Mkuu wa Uendeshaji wa kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Peter Correia(katikati) akimkabidhi Mganga mkuu wa Hospitali ya Mwananyamala Suleiman Mutani (kulia) moja ya vitanda vilivyotolewa na Vodacom Foundation vyenye thamani ya shilingi milioni 40 katika kusherehekea siku yao,(kushoto)Mkuu wa Vodacom Foundation Mwamvita Makamba.
Mkuu wa uendeshaji wa kampuni ya simu za mkononi Vodacom Peter Correia akimkabidhi Bi Mariam Hamidu aliyelazwa katika hospitali ya Mwananyamala moja ya zawadi zilizotolewa kwa wagonjwa wakati wa kusherehekea siku ya vodacom foundation Day ambapo walikabidhi msada wa Vitanda kwa Hospitali za mkoa wa Dar es Salaam vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40.
Mfanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom akiwa amembeba mtoto mchanga katika hospitali ya Temeke mara baada ya kutoa msaada wa vitanda na mashuka yaliyotolewa na Vodacom foundation yenye thamani ya shilingi milioni 40.


Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania jana imesherehekea siku maalumu ya mfuko huo wa kusaidia jamii ( Vodacom Foundation) katika kusherehekea siku hiyo, Mfuko huo wa Vodacom umezikabidhi hospitali za wilaya za mkoa wa Dar es Salaam msaada wa vitanda maalum kwa akina mama wajawazito vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 40.

Msaada huo ulikabidhiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Vodacom Tanzania, Bw. Dietof Mare kwa Waganga Wakuu wa hospitali hizo.

Baadhi wa waganga hao waliipongeza Vodacom kwa msaada huo kwani utasaidia kuboresha utoaji wa huduma katika hospitali zao.

Hospitali zilizofaidika kwa msaada huo ni Amana (Ilala) ,Temeke na Mwananyamala (Kinondoni) .

Sanjari na utoaji wa msaada huo kwa mkoa wa Dar es Salaam, Vodacom ilitoa misaada ya aina hiyo katika hospitali za serikali katika mikoa ya Kigoma,Iringa,Kagera na Tanga kupitia kwa wawakilishi wake waliko mikoani.

Waganga hao walisema msaada huo ni uthibitisho wa ushirikiano imara baina ya Vodacom na sekta ya afya hapa nchini na kwamba ushirikiano huo umekuwa ukiimarika kadri muda unavyokwenda.

Walisema serikali mara nyingi imekuwa ikiiomba sekta binafsi kushiriki katika kuboresha mazingira ya upatikanaji wa huduma bora za afya hapa nchini, hivyo basi ushiriki wa Vodacom ni sehemu ya mchango wa sekta binafsi kwa maendeleo ya jamii.

"Tumefarijika sana kuwaona Vodacom wanashirikiana katika sekta hii muhimu ya maendeleo ya jamii," walisema.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Dietof Mare, alisema Vodacom Tanzania kupitia mfuko wake itaendelea kuiunga mkono serikali katika kuboresha sekta ya afya hapa nchini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Jengo hili limejengwa kwa msaada wa Japan! Uwanja huu China! gari hili USAID! vitanda hivi VODA! Na Mashaka atengeneze vijilebo viwe vikiwekwa kwenye mablanketi atakayotoa next time uchumi wa US & A ukichukua tena kasi akaendeleza dili za Investment Banking - au siyo? Yeees - I think so! Kitu kama "MSAADA WA JOHN MASHAKA, Investment Banker US & A"

    Nguo yoyote uliyowahi kumpa mtu wewe mdau, au Mheshimiwa DC, umewahi kudarizi kifuani au kwenye kola chata yako kama "AKUMBUKWE DC MILELE!!"? Mbona serikali za nje zote zinafanya hivyo kwa kila vijimiradi wanavyofanya? Kama kweli hizo ni zawadi na misaada tu?

    Au na sisi kama nchi twende kwenye mipaka ya nchi zote tulipotuma wanajeshi wetu na tuweke na kulipia mabango katika lugha za wenyeji "NCHII HII ILIKOMBOLEWA TOKA MIKONONI MWA NDULI ...... KWA MSAADA WA JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA. Halafu uone reaction ya raia. Watachukia - tena hivi sisi sio Wadhungu!

    Tunapendwa Watanzania jamani na haya makampuni!! Hii misaada yote bureee kabisa!! Idumu Voda na fikra zake kama Chama Chetu na fikra zake!

    Kuna kitu nashindwa kuki-articuRate hapa lakini hii mambo ya kushangilia misaada inabidi tuyapunguze. Labda kuna kizazi kitafuata kitakachotambua kwamba kama ambavyo haya makampuni yanavyotumia hii "misaada" watu wote tukapiga makofi, ndivyo na nchi zenye hela zinavyotumia misaada yao na kisha kutupeleka wanavyotaka. Baada ya misaada yote hii ya VODACOM ndo baadae serikali ipate ujasiri wa kuwakomalia VODA na wenzao waingie gharama ya kuweka mitambo ya kutambua kila namba ya simu nani mmiliki? Si watatishia kusimamisha hii misaada sasa!

    Pamoja na uozo na uvundo wa serikali yetu kuna mambo kidogo wanafanya na hakuna anayempa mtu yeyote credit. Tunawaona wote hawafanyi kazi na ni wezi tu. Mpaka atokee mtu anayeelewa athari za kutujaza watz huu utegemezi ndo asubuhi itakuwa imeingia.

    Kama Dr. Nishomire mimi ningekuwa nafanya maongezi na Waziri fulani muhusika - wa Ailim, Utamaduni au wizara stahiki ningeleta hoja binafsi kuzuia kabisa yeyote anayetoa misaada na kudai chata zake za kudumu ziwekwe kwenye magari, majengo n.k -- kwa sheria kupitishwa -- kwamba huu utegemezi wa nchi yetu na raia wake umeingia sana ndani ya bongo zetu. Hata wananchi hawajui kama Serikali inafanya kazi yoyote ile!! Wakati wa kuzuia kuenea kwake ni sasa. Futa mabango yote ya "Msaada wa ........ Toa ajira kwa vijana kufuta mabango yote hayo. (Kama walivyositisha namba nyekundu za kizayuni za "TX")

    Hawa watoa misaada wataendelea kutoa tu, watatafuta jinsi nyingine ya kuharibu watoto wetu akili lakini kwa sasa tutakuwa tumeenda nao sambamba

    Wasalaam, Dr. NG

    ReplyDelete
  2. stella mama you ROCK !! even in a uniform

    ReplyDelete
  3. Hongera Vodacom (T) Ltd. Tunashukuru kwa misaada hiyo na kukumbuka kuwa nchi yetu ina uhitaji mkubwa wa Makampuni kama yenu.

    Sasa kuhusu hizo t-shirt zenu kweli huwa zina waangusha mno. Yaani ukiifua mwisho mara MOJA. Baada ya hapo ni ya kupigia deki tu!! Niliipata moja kwenye promo yenu inayoendelea kwa sasa. Ushauri wangu jaribuni kutengeneza kitu quality kama huduma zenu zilivyokuwa bomba!!!!. Watani wenu wa jadi wanakushindeni wakati nyie ndo mko JUU!!!!

    ReplyDelete
  4. Misaada wowote ni mizuri,ila kwa kitambo tu.

    ReplyDelete
  5. ni kweli annon asa msaada ukiwa ni t-shirts na sabuni au colgate..

    vitanda vingapi?ok anyway
    asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...