poleni kwa kazi za kutwa nzima wewe na wadau wengine. Nimatumaini yangu kuwa wewe na wadau wengine mmeshawahi kusikia kwamba kuna generation mpya ya magari, kwamba kuna gari linaloruka kama ndege liko kwenye pipeline linakuja. Jamaa wameshatangaza kulileta sokoni hivi karibuni iwapo majaribio yatafanikiwa.
Mimi mwanzo nilihisi kuwa hiki kitu wenda ikachukua muda mrefu sana kuwa kitu cha kweli lakini mambo yamekuwa mambo. Inawezekana kuna wadau wengine hawajawa na picha kamili jinsi hilo gari lilivyo. Nimeambatanisha baadhi ya picha hapa ili wadau wengine ambao hawajaliona wapate picture how it looks like.
Wadau Hili gari likija huko Bongo itakuaje?. Du! mimi sipati picha, itakuwa noma. Nahisi kama patakuwa hapatoshi kwa jinsi tunavyojua kushangaa.
Mdau
Cardiff
Mdau
Cardiff
kazi wese likuishie huko juu
ReplyDeleteEEE MUNGU NIPE MAISHA MAREFU NIWEZE KUYAONA HAYA MAAJABU LIVE. LAKINI SWALA LA AJALI HAPO SI NI NOMA SANA KULIKO MAGARI YANAYOPITA BARABARANI? HAPO NI WAPI NI MAREKANI NINI?
ReplyDeleteHapo powa hakuna kupigwa bao na wapenda rushwa hahaha
ReplyDeleteNi kitu poa sana, manake ukiwa katikati ya foleni kama vp unachelewa unaamua kupaa tu. Ila kukimiliki sijui inabidi uwe na leseni class gani ya udereva/pilot au??? na ukishapaa angani kuhusu kutua inakuwaje? manake barabara za Bongo...mh
ReplyDeleteHao wazungu nao sasa wanazidisha, it's either ndege or gari period! Kutaka kuongeza msongamano tu na hewani nako...ebo..
ReplyDeleteebo kweli hii ni noma! safi sana
ReplyDeletesafi sana
ReplyDeleteKwavile barabara za bongo zimejaa msongomano ukitaka kwenda airport inabidi ukashukie mbagala au kibaha ndio upate kuingia airport na huko juu isje ikatokea siku ikakutana uso kwa macho na twiga mnyonge wetu kimeo (TANZANIA AIR)manaake sijui hata kama hio tanzania air hata breki inazo ni EKSIDENT TU ZIKIKUTANA ANGANI HUKO
ReplyDeletekweli technology inakua!!!DUH!!!Sayansi jamani!!nawashauri madenti msiogope masomo ya sayansi mtagundua zaidi ya hii!!
ReplyDeleteJamani heshimuni mawazo yenu na ikibidi yatafutiwe hati miliki.Mimi kuna siku nilikwama kwenye foleni Jangwani mwaka 2005 nikawa nawaza hivi haiwezekani kweli kutengeneza gari linalopaa angani watu tukaondokana na adha ya foleni,leo nimeshangaa kuona kile nilichokuwa nakiwaza kimetendeka...inashangaza sana!!!!!
ReplyDeleteSasa tutahitaji trafiki wa angani hakyababa..
ReplyDeleteJamani he! naomba niulize sasa zitatuaje!! foleni za bongo, na pia huku uswazi mitaa hata mikokoteni haipiti. he! mi simo!!
ReplyDeletelakini kazuri kwa kukodisha maarusi!
Duh Na- imagine traffick police yuko kwa Parachute afu anakuonya umepita taa Nyekundu barabar...Ooops sorry ..angani. Teh teh teh!
ReplyDeletekwa wale walevi sisi inakuwaje?tunaruhusiwa kuendesha tukiwa mitungi.unatoka mwenge kwenda tegeta unajikuta zanzibar maana ulilala kidogo teh!teh!
ReplyDeletenimesikia hiki kidude kama kipo juu mafuta yakwisha kinakulazimisha kutua, kama mkao wa parachuti.
ReplyDeleteLINK YA HIYO GARI NI http://uk.cars.yahoo.com/12012009/36/flying-car-takes-skies-0.html
ReplyDeletewe francis kinakulazimisha kutua!!sipati picha iwapo upo katikati ya jangwa ambalo limepigwa moto moshi unafuka kote!!!! nawe inakubidi utua!
ReplyDelete