Pole na mihangaiko ya kila siku ya kutu Update!
Natumaini u mzima kabisa!Mimi ni mdau mkubwa sana wa Blog yako kutoka A-taun!Nimependa kuwapa hii na nyie wa mijini mjionee wenyewe!Kwa Picha kidogo najitahidi! Bongo tuko juu!
Mdau Noel Otaro



A-taun

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. VIVUTIO kweli vipo. lakini sioni kama ni jambo la kujivunia sana.

    ...hatusafirishi maua wala matunda ya kutosha kwenda nje. achilia mbali ngozi .

    Nchi kama Ghana wanahaki ya kujivunia mali asili yao kuliko sisi kwa sababu manufaa yanaonekana .

    Mandhari nzuri ya hiyo picha yanamnufaisha vipi mwana kijiji hapo porini?

    ReplyDelete
  2. Bongo tuko JUU kwa vivutio vinavyo wanufaisha mafisadi

    ReplyDelete
  3. HIVI NI VIVUTIO VA KITALII NA VITANUFAISHA WANAVIJIJI KWA NJIA NYINGI MNO NITAKUPA MFANO MMOJA PORTER WA MLIMA KILIMANJARO WAMENUFAIKA KWA KUPATA KAZI VINGINEVO WANGEKUWA WEZI NA WAKAJA KUKUIBIA WEWE UNAYESEMA MWANA KIJIJI WA PORINI ATANUFAIKA VIPI KUANZIA WEWE MWENYEWE LAZIMA UTUMIE AKILI KUJINUFAISHA KWA WATALII WANAO KUJA HAPO SIO UNABWETEKA TU NA KULAUMU SERIKALI MFANO MWENGINE UNAWEZA KUTENGENEZA AINA YA VITU UKAVIUZA KWA WATALII WANAOKUJA HAPO AU UNAWEZA KUVAA KIMASAI UPIGE NAO PICHA WAKULIPE. YAPO MANUFAA MENGI SANA KAMA UNA AKILI YA MAISHA.KUMBE UNAJUA KUNA SOKO LA MATUNDA NA MAUA NJE MBONA HULIMI? UYAPELEKE NJE?UNASUBIRI NANI ALIME AKUPELEKEE SIKU NJEMA HAYO NDO YANGU KWA LEO MDAU WAPORINI WINELAND

    ReplyDelete
  4. Mdau Noel Otaro, hapo ni wapi? ni katika mlima gani? ni kweli mdau wa 28feb2009, 11:05am,watu hawajishughulishi, wanataka sijui nani afanye wenyewe ni kulalamika tuu,

    ReplyDelete
  5. samahani naomba ufafanuzi hio picha ya kwanza kama bwawa la maji ni kitu gani na ni wapi hapo i mean jinaz

    ReplyDelete
  6. lovely pics... Mdau A taun tuletee Meru ukiwa na barafu... i saw that once ilikuwa phenomenal!

    ReplyDelete
  7. SAFI SANA ULIYELETA PICHA HIYO KWA MISUPU, UMETEKELEZA WAJIBU WAKO KAMA MTANZANIA MWENYE AMPENDO NA NCHI YAKE.MUNGU AKUTANGULIE ,HIYO NDO TANZANIA ITAKAYOJENGWA NA WATANZANIA WENYE MOYO.
    TANZANIA NZURI,JAPO WATU WAKE WAMEKATA TAMAA.
    MSIKATE TAMAA,MAISHA YAPO TANZANIA,TUSIWE WAZEMBE WA KUFIKIRI.

    ReplyDelete
  8. Huwa nasikitishwa na maoni ya baadhi ya watu kwamba Watanzania hawataki kujishughulisha. Nenda kwenye kijiji chochote Tanzania utakuta wenyeji wanalima kama hawana akili nzuri kwa kutumia jembe tulilorithi kutoka kwa Adamu na Eva. Watu wako tayari kufanya kazi. Tatizo ni kuwa wanaojua kwamba tunaweza kuuza maua nje ama hawataki au hawawezi kulima maua hayo. Nao ndugu zetu wanaolima kwa bidii vijijini wanalima kwa mazoea. Sehemu inaweza kufaa kulima dengu lakini watalima mahindi kwa sababu ndicho walichozoea kulima. Mabwana shamba na mabibi mifugo wote wako mijini ambako hakuna sehemu yenye shamba. Magazeti ya ukulima wa kisasa hayapatikani tena. Hata yakipatikana watu wengi zaidi hawajui kusoma. Tunahitaji kufanyia kazi elimu ili tuweze kutumia vizuri raslimali zetu kujiletea maendeleo ya kweli kuliko kuvaa kimasai ili tupige picha na wazungu.

    ReplyDelete
  9. Hilo ni bwawa la maini au?

    ReplyDelete
  10. REMEMBER ..
    UCHUMI TUNAO ILA TUMEUKALIA....

    ReplyDelete
  11. watu wengine bana, wewe unatuwekea picha halafu husemi ni wapi, unakuwa useless

    ReplyDelete
  12. Wafanya biashara wa utalii/tour operators jitahidini ku organize safari ambazo mtalii atakuja Tanzania Apokelewe Airport na atembezwe mahali mkubaliane na mtalii kabla hajaja nchini achague sehemu za kutembelea na bei iwekwe wazi.Na hata kutembezwa vijijini au mijini ktk nyumba za kale au vivutio vya utalii. Tuko nyuma sana kwa hilo kwani watalii hawapendi kutembea na pesa nyingi na pia mtu ajue toka atokako kuwa anakuja Tanzania kutembelea sehemu ipi na ipi. Sehemu nyingi za vivutio vya utalii hazijulikani au kutambulika kutokana na sisi wenyewe kuzembea kuwatembeza wageni wetu. Na wenyeji pia hatuzijui/hatuna historia za sehemu nyingi za nchi yetu.
    Kwa kifupi biashara ni matangazo. Usipojitangaza nani atakujua au kukusikia? Matokeo yake tunalalamika ooh wakenya wanatutumia. Tujiulize hao wakenya wanatumia mbinu gani kupata watalii? Tuake sasa.
    C3

    ReplyDelete
  13. Kwa wale msiojuwa jiografia kidogo huu ni Mlima Oldonyo Lengai. Samahani kama nimekosea Spelling maana jina lipo katika Lugha(kimasai) ya watu na si kiswahili tulichokizoea.Na mimi nimeishia Darasa la 4,Sijasoma spelling za Lugha kubwa duniani ya Kabila la Wamasai.

    ReplyDelete
  14. Kwa kuongezea hiyo unayoiona katika picha ya kwanza ni Live Lava sema haina nguvu ku over flow na kuleta athari kwa wananchi waishio ktk maeneo hayo.Kama kuna mwingine anayeweza kuelezea vizuri aendelee.

    ReplyDelete
  15. live lava??maskini hata wewe mwenyewe ulieiona huijui sasa sie unaotuonyesha hizo picha tutaringishia vipi?tukiulizwa ni kitu gani na kinaitwaje tusemeje?swimming pool au ziwa victoria??mi nitaitungia maelezo yangu ninayoyajua mimi tu hii picha kwamba hilo ni ziwa victoria lipo kando ya mlima kilimanjaro

    ReplyDelete
  16. Bora video ya 'Msimu kwa Msimu' ya vijana wa Arusha kwa jina Xplastaz ktk www.YouTube.com

    au vijana wengine wa Arusha jina la video 'Arusha JCB and all stars' ktk www.YouTube.com vina maelezo kamili juu ya mazingira waliyofanyia shooting ya video.

    Huyu Mdau aliyeleta hii picha isiyo na maelezo kwa wadau, halafu Kenya wakisema hii picha ya crater juu ya mlima ipo kwao Loitoktok wabongo tuna piga kelele.

    ReplyDelete
  17. Mbigiri - live lava, in blue????? That looks like crater lake (Lake Ngozi?)in Mbeya region. I wanted to say Lake Momela in Arusha national park or Lake Duluti, which are all crater lakes, but that's are not them.

    ReplyDelete
  18. Hiyo ya mlima ni mlima Oldonyo Sambu upo umasaini Arusha ukiwa unaenda Mererani mwendo wa dakika kadhaa kutoka Tengeru ukitazama kushoto utauona. Hiyo ya kama kimto ni Ngorongoro Crater ipo katika hifadhi ya Ngorongoro.

    Jamana utalii sio kwa ajili ya wazungu tu! hata sisi pia tunastahili kutaliaa na TANAPA kwa kujua hilo wamepanga bei ndogo sana kwa watalii wa ndani mfano kutoka Arusha kwenda kutalii Ngorongoro kwa mbongo haifiki hata laki!!! tusiwe wageni kwenye nchi yetu!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...