Mh. Balozi,Nimekutana na nakala hii fupi ya mahojiano kati ya mwanadada mchumi mwenye asili ya Zambia, Dambisa Moyo na gazeti la New York Times. Naomba uirushe hewani, wadau wajadiliane na watoe maoni yao juu ya msimamo wa dada Moyo.
Kwa kifupi, anatake misaada kwa serikali za nchi za kiafrika isitishwe, na badala yake, anasema uchumi utakuwa kwa kuwawezesha wajasiriamali. Mahojiano haya yapo katika lugha ya malkia (kiingereza)
-Mdau
----------------------------------------------------------

Q: As a native of Zambia with advanced degrees in public policy and economics from Harvard and Oxford, you are about to publish an attack on Western aid to Africa and its recent glamorization by celebrities. ‘‘Dead Aid,’’ as your book is called, is particularly hard on rock stars. Have you met Bono?

A: I have, yes, at the World Economic Forum in Davos, Switzerland, last year. It was at a party to raise money for Africans, and there were no Africans in the room, except for me.
Q: What do you think of him?
A: I’ll make a general comment about this whole dependence on “celebrities.” I object to this situation as it is right now where they have inadvertently or manipulatively become the spokespeople for the African continent.
Q: You argue in your book that Western aid to Africa has not only perpetuated poverty but also worsened it, and you are perhaps the first African to request in book form that all development aid be halted within five years.

A:Think about it this way — China has 1.3 billion people, only 300 million of whom live like us, if you will, with Western living standards. There are a billion Chinese who are living in substandard conditions. Do you know anybody who feels sorry for China? Nobody.
Q: Maybe that’s because they have so much money that we here in the U.S. are begging the Chinese for loans.

A: Forty years ago, China was poorer than many African countries. Yes, they have money today, but where did that money come from? They built that, they worked very hard to create a situation where they are not dependent on aid.
Q: What do you think has held back Africans?

A: I believe it’s largely aid. You get the corruption — historically, leaders have stolen the money without penalty — and you get the dependency, which kills entrepreneurship. You also disenfranchise African citizens, because the government is beholden to foreign donors and not accountable to its people.
Q: If people want to help out, what do you think they should do with their money if not make donations?

A: Microfinance. Give people jobs. But what if you just want to donate, say, $25?
Go to the Internet and type in Kiva.org, where you can make a loan to an African entrepreneur.
Q: Do you have a financial interest in Kiva?

A: No, except that I’ve made loans through the system. I don’t own a share of Kiva.
Q: You just left your longtime job as a banker for Goldman Sachs in London, where you live. What did you do there, exactly?

A: I worked in the capital markets, helping mostly emerging countries to issue bonds. That’s why I know that that works.
Q: Which countries sought your help?

A: Israel, Turkey and South Africa, primarily.
Q: Why didn’t you get a bond issue going in your native Zambia or other African countries?

A: Many politicians seem to have a lazy muscle. Issuing a bond would require that the president and the cabinet ministers go out and market their country. Why would they do that when they can just call up the World Bank and say, “Can I please have some money?”
Q: I keep reading about a new crop of African presidents who are supposedly free-market guys, including Rupiah Banda, the president of Zambia.

A: There are lots who are nominally free market, but they haven’t been aggressive about implementing those policies.
Q: What do your parents do?

A: My mother is chairman of a bank called the Indo-Zambia Bank. It’s a joint venture between Zambia and India. My father runs Integrity Foundation, an anticorruption organization.
Q: For all your belief in the potential of capitalism, the free market is now in free fall and everyone is questioning the supposed wonders of the unregulated market.

A: I wish we questioned the aid model as much as we are questioning the capitalism model. Sometimes the most generous thing you can do is just say no.
INTERVIEW CONDUCTED, CONDENSED AND EDITED BY DEBORAH SOLOMON
<
http://www.nytimes.com/2009/02
/22/magazine/22wwln-q4-t.html>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. Kitabu cha huyu mwanadada kilishatua bongo toka Januari na kinapatikana maduka ya Novel Idea Bookshops Slipway, Shopers Plaza na Steers jijini Dar. Wasomi haya wahini. Haya aliyokuwa akiyasema ndo ya Kagame kama alivyoituanikia Kaka Michuzi jana na gazeti la The East African la jana. (Lakini hili gazeti bado ladha yake ya kenya mno labda libadilishwe jina liitwe The Kenyan)

    ReplyDelete
  2. Aidha kwa ndugu wafuatiliaji wa haya maswala dada alishafanya majadiliano na The FINACIAL TIMES (of London, not of Mengi) kama wiki mbili zilizopita kuhusu kitabu chake na mustakabali wa uchumi na aid katika bara letu. Haya wasomi fuatilieni guguluni (google) hayo mahojiano.Lakini si ndiyo kujitegemea alikuwa anasema mchonga sasa eti kila mtu anaitikia kama fasheni vile.Munugu ailaze peponi roho yake- watanzania hatutapata mwingine, maana lightning never strikes twice at the same spot- tuliichezea shilingi chooni, kwenye miti hakuna wajenzi.

    ReplyDelete
  3. Anonymous wa February 25, 2009 12:04 AM emenena. Hayati Mchonga aliimba kweli wimbo wa kujitegemea, akasisitiza taifa liwe la wazalishaji yaani wakulima na wafanyakazi. Akaibuka na Azimio la Arusha. Watu wakaenda kulizika Zanzibar. Tukaibuka na tabaka la "wafanyabiashara". Watanzania wakabadilika kutoka watu wanaotaka kufanya kazi kwa bidii ili wajitegemee na kuwa watu wanaotaka kuwa mabwanyenye, mabepari uchwara, walanguzi, madalali, mafisadi nk. Sasa hivi mawazo yetu yamelenga kula bila kufanya kazi. Dada amechokonoa mada ya msingi japo hatuwezi kuukumbatia ubepari au ujamaa kwa asilimia mia. Inabidi tutengeneze mfumo wetu sisi kwa manufaa yetu sisi sio kuigilizia kila kitu.

    ReplyDelete
  4. Mngejua serikali ya sasa inavyolilia misaada, wala msingesema.

    ReplyDelete
  5. Nakubaliana na mdada huyu,naomba Viongozi wote wa Tanzania ambao wanaona hatuwezi bila kupata misaada wabadirike.Maendeleo yanawezekana bila misaada kama hawaamini waangalie filam za cowboy huko zamani na leo wako wapi na ni nani aliwapa misaada kufikia hapo walipo.
    Achaneni na excuses za kwenye kitabu cha Walter Rodney eti How Europe Underdeveloped Africa.Tumepata uhuru lini mpaka leo Rais bado anaenda kutibiwa Ulaya.Mfano mdogo tu Ghana imepata Uhuru kabla ya Malasyia ukizilinganisha kiuchumi huwezi kuamini.Nafikiri Dr Watson alisema kweli kuwa waafrika ubongo wetu una mapungufu fulani..Ni kuuana tu na kuzini na ufisadi...What a disgrace!

    ReplyDelete
  6. Nakubaliana na baadhi ya vitu huyu dada amesema....lakini sidhani kama solution yake ya wajasiriamali kupewa mikopo itatuondolea umaskini na kutupeleka kwenye mkondo wa kujitegemea.......Kama mikopo, ama misaada kutoka benki ya dunia haitusaidii watu wa chini...ambayo ni ukweli...mikopo kutoka kwa watu binafsi...hata kama itamfikia mtu wa kawaida...sidhani kama tofauti itakuwepo. Hayo ni maoni yangu tu.

    ReplyDelete
  7. This is exactly what "Mchonga" was talking about. If you enjoy "free" stuff you will never become independent. Most African leaders keep on stealing the monies because they know there is a way to recover (Aid). If we were to live with only what we collect from Taxes, no one could touch our money because, first it's not enough and second, we would have developed a more strict system to monitor how it is been spent. Wewe dada umesema yaliyo ya kweli kabisa. Misaada inatumaliza...!!

    ReplyDelete
  8. Huyu dada namsifu sana kuwa ujasiri wa kuandika kitabu hiki. Aliyo yasema hayapendezi mbele ya viongozi wengi wa Africa na hapa sizungumzii maraisi tu. Hii misaada ni sumu ya maendeleo hasa kwa bara la Africa. It is Manna from heaven. We hebu angalia NGO's zilivyo shamiri Tanzania kwa mfano, utazania grocery za beer. Wahadhiri wa chuo kikuu wanaacha kutumia elimu yao ya kitaaluma kuedeleza entrepreneurship na maendeleo ya kiuchumi (wanaenda kuendesha NGO. Hivi kweli elimu ya uprofessa inahitajika kuendesha NGO?. Hizo NGOs zina piga panga misaada yenyewe hata walengwa huko vijijini hawapati kitu. Majumba na magari yananunuliwa mijini na hizo NGO. Matokeo yake hakuna maendeleo ya kiuchumi katika uzalishaji na kutoa ajira. Let me tell you my friends... ONLY efforts that are geared to entrepreneurial creation are the ones that will bring true economic growth in Africa because entrepreurial activities will produce goods, provide employment and increase total income of African nations. Siyo hii misaada. Misaada inainyonga africa vibaya sana. Misaada itolewe tu kama kuna Kimbunga/tufani limeikumba afrika lakini hii ya rejareja. Hakuna kitu. Haijengi kabisaaaaaa. Inalemaza vibaya vibaya.

    Ni mimi mchukiamisaada

    ReplyDelete
  9. Huyu dem kichwa...
    achana na wale wenzangu na mimi ambao wako busy ku-copy paste ishu za kwenye magazeti na kuja kuziweka kama post hapa kwa michuzi.

    ReplyDelete
  10. Wale mabankers na wanauchumi mahiri wa kuandika andika viinglishi hapa kwa Michuzi mnaona mfano huo??

    Huyo demu ni banker mwenzenu, na yeye anafanya biashara ile ile ya kuuza bonds.

    Haya rudini chumbani mtengeneze vitabu ili mawazo yenu yajadiliwe kwa mapana na ikiwezekana yadumu milele.

    ReplyDelete
  11. amen sister

    lakini atuambie alisomaje hizo ivy league colleges? au baada ya yeye kupata msaada wengine basi?

    Ukizungumzia misaada sio kwa misaada ya kupelekewa nchi tu bali hata hizi scholaship za kinafiki tunazoziona kila siku ni hizo hizo tu. Wanatupa major ambazo watu wakimaliza shule na kurudi bongo wanakua useless

    ReplyDelete
  12. kIVA .ORG IKO JUU. Ntajaribu kupata mkopo huko nifanye wealth creation.

    Kitabu hiki ni muhimu saaaana. Naona enzi hizi serikali zetu zimekazania sana poverty alleviation projects ambazo ziliintroduciwa na IMF for their own interest. tunachihitaji jifunza Serikali haijachelewa na wala wananchi hatujachelewa tunahitaji kuwa na mtizamo wa kujenga mali/uwezo kuwa wajasiriamali zaidi yaani kuwa na bidii ya wealth creation zaidi.

    Tatizo nilionalo Tanzania ni suala la utegemezi kwa misaada toka nje na serikalini. Vile vile kuna hali ya kuiga. Utakuta watu wengi hawako creative kubuni miradi yao wenyewe badala yake wanasubiri wakiona mwenzao kaja na wazo zuri basi wanaiga na matokeo yake kunakuwa na concentration katika dhana moja ya ujasiriamali. Tunahitaji kujikomboa wenyewe kwa kuwa na bidii kama huna hela za biashara jitahidi upate kazi ulimbikize capital na kisha uanze biashara ukiwa ungali kazini na ikitake off ujiendeleze zaidi kwa ubunifu.

    Na napenda kumuambia Rais Kikwete asidharau KILIMO. Njia moja ya kutukomboa whether we like it or not ni Kilimo. Nasikitishwa kila mara kusikia Tanzania ni miongoni mwa nchi maskini zaidi duniani hivi hatuvuki beyond hapa? au tunafurahia kuwa kwenye hii bottom billion list ili tuendelee kupewa misaada? Misaada yenyewe sijui ndo ilinunua Kiwira etc? Enewei,

    Tanzania ina ardhi kubwa na ya ajabu na Rais Kikwete ukitoa tamko la vijana kwa mfano kuanza kuvuna ocean weeds au walime mazao kadhaaa kama korosho, maharage, nyanya, matunda mbali mbali kwa ahadi kwamba serikali yako itasaidia kumarket hizi products nje nina imani wengi wataitikia wito na kufanya maendeleo yanchi yaende kwa kasi zaidi.

    Huyu binti ni mfano wa kuigwa. Mliokuwa nje mtumie nafasi hizo kubeba mabox na kusoma pia. Elimu haina mwisho na sijutii kamwe kupata elimu na kurudi Tanzania kwani sasa hivi napata consultancies hata nje ya nchi.

    ReplyDelete
  13. mimi sikubaliani na yule aliezikandia NGO, sifanyi kazi kwenye NGO ila misaada mibaya ni ile inayokwenda serikalini maana huko ndiko inaliwa sana, NGO kwa ujumla zinajitahidi kufanya kazi nzuri na hizo pesa wanazopata kutoka kwa wafadhili wao kuliko serikali inavyotumia pesa inazozipata kutoka kwa wafadhili wao kasoro ni kwamba zipo NGO Uchwara pia, lakini bahati nzuri kuna ushindani kwenye Sekta ya NGO ila hakuna ushindani kwenye kuendesha selikali. kwa hiyo ukiharibu sana wafadhili nao wanakukimbia, na wanaanza kumfadhili mshindani wako sasa point yangu ni kuwa ni rahisi kuzibana NGO uchwara ila kuwa na SELIKARI UCHWARA NI BALAA, maaana wafadhili wa selikali mara nyingi hawakimbii hata selikari ikiharibu pesa maana wana nia nyingine ya kuchukua rasilimali zetu, kwa hiyo watatoa msaada selikarini na watendaji wachache wa selikari wataiba hizo hela ila wafadhili nao wataendelea kutoa maana wanaiba dhahabu zetu au hata wanyama pori hai kwenye mbuga zetu

    ReplyDelete
  14. Hamna lolote huyo Dada hana jipya, nifursa yake kuandika uupuzi ulioja kichwani mwake ilituu kujijengea Jina hebu atueleze tutaimpliment vipi hizo pumba zake?

    ReplyDelete
  15. Huyu dada kweli kasema katika hiki kitabu chake. hata hivyo kama wengi walivyosema hakuna jipya kwa Watanzannia ambalo huyu dada kaongezea zaidi ya kutukumbusha mawazo ya hayati Mwalimu Nyerere. Lakini pia kuna Professor Severin Rugumamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Institute of Development studies) alishasema sana mambo haya ya misaada na madhara yake (Soma kitabu chake: Lethal Aid... na summary yake ni : Despite massive infusions of financial and technical assistance from the northern hemisphere, Africa is worse of today - economically, societally, and environmentally - then it was 30 years ago. Taking the Tanzanian experience as an example, this book examines the true role of foreign aid in the development process and exposes certain widely-held myths about that role). Lakini pia kasema analytically katika kitabu chake kilichotoka mwaka 2005: Globalization Dymistified: Africa's Possible Development Futures. Hawa ni wawili kati ya Watanzania wengi walozungumzia kuhusu suala la faida na hasara za misaada. Kipya katika mjadala wa huyu dada ni hii ya KIVA.

    Hata hivyo ni vema kusikia kutoka kwa watu wengine ili ionekane kweli ni tatizo maana labda likisemwa na Watanzania wenzetu inakuwa vigumu kueleweka.

    Tatizo ninaloliona kwa Viongozi wa tanzania na labda Afrika ni kutotumia mawazo ya wataalamu wetu na ya wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.

    Imbombo Jilipo!

    ReplyDelete
  16. mama na baba yake ni mafisadi zambia na wamemlipia ada oxford, hana njaa na tabu za wazambia wengine

    sasa hivi ana promote kiva na kila mtu anajua

    ni gani ya africa ambayo miaka arubaini iliyopita ilikua na viwanda zaidi ya china? jibu hamna. kwa hiyo hata hiyo statement ni ya uongo.

    tunarudi palepale watanzania critical thinking inahitajika mtakua mnapelekwa mputa tu na kila muafrica ambaye anataka kuitumia elimu yake kwa manufaa yake binafsi.

    hata liyumba anajua wa tz ni wazembe .....

    ReplyDelete
  17. Dambisa Moyo hajaandika jambo jipya sana.She's a re-known intellectual but for those who read books about the destiny of Africa,there is a book,"Lords of Poverty" by Graham Hancook.It's the same issue!Afrika imeshazama kitambo!!!

    ReplyDelete
  18. Ndugu wadau wenzangu wa blog hii ya jamii,

    Hata aliyosema Mwl. Nyerere hakusema jambo jipya. Athari za misaada unazijua ukijifunza uchumi (Macroeconomics). Alichokuwa anafanya Mwl. ni uenezi wa jambo hili kwani Baba wa taifa licha ya kuwa mahiri wa uchumi alipenda sana kujisomea ni mwalimu na mwana siasa alikuwa ana wamegea watanganyika ili wafahamu nini kinaendelea.

    Hata leo kuna watu ukiwapa hesabu ya 5 - 10 watakuwambia kuwa haiwezekani. Kama hawajajifunza hasi na chanya.

    Hao wate wanaosema kuwa jambo hili si-jipya siwaelewi. Nia ya huyu dada kuandika kitabu hiki ni kuwa amsha na kuhamasisha waafrika. Kwamfano, kuna watu wengi sana wanafajamu kuwa kufanya tendo la ndoa bila condom unasabisha sio tu mimba bali unaweza kuambukizwa ukimwi na magonjwa ya zinaa LAKINI bado wanafanya ngono hovyo. Kuelewa sio kutekeleza. Nakama haya yasemayo siyo mapya basi hata vitabu vipya vya hesabu (mathematics) visinge andikwa kwani esabu zimeanza kumika sio leo.

    Hii inanifanya nikubaliane mia kwa mia na Kaka Michuzi kuwa watanzania wanapenda kushushana chini. Kumbuka alivyo andika kuhusu Bi. Sophia Kondo siku za nyuma. Watanzania wengi kila kitu wanakijua wao lakini hawatendi akitenda mwingine wanaanza kubwata na kumpiga madongo. Acheni roho ya korosho jamani. Na ombi hili pia sio jipya.

    ReplyDelete
  19. Wewe Mheshimiwa wa February 25, 2009 7:06 PM unaonekana uwezo wako wa kuona mambo kitaaluma ni mdogo na mifano unayotoa wala haina muoano na jambo linalozungumziwa. Mathalani unasema kwamba madhara ya misaada zinajulikana ukijifunza macro-enonomics. Hii ni ajabu kabisa. Kwa taarifa yako kuna maeneo mengin sana ambayo unaweza ukajifunza madhara ya misaada bila kujifunza macro-economics. Hata ukijifunza micro-economic kwa mfano utajifunza madhara ya misaada.

    Naomba nikukumbushe pia kwamba katika kujadili mambo ya kitaaluma na kimaisha kama haya usikimbilie kusema eti ooh watu wana roho ya korosho. Jenga hoja ili watu wakuelewe. Unaposema kwamba watu wana roho za korosho una maana gani? Ina maana hata kama mhusika kasema jambo lisilo la kweli au la kupotosha watu wakae kimya au wakubaliane nae tu ili waonekane hawana roho ya korosho. Ndugu zangu tunaenda wapi!

    Hata katika mifano ya hesabu uliyotoa, kuna mapya ambayo watunzi huwa wanaongezea mfano mifano, hoja, uhalisia nk nk. Kama kitabu hicho cha hesabu hakina jipya watu watasema tu hakina jipya.

    Wanaosema mwandishi hana jipya nao tutawapima kwa hoja wanazozitoa na pengine wao ndio hawana jipya. Lakini kukimbilia kuwahukumu watu 'mna roho za korosho' ni jambo ambalo halikubaliki na halifai.

    Katika hoja yako nyingine unazungumzia kusema ama kuelewa na kutenda. Inaonesha unataka kusisitiza mrudio wa mambo ili kuwakumbusha watu kuhusu masuala au tabia fulani. Lakini kama lengo ni kuwakumbusha tu watu basi ni jambi jema lakini si jambo jipya maana unarudia lile wanalolifahamu. Ni kama ilivyo katika vitabu vitukufu mambo mengi yamo mle karne kwa karne ila kazi ya viongozi wetu wa dini ni kutuelewesha, kutafsiri, kutuasa na kutukumbusha.

    Mheshimiwa jenga hoja na sio kukimbilia kushutumu watu.

    Ya Nchito

    ReplyDelete
  20. akina dada/mama wa zama izi!!
    mnatisha sana dah!!

    mko vibaya-vibaya

    wanaume mnawaweza awa kina dadaz/mamaz?????

    ReplyDelete
  21. Swala la Afrika kutegemea misaada ni kutokana na ukoloni mambo leo.Naamini Afrika ni bara tajiri na linauwezo wa kutosheleza kwa kiasi kikubwa tu kama kutakuwa na muungano wa kweli.
    Angalia mfano wa nchi kama Tanzania,tunavipindi vingapi vya kuweza kupanda mazao na yakatowa mavuno?Kuna nchi zina kipindi kimoja au viwili vya kupanda mazao na kuvuna kwa mwaka na wanaweza kujitosheleza kichakula na hata kutowa misaada kwa nchi zenye ukame kama Somalia nk
    Ni aibu sana kuona Afrika inategemea misaada tu kila wakati huku ikiwa na utajiri mkubwa wa malighafi kuliko bara lolote lile duniani.

    Umoja wa Afrika utakuja tu taka tusitake! na soko la bidhaa za Afrika litapangwa na waafrika wenyewe.
    Hatutaki misaada ya kulazimishwa na kuchukuliwa kama omba omba wakati tuna uwezo.
    Saidia kwa moyo na siyo masimango!
    Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...