mwenyekiti wa yanga imani madega akimtania profesa juma kapuya kwa kumpa kipeperushi cha yanga huku katibu wake mkuu lucas kisasa akishuhudia neshno leo kabla ya mechi kuanza
profesa kapuya. uzalendo uliooneshwa kwenye gemu hii ni wa hali ya juu. hakukuwa na yanga wala simba wote walishangilia utaifa. kikosi cha yanga kilichoua leo
wachezaji wa commoro wakila jalamba. masikini hata mpira wa kupigia tizi walikuwa hawana. ilibidi wachezaji wa yanga wawaazime yao
uzalendo ulitawala leo neshno ambapo mshabiki mkubwa wa simba magoma moto alitinga kiyanya-yanga na kupeperusha kipeperushi cha jangwani. hakuna mtu ambaye uzalendo ulimshinda leo
mshabiki machacahri wa yanga, papaa mbaga, akijidai leo neshno kwa bao 8-1

hatari langoni pa wakomoro
mashabiki wa yanga leo meno nje. hapo namwona mustafa romeja akiwa na raaaaaaahaa
yanga bomba a.k.a manji's army koo ziliwapasuka kwa kushangilia watoto
kuwa yanga bomba kwahitaji ujasiri wa kuambaa na bomba hadi juu katika jukwaa ka kijani. chini ni simba.....ukichelewa hapishwi mtu

YANGA BOMBA WAKISHANGILIA BAADA YA TIMU YAO LEO KUICHAPA MABAO 8-1 ETOILE D'OR MILONTSY YA VISIWA VYA COMMORO KATIKA MCHEZO WAO WA MGUU WA KWANZA WA KOMBE LA LIGI YA MABINGWA WA AFRIKA KATIKA UWANJA WA KALE WA NESHNO. GEMU LIMEISHA MUDA MFUPI ULIOPITA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. Bado Simba...

    ReplyDelete
  2. Yanga ni noma hakiyanani

    ReplyDelete
  3. Premier League Uingereza Leo:

    Mechi iliyoanza mapema matokeo:
    Stoke City 1 - Man City 0

    Mechi zinazoanza Leo 15:00 GMT:
    Arsenal vs West Ham united
    Aston villa vs Wigan athletic
    Bolton Wanderers Vs Tottenham
    Fulham vs Portsmouth
    Hull City vs West Bromich Albion
    Middlesbrough vs Blackburn Rovers

    Mechi itakayoanza Leo 17:00 GMT
    Manchester United vs Everton

    Kesho pambano ktk wanja la Anfield jijini Liverpool ni kati ya Liverpool vs Chelsea.

    ReplyDelete
  4. Hii ndio inatakiwa washikaji mtu akitokea kakaa vibaya anajilaumu. Sasa aje anayejiita mnyama inatakia kitu mfano wa hapa. BRAVO VIJANA

    ReplyDelete
  5. kwani mchezo huu ulikuwa netiboli au basketiboli?mie sijawahi kuisikia bongoland wajulikane kama taifa la futiboli!!!

    ReplyDelete
  6. Wamekaa kama Wazanzibari.

    ReplyDelete
  7. mbonaaaa rahaaaaaaaaaaa arsenal dumbwi tena jaman wenger arshavin vip walau aokoe jahaz hilo lazamishwa jamaa ka

    ReplyDelete
  8. Matokeo ya mechi za premier league Uningereza:

    Katika uwanja wa Emirates:
    Arsenal 0 West Ham 0. Kocha Zola wa West Ham anazidiha kufifisha ndoto za Arsenal suala la ubingwa.

    Aston Vila 0 Wigan Atheletic 0 ndani ya wanja la villa park.

    Bolton 3 Tottenham 2 Reebook stadium.

    Fulham 3 Portsmouth 1

    Hull City 2 West Bromich albion 2

    Middlesbrough 0 Blackburn 0 wanja la Riverside.

    ManCity 0 Stoke 1.

    ReplyDelete
  9. MNAJISIFU KWA KUWAFUNGA HAO CHA NDIMU?? SI AJABU MKASEMA USHINDI HUO UNAASHIRIA KUWA KIWANGO KINAONEKANA KUPANDA. SUBIRINI KIPIGO CHA SIMBA, MWAKA HUU HAKUNA HURUMA... NYAU NYIE.

    ReplyDelete
  10. hiyo timu ya comoro iliundwa tu na watoto wa mitaani alafu viongozi wa michezo kule comoro wakaipandisha hadi daraja la kwanza, tuseme kama kipindi kile cha mpira wa vichangani zile timu zikacheze na simba au yanga unategemea nini hapo kama si kapu la magoli!!! ndio maana ya wakaitumia hiyo nafasi ya kuteremsha kibonde hiko cha uonevu!!! wale jamaa sio wachezaji wale, kwa hiyo yanga msitambe kwa kula ugali na harufu ya samaki bado mnatakiwa mjifunze mpira kwani mananiboa sana arafu mnachekelea hiko kiushindi mweeeeeeeeeee!!!


    Mdau wa mbekenyera!!!!!

    ReplyDelete
  11. House endorses revocation of hunting...

    2009-01-31 11:30:26
    By Lydia Shekighenda, Dodoma


    The National Assembly yesterday endorsed the revocation of the three-year extension of hunting terms granted to hunting companies in the country because they contravened the resolutions approved by the 11th meeting of the august House.

    The House wants the reallocation process to be completed in 2010 and not 2012 as proposed by the Natural Resources and Tourism ministry.

    Moving a private motion here yesterday, Kwela MP Chrisant Mzindakaya said failure by the government to implement the resolutions was in breach of parliamentary rights.

    His motion was against the government statement tabled in the House on Thursday by Natural Resources and Tourism minister Shamsa Mwangunga, which only explained why the government was yet to implement the resolutions as directed.

    During the 11th parliamentary meeting, MPs recommended that the government reallocate and set new charges for hunting blocks whose term of ownership would lapse this year, but the government instead extended the hunting terms to 2012.

    Mzindakaya argued that failure to implement the House resolutions meant defending the interests of the hunting firms through the Tanzania Hunting Operators Association.

    ``Any act by the government to intervene in the process of the implementation of parliamentary resolutions on the reallocation of the hunting blocks means interfering with the parliamentary powers and breaching its rights,`` he said.

    In her response, Mwangunga apologised for not informing the House about the decision to extend the hunting terms.

    She said she took it for granted that informing the parliamentary committee on natural resources was enough to push the decision through.

    Contributing to the motion, Kigoma North legislator Zitto Kabwe said the government had breached parliamentary rights and not taken into consideration the fate of the country`s national resources.

    He said a report on Tanzania`s economy showed that the tourism sector contributed 15bn/- to the national income in 2006 and only 7bn/- in 2007.

    Kabwe said cancelling the extension would not cause a loss because even the revenue generated was not much and could be recovered from other sectors.

    Kishapu legislator Fred Mpendazoe warned that the giving of simplistic answers given to serious issues had made many African countries fail to develop, adding: ``The government is supposed to be accountable to Parliament.``

    The MP demanded that a government leader who went against Parliament’s directives should not bother with explanations but should instead submit a resignation letter.

    Explaining the delay, minister Mwangunga said the government was trying to avoid negative effects during the preparation of the new law that also covered revenue losses.

    SOURCE: Guardian

    ReplyDelete
  12. Watu wengine bwana..ovyooooooo!! wewe anony wa 3, si uanzishe thread ya kwako!!. we si unaona wadau wenyewe wa simba leo wamevaa uzi wa jangwani, wewe unaleta longolongo.Kwani umeambiwa hii ilikuwa mechi ya Premier ligi ya Uinereza. Unataka kuwaharibia wenzio stimu tu hapa. Siku nyingine anzisha yakwako.

    ReplyDelete
  13. Hatusikii tena Premier league.Baiskeli ya mbao imeishia njiani.Taniboi alipewa kuendesha basi ikawa kelele mjini.Sasa mwenyewe karudi Michuzi hapendi.Hatusikii Bwawa la maini wala la utumbo.Ilikuwa tabu afadhali amani imerudi.

    ReplyDelete
  14. Matokeo ya mechi ya mwisho ya leo ya premier league:

    ManUTD 1 Everton 0. Goli la ManU lilifungwa kwa penalti na Rolnaldo katika dakika ya 43 kipindi cha kwanza. Mechi ya leo ili kuwa 'man-to-man' kwa sana.

    Kutokana na matokeo hayo ManU inangoza ligi kwa kuwa na pointi 53, nafasi ya pili Chelsea pointi 48, nafasi ya tatu Liverpool pointi48 ,nafasi ya nne Aston villa point48 nafasi ya tano arsenal point 43.

    ManUTD sasa wameshinda mechi 12 mfululuzo bila nyavu za kipa wa ManUTD Van der Sar kuguswa. Katika mechi 10 zilizopita ManUTD wameshinda mechi 7 kwa ushindi wa bao moja moja tu. Mechi zilizobaki ManUTD kumaliza ligi ni 16. Mechi inayofuata wikiendi inayokuja ni dhini ya West Ham United.

    Timu: ManUTD Van de Sar, Neville/ Wes Brown, Vidic, Ferdinand, Fletcher/ Ryan Giggs,Carrick, Ronaldo, Oshea, Park, Babertov na Tevez.

    Everton: Howard, Hibbert, Jagielka ,Lescott, Baines, Piennar, Phil Neville, Arteta, Osman/Anichibi

    Kesho Liverpool itaingia uwanjani nyumbani Anfield kukwaana na chelsea kupunguzwa tofauti za point na ManUTD.

    ReplyDelete
  15. Obama half-brother on drug charge

    George Obama is the President's younger half-brother
    The Kenyan half-brother of President Barack Obama has been arrested for alleged marijuana possession.

    George Obama was arrested in Nairobi with one joint of marijuana, police chief Joshua Omokulongolo said.

    "He is not a drug peddler. But it is illegal, it is a banned substance," he said. Mr Obama has denied the allegations.

    The US president and George Obama share the same father, but are thought to have only met each other briefly.

    George Obama, who is in his 20s, is due in court on Monday.

    "They took me from my home," George Obama told reporters in Nairobi from his jail cell. " I don't know why they are charging me."

    Kenyan family

    Last year, George Obama told Vanity Fair magazine that he had only met his more famous half-brother twice, once when he was five and once when he visited East Africa in 2006.

    Of their second meeting, George reportedly said:"It was very brief, we spoke for just a few minutes. It was like meeting a complete stranger."

    He has also said that he is studying to be a mechanic and works with a local youth group in Huruma, the area in Nairobi where he lives with his extended family.

    He is the youngest of his father's seven children and was born six months after his father died in a car crash in 1982.

    Several of the president's Kenyan relatives went to Washington for his inauguration on 20 January, though George Obama did not.

    The American president described his half brother as a " handsome, roundheaded boy with a wary gaze" in his book, Dreams From My Father.


    Source:bbc.co.uk @15:30hrs GMT

    ReplyDelete
  16. Hongereni saaaaaaana wanajangwani. Furahini kwa leo lakini furaha yenu inaishia raundi hii tu maana wababe wenu waarabu wanakuja raundi inayofuata. Si mnajua mambo ya waarabu lazima mtuoe t...

    ReplyDelete
  17. Yanga!!! Mmekutana na vibonde halafu mnajifanya mnaujua mpira! haya hongereni sana lakini dawa yenu iko jikoni. Ngoja waarabu waje wawanyoe bila maji. Jitayarisheni tu cha moto kiko just around the corner. Mtamfukuza hata huyo kocha wenu kwamba ameuza mechi!
    Mdau

    ReplyDelete
  18. Michuzi wacha kutuongopea bwana kama kweli ulikuwa uwanjani hebu nambie baada ya wacomoro kusawazisha bao la kwanza jukwaa kuu upande wa Simba walikaa kwenye viti vyao au walishangilia?? Kwa taarifa yako uzalendo upo kwenye timu ya Taifa tu huku kwenye simba na yanga hakuna anayependa mwenzake afanikiwe kama huamini ngoja uone game na wamisri uone the way watani watakavyoshangilia

    ReplyDelete
  19. hata pamba ilifanya hivyo kwa kufunga goli 12 kwa 5 ila iliishia hapo hapo.

    yaani unaifunga timu ya mchangani unashangilia.????????

    ReplyDelete
  20. Hongera Yanga! Hata kama ni timu ya mchangani lakini ni mabingwa wa Comoro, ndio maana walifika hapa kucheza na Yanga, mabingwa wa Tanzania. Na Yanga ikifuzu raundi hii inakwenda kupambana na bingwa wa Misri - sasa tatizo lipo wapi?

    Hata kama Al Ahly waliweza kuwafunga Yanga miaka ile, mwaka huu nadhani itakuwa tofauti kidogo kwani wachezaji wengi wa Yanga wamepata experience za kimataifa in the last 2-3 years. Kuna kauprofeshnalizimu japo kidogo - wachezaji 10 wapo Taifa Stars ambao wame[itia two seasons za Africa Cup of Nations; unganisha na watatu kutoka Kenya, mmoja kutoka Malawi, Serbia, na kocha wa nje.

    Vilevile, na sisi Yanga tutafanya yaleyale waliofanya Simba kumtoa Zamalek - kulala Yemen na kuingia uwanjani wakati ule wa mchezo. Tumeshaongea na Twalib Hilala naye katuhakikishia tusilale Cairo, twende na maji yetu ya bongo na kula kwa balozi!!

    Hata Al Ahly wakitufunga itakuwa kwa tabu sana, ngoja uone!

    ReplyDelete
  21. I am a die hard fan of Yanga na Taifa stars ila hizi timu mbili jezi zake zinatia kinyaa too cheap, halaf hazivutii, yanga hiyo full yellow haipendezi kuja jezi nzuri sana za rangi yanga i dont know anaye wanunulia hizi jezi cheap anazichukua wapi wangeweza kuvaa jezi ya njano na bukta black, yanga club kubwa mnadeserve big name kama nike, adidas, puma etc, hata taifa stars the same problem kuna rangi nne kwenye bendera ya taifa lakini wamestick kwenye rangi moja tu, mbaya zaidi ndio hizo hizo cheap products cmon guys u got to be serious

    ReplyDelete
  22. JE CHELSEA INAITWA ABRAHAMOVIC ARMY!!!
    WANA YANGA SHILINGI MBILI ZISIWAPONZE

    HATA AZAM HAIITWI "BAK ARMY"

    KUNA KITU HAYO MAANDISHI NI MAZITO

    ReplyDelete
  23. Nakuunga mkono mdau wa 5:28. Shilingi mbili zinanawaponza yanga. Kwani ni lazima iwe Manji's Army?? Kwa nini basi isiwe 'BEER's ARMY' maana ndio wanaofadhili timu kwa mapeza mengi zaidi kuliko Manji? Si Yanga hii hii iliyotaka hata kuweka Picha ya Mfadhili mwingine Kwenye kadi za Uanachama wa Klabu?? Hamuachi TU?? Njaa Itawaua nyie!!!

    ReplyDelete
  24. Jamani Yanga Army ni hilo kundi la washangiliaji (Yanga Bomba) na wala sio timu, klabu wala wachezaji. Mnashindwa hata kusoma bango tuu between line? Nyue Mdudu (sio mnyama) naona mmeishiwa, ndo maana mnaleta habari Manchester, Obama oo mara Manji, mnataka kutupotezea mwelekeo.

    Nyie mbona mkifunga Vila, Polisi Moro, sijui vibende gani wenzenu huko mkiani mnashangilia usiku kucha? Iweje Yanga ifunge mabingwa wa Comoro muzuie watu kufurahi?

    Mbona Stars ilifungwa na Somalia juzi. Somalia na hawa wacomoro wana tofauti gani. Ningewalewa Kama yanga ingefungwa, kutosha sare au kupanda ushindi wa mbinde. Lakini walichofanya ni kuonesha kuwa Yanga haiko level moja na hii timu ya Comoro wala na Simba, ndo maana kuna tofauti ya point 16, na Thimba haishiriki hata mashindano ya chandimu nje ya nchi.

    Kwaherini!

    ReplyDelete
  25. Anonys wa February 01, 2009 5:28 PM na February 01, 2009 8:34 PM, Manji's Army ni kutokana na uelewa wa wapenzi wa Yanga na majina kama hayo yako traced back to North and South Amerika. Wale traveling fans wa timu ya taifa ya USA wanajiita "Sam's Army". Vile vile, wale wapenzi lukuki wa timu ya Boca Juniors ya Argentina nao wanajina lao "Bosteros" vilevile hasa wakiwa katika uwanja wao wa nyumbani wa La Bombonera.

    Yanga wameleta mfumo huo Afrika Mashariki! Yanga Bomba na Manji's Army are just fans of Yanga - get a life and lay off them fans!!

    ReplyDelete
  26. ...Acheni kutetea NJAA! Kwa nini iwe Manji's Army? Kwa nini Isiwe MADEGA'S Army ama angalau basi hata JANGWANI'S Army tu? Hio mifano yote uliyotoa hakuna jina la mfadhili hapo! Acheni njaa na kupapatia matajiri!! Uchumi mnao mnaukalia kungoja wafadhili wafedhuli!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...