MwenyekitiIssa,
Hii ni view kidogo ya hilo liitwalo soko la uzunguni hapa 'jijini' Tanga. Naiomba Manispaa ifanye mambo kidogo hata yaani hata 'danganya tot' kwa kulipiga soap soap kwa jaaaaaamu....
Mdau
Kwa Minchi


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. duu Mdau umenikumbusha home i miss this place japo viongozi wetu wamejisahau mno mji unazidi kuchakaa tu manake enzi zile jirani kuna pharmacy moja kona pale inaitwa Khanbay hivi bado ipo ile manake miaka kumi sijarudi Home hasa wabunge wetu ndo wanarudisha nyuma Tanga yetu mikoa mingine imetupita sana na ilikuwa nyuma yetu fanyeni kazi kwa bidii acheni kukaa vibalazani na kucheza bao ndugu zangu

    ReplyDelete
  2. Subirini 2010, jamaa watakuja na mapaje yao, huku wamefungasha zawadi za mtego wa panya ndani ya viropa, zikiwa zimesheheni khanga na kofia. Nafikiri hapo mtapata majibu mazuri, na huenda wakawapakia rangi ya pakaza tupite.
    Amakweli wajanga wana hila,zidumu, fikira za wajanja, oh, siku hizi, ari mpya na nguvu mpya na ...
    m3

    ReplyDelete
  3. Mdau wa Tanga asante kwa picha ya soko la "uzunguni" umenikumbusha mazingira niliyokulia. Chakushangaza ni kwamba hilo soko la uzunguni halifanani na jina lake hata kwa chembe.Toka nikiwa mdogo soko liko hali moja mpaka sasa, miaka kibao imepita hakuna matengenezo hata ya kulipiga rangi basi. Kwani makopo matano ya rangi yanatosha kulibadilish muonekano wake. Naiuliza Manispaa ya Tanga kopo la rangi ni shs ngapi? Je hamana hata hiyo pesa ya kununulia rangi? Pleaaaase! Do some thing ni aibu! Au badilisheni hilo jina na kuliita jina linaloendena na mahali.

    Mkereketwa,
    AM Boston

    ReplyDelete
  4. kwa kweli hili soko limegusa wengi, nami ni mmoja wao, ni soko la siku nyingi sana, nakumbuka nilikuwa nikitoka shule, napita hapo sokoni kuna jamaa anaitwa Ali (Sijui siku hizi yuko wapi) alikuwa ananiuzia papai fresh kwa sh 5 au 10 tu, kweli limenikumbusha mbali sana.
    Kitu kingine naomna nisema hapa ni kuwa wengi tumezoea sana kulalamika tu, nani akujengee Tanga yako? wewe mwenyewe umejificha ughaibuni? hapo siku zote ndio mimi huwa siwaelewi watu, wengi hako huko nje, wamesoma, wana elimu ya kutosha, watanga kibao,wenye elimu, badala ya kurudi nyumbani kufanya mabadiliko kwao, wao wameng'ang'ania tu kukaa nje ya nchi, huu ni ujinga uliopita kiasi, wanafanya nje kabisa ya taaluma zao, kazi za kishenzi kabisa wakati wana elimu nzuri tu ambayo ingeleta mabadiliko mengi nyumbani, mawazo mapya nk, rudini nyumbani, mmeona wenzenu wanafanya nini, na nyinyi kafanyeni kwenu, wewe mtu wa tanga unalalamika mji umedumaa unategemea mtani wako mkuu wa mkoa wa Tanga asiyekuwa na asili ya Tanga atafanya kitu? mtaishia kulalamika tu, badilisheni mitazamo wenu wa mambo, angalieni vitu na kutafakari katika kupata ufumbuzi sio kulalamika tu.pumbavu zenu!!!

    ReplyDelete
  5. SOKO LA UZUNGUNI NI LIPI HILO? NI LILE NYUMA YA STAND YA MABUS?

    ReplyDelete
  6. we mwenyewe uko wapi au unaosha vi.....i, unadhan kila alioko nje anafanya kaz za kishenz hebu fikiria utakuja kuwekeza sehem abayo haiwekezek kila mtu hapo tanga ni mfanyabiashara sasa nan anunue ya mwenzake inabid kuwe na mchanganyiko viwanda vyote wameua sasa watu wafanye nin maana watu wote wamekimbilia kama si dar, arusha mwanza na wamewekeza huko we mkoa una kila kitu bandar na kadhalika, shenz yako!

    ReplyDelete
  7. lazima viongozi wa manispaa wawajibike wao sio ndio wanakusanya ushuru hapo sasa unategemea mtu akitoka nje ndo apige rangi au afanye nin?lazima walalamikiwe, we uje hapo na useme unatoka nje sasa kutoka nje kwako ndo utawaambia kina kisa....!nin hebu fikiria sio kama unasema tu ndo ukitoka nje ugombee umeya au ubunge jaribuuuu nyamaf we!lazima tulalamikie hata huku nje serikal kama zinafanya ujinga zinalalamikiwa sebuse bongo

    ReplyDelete
  8. Jamani asante kwa kunikumbusha nyumbani na kumiss kweli.Ukweli ni kwamba hapo patengenezwe na sisi watanga wenyewe tutasubiri serekali mpaka lini tumekaa tunajisahau kuendeleza mji wetu.Mimi nikiwa moja wapo

    ReplyDelete
  9. mtuma hii post naishi Ndorobo si Kwa Minchi kama Mwenyekiti alivyoonyesha. Pharmacy ya Khanbay iliyokuepo ooposite na CRDB Bank haipo kwa sasa. Soko hili lipo

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...