JK amemteua Mheshimiwa Jaji Mkuu Mstaafu Barnabas Albert Samatta (pichani) kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe kuanzia tarehe 13 Mwezi wa Kwanza 2009.

Kwa mujibu wa taarifa ilyosainiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Hamis Dihenga imesema Uteuzi huo wa Jaji Mstaafu Samatta umekuja baada ya aliyekuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Balozi Dokta Ibrahim Kaduma kumaliza kipindi chake cha uongozi.

Wakati huo huo Rais Kikwete amemteua Balozi Nicholas Alfred Kuhanga kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kwa kipindi kingine cha miaka minne kuanzia tarehe 1 mwezi wa 11 mwaka 2008.

Aidha Profesa Idris Kikula ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kipindi cha miaka minne kuanzia tarehe 29 mwezi wa kwanza mwaka huu kufuatia Profesa Issa Omari kumaliza kipindi chake cha Uongozi

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 13 mpaka sasa

  1. naungana na wadau waliosema rais apunguziwe madaraka,kwani huu uteuzi wa kila kitu unamfanya ashindwe kuwajibika kwa wananchi kiufasaha.
    pole kwa chuo kikuu mzumbe kwa uteuzi wa jaji samata kwani uadirifu na roho mbaya nyingi sana pale. kumbuka hakutakiwa hata kuwa jaji mkuu na kaondoka pale akiwa na mabifu kibao na majaji wengine.

    ReplyDelete
  2. Kuna uhusiano wowote wa hili na ile taarifa ya TCU kuwa kuna Ph.D feki lukuki pale? What happened to mkuu wa zamani?

    ReplyDelete
  3. Huu ni mchezo wa Kuchanga Karata tu,msiwe na wasiwasi wa garasa!We are trying to be very carefull jamani!

    ReplyDelete
  4. BIG UP MR HIS EXC. JK ,...

    umechagua viongozi waadilifu!


    kwa mliochaguliwa ..Kazi ianze kwa kasi mpya,nguvu mpya na ari mpya..

    na msije mkaanguka kama MNALI!

    ReplyDelete
  5. Nicholas Kuhanga amekuwamwenyekiti wa baraza SUA kwa muda mrefu mno, nadhani angebadirishiwa kazi, maana hajakifanay chuo kweli kibadirishe sura ya kilimo nchini

    ReplyDelete
  6. Huyu aliyechaguliwa SUA si ndio yule yule wa miaka nenda miaka rudi. Mbona hakuna maendelo yoyote SUA na viongozi wanaacha wale wale. Au hawa ni viongozi wa kuhudhuria vikao, kuvuta mshiko na kuhudhuria mahafali. Nadhani wakati umefika vyuo viwe vinachagua viongozi wake wa kuwafaa na pia viongozi wasikae muda mreu kuliko hata muda wa urasi.

    ReplyDelete
  7. hongera mh samamtha! chuo kikuuu mzumbe sasaivi kinakuwa na viongozi wazuri kama prof kuzilwa pia nae ni mzuri sana na ana sifa nzuri sana ila sasa waalimu wa hiki chuo kwa kweli wengi bado bado kabisa hawana sifa za uazili wa chuo kikuu wengi wao wana chuki zaidi na wanafunzi mimi nilisoma pale si mchezo shule sio ngumu ila walimu ndo wabaya wanacomplicate sana

    ReplyDelete
  8. Rais wetu ana mamlaka mengi sana jamani, hata wakuu wa chuo wanateuliwa na Rais.

    ReplyDelete
  9. Nyie mnalalamika nini CCM si ileile na watu ni walewale, JMK mwenyewe si mpya bali mtoto wa chama tumeanza kumsikia tokea akiwa dogo ndani ya chama sasa unataka nini tofauti. Na wakibadilika ujue watoto wao wanapandia hapo hadi CCM ingolewe ndio mambo tofauti la sivyo sahau na kubali matokeo!!!
    Mzawa

    ReplyDelete
  10. Mimi nimekosa imani kabisa na huyu mkuu wa wilaya ya Tegeta mpinga Usenene: Hii habari ya Mawaziri na Wabunge wenye vyeti feki ameibania sana hataki kuiweka ukurasa wa mbele ili watu wachangie.
    Sasa tutaipeleka majukwaa mengine yasiyo na upendeleo. Habari yenyewe imeandikwa na Gazeti la kwake na ambalo ni la Serikali: Dele News. Na matamshi yametolewa na Professor.
    Hawa watu ndio wanaotuangusha, na ndio wanaoturudisha nyuma na kumfanya Raisi aanze kufuatilia Risiti wakati wao wako Bwagamoyo wanapiga Ramli nani mchawi.
    Ila kwenye Jukwaa letu hili nahisi mpinga usenene ndio mchawi wetu:

    Nanukuu tena kutoka Dele News:

    "We must do something before it is too late … we have to safeguard the country’s image and that of our institutions,” Prof Nkunya said. Meanwhile, Prof Nkunya has said he was prepared to advise the government and the National Electoral Commission (NEC) on how to introduce vetting mechanisms of academic credentials of candidates who will vie for political posts in future general elections.

    The move comes amid widespread reports of some cabinet ministers and Members of Parliament holding fake academic credentials. “We intend to advise the electoral body on the exercise so as to get rid of this shame … Uganda is already doing this,” he said. Citing the enormity of the problem, Prof Nkunya said that some MPs holding fake PhDs had since approached some of the universities hunting for part-time teaching"

    Jamani hili ni muhimu sana tulivalie njuga tena wakati huu Bwana JMK anapodiriki kutamka eti nchi ina viongozi shupavu!!(Dele news tena)

    "Africa has competent leaders - President
    Most Read
    # Indian held over grisly murder of Dar businessman
    # News of the screws
    # Man held in Dar for possession of counterfeit notes
    # Mzumbe dons in PhD scam
    More News
    # EA ministers raise red flag as Nile Perch stocks decline in Lake Victoria
    # Blind German scales ‘Kili’ roof
    # Fake goods go up in smoke
    # EWURA gives Songas nod to fulfil infrastructure conditions
    # Zanzibar, Japan sign water agreement
    # Court asked to order arrest of advocate
    # VP directs village leaders to educate people against deforestation
    # Remain committed to development aid, PM tells partners
    # UN chief: Stop this violence
    # EWURA gets tough on 132 fuel stations
    # Legal centre told to take aid services to remote areas
    # Ban Ki-moon to address ICTR staff
    # Court admits caution statement on EPA case
    # Court gives prosecution more time to probe Richmond case
    # Pinda hails Ireland
    # Dons decry graft in police force
    # Defence seeks to save Liyumba
    # Witness to testify over Mahalu’s 2bn/- sabotage case on video
    # Dons decry graft in police force
    # TMA presses for modern weather radar


    JIANG ALIPO, 25th February 2009 @ 10:32

    President Jakaya Kikwete has said that development was a process which cannot be achieved in a short period of time like a dream, adding that Africa being backward in development was not caused by incompetent leadership.

    President Kikwete said that today when he was addressing a group of exchange programme students from African countries and Germany when he met them at the State House. The group of 25 students from Tanzania, Kenya, Ethiopia, Mauritius, Uganda, Rwanda and Germany are participating in the Go Africa, Go Germany programme aimed to reinforce the dialogue between young Germans and Africans.

    Answering a question from one of the students who wanted to know why Africa has remained backward in development and why its development was slow, President Kikwete said: “All nations in the world at one or another point in history were poor. There are many reasons for Africa being backward and one of the reasons is colonialism which turned the continent into a source of natural resources for the rich nations ruling it.” -Sasa sijui wakina Malasia, Thailand, India nao wasemeje hawakutawaliwa???? Ina maana Tusingetawaliwa tungekuwa kama Uswiss nini??? vipi basi Ethiopia maana haikutawaliwa???
    Huu ni umaskini wa fikra.

    Mungu ibariki Tanzania,
    Mungu iokoe Tanzania
    Mzawa

    ReplyDelete
  11. na hicho chuo cha mzumbe sasa mchague walimu wenye sifa na exposure kidogo mimi ngazi ya juu kama mh samatha naona haina shida ata prof kuzilwa pia ni mzuri sana ila walimu hawa wa chini hasa faculty ya uchumi na uongozi kwa kweli wengi ni wamatumbi kwanza washamba pili wanachuki tatu hawana ujuzi wa kutosha unakuta mtu kamaliza hapo degree mwaka huu eti mwakani unamuona nae ni mwalimu wa chuoni hapo hapo kwakweli hii ni aibu sana kwa nchi yetu. mh inabidi sasa uangalie ilo swala utakuwa umefanya kazi kubwa sana

    ReplyDelete
  12. na we annon hapo juu usilete chuki zako binafsi! Usijifanye unawajua sana viongozi huyu mzee mbona yuko safi na majukumu yake anayatimiza kama inavyotakiwa tatizo lenu watanzania hamtaki viongozi walio serios akiwa anajituma ooh kimbelele akiwa mvivu hayuko makini ooh maneno sasa nyie mnataka nini? acheni ulimbukeni

    ReplyDelete
  13. wewe anonymous wa saa 7:56 uwe kidogo unafikiria kabla haujacomment...sasa mtu ana first class kwanini asifundishe as tutorial assistant..nafikiri anonymous wa saa 10:35 big up unajaribu kuwaelekeza mtu akiwa na akili or anaringa mara nini..we need to work hard..

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...