ikiwa inapita ili picha iwe na uhai! sasa hapo focus yako ni nini? Uwanja au majengo? Acha papara! teh teh teh teh! Michuzi usibane.

    ReplyDelete
  8. bwana michuzi huo uwanja na majengo yake yanapendeza sana. ninakushukuru sana kwa kutuonyesha sehemu mbali mbali za tanzania. HAPPY NEW YEAR MR. MICHUZI.

    ReplyDelete
  9. Bro Michu,
    Asante kwa picha ila mimi bado nalia na watu wa Planning hivi kweli wapo Tanzania au watu wanajijengea tu? hebu angalia hayo majengo yalivyo karibu na uwanja hivi uwezekano wa kuupanua huo uwanja na kuweka majukwaa upo kweli au ndo taratibu taratibu unafukiwa na majengo kuzunguka uwanja huo?....

    ReplyDelete
  10. Kaka Michu

    Kweli the taswiraas haina uhai labda fafanua!

    ReplyDelete
  11. Jamani kwa taarifa yenu hilo jengo la Machinga Complex limejengwa kwenye mtaa wa Lindi street siku hizi Sofia Kawawa Street, pale yalipokuwa majengo ya watumishi wa UDA.Kwa maneno mengine liko nyuma ya Karume Stadium. Raha yake ni kuwa lina wing ya pili ambalo linaunganishwa na daraja kama vile Manzese na kuvuka Kawawa Road hadi upande wapili ya barabara. Kuhusu parking itabidi lile eneo lenye makaburi litumike kama parking. Sasa sijui kama bodi ya maching complex au Meya Kimbisa analijua hilo.

    ReplyDelete
  12. HAHAHAAAA!

    WADAU HAPO JUU WANAONIKABA KOO KWA TASWIRA KUKOSA 'UHAI' KWANZA NASHUKURU KWA KUWA SOMO LIMEWAINGIA NA MNAJALI. ILA KWA HAPO NAOMBA NIJETETE... UHAI UPO SANA TU. CHEKI GOLINI KULE KATIKATI MUONE JAMAA ANA TREKTA ANAWEKA SAWA NYASI ZA BANDIA....

    MPO HAPO????

    ReplyDelete
  13. wadau hapo juu mnaolalamika kwa maneno ya kuonyesha kama vile hamuhusuki, kumbukeni fikra sahihi huja kwa lugha sahihi na mahala palipo sahihi. Ukitaka ule ugali ulioiva shika mwiko ukasonge au mwelekeze anayekupikia siyo unakaa mezani unasubili kulaumu tu.
    Watu wengi mmetoa maoni mkionekana kufahamu vitu lakini la kushangaza mnaishia kusema huko au kule London iko hivi au vile. Tujaribu kutumia nasi nafasi zetu tulizonazo kuonyesha mabadiliko au turudie msemo wetu wa mwaka jana wa kuosha VINYWA??.
    Kama mdau alivyosema hapo juu wala planning ya ujenzi wa hayo majengo iko separate na uwanja huo ukiangalia kwa makini utaona ukuta wa uwanja, kwa hiyo kwa kutumia picha hii uwezi jaji hata suala la parking.
    Ingawaje hiyo ni fani ya watu lakini naweza shauri kuwa kwa kuwa miundo mbinu ya hapo awali ya jiji haikujali sana parking naonelea ni suala la serikari kwa sasa kwa maeneo yote ya city cetre pamoja na maeneo ambatano kama haya wajaribu kufanya utaratibu wa kuincourage public transport kwa kuboresha. Hii ni kwa sababu hatuna budi kuuhita mji wetu huu kuwa wa historia kama ilivyo stone town zanzibar kwa muda mchache ujao. Kichwa cha paka ni kidogo ukilingani na kilivyowekewa; macho pua, mdomo, masikio. Na tanzania inalifanya eneo la jiji kama kichwa cha paka. tuanzishe mji mwingine mpya wenye proper planning focus. Maoni yangu wakuu, wengine watafikiria vingine ambavyo pia ni sahihi

    ReplyDelete
  14. Kwa uzoefu wa haraka hiyo picha ilipigwa to nje ya uwanja wa Karume ndo maana sehemu ya uwanja imeonekana zaidi, kwa kudandishia hoja(BY THE WAY) wadau tusifananishe miji ya huku ughaibuni tulipo sasa kwani wao walitutangulia sana, naomba niungane na anonymous wa 13, kwamba ufike wakati tuanzishe satellite cities mbembeni ya jiji la Dar es Salaam, ili kupunguza msongamano city center, sema shida mafisadi waliojenga maghorofa kariakoo watabana kwani ukianzisha satellite city maana yake unaiua kariakoo na watu washawekeza EPA zao pale.

    Ada ya mja ni kunena….

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...