Globu ya jamii inapenda kumpa pongezi JK kwa kuwashushua viongozi wa jiji la Dar kwa tabia yao ya kuwanyima raha wakazi wake kwa kupanga matumizi ya sehemu wazi wanavyojua wao.
Globu hii, ambayo ilikuwa mstari wa mbele kukemea hayo, ikiwa ni pamoja na kuzuiwa wadau wasiende kwenye fukwe kama pale Aga Khan kupiga picha, imefurahishwa sana, sana kwa mshushuo huo wa uhakika.
Sijui hawa viongozi wa jiji hili wana tatizo gani. Globu hii inadhani wana utindio wa ubunifu kwani kama ingekuwa vinginevyo mambo yangekuwa mswano kila mahali.
We fikiria unazuiwa kwenda bichi, bustani ya Mnazi Mmoja imepigwa kufuli saa zote, na zingine kama za pale Magomeni, Temeke, Mwananyamala na kweingineko hata hazitamaniki. haishangazi kukuta kila mtu anaelekea Coco Beach kila siku ya mapumziko kutokana na unoko wa viongozi wa jiji.
JK wala hakuwalazia damu. Aliwataka madiwani hao wa jiji hili (hata sijui wanafanya kazi gani) kuhakikisha kuwa viwanja vya Jangwani vinabakia kuwa vya matumizi ya umma hasa michezo na sio vinginevyo.
JK aliyasema hayo wakati akizungumza na madiwani wa Jiji la Dar es Salaam katika viwanja vya Karimjee hivi karibuni.
Alisema kumekuwa na tabia ya mamlaka za Jiji kuvamia viwanja vya wazi vilivyotengwa kwa ajili ya michezo na kutoa mfano wa viwanja vya Jangwani, akishangaa magari ya mizigo yakiwa yameegeshwa eneo hilo.
Alisema mwanzo alifikiri magari hayo yamevamia eneo hilo, lakini baadaye alikuja kufahamu magari hayo yalielekezwa na mamlaka husika kuwa hapo, ambapo alisema uamuzi huo haukuwa wa haki.
“Tafadhali tafuteni mahala pengine pa kuegesha magari yenu na viacheni viwanja hivyo kwa ajili ya watu kufurahi na kucheza, mji uliopangwa vizuri ni lazima uwe na mahali palipotengwa kwa ajili ya michezo.
“Nakumbuka enzi zetu nilikuwa natembelea maeneo ya Gerezani kwa ajili ya mchezo wa mpira wa kikapu, ambapo ilikuwa ni muda mwafaka kwa vijana kufurahi na kubadilishana mawazo,” alisema.
Pia JK alishangaa kusikia kuwa mamlaka zinawakataza wananchi kutembelea maeneo ya fukwe hasa wakati wa sherehe za harusi.
Alisema hakuna cha kupoteza kama wahusika wataenda kwenye fukwe hizo na kupiga picha kwa muda mfupi katika matukio yao muhimu na kwamba kinachotakiwa si kuwazuia, bali kuweka utaratibu maalumu.
Pia alisema fukwe hizo zinaweza kuwa vyanzo vizuri vya mapato kama zitatunzwa vyema.
Leo nimepita hapo bichi ya Aga Khan nimekuta hakuna tena yale mabango ya kukataza watu wasile raha sehemu hiyo. Yaani hadi raha.
Ila hapa cha kujiuliza; hivi ni hadi JK aache shughuli za maana za kitaifa na kimatifa aje awafunze kazi madiwani????
Wadau hii imekaaje?
-MICHUZI

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. michuzi unamfagilia sana jk bwana na wewe,mi bado hajanifurahisha ipasavyo anakemea vitu laini laini kutuziba macho tu watanzania tuna kero zetu na bado hajazitatua zaidi ya kusogeza sogeza siku tu na ngonjera ngonjera zake hizo za vijiweni,mi naona nafuu asingewakeea madiwani akamgeukia lowassa akamkemea kwanza,serikali za wenzetu zinawasaka THE BIG FISH SIO VIDAGAA,jk ajue watanzania kero zetu ni AJALI ZA BARABARANI ambazo zinachangiwa na mamlaka ya usalama barabarani kwa kuzembea zembea kwao tu,na pesa nyingi sana ambazo zinapotea nchini kwetu kirahisirahisi tu(UFISADI)NAAMINI HAMNA HATA FISADI MMOJA ALIEFUNGWA HADI SASA HIVI TUNAPOONGEA HAPA,why????ila kuna jela zetu zimejazana vibaka walioiba simu tu huu ni ushenzi

    ReplyDelete
  2. Tatizo hawa madiwani hawatembei, sana sana wakisafiri sana Chalinze,wapatiwe vitrip hata kwa kwenda Moshi au kwa watani zetu wa jadi wakajionee wenyewe wenzao wanavyofanya kazi.Nafikiri hio itasaidia kwa kiasi kikubwa.
    Nawakilisha.

    ReplyDelete
  3. Mimi nimefurahishwa sana na kitendo cha mheshimiwa Rais kuwaeleza ukweli madiwani hawa, tujaribu kuiga kwa mataifa yaliyoendelea yanavyotumia maeneo kama hayo kwa kujipatia mapato, wanatengeneza mazingira mazuri na kuweka watu watakao angalia maeneo hayo, maeneo yakiwa ya kuvutia kila mmoja atatamani kwenda huko bila kuja gharama. naungana nae sana.

    ReplyDelete
  4. UKWELI UNABAKI PALE PALE TANZANIA SIJUI TUPO KARNE YA NGAPI??TUPO NYUMA HAWA MADIWANI WAPI?? WAMETEMBEA ANGALIA FUKWE ZA WENZETU MAKINI MOZAMBIQUE NA KENYA SISI NI AIBU TUPU,HUWA NAWAZA SANA TATIZO LA TANZANIA NI NINI????TUNA AMANI LAKINI TUNAKUWA NYUMA HATA NAWANAOKUWA KWENYE MIGOGORO AU VITA, HAWA MADIWANI SANA SANA HATA ARUSHA HAWAJUI ???? VIWANJA VYA KUCHEZEA WATOTO WAMEUZA,WAKATI RAIS MWINYI ALIFIKIA KUUZA MPAKA MNAZI MMOJA KWA MHINDI ANAITWA BAGDAD,AIBU TUPU WATOTO WATACHEZA NA KUPUMZIKIA WAPI??? TUTAENDELEA KUZALISHA MAJAMBAZI NA VIJIWE TU SIONI FUTURE YA TANZANIA HUKO MBELENI HAPA NI SERIKALI INAYOKWENDA KISANII TU----------

    Isma Kabengo,Kpl,Ug

    ReplyDelete
  5. KWA MTAZAMO WANGU, Sidhani kama viongozi wa awamu hii wako makini na kazi zao. Hata ukiangalia baraza la mawaziri,maamuzi mengi ya wizara inabidi mpaka rais aje aamue ndipo yatekelezwe.Je kuna haja gani ya kuwa na mawaziri kama hawawezi kuyatolea maamuzi matatizo ya wizara zao??Angalia issue ya ATCL, Railways,....Na hili la jiji tena, na kuna mengi yatakuja anavyoendelea kutembelea mawizara pia. Ila hii ni mitazamo wangu

    ReplyDelete
  6. Michuzi
    Nazidi kushangazwa na mtoa comment aliyesema unamfagilia JK, hebu tubadilike jamani hii tabia ya kulalama ndio inayo tufikisha hapa. Hao anao wasema big Fish.. big Fish si apeleke ushahidi mahali husika ili wachukuliwe hatua kuliko kuleta maneno ya vijiweni. Na yeye asiwe Fisadi wa mawazo. Tabia ya mawazo mgando, Mzee Mbeki siku moja aliwaambia chuo kikuu, msilalamike tu kuwa viongozi hawafanyi hivi, toa malalamiko na ushauri, na unapo msema mtu hakikisha una ushahidi wa kutosha, tuache maneno ya vijiweni na ya ushabiki TUJENGE TAIFA LETU.

    NAMPONGEZA MH. RAIS KWA HATUA NYINGI ANAZO CHUKUA KUJARIBU KUBADILISHA TAIFA LETU. KILA MMOJA WETU AJITAHIDI PALE ALIPO KUFANYA JEMA MOJAWAPO KWA TAIFA.

    ReplyDelete
  7. Kosa ni letu kuchagua madiwani ambao ni vibabu vya uswahilini. Hebu linganisha madiwani hawa na upeo wao duni, na madiwani wa sehemu kama New York. Hatuwezi kuendelea kwa uswahili swahili. Hawa ni watu ambao pamoja na kukaa kwenye mji wenye bichi, hawajui matumizi ya bichi. Nchi yetu iko nyuma kwa sababu tuna watu wa aina hii wengi.

    ReplyDelete
  8. Tatizo zima ni utamaduni wa kisiasa ambao umezoeleka miaka mingi ambapo kuanzia mwenyekiti wa kijiji hadi waziri anasubiri kutekeleza yale ambayo rais amesema au ameagiza. Basi!! juzi jzi tu rais amekuwa akikutana na wakuu wa wizara na mashirika ya umma kuwaeleza na kuwaelekeza jinsi ya kuongeza ufanisi katika vitengo vyao!! tunaweza kumpongeza jk kwa kuanza taratibu kuwashushua hao watendaji, lakini pengine badala ya kushushua kwa njia ya masimulizi ingefaa kama angetoa agizo kwa njia ya waraka rasmi akihimiza ubunifu miongoni mwa watendaji kuanzia kata hadi wizara.

    ReplyDelete
  9. nakuunga mkono mdau uliyesema makosa ni yetu kwa kuchagua madiwani vibabu wa uswahilini. ni suala la Shule tu na njaa ya watanzania. Usikute pale Beach waliamua kupafunga kwa vile tu labda kuna hospitali ilikuwa inaona bughudha kwa waswahili kuja pale na kuburudika na matarumbeta ya harusi zao, na wakakata pochi na madiwani wetu wakakubali kupafunga bila kujali madhara kwa watumiaji wengi zaidi. Nchi Hii??!!!

    ReplyDelete
  10. tatizo la waswahili ustaarabu hakuna kabisa,hizo bichi zitageuka vyoo,majalala.sasa umefika wa kuchagua watu walio enda shule kuliko hivyo vibabu,halafu kazi ya mkuu wa mkoa nini?kazi ya meya ni nini?yaani bongo kazi ipo raisi anaacha kazi zake zote,na nilisahau kuna mawaziri wahusika,i m fed up with bongo.

    ReplyDelete
  11. michuzi ninaona rais wetu anasoma blog yako. ili jambo la beach na parks tulikwisha lihoji kwenye blog yako. viongozi wetu wajue kuwa kutolewa makosa si vibaya kwani hata watu wenye akili sana hujifunza kutoka watu wengine. hili jambo la miji yetu kutopanga sehemu za parks au public beaches sio zuri. wanatakiwa kujua kuwa wanaweka fungu fulani la pesa kuzitunza hizo sehemu. wasisahau pia kujenga choo. infact wanaweza kutoza watu pesa kutumia hizo choo na hizi pesa zitatumika kuajiri watu kusafisha hizo choo. ningependa waende nairobi wakaangalie jinsi wanavyofanya. nairobi kila sehemu kuna choo za kulipia na ni safi mno. kitu kingine wasisahau ni vitu vya kutupia takataka. i am sure wanaweza kugundua vitega uchumi ambavyo vitawawezesha to run these places. i am sure kuna vitu vingi vya kuinua nchi yetu kiuchumi kama viongozi wetu watawapa support wataalamu wetu wa kitanzania. tuache mchezo wa kuwadharau wataalam wetu na kukimbilia wageni. tusitegemee wageni watatuendeleza kiuchumi. wao wakija afrika wanakuja kujitajirisha na kuchukua kila kitu kwao. kwanini wageni wanaweza kuingia mpaka kwenye misitu yetu na kukata miti yetu kisha kusafirisha kwao. jee mtanzania anaweza kupewa kibali kukata miti uchina au amerika na kupeleka tanzania. serikali isikae ikilia kuwa miti inakatwa na huku wageni wanakata miti na kuisafirisha nje. watu ambao wangeruhusiwa kukata miti ni watanzania peke yao na kwa kibali tu. pia tusiruhusi mbao kupelekwa nje ovyo. tukifanya hivi tutalinda mazingira yetu.

    ReplyDelete
  12. Mtalii analipa pesa nyingi kuja kula raha kwenye fukwe zetu. Sie tupo hapahapa hata kwenda Agha Khan haiwezekani kisa pamezuiwa. Kwa hiyo mwenyeji anadhulumika, mgeni anatanua kwenye fukwe zetu mbalimbali

    ReplyDelete
  13. aghakhan nyie hamjui ni wahindi pale?
    afu panabomoka sana zile kuta.
    madiwani wapewe shule tu na waziri mkuu Pinda basi.wee annon unaesema Lowassa vipi box zinakuzingua eee?

    ReplyDelete
  14. Habari za ndani ni kuwa mameya wa manispaa za Ilala na Kinondoni hawakutaka kabisa Rais JK aje kwenye chakula hicho cha usiku. Ukweli ni kuwa aliyemwaalika Rais ni meya Kimbisa na hao mameya wengine alikuja kuwaambia baada ya Rais kukubali mwaliko. Hawakutaka waje kwa sababu walihofia kusutwa kutokana na uzembe wao wa kushindwa kuibadili sura ya manispaa zao.

    Kama hio haitoshi hawana raha na Kimbisa kwa sababu yeye ni msomi halafu ni modern. Kwa mfano ukiangalia kata anayoiwakilisha Kimbisa kata ya Kivukoni inaonekana safi kuliko ya jangwani ambaye diwani wake ni meya wa Ilala Abuu Jumaa. Si hivyo tu machinga complex ni babies wa Kimbisa. Huo ndio ukweli na hawa wazee wa kiswahili wanamuonea wivu haswa. Huyu mzee Abuu Jumaa ni diwani for the last 25 years. Lakini na umeya wake bado Jangwani ndiko kuchafu na cases za ubakaji na madawa ya kulevya nyingi tu. Really pathetic. Tatizo ni nini? Wasomi hamtaki kugombea udiwani. Matokeo tunaongozwa na watu wasiosoma na wasiokuwa na vision. Really horrible.

    Lifanyike nini? Unda tume kama ya Keenja na unda wizara responsible for Dsm. Halafu awepo meya mmoja tu wa jiji. Hao wengine wawe deputy mayors. Muundo wa mkoa wa Dar uwe tofauti nay a mikoa mingine.

    ReplyDelete
  15. elimu ni ya maana sana ila sio wote wamepata iyo nafasi/uwezo hakuna.
    ila tutafika tu dar

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...