Waziri wa nchi ofisi ya makamu wa rais (muungano) Mohamed seif Khatib (pili shoto juu, na tatu shoto chini) mbali ya kuongoza msafara wa Taifa Stars huko Abidjan pia anafanya ziara nyingine kadhaa za kuangalia miradi ya maendeleo kama hapa akionyeshwa jinsi ya upandaji wa migomba katika ziara yake leo hii



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. mh waziri tunaomba ufanye tulokutuma tunasubiri urudi na kombe tz ahsante.

    ReplyDelete
  2. jamani uzalendo sio bendera!

    ReplyDelete
  3. KATIKA KITU AMBACHO KINA TURUDISHA NYUMA WATANZANIA NI MAJUNGU CHUKI NA UBABAISHAJI,JANA KABLA YA MATOKEO MAZURI YA TAIFA STARS,NIMESOMA COMMENT 2 KATIKA GAZETI LA MWANANCHI,ZIMETIA KICHEFUCHEFU,SILVESTAR MZIRAY NA MSHANGAA SANA FROM DAY ONE AMEONYESHA KUMBONDA MAXIMO WAKATI YEYE HAJAWAI KUFIKA HATA YA ROBO YA MFANIKIO MAXIMO ALIOTULETEA,KAMA NI MAKOCHA TANZANIA HAITOWASAHAU KWA KULETA MAPINDUZI YA SOKA LA NDANI YA BONGO,NI PROFESAR VICTOR,NABBY KAMARA,TAMBWE LEYA,MARIJANI RAJABU,PAUL GWIVAH NA JOEL BENDERA,KITAALUMA MZIRAY NI MWALIMU WA VIUNGO ANAWEZA KUWA KOCHA WA NGUMI,MIELEKA ATA RIADHA,NA HUYU MCHAMBUZI WA KIJIWE CHA GAZETI LA MOTOMOTO SALAMANDER HUSSENI SAPI,HAJUI CHOCHOTE KUHUSIANA NA SOKA NI MMNAZI TU,VYOMBO VYA HABARI ZA MICHEZO HUKU MAJUU VINA WAPA WACHAMBUZI WALIO BOBEA KATIKA FANI YENYEWE AIDHA WACHEZAJI MAHILI WA ZAMANI AU WALIMU WASOKA,SAPI ATA CHANDIMU MCHANGANI AKUCHEZA UBISHI WA YANGA NA SIMBA MSITULETEE KATIKA TIMU YETU YA TAIFA NA PIA VYOMBO VYA HABARI VINAPO MPA MTU KAMA SAPI KUCHAMBUA,NAVYO NI VYA UBABAISHAJI,KUNA WATU HUKO LIWALE HAWAMJUI SAPI WANAMUONA KATIKA VYOMBO VYA HABARI,WATAAMINI BONGE LA MTAALAMU KUNA WATAKAO MUUNGA MKONO UTUMBO WAKE,LAZIMA TUBADILIKE MAXIMO ANAITAJI KUVIKWA SHADA LA MAUWA KAMA SI KUMPA KIGOLI WA KIZARAMO ILI ABAKI,KUMALIZA KAZI ALIO IANZA NA KUNYESHA MAFANIKIO KWA MUDA MFUPI. NA SIO MKUNANGA,NAAMINI MAONI YAO WOTE WALIYATOA UKU WAKITEGEMEA STARS ITAFUNGWA NA IVORY COAST ILI WAANZE MAJUNGU,MAXIMO,WACHEZAJI,TFF,VIONGOZI WOTE NA MASHABIKI MLIOAMBATANA NA TIMU HONGERENI SANA KWA KAZI KUBWA NA KUTUWAKILISHA VYEMA. WATANZANIA TULIO WENGI TUKO PAMOJA NANYI,MUNGU IBARIKI TANZANIA,BILA KUSAHAU BLOG YETU HII NA MDAU ANAE TUNGANISHA TOKA ABIJAN MDAU CARDIFF.

    ReplyDelete
  4. sasa hiyo migomba itamsaidia nini mheshimiwa waziri?au alikuwa anafanya utalii wa kilimo?Ninavyofahamu Tanzania kuna wataalamu wa migomba wengi na wanafanya kazi sana tuu.

    ReplyDelete
  5. Watanzania kwa kukosoa tu,sasa kama alikuwa na mda wa ziada kutembelea na kujifunza nini kinaendelea kwa wenzetu kuna ubaya gani?Jamaa wametuzidi kwani sisi tuko milioni 4O karibu na hatuna hata mchezaji maarufu wa kimataifa Ulaya....Na wao si waafrika kama sisi tu tena hawajazaana sana kama sisi.Tatizo tuna midomo sana matendo ziiii!

    ReplyDelete
  6. Samahani wadau hapa si sehemu yake, ila wewe Anon wa feb 26, 11:55 pm imenigusa mtima wangu,umeongea jambo ambalo lilikuwa linanisonga moyo kwa mshangao wa kauli na hoja za Mziray juzi kabla ya mechi ya Taifa star,nilitegemea wadau wangeliongelea juzi siku tulipopata ushindi ila watu walijawa na furaha ya ushindi sikusoma kama mtu aliliona lile, mimi si mshabiki wa mpira sana ila hata mimi yale maneno alokitamka Mzirai kwenye luninga juzi kipindi cha habari za michezo, ukweli aliniacha mdomo wazi na kumshangaa, nikajiuliza huyu ananini na Maximo /Masimo ukweli alimponda bila kumsaza, ukweli upupu aloumwaga ulipaswa kumuwasha kabisa kabisa yule kocha wa brazil ukweli kauli zake, ziliashiria chuki na roho mbaya au wivu mtupu, Huyu baba ameiinua sana hii timu pamoja na mijineno ya baadhi ya watu walomkatisha tamaa lakini bado anamoyo wa kufundisha kwa bidii na ari kabisa ukweli anastahili pongezi, ingawa wengi timu yetu ikifungwa lawama na timu inakuwa ya Maximo peke yake jamani.

    ReplyDelete
  7. MDAU UMENIKUNA NA COMMENT YAKO KUHUSU MZIRAY:HUYU BWANA ANACHOTAKA WATANZANIA WAMUONE MUNGU MTU KWAMBA YEYE NI BORA ZAIDI YA MAXIMO NA ANAUJUA MPIRA KUUCHAMBUA KAMA KARANGA VILE.(1)HATUTAKI MCHAMBUZI WA SOKA KAMA WEWE MZIRAY NDIO UWE KOCHA WA TIMU YETU YA TAIFA(2)WEWE SIO KOCHA NI TRANNER WA VIUNGO HUZIJUI MBINU ZA MCHEZO ZAIDI YA PHYSIC TU(3)USICHAMBUE TIMU INAPOBORONGA TU INAPOFANYA VIZURI UNAZUGA UKO BUSY(4)WATU WA AINA YAKO NDIO MNAODUMAZA SOKA LETU BINAFSI MIMI NAKUCHUKULIA KAMA MTU MWENYE ROHO YA FIHI TU KWA MWENGINE KUONEKANA KAPATA MAFANIKIO.HIVI KABLA MAXIMO HAJAJA MZIRAY ALIKUWA WAPI HUYU???ANA KAZI YA KUPONDA MAFANIKIO YA STARS TU SIKUZOTE KWENYE VYOMBO VYA HABARI ILI APEWE KIBARUA CHA KUINOA STARS,AMIN NAWAHAKIKISHIENI SIKU TUTAKAYOMPA NAFASI KIDUDU MTU MZIRAY NDIO AWE KOCHA WETU TIMU YA TAIFA TUMEIZIKA SOKA YETU BONGO.MIMI NI MCHEZAJI MPIRA SIPO IVORY-COST NA TIMU YA TAIFA KWASASA HIVI LKN NIMESHAKUWEMO KWENYE KIKOSI CHA STARS HII YA MAXIMO.NAJUA SOKA LINAVYOENDESHWA KISASA NAMKUBALI MAXIMO KAZI ANAYOIFANYA,MZIRAY ATAWADANGANYA WANAZI WA SOKA LKN SIO SISI WADAU WA SOKA,SIELEWI KWANINI HUYU BWANA ANAKUWA NEGATIVE SANA NA TIMU YETU YA TAIFA NA HASWA MWALIMU.JAMANI MZIRAY SASA INABIDI TUMTIZAME KWA JICHO LA 3.NINGEFURAHI KAMA MZIRAY ANGEINGIA KWENYE HII BLOG AKATAKA KUNIJUA MIMI NI NANI NISINGEMFICHA JINA LANGU ILI AJUE ANACHOKIFANYA WENGI HATUPENDEZEWI NACHO.MDAU DENMARK NAWAKILISHA

    ReplyDelete
  8. Huyu Waziri haogopi kupigwa, jamaa wana hasira ya kufungwa hawa

    ReplyDelete
  9. kila binadamu ana kasoro yake,mzirai ameonyesha dhahiri chuki binafsi kwa maximo na sio mara ya kwanza kumkatisha/kutukatisha tamaa watanzania juu ya maximo,kama angekuwa mtu makini na kocho kweli alipaswa kumuunga mkono na kutoa ushauri wa kwenda mbele ukiona kocha yeyote kila kwenye timu kunapokuwa na migogoro anapewa yeye timu ujue kuna namna,alipewa timu yanga wakati wa migogoro,simba mara tatu inaeleweka,plisner aliikuta tayari inawachezaji watoto wamjini wenye vipaji binafsi taifa star enzi ya wambura we waza,tuna tatizo la timu ya ngumi ya taifa aifanyi vizuri timu ya mileka ata aijulikani iliko na mwalimu wa viungo tunae mzirai kwa nini wizara isimpe izo timu,please mwache maximo afanye vitu vyake,its too late watanzania sio wajinga tunaona mabadiliko alio tupa maximo.

    ReplyDelete
  10. Yaani leo mmeongea points huyu bwana ni kocha wa viungo mwenye roho mbaya ya chuki na wivu usiojenga,kwanini akazanie kuiponda timu yetu ya taifa na kocha wetu tu?anajipigia debe apate unga ili atukere baadae,hao ndio viongozi wetu wa soka bongo mchezo tunaoupenda kuliko wote wa aina hii ya mziray na ndio maana soka letu bongo lilikuwa linazidi kudumaa,viongozi wengi wa mpira bongo wamejaa chuki,majungu,ubabaishaji,roho mbaya na uselfish kama wa huyu bwana anaejali maslah yake yeye kwanza na sio timu yetu ya taifa.anachofikiria kwenye ubongo wake apigiwe debe kwa kumponda maximo ili ulaji apewe yeye tu na sio timu ifanye vizuri.ABED AYEW PELE AMEKIRI KUWA TANZANIA NDIO NCHI PEKEE KWASASA HIVI INAYOSIKIKA HUKO EAST AFRICA KWA UBORA WA SOKA NA HILI HALINA UBISHI.SASA SIJUI MZIRAY ASICHOKITAKA NI KIPI HAPO??MIMI NAAMINI KAMA MIOYO YETU INGEKUWA INAONEKANA NJE MZIRAY MOYO WAKE HAUTAKI KABISA KUIONA STARS INASONGA MBELE ILI MALENGO YAKE YATIMIE.KUNA MDAU HAPO JUU KAONGEA KITU KIMOJA KIKUBWA SANA "UKIONA KOCHA KILA TIMU INAPOKUWA NA MGOGORO NDIO ANAPEWA YEYE BASI UJUE HAPO KUNA NAMNA TU NA SI BURE"LAZIMA ATAKUWA ANACHOCHEA MIGOGORO CHINICHINI ILI APEWE ULAJI .NA MAMBO HAYO KAWAFANYIA SANA YANGA NA SIMBA TENA WA ENZI HIZO LKN SIDHANI KAMA SASA HIVI ANAWEZA KUFANYA UPUUZI WAKE HUO KWA VIZAZI VYETU HIVI.USHAURI WANGU KWAKO MZIRAY"TAIFA STARS SI YANGA WALA SI SIMBA NI TIMU YA WATANZANIA WOTE DUNIA NZIMA, KWAHIO CHUNGA SANA DOMO LAKO NA MDOMO SIKUZOTE UNAPONZA KICHWA"USIDHANIE NCHI NI KAMA KIJIWE CHA KAHAWA TU UNA REKODI GANI WW KATIKA SOKA????NENDA KAFUNDISHE NGUMI HUKO ACHA KUGANGA NJAA YAKO KTK MPIRA.MKEREKETWA

    ReplyDelete
  11. Kaka Michuzi, usibanie maoni yangu tafadhali.
    Napenda kujua, je waziri wetu Khatibu alienda na wakulima wangapi wa ndizi kutoka Kagera, Mbeya na Kilimanjaro? Naomba ututundikie idadi ya wakulima aliokwenda nao ili tujue kama hiyo elimu anayoipata hapo migombani itawasaidia wakulima ama la!
    Ni hayo tu.
    Mdau wa Kijitonyama

    ReplyDelete
  12. Mdau wa February 26, 2009 11:55 PM, umesema yaliyokuwemo mawazoni mwangu. Kuna mdau alitaka kuweka dau kwamba hatuwezi kuwafunga Ivory Coast lakini amejirudi akarejea globuni kuomba radhi. Huyo Sapi ameng'ang'ania tu kwamba makocha wa Brazil hawana historia nzuri nje ya nchi zao akitoa mifano miwili mitatu. Aje na takwimu za idadi ya makocha wa Kibrazil waliowahi kufundisha soka nje, hususan Afrika na vipimo halisi vya mafanikio, sio kutoa maoni ya hisia. Supa kochi naye timu ikishinda anakuwa mgumu kukubali, ikifungwa tu wa kwanza kutoa kasoro. Takwimu zinaonyesha kwamba Maximo ameshinda mechi nyingi kuliko alizofungwa na hajawahi kufungwa kwenye mechi ya kirafiki uwanja wa Taifa. Hata kwenye mechi za mashindano ni Msumbiji peke yao walituotea.
    Kusema makocha kutoka Brazil hawawezi ni sawa na kusema wachezaji wa Kitanzania hawawezi kucheza mpira. Maximo apimwe kwa mafanikio yake kama yeye, sio kwa mafanikio ya makocha wengine kutoka Brazil. Miaka mingi imepita tunaangalia tu mashindano ya ngazi ya bara Afrika kwenye luninga huku tukiparamia mataifa ya watu. Ikianza ACN waTz wengine wanakuwa Wanigeria, Waghana, Waivory coast, Wamorocco, Wakenya. Sasa hivi kuna mashindano ya kiafrika ambayo Watz tunaangalia kwenye luninga wengi wetu tukiwa ni Watz. Japo si makubwa kama ACN lakini ukweli unabaki pale pale kwamba katika timu zinazoundwa na wachezaji wa ndani, timu ya Tanzania ndiyo bora kuliko zote za Afrika Mashariki na ni miongoni mwa nane bora Afrika nzima. Tena basi hata katika nane bora sio ya nane. Tunawazidi Ivory Coast maana tumewapiga bao. Na bado tutawapiga Zambia na kwenda nusu fainali.
    Hao kina Mziray na Sappi wakate tiketi kabisa wakimbie nchi kwa muda maana vijana watarejea na kombe hapa. Itakuwa ngumu kupata sehemu za kuficha uso kwa aibu. Tutoe maoni ya kujenga, sio kubomoa. Watu walimpiga madongo Maximo kwa kuwachukua kina Kigi Makasi na Tegete kwenye ziara za mafunzo. Mechi ya kwanza ilivyokuwa ikiendelea hao hao waliokuwa wanalaani chipukizi kufanya ziara za mafunzo wanasema 11 angekuwepo Makasi mambo yangekuwa mazuri. Hata Tegete japo gemu lilimkatalia lakini kocha wa Ivory Coast alimtaja kama mmoja wa wachezaji waliokuwa wanampa homa.
    Maximo ametishia kuongezea vijana saba kwenye kikosi chake na kutema wachezaji wenye majina bila msaada kwa timu. Hii ni dalili kwamba baada ya kulileta kombe la CHAN anataka abaki atupeleke ACN kwanza. Shughuli hapo!

    ReplyDelete
  13. mziray amejidhalilisha sana kwani haiwezekani sehemu kubwa ya watanzania wayaone mafanikio ya Maximo, yeye anayejiita kocha hayaoni!!! why? anataka kuturudisha enzi za Ragge, Wambura na Ndolanga? Anatakiwa asome alama za nyakati kwani watanzania wa sasa siyo watu wa kufurahia majungu ila ni watu wa kutafuta mafanikio ambayo tumeyakosa siku nyingi.

    Namuomba anayeijiita mdau wa Cardif atuombe radhi wazaramo kwa maandishi yake yanayotaka Maximo apewe kigoli wa kizaramo ili abaki. Kwangu mimi maneno hayo yanaonyesha dharau kwa kabila letu

    ReplyDelete
  14. MIGOMBA TENA???????????????????
    hahahahahaaaa mawaziri wetu wamejaa wehu mtupu...

    mpira+ndizi=ushindi Taifa staz

    u made my day

    ReplyDelete
  15. MIMI NADHANI MZIRAY AKAPIMWE AKILI!
    KILA SIKU KUTOA MAONI MABAYA TUUUU JUU YA MAXIMO, HIVI TANGU AWE KOCHA AMEIPATIA NINI TAIFA STARS, NA NI WIVU? MAANA INAWEZEKANA ANAONA MAXIMO ANAFAIDI SANA HELA, NA YEYE AENDE NJE AKAFUNDISHE SOKA, SOKA LA MZIRAY LIMEISHIA HAPO ALIPO, MAXIMO HATA KAMA HAJUI LAKINI KALETA KITU KIPYA, KAANZISHA TIMU HADI SASA INAONEKANA, YALE MAKAPI YOTE KAYATUPA SASA KAANZA NA MOJA, FAIDA TUNAIONA SIO WAO KILA SIKU KUITA MTU MMOJA. MZIRAY KAA KIMYA, JUZI TU SIMBA WAMEKUSHINDA ITAKUWA TAIFA STARS! ANZISHA TIMU YAKO BASI TUONE INACHUKUA UBINGWA MFULULIZO WA LIGI KUU, NA MAKOMBE YOTE ILI IWE TIMU YA TAIFA. SIO MWENZIO ANAJITAHIDI WEWE UNABAKI KUBWABWAJA, MCHAWI NINI?- BUBE

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...