AMATUS LIYUMBA

HABARI ZINASEMA KWAMBA, AMATUS LIYUMBA, MMOJA WA WASHTAKIWA WA KESI YA WALIOKUWA MAOFISA WAANDAMIZI WA BOT WANAOKABILIWA NA MASHTAKA KADHAA KUHUSIANA NA GHARAMA ZA UJENZI WA MAJENGO PACHA A.K.A TWIN TOWERS, HAJULIKANI ALIKO.

HABARI HIZO ZA UHAKIKA ZINASEMA WADHAMINI WAKE WAWILI AMBAO WALIMDHAMINI ILI AWE NJE WAKATI KESI INAENDELEA WAMETIWA MATATANI. WAMEAMRIWA KURIPOTI OFISI ZA TAKUKURU ASUBUHI.

KISHERIA ENDAPO MSHATAKIWA ATAINGIA MITINI MDHAMINI INAWAJIBIKA MOJA KWA MOJA PAMOJA NA MALI AMA PESA KUCHUKULIWA.

LIYUMBA HAKUONEKANA MAHAKAMANI LEO KAMA ALIVYOTAKIWA, NA ALIPOFUATWA NYUMBANI KWAKE HAKUONEKANA NA KILA JUHUDU ZA KUWASILIANA NAYE ZIMESHI NDIKANA.

KWA HABARI KAMILI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 70 mpaka sasa

  1. du kakiona cha moto gerezani kaamua kuchepa na unajua katoa passport iliyo kwisha inaelekea ana nyengine valid hii kali waliokuwa nje ya nchi kaeni macho lazima atakuwa kazama out of contry must

    ReplyDelete
  2. mahakama ndipo pahala pa kuonyesha umma kuwa haki iko wapi, na nani anasema ukweli na nani anaongopa,

    kama liyumba anaiogopa mahakama basi wenye macho ya kutazama na wenye kujuwa mantiki mtafahamu mbivu na mbichi.

    wenye masikio na wasikie.

    ReplyDelete
  3. WIZI MTUPU!

    ReplyDelete
  4. Bwana Michuzi acha utani bwana! Si tuliambiwa Serikali ina mkono mrefu?? April Mosi bado

    ReplyDelete
  5. aisee! kweli hii nayo ni break news. mtu mwenyewe dhamana yake aliyotolewa nayo ina utata kwa nini asitokomee anakojua yeye.

    ReplyDelete
  6. HALAFU SAMUELI SITTA AKISEMA MAHAKAMA IMEJAA RUSHWA NA HAITENDI KAZI YAKE SAWASAWA MNAMSHANGAA. HAYA SASA. ANGALIENI UJINGA ULIOFANYIKA MPAKA LIYUMBA AKAISHIA. NCHI HII UPUMBAFF MTUPU.

    ReplyDelete
  7. Ahhh jamani kaenda nyumbani I mean kuleeeeee kwa babu kutambikiwa na kufanyiwa dawa kidogo si mnajua tena hii issue ni nzito.Hajakimbia wala nini bado yupo yupo ila anajipanga tu.

    ReplyDelete
  8. Mbingu ni zako ee bwana na nchi ni yako,
    Ndiwe uliyeumba binadamu na kila kitu
    kilichomo!

    Ndiye wewe mtawala pekee
    Mwenye enzi na enzi,
    Peke yako wastahili kuabudiwa!

    Ninaagiza nguvu zako toka Mashariki
    Na uweza wako toka Magharibi,
    Ninaita upepo na moto, mvua na radi
    Ninaita kisulisuli na kimbunga
    Ninaita nguvu zote za asili ya ulimwengu,
    Na nguvu zote ulizoziumba

    Zile njama mara hii tena
    Mara hii zikubaliane
    Na mara hii tena zikutane
    Na kufanya kila mpango wa Liyumba kuporomoka na kuvunjika
    Ndani ya masaa 24 kuanzia sasa awe mbaroni au ajisalimishe mwenyewe

    Kwani kuanzia sasa yeyote atakayemsaidia au anayemsaidia kutoroka
    Napandikiza laana kwake kwa ajili ya roho za watu wote ambao
    kutokana na Liyumba au washirika wake au watuhumiwa wengine
    wenye mipango kama yake wamepata madhara yoyote yale!

    Ninamuita Dubu, na ninamuita Leo
    Ninawaita mashujaa wa kale
    Wala njama wa milele
    Kwa pamoja wanyanyuke na kuweka pingamizi!
    Ili haki itendeke!

    Kwa jina lake yeye ambaye aliyeko, aliyekuwako na anayekuja!

    Na hili nalo litakuwa Ushuhuda!

    ReplyDelete
  9. Hee jamani, mbona kawatia kwenye mkenge walomdhamini?

    ReplyDelete
  10. WIZI MTUPU!!!

    ReplyDelete
  11. ndio mlioyataka hayo.wewe toka lini kesi la billioni 200 mtu akapewa dhamana.mahakama ina haki ya kukataa kutoa dhamana sio mnaendekeza upumbavu.sasa hela hio hio iliopotea ndio katumia kidogo kujiekea dhamana na kashatoeka anaenda kula maisha na fungu lilobaki.nchi inaongozwa na vichwa vya mwendawazimu tatizo.
    mdau "cha mtu mavi"

    ReplyDelete
  12. huyu ni jambazi kabisa....

    ReplyDelete
  13. ha ha ha ha huyo yuko so guilty sidhani kuwa atakua na cha kujitetea wakimshika bond yake ilikua ngapi? itatusaidia kurepair mahakama zetu kwavile hela aliyoiba ukweli hatutaipata tena

    ReplyDelete
  14. boss wake alifia ughaibuni na akazikwa hukohuko,yeye katoweka.nilijua tu ule mchezo wa mahakamani eti passport ya liyumba ime expire tangia 2007,jamani lets be REALISTIC for a minute,mtu kama liyumba atakosa passport kweli.,yupo nairobi sasa hivi boarding next flight to london..haha bongo tambarare for sure.

    ReplyDelete
  15. Jamaa tumemwona hapa Swiss ametulia tulii

    ReplyDelete
  16. Sasa kasheshe FISADI kaingia mitini! Twafwaaa maana kamjamaa katasambaa kweli.
    Nasikia PP alipinga na kwamba iliwasilishwa passport kimeo ie out of date, dhamana kiduchuuu. Huyu kama katoweka kweli ni mwizi aliyekubuhu.
    Hapo sasa sirikali ionyeshe umahiri wake kwa kumrejesha mapema apelekwe SEGEREA sasa. kwanza miezi sita ya chai ya kukimbia chini ya dhamana na kisha kesi palepale.

    Wadau tutoe ushirikiano apatikane huyu FISADI
    Kila la heri Jamhuri dhidi ya Mwizi mzoefu.
    Mdau Oslo, Norway

    ReplyDelete
  17. TANZANIA.. ARE WE STUPID!!!!!; Mahakama itarusu vipi mshtakiwa asalimishe PASSPORT iliyoEXPIRE?
    Mdau Bremen.

    ReplyDelete
  18. Hili Deal, Jamaa atakuwa alishakula mpango na wadhamini amewamegea pesa iliyowekwa kwa ajili ya dhamana mahakama wanayo tayari, jamaa mitini, alafu watalipa, mil.55 ni nini ukifananisha na mabilioni waliyovuna. Hakimu alikuwa sahihi kuwa huyu Jamaa alipe zaidi ya Bilioni kadhaa.

    Malawi, Zambia, Kongo huhitaji Pasport Kuingia huko kuna mipenyo kibao.... alafu Kupata pasport kwa mwenye pesa sio shida anaweza hata akawa na kitambulisho cha Botswana saa hizi au hata Marekani inawezekana.

    Kwanini hawa hawashitakiwi kwa sheria ya uhujumu uchumi hakuna Dhamana, Sokoine as right.

    ReplyDelete
  19. Yaaaaaani... WE ACHA TU!

    Hii ngoma imeona JMK is for REAL, akaamua mhn, wacha nile ndogo~ndogo (kuondoka bila kuaga)


    = = =
    Buffalo,
    New York (kule ndege ilipoanguka na kuungua)

    ReplyDelete
  20. Isiwe tabu ata mimi ningeanza, mfumo wet wa maisha ndio unasabisha wizi. Kuna wakati kulikuwa hakuna mikopo kwa mfano kama ilivyokuwa THB lakini kulikuwa na mashindano ya kuporomosha majumba. Hata chizi anajua kwa mijumba hiyo hakuna mshahara unaotosha! asilimia yetu kubwa ni wezi na hiyo ndio njia ya maendeleo. Usipoiba unachekwa

    ReplyDelete
  21. DUH....!!
    Kuna harufu ya mchanga wa macho hapa.Mara tututasikia ooh..yuko ughaibuni taaban,mara ooo ametutoka kama balali.Haya ngoja tuone, tena tunasikia hata masharti ya dhamana hakutimiza.Vijisent alivyotoa ni pungufu ya dhamana aliyotakiwa kulipa..

    ReplyDelete
  22. Aisee hapa ndio unagundua kuwa huyu jamaa ni fisadi,kwa kujiuliza kwa nini kakimbia?? Yaani ameipa serikali hasara ya mamilioni na sasa ameamua kuwageuka hata watu waliomsaidia. Kweli jamaa noma.

    ReplyDelete
  23. Haya ndiyo yale yale ya Balali..tutasikia amekufa na amezikwa huko huko mafichoni. Kumbe anakula raha na mzee Balali kwenye Island fulani..Kweli Bongo tambalale

    ReplyDelete
  24. Hivi hakimu alipopokea passport iliyo"expire" alitegemea nini ?! Hiyo Mali isiyo hamishika ya millioni 800 ukilinganisha na Billioni 50 ni nini? hata mkichukua hizo yeye hajali,pengine alizonazo ni nyingi zaidi, Labda 10Bil hivi, maisha yanakwenda.Duh sijui tutaacha lini kuwa kichwa cha mwenda wazimu ? Kila mtu anafanyia mazoezi yake hapo>

    ReplyDelete
  25. Kaenda kwa Sangoma huyo ndo hamumuoni tena Ng'oooo !!

    ReplyDelete
  26. Huu ni ujinga na utoto.

    ReplyDelete
  27. Atakimbilia wapi wewe kwenye hiki kijiji???!!! Atapatikana tu labda ajifie ka bosi wake na hapo tutafunga kaburi munyororo.....
    Na sasa kajiongezea kosa....Kudharau mahakama.
    Mzawa

    ReplyDelete
  28. HIOOOOOO MIBONGO MIZUMBU KUKU KILA SIKU WANACHEZEWA TU NA MTAENDELEA KUIBIWA MPAKA KIAMA.WATU WAMECHONGA DILI HAO NYINYI.TOKA LINI MAHAKAM IKAPOKEA PASSPORT ILIO EXPIRE? MTAENDELEA KUFISADIWA MPAKA KIAMA.

    ReplyDelete
  29. Hivi jamani huu ufisadi wa kuijumu nchi utaisha lini???? mbona tunaliangusha taifa!! yanaonekana mataifa masikin, kumbe watu wachache wanajichotea mahela kwa utajili wa bandia. ili kujitajirisha na kujilimbikizia mahela kedekede!!! Ina sikitisha nchi inajengwa na wanachi wenyewe! alafu inangushwa na wanachi wenyewe! hebu hamken sio utajili huo ni wizi, tunaibiana wenyewe kwa wenyewe! hizo hela zingejenga mashule, mahosipital,kila siku manasubiri misaada ndio mjengewe!!! watawachoka!!!! ndio maana kila siku yanaitwa mataifa masikini kwa kutokuboresha mfumo wa maisha ya raia wake! vingozi wizi, wanaokabiziwa madaraka wizi!! wizi wizi tu!!!!! watawachoka na hou mnaouta nchi masikini wakati mnajiabisha wenyewe kwa wenyewe mahela kibao sijui ya nini hayo yote! mabilioni na sujui wanataka weashindane na bill gate wawe matajili wa Dunia kwa hela za wizi,manake nchi masikini hayo mahela ameyatoa wapi nae ni mfanyakazi wa kuajiliwa.

    ReplyDelete
  30. Ni mapema mno kusema lolote.

    ReplyDelete
  31. Watanzania Hebu tuamke kutoka usingizini.Hapa kuna harufu ya changa la macho kama wadau waliotangulia walivyosema.Haka ni kamchezo fulani,huyu jamaa hela hajala pekeyake,angekua amekula pekeyake,mambo yangeshamwalibikia zamani sana.
    Dawa ilikua kumtoa na kumpoteza kama hivi alivyopotezwa,kweli kabisa baada ya siku mbili tatu utasikia,aaaah,kwanza si kitu kwa sababu mtu mwenyewe keshakufa.
    Well,mimi nasema usipoziba ufa,hutajenga ukuta.Kwa nini kutokana na somo hili tusikamate RAMBA,YONA,MGONJA NA MAFISADI WOTE WA EPA tukawarudisha Segerea.Je tuna hakika gani kama bado wapo wote hapo nyumbani.Jamani kuna mambo mengine bora usiyajue,unaweza ukaumia roho mpaka ukafa wallahi.

    ReplyDelete
  32. nasikia kutapika!!wizi mtupu!!kweli inasikitisha,kukatisha tamaa na ni huzuni pia kuona wachache wanavyojichukulia pesa bila kuwafikiria wenzao na kuishia kinyemela.sisi tulio nje ya TZ habari hizi zinatukatisha tamaa kabisa mpaka mtu unaona uende nyumabani kufanya nini?bora nibaki huku nikijibebea mabox,nalipa kodi halali na naona inanifaa,na nikikatwa zaidi wananirudishia ile haki yangu, nafarijika.sio bongo ni kuiba kwenda mbeleee!!ooh poor my fellow Tanzanians, tufanyeje?huyu mtu,ukimwi kasambaza, hela kaiba na sasa kaishia. kweli akipatikana afungwe maisha tu.mdau,Oslo.

    ReplyDelete
  33. halafu wabongo ndio wanajiita wajanja

    kila mtu anaigeuza tz kichwa maji....

    mkiambiwa mnasema watu wa nje wanawazarau , wa beba maboxi , hawajui kitu,......

    ReplyDelete
  34. angekuwa uk angepigwa tag ya mguuni kila anapokwenda inajulikana

    ReplyDelete
  35. Huyu jamaa anajidanganya mwenyewe na kutafuta kujiongezea matatizo zaidi. Amewaharibia akina Mramba, Mgonja na Yona. Itabidi dhamana zao zifutwe. Akipatikana mambo yake mazito. Labda afie huko kama Balali.
    Mdau

    ReplyDelete
  36. hapa kuna mchezo mchafu mwingine. huyu jamaa anajua kuchezo rafu za hivyo. huyo hakimu na pp wake wahojiwe. wanajua alipo.

    yaani; pasport expired, dhamana ilitakiwa... ikatolewa ....mmhhhh!!!!wajinga ndio ...

    ReplyDelete
  37. NIKIFANIKIWA KUMLETA UKU USA MAMAYANGU BASI, SITA JIUMIZA TENA KICHWA KWA KUSOMA UPUMBAVU WA TANZANIA

    ReplyDelete
  38. Wananchi acheni kusheherekea ya wenzenu wakati yenu yanawashinda, kama kala hizo pesa ajala peke yake na inajulikana kabisa kuna vigogo wameshiriki kwa hiyo kama katimua ni sawa tu, kwa nini aumie peke yake wakati wengine bado wanapeta? Hata kama aliajiriwa anapewa maagizo na yeye anajichotea chake kidogo afanyeje.

    ReplyDelete
  39. Too Good to Be True

    ReplyDelete
  40. @ anon, feb.19; 6:30pm

    In Jesus Name, Amen

    ReplyDelete
  41. LIUMBA YUPO MALAYSIA NIMEMWONA LEO ASUBUHI,ANAISHI CYBERJAYA SEMA SIJAJUA NI NYUMBA GANI

    ReplyDelete
  42. Safi sana.

    ReplyDelete
  43. MKUU WA WILAYA MI KWA MACHO YANGU NIMEMWONA SEHEMU FULANI HAPO MOSHI SITAKI KUSPECIFY ILA KWA ANAYETAKA KUJUA NILIPOMWONA TUWASILIANE KWENYE NAMBA 0715 575 1768. kutajana majina hakuna

    ReplyDelete
  44. I HATE TANZANIAN GOVERNMENT AND SYSTEM!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  45. bora nijichukulie uraia wa kijerumani maana there is no meaning of kuwa mlipa kodi halafu huoni matunda yake.
    ni bora kubaki hukuhuku tutakuja kutembea tu huko ufisadini...
    mdau Technischen Universität Berlin

    ReplyDelete
  46. HUU NI MPANGO ULIOFANYWA NA SYSTEM NZIMA BINAFSI NAICHUKIA SANA SERIKALI YANGU KWANI UOZO MWINGI UNAFANYIKA AS IF SISI WATANZANIA WOOTE NI WATOTO WADOGO. JK JITAHIDI NA TEAM YAKO NZIMA KUBADILISHA HALI TULIYONAYO SASA YA KILA MTU AKIINGIA KWENYE SYSTEM NIKUJICHOTEA CHAKE. BINAFSI NIMEANZAKUFIKIRIA KWAMBA MOJA YA MAMBO YANAYOWAFANYA WATU KUKWEPA SANA KODI HAPA TZ NI HII HALI YA WATU KUKUSANYA KODI ILI WAGAWANE WACHACHE. NAICHUKIA SANA TANZANIA.

    ReplyDelete
  47. Nyie mnaosema mmemuona, this's not a laughing matter, it's a shame to our government.
    Be serious people.

    ReplyDelete
  48. Tanzania nakupenda kwa moyo wangu wote,lakini mambo yanavyoendelea inatia aibu! Naona hata uvivu kuitwa mtanzania,nchi inaelekea wapi jamani? WIZI MTUPU!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  49. hivi watanzania tutafanywa wajinga mpaka lini?

    kweli tumeamua kuwaacha mafisadi waendeshe nchi wanavyotaka?

    Inauma sana, inauma sana mjomba!

    ReplyDelete
  50. Duu Watu wamemariza hasira zao hapa. KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI?

    ReplyDelete
  51. HIVI KWELI NCHI YETU INA WANASHERIA?? HUYU ALIKIMBILIA MAHAKAMA KUU KUOMBA DHAMANA IPUNGUZWE AKATUPWA, HUYU HAKIMU ALIYEMPUNGUZIA HIYO DHAMANA NAFASI YAKE IKOJE? AMEKULA MLUNGULA? DU!! AMA KWELI SIE WADANGANYIKA!! JAJI MKUU HEBU SHUGHULIKIA HUYO HAKIMU ALIYEPOKEA VIDHIBITI VYA KUCHONGA.

    ReplyDelete
  52. THATS'S WHY I LOVE BONGO!!

    ReplyDelete
  53. Mdau wa Feb 20 12:09am, umewahi kusikia herufi inaitwa R?
    mfano..
    Rafiki sio Lafiki
    Raha sio Laha
    Ringa sio Linga
    Rushwa sio Lushwa.
    Maneno mengine yanayoanza na herufi hiyo ngeni kwako ni pamoja na,
    Roho, Rungu, Rudi, Roho, Riba, Riziki, Rehema, Remba, Redio, Ruksa.
    Halafu English sio ndio itakuwaje sasa... Hee kazi tunayo.

    Tukirudi kwa huyo jangili aliyetuibia pesa zetu, ni fala gani aliyemkubalia dhamana? kweli nchi imeoza.

    Mdau, Boston, US

    ReplyDelete
  54. HIYO PESA ILIYOTOWEKA NI NYINGI SANA.HAIWEZEKANI HATA KIDOGO HUO WIZI KUWA WA MTU MMOJA.UKWELI NI KWAMBA PESA HIYO ILIIBIWA KWA KUSHIRIKIANA NA VIGOGO WAZITO SANA,NA HAO NDIO WAMECHEZESHA HUO MCHEZO WA KUMTOROSHA MSHATAKIWA,KWANI ANGEWATAJA NAKUTOA USHAHIDI.BADO MKAPA ATASHUKIWA HATA KWENYE HII DEAL!!!
    ILI KUUWA USHAHIDI AMEPAKIWA KWENYE PRIVATE JET,KAONDOKA NA PASSPORT YA MALAWI.ATAKUWEPO KWENYE VISIWA VYA BAHARI YA HINDI ANAKULA UPEPO.HAWEZI KWENDA MAREKANI WALA ULAYA.HII NDIO NCHI YA WAJINGA NA HAKUNA NCHI YENYE WAJINGA WENGI DUNIANI KAMA HII.KUMBUKENI CHARLES TAYLOR ALIPOTOKOMEA NIGERIA.BUSH AKAPIGA MKWARA TOSHA, BASI JAMAA WALIMTOA BAADA YA MASAA MAWILI NA HAO WALIKUWA NI SERIKALI YA NIGERIA WALIO KUWA WAMEMFICHA.KWA HIYO BASI WANANCHI WA BONGO WAKIENDA BARABARANI JAMAA ATAPATIKANA TU,LASIVYO IMETOKA HIYO!!!

    ReplyDelete
  55. bora jk ampishe mkuu wa wilaya wa zamani pale bukoba, "kanali" mnali aje achalaze bakora, maana yeye anapita kila wizara kucheka cheka tu, bila bakora nchi hii mambo hayaendi.

    ReplyDelete
  56. ANYWAY TIME WILL TELL.....YANA MWISHO HAYA.....WALA MSIKONDE WATANZANIA, HIZO PESA WANAZOCHUKUA SIO MSAADA KWAO NI LAANA TUPU....

    ONE DAY YES TUTAPATA KIONGOZI BORA...DAMU ZINAMWAGIKA HOSPITALINI KWA KUTOKUWA NA HUDUMA BORA...BARABARANI KUTOKUWA NA MIUNDO MBINU BORA...JAMANI..YAANI UKIENDA SIO MBALI TU KWA JIRANI ZETU HAPA AFRICA UNAWEZA UKATOA MACHOZI...UKIONA MAISHA YAO....PURCHASING POWER IS UP...MADUKA YAMEJAA WATU..HOSPITALINI HUDUMA ZA KUTOSHA, BARABARA NDIO USISEME....SASA SIJUI SIE TUMELAANIWA.....

    ReplyDelete
  57. We anonymous wa 12:12 pm hata mimi nakunga mkono kwa wazo lako! yule jamaa kanali Mnali aludishwe tu kwenye madaraka! na ikiwezekana agombee urais! nchi itakua safi kabisa na poa! manake jamma hana mchezo! nakwambia wanatakiwa watu kama hao! WAKINA KANALI MNALI ili nchi ikae vizuri! WIZI WOTE HUTAISHA! HANA MCHEZO KANALI MANALI BWANA.

    ReplyDelete
  58. I hate the saying that you can not point fingers at somebody as you yourself is doing the same thing, we should be condemning the behaviour and at the same time learn form others payments!!
    It is no use to keep silent just because you once did it in smaller version.

    ReplyDelete
  59. ni kweli hii issue ni kama ya balali .................na huyu anaenda kutulia zake marekaniiiiiiii

    basi lowasa walimwonea tuuuuuuu

    kwa sababu wote wizi mtupu......ila hawa mafisadi wanatufilisi sana wanakula hela zetu za kodi wakati watu tunakosa hata mlo wa siku

    madau netherlands

    ReplyDelete
  60. nakuunga mkono we anon hapo juu. kanali Mnali anafaa sana kurekebisha nchi. hii mambo ya kuchekeana mpaka lini. tandika bakora.

    vingine tuige sheria za China. fisadi auawe. piga risasi hao wapumbavu, wauaji wakubwa, wanyonya damu

    ReplyDelete
  61. Nakubaliana na mdau Feb 20, 12:12pm

    ReplyDelete
  62. Hellow Michuzi,

    Hivi wewe Michuzi na utahalamu wako wa Uhandishi wa habari wotw huo haujasikia "Radio Twins Tower" kutoka hapo jijini Dar ,kuwa huya jamaa alifariki ghafla juzi usiku na kuzikwa kwao Huoston ,Texas nchini Marekani...???!!!Na mazishi yake yameuzuliwa na watu mahalamu tena kwa muhariko mahalumu wa mahandishi..!!!.Habari zilizidi kusema kuwa waziri kijana tena msomi amepiga marafuku kuendelea kumjadili huyu bwana,kuwa atakayeendelea kumjadili atakuwa amesaini mwenyewe consent ya kufilisiwa mali zake zooooote...!!(Mpaka nguo).Sasa wewe Michuzi unataka tuendelee kujadili hili suala alafutuje kufilisiwa au...???!!!.

    ReplyDelete
  63. anno "kiu" na feb 19,6.30pm
    katika jina la Yesu na iwe ivyo

    tunasimama!

    ReplyDelete
  64. kakimbia???haonekani??
    acheni mas'hala nyie watu yupo tu habari za kuaminika bado hazijatoka toka PCB,ila izi pesa kala na wakubwa utakuta yeye kala kiduchu simply kapitihsa file,,jamani ma-administrator tuna kazzzzzzzii kweli-kweli boss wako akitaka kula yani either ujivue madaraka-resign or pitisha file lake-afu wapewa "asante"kama kesi ya Zombe vile kwa yule askari "aliyepongezwa kwa kazi zuri adi anashangaa kwa kazi ipi aswa?mana hajawai pewa hongera toka aanze kazi kumbe nae kaunganishwa ktk kesi sasa!!
    sijui sana anyway
    the history will tell

    ReplyDelete
  65. MI NAWAUNGA MKONO HAO JAMAA WA HAPO JUU! JUU YA KANALI MANALI! ANAFAA KUWA KIONGOZI KATIKA. NCHI KAMA HII. JAMAA HANA MCHEZO. WATOTO WAMEFELI AMEGUSWA.NI KWELI KAMA NI WAZEMBE WA KAZI JE. NI FUNDISHO TOSHA WANAFANYA UZEMBE ILI TAIFA LIWE LA WATU MBUMBUMBU! NA ANAFAA SANA KUWA RAISI! KWA KUWA HATAKI UJINGA ANATAKA HAKI NA KAZI ITENDEKE! HAWA MAFISADI WA WIZI NAKWAMBIA WOTE WANGEISHIA. NA NCHI INGEKUA SAFI KABISA NA YENYE MAENDELEO! HUO WIZI MBONA UMEZIDI! MAHELA YOTE HAYO DAAA!!!! HATARI

    ReplyDelete
  66. We anon wa hapo unaesema ujichukulie urai wa german unadhani ndio sifa au umerekebisha! we asili yako itabaki kuwa pale pale Mwafrica na unatokea Tanzania. na isitoshe uko home ndugu zako wote wapo uko. Hapa bwana Ni kurekebisha kuhusu huu WIZI UMEZIDI SANA!!!!!! HUKU HOME KILA SIKU WIZI WIZI! WANAWAPIGA VIBAKA WAKATI WAO WANAKOMBA MAHELA KIBAO!!!! HUYO LYAMBA KIBAKA AKIBWIBIA ATAMPIGA KWELI KWELI!!! TENA BASI HELA NDOGO YA KASIMU ALIKONUNUA!!! ANASAHAU YAKWAMBA ANAWAIBIA WATANZANIA MAHELA KIBAO!!! NOMAA BWAN HAWA WATU SIO WA KUCHEKEWA KABISA

    ReplyDelete
  67. NDIO MAANA MIMI SIRUDI BONGO NGO', HATA WAKINIITA MBEBA BOKSI ALEKUBUHU SIJALI TENA, NATENGENEZA HELA NA KUTUNZA FAMILIA BILA SHIDA, HIZO SHIDA ZA BONGO MIMI SIZIWEZI.
    VIJANA NDIO WANAOTESEKA BONGO, UNATEGEMEA KIONGOZI ULIEMCHAGUA AKUSAIDIE KUMBE MWIZI HALAFU ANALINDWA NA SERIKALI, JE MIMI RAIA WA KAWAIDA NANI ATANILINDA?KAENI NA BONGO ENU HIO IMEJAA MAFISADI, HAKUNA LOLOTE!!

    ReplyDelete
  68. Nahisi siasa sa kenya zinaingia kwetu, sitashangaa kusikia amefariki dunia kwa kujiua!

    ReplyDelete
  69. wewe anonymous nikisema nachukua uraia wa germany ni ili na mimi niexrcise haki zote kama raia wa hapa na of course i will remain mtanzania na mwafrika(a proud one hehe) ila sioni sababu nikimaliza masomo yangu (ambayo sijalipiwa na hao mafisadi ila nimejipinda mwenyewe na tubox hehe)nije huko kulipa tax wakati zinachukuliwa na mafisadi why?si bora niishi maisha kama raia wengine wa nchi zinazojali what it means to be a tax payer?kuna mdau kasema yeye anampeleka mama yake USA hiyo ni decision yake ila mimi kwa sasa bora niishi huku tu nilikuwa nafikiri sana kurudi kufanya kazi huko nimeona opportunities kibao za computer engineers ila na mind vitu vidogo kama hivi kwa hiyo sitaki kukasirika maana walah ningekuwa huko halafu kuna ujinga kama huo unafanyika ningemlipua mtu so bora nibaki huku tu nisahau hayo ma issue ya kifisadi
    pamoja sana!
    mdau berlin

    ReplyDelete
  70. Anon wa 21Feb,2:34 uliesema utachukua uraia wa German napenda sana kukuunga mkono,mimi pia nilikuwa sana na mawazo tofauti wakati nakuja huku nje,lakini baadae nikabadilisha mpango mzima wa kurudi Bongo nilivoona kuwa hali inazidi kuwa worse. Hivo basi mimi sirudi bongo ambako najua nitakuja kuteseka maana nchi imetekwa na wezi watupu, ninaipenda Tanzania lakini kwanini niishi huko wakati sina haki kama Mtanzania, milango pande zote imefungwa, bora kuwa na uraia wa nchi ambazo zinajali haki, nalipa tax na ninakula matunda ake, nathaminiwa kwa jasho langu, Tanzania hathaminiwi mtu, walio na uwezo ndio watakaosurvive Tanzania na si mtu wa kawaida kama mimi, waache waseme wee mpaka wachoke eti ooh mnazikimbia nchi zenu! ukweli uko pale pale kama wewe ni kijana na unataka kupiga hatua katika maisha lazima utakuwa na mawazo kama sisi! Tanzania inatisha sasa hivi, jinafasini sasa kwani hapo baadae itakuwa shida tu, unless waprove mabadiliko. Ilitakiwa sisi vijana ndio tulete mabadiliko kwene nchi zetu, lakini tutaanzia wapi wakati vigogo wote wameng'ang'ania uwizi tu, mimi inaniiuma sana sana.
    Mdau Canada.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...