Napenda kuwatahadharisha wadau wote kuwa muwe makini zaidi mkiwa barabarani hasa kwenye foleni jijini Dar kwani kuna kundi la vijana zaidi ya 30 maarufu kama 'KIBOKO MSHELI' wanaovamia magari wakiwa na mapanga,nondo na visu kwa lengo la kupora chochote ulichonacho na halikadhalika wanauwa ama kujeruhi.
Maeneo hatari ni maeneo ya Jangwani- Morogoro Road,Ocean Road, Seaview, Salender Bridge, Bonde la Kigogo ukitokea Ilala kuja Magomeni, Daraja la Ubungo karibu na njia panda ya kwenda UDSM na barabara ya Mandela Road ukitokea Tazara kuja Ubungo (NDIPO ALIPOVAMIWA RAFIKI YANGU)
His Case.
Akiwa kwenye folen majira ya saa mbili usiku, ghafla lilitokea kundi la vijana kama kumi na mapanga na kuanza kupiga vioo vya gari
wakitaka kuvunja, aidha waliongezeka ghafla na wakafunga barabara kama kwa dk 7 hivi wakiendelea kumshambulia (kwenye gari walikuwa watatu),kumbuka kwenye foleni huwezi kukimbia popote, Mungu aliwasaidia sana kwani milango ya gari ilikuwa imefungwa/locked, na vioo vilikuwa vimefungwa kasoro kimoja kilikuwa wazi nusu.
Baada ya mapambano na kelele za kuomba msaada,ndipo msamalia mwema aliyekuwa na silaha aliingilia kati na ndipo alipowatawanya.Kwa mujibu wa Taarifa mbalimbali, haya matukio yamekuwa yakiongezeka sana katika siku za usoni, kwa hilo nawatahadharisha msinunue vitu ovyokwenye traffic light, vioo msishushe ovyo na lock za milango ya magari mfunge, muwe makini.
Ujambazi huu unafanyika kila siku sehemu tofauti kuanzia saa 12 jioni kuendelea.
Namshukuru Mungu hakuna aliyeumizwa sana, japo walifanikiwa kupata baadhi ya vitu ikiwemo simu ya mwenye gari.Natambua unaweza kuona kama sinema,ila haya ndio yanayotokea katika jiji la Dar kwenye foleni za magari.
Mdau Dar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 18 mpaka sasa

  1. Naam, bongo tambarare ka Jo'Burg vile, unaweza kupoteza uhai kwa kitu kidogo sana.

    ReplyDelete
  2. hii ni hatari sana .........tunaomba jeshi la polisi waweke usalama kwenye hayo maeneo ........kama tumefika huko sasa ni kubaya

    mdau dutch

    ReplyDelete
  3. Haya ndio matokeo ya UFISADI; unapokula pesa ambayo ingenunua madawa hospitalini kisha mzazi akakutwa na mauti kwa kukosa dawa na kuhacha mjane na yatima unadhani yatima atafanya nini? Jibu, lazima atakusubiri barabarani ukiwa na gari uliyonunua kwa kufisadi fedha za kodi. HUU NI MFANO, pole kwa uvamizi tulinde roho zetu na za jirani zetu.

    ReplyDelete
  4. BONGO TAMBALALE

    ReplyDelete
  5. Tumeanza kuvuna matunda ya "Explosive Youth Unemployment";"Exportation of Domestic Jobs overseas";"the widening and growing income inequalities";"the repressive domestic taxation regime";economic slump;irresponsible government and civil management;distorted and misdirected economic policies;poor incomes and inflated basics;....niendelee au nisiendeleeee?.......aaaaah!usiendelee una BORE bwaaaana!.....well check me out!piss

    ReplyDelete
  6. Serikali inakataha kuwasomesha vijana kwa madai gharama kubwa,wakati kilasiku MAFISADI mnachota kiasi kikubwa cha pesa.Wangekua na elimu nawao wangetumia wizi wa kalamu

    ReplyDelete
  7. Hiyo Jobegi ilimkuta pia rafiki yangu maeneo yha bonde la kigogo/ mikumi. Kuna haja yha kutafakari je bdo nchi yetu ni kisiwa cha amani??????

    ReplyDelete
  8. LAURE MASHA, HA...HA..HABARI NDO HIYO. NASIKIA HARUFU YA ANKARA....,
    HA...HA...HABARI NDO HIYO. NASIKIA HARUFU YA EPAAAA...


    Mdau
    Cardiff

    ReplyDelete
  9. hii mbona haitoshi! inabidi tufanyiane kwanza kama rwanda na burundi. ingawa ya kwao ilikuwa ya watusi na wahutu, yetu inabidi iwe ya watawala na watawaliwa. Huu ndo mwanzo wa kurekebisha mambo. Bigz up kiboko msheli lakini inatakiwa kuelekeza mapambano kwa watawala kwanza.

    ReplyDelete
  10. Jamani hayo ni matokeo ya uchumi wa Dunia (Marekani) kuyumba ndio mnaona side affects zake. Sijui serikali itafanyaje ku-create employment

    ReplyDelete
  11. Hee jamani tunakoenda ni kubaya tene sana.kama tusipoangalia tutachinjana kama kuku, lakini sababu inajulikana, ni ugumu wa maisha unao sababishwa na MAFISADI, mtu mmoja anaingiza dola laki kwa siku, mwingine hana hata cent moja, hajui atakula nini, kwa hiyo wanakuwa na njia za ajabu ajabu za kujipatia ridhiki. siwasapoti kwa wanayoyafanya, lakini inabidi uchunguzi wa kina uwepo kwa nini mpaka wanaamua kufanya unyama wa namna hiyo, sio swala la POLISI peke yao. niko karibu na Burundi na Zaire ndiyo walivyoanza hivyo hivyo,mpaka ikaumuka VITA na kama hamuamini maneno yangu VITA vinanukia,Mdau kigoma.

    ReplyDelete
  12. KAMA JOBERG, SOUTH AFRICA NI HIVYO HIVYO TENA KULE HATA MCHANA MWEUPE, WAO WALICHOFANYA AMBCHO KINASAIDIA KIDOGO NI KUWA WALIAMUA KUWEKA CCTV JIJI LOTE ZIKIWA ZINAKUWA CENTRALLY MONITORED AT CENTRAL POLICE NI ZA KISASA KITEKINOLEGIA, HATA HIVYO BADO WATU WANAFANYIZIA KWANI CAMERA ASHIKI MWIZI INACHOFANYA NI KUTUNZA TASWIRA/SURA ZAO NA KUWAFUATILIA NA KUWAKAMATA NA PICHA KUTUMIKA KAMA USHAHIDI MAHAKAMANI, ZINASAIDIA, WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA SAID MWEMA IGP WAENDE WAKAJIFUNZE HUKO. PIA HUO NI UDHAIFU WA POLISI, MIMI NINAVYOJUWA KAZI YA POLISI NI YA 24 HOURS NA OFISI ZAO NI MITAANI WAACHE KUKAA OFISINI TU, WANATAKIWA WAWE MITAANI SASA ZOTE NA VIFAA VYA KISASA VYA MAWASILIANO IKIWA NI PAMOJA NA MAGARI YENYE MBIO YA KISASA, NA HELICOPTER YA KISASA YENYE MBIO PIA NA VIFAA VYA MAWASILIANO VYA KISASA. MPAKA AVAMIWE WAZIRI AU MKEWE NDO TUTAONA ACTION SISI WALALA HOI TUFE TU. NDO BADO MNASIFIA SERIKALI NA BUNGE LETU BOVU.

    ReplyDelete
  13. rgus us so true. dada yangu nimeongea naye kwa simu anaishi osterbay wamemnyang'anya simu yake over the weekend alikua kwenye gari akielekea nyumbani kwake anasema karibu na mbuyuni primary alikua mwenyewe na aliogopa sana..walikua vijana watatu

    ReplyDelete
  14. SASA MIMI NSHANGAA NYIE MAFISADI MABILIONI YOTE YALE MLIOIBA SISI TUKIWANGOJEA KUWACHUKULIA JAPO SIMU ZENU ZA MIKONONI NA VIPOCHI VYENU MNAHAMAKI KIASI HIKI?MNATEGEMEA SIE TUKALE WAPI?????HIVI MTU ALIEKWIBA BILIONI 15 TU AKIIBIWA SIMU KILA WEEK ATAPUNGUKIWA NA NINI?KWA MWENDO HUU MSILALAMIKE NYIE MWAIBA KWA KALAMU WENZETU SIE NDIO TUNAJILIPA NAMNA HII NA SISI,KWAHIO KILA MTU ANAKULA KIDIRISHANI KWAKE SI MMETAKA WOTE TUWE MAFISADI TUENDELEENI TU TUUONE MWISHO WAKE

    ReplyDelete
  15. bongo bongo bongo unapesa zako lakini wasiwasi kibao,wapi jeshi la polisi ,wapi viongozi wetu tuliowachagua,mbona hilo ni swala dogo sana,ningekuwa mkuu wa polisi apo dar wangenikoma,kwanza ningeomba niogezewe polisi mara mbili zaidi ya walioko dar, na naweka patrol kila kona ya dar polisi wa miguu ,baiskeli na waendao kwa miguu 24/7, nini chenye
    thamani kuliko maisha??

    ReplyDelete
  16. Kila siku nazidi kuongeza sababu za kuishi Ughaibuni na kutotaka kurudi kuishi africa, tena africa nzima (bongo ikiwepo)....CCTV africa nzima zipo ikulu na bank, wahalifu mtawakamataje?? Poleni sana wadau na wote mliolumbwa na mkasa huu, mi yashanikuta nilipokuwa likizo hapo,
    Kuna mtu anasema mafisadi wanaibiwa, Hivi jamani hata mie mtoto wa mlala hao niliyekimbilia ulaya kwa kupitia souz tena kwa hela ya kubangaiza naitwa fisadi kisa natembelea gari na kwa mama yangu nimemuwekea makazi mazuri na salama??? ama kweli nchi zinaenda majini hizo.

    ReplyDelete
  17. Wadau,hii hali si mchezo.haya ndiyo matokeo ya kuendelea kuishi kwa matumaini ya kwamba kuna ajira mil.1 zitapatikana kwa vijana!Je,hawa wanaopoteza ajira wanafanyaje?Je,ajira hizo zinapatikana lini wakati kwa sasa wawekezaji wanafunga majanvi yao na kuondoka kwa ajili ya mtikisiko wa kiuchumi,si kilimo maana mvua nazo zimegoma mwaka huu,Wazee na viongozi serikalini hawataki kuwapisha vijana washike hatamu,Jumuia ya Afrika Mashariki nayo yaja wakati yaelekea sisi wa-TZ hatuko tayari(hasa kielimu maana kama tunasema hatuna hata waalimu wazuri wa hisabati basi wenzetu watakuwa na nafasi nzuri ya kuja kutupigia mahesabu yetu na pia kutusaidia kuongea Kimombo!)Kama hao vibaka wa sasa ni wale walioishia elimu ya msingi,basi subirini zamu ya wale waliosoma zaidi na kukosa ajira.Jamani,hili si suala dogo,ni bomu kubwa ambalo limebakiza muda kidogo tu kulipuka!

    ReplyDelete
  18. Kuna Naibu Waziri mmoja aliniacha hoi sina mbavu asubuhi moja katika TV LIVE,pale aliporushiwa kombora moja abaelezee watanzania kuhusu tatizo la ukosefu wa ajira nchini limeshughulikiwaje na serikali yake,alipojibu kwa ujasiri mkubwa,"kuhusu ajira najisikia raha kutamka wazi bila kificho watanzania wote wanisikie hata wale viziwi kwamba serikali imefanikiwa kutengeneza nafasi za ajira milioni mbili,hivi ninavyozungumza nanyi,ajira mpya milioni mbili zishatengenezwa kupitia mikakati ya kimapinduzi na mipango imara ya ujasiriamali kama ilivyoghani Ilani ya Uchaguzi.Ni ajira mpya kwa kwenda mbele!Atakayechukia na animeze,wala havinitishi".Alipobanwa zaidi athibitishe kauli yake kwa kutoa vielelezo na takwimu sahihi,Naibu Waziri alijibu,"ebo yaani huiamini serikali wewe?vielelezo vya nini kwanza,umesikia tuko Polisi hapa?na huyo atakayetaka takwimu mie sitembei na LapTop hilo ulijue,lakini kukuthibitishia wewe king'ang'anizi wa takwimu ni hivi,hiyo ajira mpya ya milioni mbili utaipata katika 'informal sector baba'!Kumbe,ulifikiri 'formal sector?'.Unafikiri sisi wajinga,tukwambie iko katika 'formal sector'upate urahisi wa kwenda kucheki?Hapo umeangukia pua,labda mngoje Naibu Waziri mwingine atakapo teuliwa!Na hiyo sijui lini!Mipete unaiona hii kibao kwenye madole yangu,mchezo?Kila pete hapa lina kazi yake.Eeehe,ukiutaka uwaziri babu shurti uuvulie nguo babu,nshakupasha!tehe tehe tehe tehe!ipo kazi inji hii!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...