Wafanyakazi ya Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited wakiwa wamebeba waya (fibre optic cable) kutoka ndani ya meli iliyotia nanga bahari ya Hindi ambao utawekwa katika kituo chao kilichopo Kunduchi Jijini Dar kwa ajili ya kutoa huduma ya network nchini. Toka kulia ni Mkurugenzi wa kampuni hiyo Michael Njumba akifuatiwa na Meneja Mkurugenzi Anna Rupia na kushoto ni Eng. Jon Avery.
Na Anna Nkinda wa Maelezo

Kampuni ya SEACOM Tanzania Limited imeanza kujenga kituo cha waya (Cable) kwa ajili ya kutoa huduma ya network itakayowawezesha wadau wa mawasiliano nchini kupata huduma hiyo kwa gharama nafuu.

Huduma hiyo inatarajia kuanza mapema mwezi wa sita mwaka huu mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa kituo hicho kilichopo Kunduchi jijini Dar es Salaam.

Meneja Mkurugenzi wa kampuni hiyo Anna Rupia ameyasema hayo leo wakati akiongea na waandishi wa habari waliofika katika kituo hicho kuona maendeleo ya ujenzi wa Cable hiyo ambayo itafungwa kutoka bahari ya Hindi na kuunganishwa na vituo vingine.

"Cable hii ya Network kwa upande wa Afrika itaanzia katika vituo vya Afrika ya Kusini, Maputo, Dar es Salaam, Mombasa na Djibout hivyo basi kituo cha Dar es Salaam kitaunganishwa na vituo hivi ", alisema Rupia.

Aliendelea kusema kuwa kwasasa makampuni ya mawasiliano yananunua satelite kwa kipande kimoja cha mega bites (1MBPS) kwa dola za Kimarekani 3000 wakati Kampuni hiyo itakapoanza kutoa huduma watapunguza bei na kuuza kwa dola za kimarekani 100.

Baada ya kumaliza kazi ya kujenga kituo hicho watasambaza network nchi nzima kwa kupitia makampuni mbalimbali za simu ambayo yatasambaza hadi nchi za jirani ambako hakuna bahari kama Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Rwanda, Burundi, Zambia.

Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Michael Njumba alisema kuwa wateja wao watakuwa ni makampuni ya Simu na Internet hivyo basi pale watakapoanza kutoa huduma ni muhimu kwa wateja hao kupunguza bei kwa kuwa watakuwa wamepunguziwa bei ya kununu mega bites.

Mkurugenzi huyo alisema, "tunategemea kuwa ifikapo mwaka 2010 watanzania wengi wataona mashindano ya kombe la Dunia kwa kupitia simu zao za mkononi kwani gharama za simu zitakuwa zimeshuka tofauti na ilivyo sasa".

Aidha Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Teknologia ya Uhandisi na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Leonard Chamuriho alisema kuwa chuo hicho kimepewa bure (STM 11) sawa na Mega Bites 155 (155MB) kwa ajili ya kufundishia wanafunzi.

Kampuni hiyo inafikiria kutoa huduma kama hiyo kwa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa siku za baadaye.

Gharama ya Mradi mzima ambao umeanza mwaka 2006 kwa Afrika ya Mashariki na Kusini ni dola za kimarekani milioni 600 na nia ya mradi huo ni kupunguza gharama za mawasiliano Nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. tatizo nji hii wajanja wanaitafuna kimya kimya, hii kwa kweli ni njia mojawapo ya kupunguza gharama za mawasiliano lakini kwa uroho, kutofikiria mbali na maslahi binafsi wapo wenye mamlaka ya kusimamia hayo yatendeke wataliona hilo kama adui na watakuwa mstari wa mbele kulipinga hili directly au indirectly, kutokuwa na ufahamu tumejikuta tunaiza nchi yetu taratiibu...once Nyerere alikataza uchimbaji wa madini kwa kigezo cha kutokuwa na utaalam na utayari wa kufanya hivyo, wakaja wasiokuwa na uchungu na upeo wa kufikiria wakafungulia matokeo yake nchi inaendelea kubaki na matobo wachache wananeemeka.. watu wa aina hii bado wapo na ndio wanaonitisha kuwa hawatapendezwa na hii fibre optic kwa wana maslahi binafsi katika makampuni ya mawasiliano..

    ReplyDelete
  2. Hii ni habari nzuri sana ila kama madau aliyetangulia hapo juu basi mambo yawe hivyotusifisadishe huu mradi kwa mandeleoyetu wenyewe

    ReplyDelete
  3. If it sounds too good to be true it is probably is!
    Mzawa

    ReplyDelete
  4. Michu!

    Ulivyo iandika habari hii, it is a bit biased, as if hao wakina rupia ndo wanalileta hilo limnyama kwa mara ya kwanza tz au ni kitu kigeni sana tz.

    Fibre optic tz ipo muda mrefu na mimi mwenyewe nimeifanya kazi hiyo almost 10 yrs ago.

    Anyway, ni jambo zuri kuona tunamove, may be tanzania inaweza geuka kuwa CALL CENTRE kwa makampuni makubwa ya kimagharibi katika kutoa huduma kwa wateja kwa bei nafuu.

    ReplyDelete
  5. huduma zitaanza june mwaka huu? mradi umeanza line? yaani baada ya miezi mitano mradi utakuwa umekamilika? ama kweli tanzania ni bongo! anyway good news to all of us

    ReplyDelete
  6. Ni kweli huduma hiyo inaweza kupunguza gharama za mawasiliano kwa kiasi kikubwa sana. Nakumbuka Iran miaka kama nyuma iliyopita baada ya kuanzishwa huduma hiyo simu nje zilishuka kutoka dola mbili kwa dakika mpaka dola senti 15.
    Mlala hoi huenda akafaidika kama mpango huo hautafisadishwa kama mingine.

    ReplyDelete
  7. Nukuu toka Mkutano wa Rais na Wizara ya Mawasiliano:

    Nyingie nyingine ya kuiimarisha kampuni hiyo ni kuipa kampuni hiyo jukumu ya kusimamisha shughuli za Mkongo wa Taifa, ambao utajengwa kwa fedha za mkopo kutoka Jamhuri ya Watu wa China, ikiwa moja ya mafanikio ya ziara ya siku tatu ya Rais wa nchi hiyo, Mheshimiwa Hu Jintao, ambaye aliondoka nchini jana, Jumatatu, Februari 16, 2009. Mkongo huo utagharimu dola za Marekani milioni 180.

    Kwenye mkutano huo wa leo, Rais Kikwete ameelekeza kuundwa kwa kikosikazi cha kuharakisha ujenzi wa Mkongo huo, kujadili na kutoa mapendekezo jinsi Mkongo huo utakavyotumika kunufaisha uchumi na hivyo kutumika katika maendeleo ya jumla nchini.

    “Mkongo huu usiwe tu wa kupunguza gharama za matumizi ya simu za mikononi tu…hili ni jambo zuri lakini ni lazima tuwe na mpango wa jinsi ya kutumia Mkongo huu katika kunufaisha zaidi uchumi wetu na kuwa nyenzo muhimu katika maendeleo ya jumla ya nchi yetu,” ameelekeza Rais Kikwete kwenye mkutano huo.

    VS

    Nukuu ya Mkongo wa kina Njumba

    Naye Mkurugenzi wa kampuni hiyo Michael Njumba alisema kuwa wateja wao watakuwa ni makampuni ya Simu na Internet hivyo basi pale watakapoanza kutoa huduma ni muhimu kwa wateja hao kupunguza bei kwa kuwa watakuwa wamepunguziwa bei ya kununu mega bites.

    Mkurugenzi huyo alisema, "tunategemea kuwa ifikapo mwaka 2010 watanzania wengi wataona mashindano ya kombe la Dunia kwa kupitia simu zao za mkononi kwani gharama za simu zitakuwa zimeshuka tofauti na ilivyo sasa".

    Aidha Mhadhiri na Mkuu wa Idara ya Teknologia ya Uhandisi na Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk. Leonard Chamuriho alisema kuwa chuo hicho kimepewa bure (STM 11) sawa na Mega Bites 155 (155MB) kwa ajili ya kufundishia wanafunzi.

    Kampuni hiyo inafikiria kutoa huduma kama hiyo kwa Chuo Kikuu cha Dodoma kwa siku za baadaye.

    Gharama ya Mradi mzima ambao umeanza mwaka 2006 kwa Afrika ya Mashariki na Kusini ni dola za kimarekani milioni 600 na nia ya mradi huo ni kupunguza gharama za mawasiliano Nchini.

    ReplyDelete
  8. Anony feb 19 1.15pm hapo ni kama kuchanganya machungwa na maembe. mkonga anaongea Rais ni mkonga wa taifa ambao utazunguka mkoa kwa mkoa unaojengwa na na SEACOM una complement mkonga wa Taifa. Mkonga wa Taifa hautaweza kupunguza gharama bila mkonga kama wa Seacom.

    Mfano mzuri ni kufananisha mkonga wa taifa kama mabomba ya maji ndani ya nyumba (full contained)halafu seacom kama pipe za dawasa zinazounganisha maji ktk hayo mabomba. Bila Dawasa mabomba ya ndani ya nyumba yataota kutu tu

    ReplyDelete
  9. We! Congo wana bahari.Bakikusikia bana ba Kin. mi simo!

    ReplyDelete
  10. Afadhali...naona bei pamoja na speed vitakuwa shwari!! Mambo ya ku-download/upload word document kwa nusu saa yataisha na ile issue ya makampuni ya simu/Internet kutupiga na bei za kufa mtu na equipment zao za uongo na ukweli yataisha..wachina nao ni vi-huwaei vyao vitakoma ubishi!! Ikiwezekana mimi najiunga na SEACOM kabisa napata supersonic speed!!

    ReplyDelete
  11. jamani nchi hii ma-engineer wa fani iyo apo wako weeengi sana,,kulikoni ilo dude?
    ivi kwanini tumlipe mzungu billion na tusimpe izo m-Tz?wapo watu waaminifu tu sio mafisadi waweza kabisa kufanya kazi iyo kitaalam kabisa
    sooo stupid

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...