WIZI ULIONIKUTA
Nimeonelea ni vema niwajulishe mbinu hii ya wizi ili isiwa fike nanyi .
Kuna kijana ambaye anadai ametoka Morogoro na ametumwa na mzee wake kununua gari kumbe ni tapeli na mwizi.
Kwa kadiri ya wiki mbili kijana alikuwa akifuatilia Gari ambayo nilikuwa naiuza na nikaitangaza katika Dar – Advert . Alisema yakuwa yeye yuko Morogoro na anahitaji kuiona gari ; mnamo tarehe 25 / 12 / 2008 asubuhi , tulipokea simu yakuwa tukutane na kijana ambaye ameondoka morogoro tumuuzie hilo gari . ( Na mpigaji akiwa ni mzee wake kutoka Morogoro; baada ya muda kijana aliomba udhuru ya kuwa tarehe 25 ni Krismasi baba yake angependa aje kuangalia hilo gari ila yeye hataweza atafika tarehe 26 / 12 / 2008 .
Saa moja asubuhi tarehe 26/12/08 alipiga simu na tukaelewana tukutane naye B.P petrol station Mbezi Beach .tulipokutana alicheki gari kama mnunuzi yeyote kutoka bodi mpaka engine.akaomba afanye road test –he is a good driver.
Alionyesha kuridhika na gari na kuonyesha nia ya kulipia fedha ambayo alikiri iko kwa jamaa ya baba yake aliyepo JM mall ambaye ni agent wa oilcom.; alipotoka JM mall alidai amepewa fedha ambayo ni dollar hivyo ilibidi tuende mlimani city kubadili fedha na kudeposit kwenye account kwani anasisitiza hapendi kulipana fedha mkononi angependa tulipane bank.
Tulipokuwa ndani ya bureau de change alikuwa akiwasiliana na jamaa zake na simu yake ilizima kwa kukosa chaji hivyo aliomba simu yangu kwa mawasiliano pia alielezea juu ya hali yake kuwa amekunya dawa amoxyline na tumbo linamsumbua kwani hajapata kifungua kinywa hivyo angependa kwenda kuchukua maziwa hivyo alitoka nje huku akiwasiliana kwa kutumia simu yangu.
Kwa vile nilishakaa naye kwa muda upatao masaa matatu na juu ya yote alikuwa ameacha bahasha yake ya dollars tulipokuwa tumekaa sikupata wasiwasi naye kabisa.
Alipotoka ndani tu katika dakika tano nilishuku hivyo nikafungua bahasha yake kuchungulia mzigo wa dolla nikakuta ni magazeti yaliyofungwa vizuri haikuchukua dakika kumi watu ambao contact zao zilikuwa ndani ya simu yangu walipokea message iliyosomeka ifuatavyo
" naomba unitumie vocha ya 5000/= nitakurudishia niko sehemu hapana duka na nahitaji sasa hivi"
Watu wengi waliibiwa kupitia kumtumia dolla.
Ninawataarifu jambo hili kwani nimegundua limemtokea na mwenzangu ofisini siku ya jumapili 21/12/08 na mimi nilituma dolla nikifikiri namsaidia kumbe naibiwa. Kwa huyu mwenzangu mbinu iliyotumika ni sawa kabisa na mbinu iliyotumika kwangu.nina wasiwasi wengi watalizwa na kijana huyu.
Kijana ni smart, knowledgeable, polite looking, courageous na kimwili ni mdogo mdogo and very friendly during the discussions si rahisi kumshuku
Kinachonisikitisha kijana yuko bright laiti angalitumia hizi sifa zake kufanya kazi rasmi naamini angekuwa mbali sana.
Haya …bomu hilo kaeni macho!!!!!!
peleka ujumbe huu kwa watu wowote utakaoweza ili kupunguza tatizo.
Ni mimi niliyeliyelizwa


Pole sana ndugu yetu na asante kwa kutuweka macho. Thanks once again.
ReplyDeletePole Kaka Michuzi itabidi nikutumie DVD inayooneshwa na BBC inaitwa Real Hustle Labda itakufundisha namna watu walivyowezi na Pic kama Ukawapelekea watu wa TV wakajaribu kula Deal na BBC waonesshe wananchi wetu wasije kuibiwa matapeli wengi bwana. Inshallah mwenyezimungu atakupa nyengine.
ReplyDeleteWow! it looks like a HOLLYWOOD MOVIE, from the beginning of your explanation tosha kujuwa kuwa huyu jamaa ni mwizi, nabado unafanya biashara kizamani sana mwaka 1947, by itself is a recipe for disaster, fanya biashara ofisini kwako si kutembezwatembezwa hivyo mitaani, mtu akisema hataki kulipa cash anataka kuweka kwenye account mwambie akaweke akuletee receipt na wewe uende bank kuhakikisha kama kweli ameweka na ukae siku kadHaa za kutosha kuona pesa imehalalishwa kwenye account yako ndo muandikeane mkataba wa kuuziana, as simpla as A,B, C.
ReplyDeleteHujamalizia stori, je ulipofungua barua ukakuta makaratasi kilifuata nini?
ReplyDeleteJe kulitokea zali baada ya bwamdogo kugundua umefungua bahasha yake bila ya kumtaarifu?
Je kijana potential buyer hakudai kuwa wewe hauna uaminifu badala ya kumbonyeza kasahau bahasha yake wewe ukaifungua bila ridhaa yake
Je watu wa Bureau de change wahakuona hicho kioja na kilikwisha vipi?
Je hizo airtime alizokomba kwa 'washikaji wako' anazifaidi vipi au ni thrill satisfaction tu kukuingiza mjini?
Mwisho Je 'image' ya bwanamdogo ilinyakwa na CCTV ya hiyo Bureau de Change, tuelezee hii kanyaboya iliisha vipi polisi au mliyamaliza?
Mdau
Inspector Morse
we anon wa saa10.32pm usijifanye mjuaji jambo kama hilo linaweza kukutokea hata wewe,shukuru mungu halijakukuta haijalishi uwe smart mfanya biashara wakisasa au wakizamani,wao pia wanambinu na techniki zao.........kwa ulie ibiwa pole ndugu
ReplyDeleteHii stori mbona ipo bachelor hivi, yaani ukiisoma inaishia kwa mama ntilie wala siyo nyumbani kula ulichopikiwa na mkeo. Huyu jamaa ana lalamika kaibiwa simu?, Vocha au gari?. Kama kaibiwa gari kweli stori ina nguvu ila kama ni simu hamna kitu hapo mbona wengi wameisha lizwa sana kiivyo ina maana hajui?.
ReplyDeleteHutakiwi kumkabidhi mtu usiyemjua simu yako ya mkononi akaongelee faragha, kama anataka privacy mpe buku aende kwenye kibanda.
Mi kuna jamaa yangu mmoja wakati tupo mlimani alicheza kitu ambacho mpaka leo huwa kinanipa tahadhari na kumkumbuka yeye. " Kuna jamaa alikuja chumbani na kusema anauza radio za SONY "KARAOKE" Za dili wanazopiga kwa wahindi ambazo huuzwa Shs 800,000 ila sisi atatufanyia Shs 400,000. Jamaa yangu akaona bora anunue. Muuzaji akasema tumpe laki mbili akamkabidhi mpigaji halafu inayobaki tutampa akileta Radio. Jamaa yangu akakubali ila akamwambia waende wote mjini atampa wakifika, wakapanda gari mpaka Kariakoo, Kufika huko jamaa akamwambia jamaa yangu amsubiri sehemu akamsubiri jamaa akazuga kama dk 15 akarudi akamwambia nikabidhi ule mzigo, jamaa yangu akamwambia wewe kaleta Radio nakupa fedha yote hapa. Jamaa akaenda dk 10 akarudi akasema jamaa anataka hata laki moja kwanza ndiyo atoe radio. Jamaa yangu akasema hapa sitoi hata shillingi, kalete radio nikupe hela yote. Jamaa akafiria akamwambia poa ngoja ntamuimbisha atakubali hebu nipe bag nikabebee basi, jamaa akaona bag la Shs 5,000 ngoja nimpe, alipompa jamaa hakurudi tena akaingia mitini kimoja.
Toka siku hiyo nikaapa sitamuamini mtu yeyote bongo katika mambo ya biashara. Huyu jamaa anayelalamika hapa ajue kuwa bongo kila mtu anafikiria atakula vipi. Next time biashara ifanyike kwenye biashara siyo kupelekana vichochoroni wanaweza hata kukutoa nafsi kwa mali yako mwenyewe.
Ndugu mtoa maoni wa January 09, 2009 10:29 PM, nadhani unakaa UK, The Real Hustle ni kipindi ambacho huwa sikikosi kwakweli hapo BBC THREE, lakini nakurekebisha tu, kama unataka kumtumia michu mtumie tu lakini nadhani ingekuwa safi zaidi ungeweka tu hata link kadhaa za youtube za kipindi hicho hewani wadau wote waone au kwa msaada zaidi, msomaji wa blog hii ingia Youtube halaf type The real hustle uangalie clips zake uone mbinu za matapeli na wezi.. anyways Kurudi katika Mada au jambo nililotaka kukurekebisha wewe mtoa maoni ya the real hustle, HIVI HUJUI TU KAMA BBC INAENDESHWA NA MALIPO YA LESENI YA LUNINGA..(TV LICENSE)... BBC ipalayer tu haionekani sehemu nyingine yeyote duniani isipokuwa kisiwani humu.. kwasababu wengine haWana haki ya kuona au kutumia mgongo wa sisi walipa kodi.
ReplyDeleteNB: NAJUA KAMA KUNA VIPINDI VINAONYESHWA NA CABLE SERVICE PROVIDERS DUNIANI LAKINI HIYO SIO DALILI YA KUHALISHWA UONEKANAJI WA VIPINDI VYOTE VYA BBC NJE YA NCHI HII (UK)
Mwisho nampa pole sana Mdau aliyetapeliwa...
MDau UK
hata mimi maswali yangu ni hayo hayo
ReplyDeleteje alivyorudi na simu yako ilikuaje mwishi wa hadithi?
Halafu unaibiwaje hela kupitia simu yako?
je hakukudai hela zake baada ya kuacha kwenye kiti?
utamuachiaje mtu simu ako ya maana atoke nayo nje? humjui hakujui?
mi hapo washikaji mnanichekesha, kwani we unadhani angerudisha simu wangemuita mwizi ahahaaaaaaaaa, mi naona story hii inaonyesha kuwa simu iliibiwa, hapo hakuna simu wala polisi, inaonyesha aliondoka na simu, na akalipa magazeti, pamoja na hayo pole muibiwa, hiiimekuwa kama filamu ya kibongo moja ninayo ila nimeisahau jina, msiwe mnadharau ma igizo ya kibongo yanafundisha. SiCeNga
ReplyDeleteKwa vile hii stori imeishia kiaina aina, mimi na kamilisha ya wadau hapo juu kwa kusema:
ReplyDelete-Huyu jamaa ni mfanyabiashara wa Bureau de Change sehemu nyingine yaani sio Mlimani.
- Anataka jamaa wasitumie huduma za Bureau de Change hapo Mlimani.
-Au huyu jamaa ana ugomvi usio wa kibiashara na jamaa wa Bureau de Change mlimani.
Mdau
Abunuasi Socrates
Duh...stori kabambe,wiki chache zilizopita mbeba maboksi mmoja kule kwa wakoloni alitangaza anataka wacheza sinema wa kibongo wanaozungumza kiswahili cha Afrika Mashariki,labda hao jamaa watumiwe kucheza hiyo stori yako...nikuhakikishie utashinda 'oscar'!!!
ReplyDeleteBro michuzi ungekuwa unakiangalia kipindi cha jumatatu saa 3.30 TBC1 cha Bongo Daresalaam, usingeliwa kirahisi hivyo kaka. Pole sana. Akina Dude hapa dar wako wengi sana. Wake kwa waume.
ReplyDeleteheheee pole we.
ReplyDeleteMimi hata ebay sinunui kitu naona kama utapeli or maybe hali halisi ya kwetu imenitraumatise.
Wadau mi nadhani tatizo letu kubwa ni kutokuwa na ujuaji wa jinsi vitu vingi vinavyo operate. Wote walioibiwa kwa style hii wanauwezo wa kuwapata wezi wao kirahisi tu kwa kushirikiana na polisi, labda urasimu ulioko polisi unaweza wakatisha tamaa.
ReplyDeleteMtu kaiba simu, akapewa salio la buku 5 na watu kibao,lazima atapiga simu kwa watu wengine, na kama si hivyo atahamisha salio kwenda simu nyingine, na kutumia simu nyingine atawapigia jamaa zake.
Mwisho wa siku all are traceble, iwe salio kuhamishwa na mtu kupigiwa simu, wanadakwa walio pigiwa na kuhamishiwa salio, kazi imekwisha.
Kwa kifupi mwizi hakuwa mtaalamu jamani, kama alimind simu, angeichukua tu, suala la kuomba salio kachemka sana, kaacha nyayo zake mchangani, anapatikana tu... atakuwa hana knowledge ya kutosha.
Hakuna ubishi utapeli ni utapeli tu unaweza kumtokea mtu yeyote. Aliitapeliwa HAYATI MWALIMU NYERERE NA MAREHEMU BATENGA itakuwa watu baki
ReplyDeleteSIO KWA BONGO AMBAKO SIMCARD INAUZWA SH 100 TU.huyu jamaa mwizi yeye anawasiliana na wezi wenzie tu tena baada ya kulihamisha salio na hao wezi wenzie sijui utawakamataje maana wote watu wa vimeo huwezi kumuuliza yuko wapi na akakwambia alipo,utaratibu wa wamiliki wa namba za simu kujulikana location zao au adress zao bongo haupo mpangilio ni VAGARANT.so kumpata ni ngumu kwa bongo anamuhamishia salio mwizi mwenzie wa kigoma huko
ReplyDeletePole sana mshikaji.Ndiyo maisha ya bongo.Alilizwa "MALAFYALE" vilap-top na visimu vyake sasa na ww umeunga tela.
ReplyDeletesomo= utalijua jiji
Jamani mbona watu wanampa pole Balozi Michu, kwani ni yeye aliyeibiwa? someni vizuri. Na wewe ndugu yangu Numero Uno, hicho unachosema, kwa polisi wa Bongo ni sawa na kuuza ng'ombe ili ukashinde kesi ya kuku. ku trace mtu aliyeiba kwa kupitia simu hiyo ni kazi ya dakika kumi tu lakini Watakutoa hela wewe mpaka ukome kwenda polisi kwa issue ndogo kama hii.Kama sio kuombwa hela moja kwa moja, basi utaambiwa nenda rudi mpaka gharama yake itazidi hiyo uliyoibiwa wewe na rafiki zako.Cha msingi ACHA KUMWAMINI MTU YEYOTE, HATA KAMA UNAMJUA. Kama anataka kununua gari, baiskeli yako whatever, nenda naye bank anajaza pay in slip, anakaa foleni yeye mwenyewe na hela zake, ana deposit hela kwenye account yako, anakupa copy ya pay in slip na wewe unampa funguo ya gari na kusainishana mkataba.Hakikisha hizo draft za mkataba zimeshaandaliwa kabla ya kwenda bank, kinachosalia ni kuanguka saini tu hapo.Tena usilogwe kwenye biashara hii ya magari eti unamleta mtu nyumbani kwako kuja kufanya hiyo transaction, yatakukuta makubwa zaidi ya hayo. Tafuta mahali ambapo unaamini ni salama mzungumze na yaishie hapo, mkitoka moja kwa moja bank.
ReplyDeleteMdau
Cardiff
Stori iliyoandikwa hapo juu ni ya kweli kabisa,
ReplyDeleteKwani hata mimi imemkuta jamaa yangu juzi tarehe 9 ijumaa.
Staili ni ile ile iliyotumika na mi mwenyewe ni mojawapo ya tuliotumiwa ujumbe wa kutuma hizo vocha ila nlishtuka.
Alieibiwa ni Mmiliki wa Petrol Station ya Engen Mikocheni aitwae Anord na kuhakikisha namba yake ni 0713 334 024.
Ni aina ya wizi ambao inabidi jamii iwe nayo macho, kwani kwa hesabu za watu naowajua, kiasi cha Tshs 150,000/= kishatumwa kama vocha kwa namba ya jamaa aliebiwa huku matapeli hao wakijisundia hizo vocha kiulaini.
hahahahaaaaaa,duh u made my day today,hahahahaaaaaaaaa uwiiiiii
ReplyDeleteati wanunua simu ya laki 9,sasa walia nini???ulitegemeani ktk life la bongo mtu sh 500 ya mchicha hana afu wee una simu ya laki 9!!!khaaaa aaaghg unaboa sana!!!wee si una pesa kanunue ingine
hawa jamaa ni wezi sana, hata mimi April nilitangaza kuuza gari gazetini, nikapigiwa simu na kijana mmoja mtanashati na anaongea kama ulivyomdescribe, tukaarange aje aione gari nikaambulia kuibiwa simu pale msimbazi kwa gia hiyo hiyo kama yako. mwezi december nikatangaza tena kuuza gari, nikapigiwa simu toka morogoro na bwana mmoja ambae akasema atamtuma kijana wake aje aione, nikamsubiri sana hakutokea siku tuliyopanga, baada ya siku saba akanipigia tena akasema aliharibikiwa na gari chalinze hivyo alishindwa kuja, tukapanga sehemu ya kuonana. nilichomstukia pale aliponitumia message ya tafadhali nipigie hapo nikaona hakuna mnunuzi, nikaamua nisimpelekee gari. lakini ulivyoeleza naona ni mtandao wao. yabidi tuwafanyie mtego.
ReplyDelete