Bro Michuzi Balozi wa Naniihii..,
poleni kwa kazi za kutwa nzima wewe na wadau wengine. Nimatumaini yangu kuwa wewe na wadau wengine mmeshawahi kusikia kwamba kuna generation mpya ya magari, kwamba kuna gari linaloruka kama ndege liko kwenye pipeline linakuja. Jamaa wameshatangaza kulileta sokoni hivi karibuni iwapo majaribio yatafanikiwa.
Mimi mwanzo nilihisi kuwa hiki kitu wenda ikachukua muda mrefu sana kuwa kitu cha kweli lakini mambo yamekuwa mambo. Inawezekana kuna wadau wengine hawajawa na picha kamili jinsi hilo gari lilivyo. Nimeambatanisha baadhi ya picha hapa ili wadau wengine ambao hawajaliona wapate picture how it looks like.
Wadau Hili gari likija huko Bongo itakuaje?. Du! mimi sipati picha, itakuwa noma. Nahisi kama patakuwa hapatoshi kwa jinsi tunavyojua kushangaa.

Mdau
Cardiff

kikiwa kimepaki nyumbani kwa balozi wa nanihiii...
kikiwa sheli kupata wese
hicho angani. wenye vibabajaji wa mwenge na tabata mbona watatukoma...




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. kazi wese likuishie huko juu

    ReplyDelete
  2. EEE MUNGU NIPE MAISHA MAREFU NIWEZE KUYAONA HAYA MAAJABU LIVE. LAKINI SWALA LA AJALI HAPO SI NI NOMA SANA KULIKO MAGARI YANAYOPITA BARABARANI? HAPO NI WAPI NI MAREKANI NINI?

    ReplyDelete
  3. Hapo powa hakuna kupigwa bao na wapenda rushwa hahaha

    ReplyDelete
  4. Ni kitu poa sana, manake ukiwa katikati ya foleni kama vp unachelewa unaamua kupaa tu. Ila kukimiliki sijui inabidi uwe na leseni class gani ya udereva/pilot au??? na ukishapaa angani kuhusu kutua inakuwaje? manake barabara za Bongo...mh

    ReplyDelete
  5. Hao wazungu nao sasa wanazidisha, it's either ndege or gari period! Kutaka kuongeza msongamano tu na hewani nako...ebo..

    ReplyDelete
  6. ebo kweli hii ni noma! safi sana

    ReplyDelete
  7. safi sana

    ReplyDelete
  8. Kwavile barabara za bongo zimejaa msongomano ukitaka kwenda airport inabidi ukashukie mbagala au kibaha ndio upate kuingia airport na huko juu isje ikatokea siku ikakutana uso kwa macho na twiga mnyonge wetu kimeo (TANZANIA AIR)manaake sijui hata kama hio tanzania air hata breki inazo ni EKSIDENT TU ZIKIKUTANA ANGANI HUKO

    ReplyDelete
  9. kweli technology inakua!!!DUH!!!Sayansi jamani!!nawashauri madenti msiogope masomo ya sayansi mtagundua zaidi ya hii!!

    ReplyDelete
  10. Jamani heshimuni mawazo yenu na ikibidi yatafutiwe hati miliki.Mimi kuna siku nilikwama kwenye foleni Jangwani mwaka 2005 nikawa nawaza hivi haiwezekani kweli kutengeneza gari linalopaa angani watu tukaondokana na adha ya foleni,leo nimeshangaa kuona kile nilichokuwa nakiwaza kimetendeka...inashangaza sana!!!!!

    ReplyDelete
  11. Sasa tutahitaji trafiki wa angani hakyababa..

    ReplyDelete
  12. Jamani he! naomba niulize sasa zitatuaje!! foleni za bongo, na pia huku uswazi mitaa hata mikokoteni haipiti. he! mi simo!!

    lakini kazuri kwa kukodisha maarusi!

    ReplyDelete
  13. Duh Na- imagine traffick police yuko kwa Parachute afu anakuonya umepita taa Nyekundu barabar...Ooops sorry ..angani. Teh teh teh!

    ReplyDelete
  14. kwa wale walevi sisi inakuwaje?tunaruhusiwa kuendesha tukiwa mitungi.unatoka mwenge kwenda tegeta unajikuta zanzibar maana ulilala kidogo teh!teh!

    ReplyDelete
  15. nimesikia hiki kidude kama kipo juu mafuta yakwisha kinakulazimisha kutua, kama mkao wa parachuti.

    ReplyDelete
  16. LINK YA HIYO GARI NI http://uk.cars.yahoo.com/12012009/36/flying-car-takes-skies-0.html

    ReplyDelete
  17. we francis kinakulazimisha kutua!!sipati picha iwapo upo katikati ya jangwa ambalo limepigwa moto moshi unafuka kote!!!! nawe inakubidi utua!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...