Mgonjwa wa saratani akipata huduma Ocean Road Cancer Insititute (ORCI) asubuhi leo hii baada ya kununuliwa kwa vifaa vilivyokuwa vimeibwa yapata wiki mbili zilizopita.
Hii ndo aina ya mashine zilizoibwa yapata wiki mbili zilizopita pale ORCI zaitwa Control Console, zimenunuliwa tena mpya kwa gharama ya Dola za US 22,000/- na hivyo wagonjwa wameanza tena leo kupata huduma baada ya kusimama kwa muda wote huo.
Mdau Bernard Rwebangira anashindwa kuelewa mashine kubwa na nyeti kama hii iliiniwaibiwaje? ungana naye kujadili hilo kwa kubofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. jamani hebu waweke security camera kuwabana watu wanaoiba vifaa kama hivi kaa watanzania bana!

    ReplyDelete
  2. control console sio machine kubwa ni hiyo remote yenye waya

    ReplyDelete
  3. HIYO MASHINE KAMA NIJUWAVYO INA MLOLONGO WA SYSTEMS SASA ALIIBA SYSTEM NZIMA AMA KIBANDE TU, KAMA MLOLONGO WOTE BASI NI HAO HAO WAFANYAKAZI WANA HOSPITALI ZAO NJE YA HAPO, SASA WEZI WEMEENDA UZA WAPI? NJE YA NCHI! WEZI NI WENYEWE STAFF NI CHANGA LA MACHO TU, NI UZEMBE MTU APO AMWAGWE MLO.

    ReplyDelete
  4. piga ua INSIDE JOB

    ReplyDelete
  5. tatizo hatuendi na wakati,namuunga mkono mchangiaji wa kwanza.Inabibidi waweke CCTV sehemu zote nyeti za hospital.Vinginevyo tuanze kuchapana viboko tu.....

    ReplyDelete
  6. haikuibiwa, iliwekwa kwenye boksi tu wakajifanya kwamba wamesahau kwamba wanayo.
    Then waka-iagiza na kuinunua mpya hewa.Fuedha wakagawana hao, hamna lolote. Kisheria huwezi vaa shati kama hilo bila koti jeupe au la kijani na kumhudumia mgonjwa.
    Tatizo Tanzania, ukishakuwa expert basi hutaki makoti au sheria za nguo zinatokaiwa kuvaliwa , unataka mashati mazuri ya ofisi na suruali za kitambaa.
    Huyu jamaa ofisa!!! au.

    ReplyDelete
  7. Acha ushamba iliyoibiwa ni control console—ambayo ni device ndogo kama kompyuta inayoongoza na kuendeshwa kwa kutumia mwanga wakati wa kumpima mgonjwa, au hilo li- CT SCan.

    ReplyDelete
  8. Aliyeeiba ni huyo huyo jmaa hapo anaeonekana ameva shati la bia. Maana ndio anajua kazi yake ni nini. na wapi pa kuiuza. Ikipotea kitu kama hicho hapa India, nafukuzwa mlinzi, na wafanyakazi waliokuwepo siku hiyo hapo ofisini siku kifaa kilipopotea. hii inawafanya watu hapa India hospitalini kutokuwa wezi. Maana kibarua kitaota majani wakati sio wao walioiiba.

    ReplyDelete
  9. hapo ilikuwa nikutembeza bakora kwa wafanyakazi wote mpaka wangesema nani kaiba.

    ReplyDelete
  10. Ninavyojua mimi hayo maeneo yana matukio ya wizi wa ajabu ajabu sana sitashangaa kusikia siku moja ikulu kumeibiwa

    ReplyDelete
  11. annon apo juu mesema kweli kabisa,,hiyo ni "biashara ya wazi"kama kawaida unanunua vifaa "hewa" afu mwagawana bonus ya mwaka,,hahahahaaa
    inauma sana,,
    ajavaa koti ndo utaratibu?

    ReplyDelete
  12. Nilitaja jina la mwizi lakini naona mwenye blog kaminya. Naelewa. Basi mkitaka kumjua mwizi muulizeni CEO wa ORCI anamfahamu vizuri sana mwizi ni nani. Na Wizara ya Afya inamjua.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...