MKUTANO wa kutathmini utendaji wa Serikali kati ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete na uongozi wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko, pamoja na taasisi zake, uliofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, kwa kiasi cha saa tisa mfululizo jana, Alhamisi, Februari 19, 2009, umefikia makubaliano muhimu yafuatayo:

*Kwamba zichukuliwe hatua za haraka kuboresha mazingira ya kufanya biashara na kuhudumia kwa ufanisi na ubora zaidi uwekezaji nchini kwa maofisa wa Serikali kupunguza urasimu, kufanya maamuzi ya haraka, kuhakikisha kuwa msimamo wa Serikali unatabirika, na kupunguza misimamo ya kisiasa inayojenga hisia za kutishia wawekezaji.

*Kwamba hatua za haraka zichukuliwe kuvutia wawezekaji katika eneo la kusindika mazao ya kilimo na vyakula, ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda vya matunda na mboga, na kusindika bidhaa za nyama.

*Kwamba zichukuliwe hatua za kuwahamasiaha Watanzania kuingia katika eneo la kunenepesha ng’ombe kama njia ya kuhudumia sekta ya viwanda vya kusindika bidhaa za nyama
*Kwamba nguvu za kuanzisha viwanda zielekezwe katika viwanda ambavyo vinaweza kupata malighafi kwa urahisi hapa hapa nchini.

*Kwamba juhudi za makusudi zifanywe kuhimiza uwekezaji katika viwanda vya saruji nchini kwa sababu ya uwezo wa viwanda hivyo kuchochea maendeleo ya haraka ya maeneo mengine ya uchumi.

*Kwamba njia ya Uhuru Corridor itiliwe maanani kama yalivyo maeneo mengine katika mipango ya uwekezaji nchini kwa sababu njia hiyo tayari inayo miundombinu muhimu na ya msingi kuweza kuchochea maendeleo ya haraka.

*Kwamba idara za viwanda na biashara katika Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko ziimarishwe kwa nia ya kuzipa uwezo mkubwa zaidi wa kuhudumia mchakato wa kuanzishwa viwanda nchini na kuimarisha biashara.

*Kwamba zifanywe jitihada kubwa zaidi kuimarisha eneo la utafiti nchini, na ili kupiga hatua muhimu katika eneo hilo, Rais Kikwete ametangaza kuwa katika Bajeti ya Serikali ya mwaka ujao wa fedha, Serikali itatoa kiasi cha asilimia moja ya Pato la Taifa kwa ajili ya utafiti badala ya kiasi cha asilimia 0.3 za sasa.

Kwa wiki hii, Rais Kikwete amemaliza mikutano yake hiyo baada ya kuwa amekutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na taasisi zake, na Wizara ya Elimu na Mafunzo na taasisi zake kabla ya mkutano wa leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 10 mpaka sasa

  1. Anakutana na Wizara ya Mambo ya Ndani lini?

    ReplyDelete
  2. 'Enzi za Mwalimu'tulikuwa na viwanda tukaviua sisi wenyewe,ona sasa tunavyohangaika.tunarudi tena tulikotoka.Sisi watanzania ni watu wa ajabu sana.

    ReplyDelete
  3. Misupu na wadau wa blog, hii "njia ya Uhuru Corridor" ndio nini na iko upande gani wa Tanzania? Naomba mnitoe tongotongo wakubwa!

    ReplyDelete
  4. MANENO YA MAAZIMIO YAO NI MATAMU...TAABU IPO KWENYE MATENDO......SI AJABU SEMINA ELEKEZI HIZI HAZIWAINGII KICHWANI WATENDAJI!

    MFANO YULE MKUU WA WILAYA YA BUKOBA HAKUWEPO NGURDOTO KWENYE SEMINA ELEKEZI?

    .......WADAU...MIMI SIJASEMA!

    BRO ISSA NAOMBA YALIYOJIRI WAKATI WA MKUTANO NA RAIS KWENYE WIZARA YA GLOBU NA MAMBO YA ICT...A.K.A . Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia na taasisi zake?

    ReplyDelete
  5. Asante na shukurani zetu kwa mheshimiwa rais JK. Hii ni hatua muhimu. 'Government-led development inahitaji kazi nzito. Serikali isiishie kutoa maelekezo tu. Ili mara hii tufaninikiwe, itabidi tuzingatie a few things: Kwanza, Mipango maalumu yaani 'action plans' zinahitajika haraka iwezekanavyo ili kuhakikisha utekelezaji wa kila moja ya haya maazimio na pia kuwezesha tathmini madhubuti kufanyika periodically ili wanachi wote waone (viwekwe kwenye mtandao kama wanavyofanya kule marekani).

    Pili, ni MUHIMU kwa kuanzia serikali ijitahidi ipate 'donor support' ili kuwekwe mfuko maalumu wa kusaidia benki zetu kutoa mikopo kwa local entrepreneurs katika sekta hizi nyeti. Lakini kiundwe chombo maalum cha rais ili Mikopo/ benki zidhibitiwe kupunguza ubadhirifu.

    Tatu, inahitajika sheria zitungwe haraka ili kupunguza mzigo wa kodi kwa viwanda vipya (vidogo vidogo) kwa miaka miwili/mitatu ya mwanzo hususan kwenye sekta hizi nyeti. Mikopo pia iwe soft loans na siyo kwa nia za mabenki kujitajirisha.

    Nne, Serikali sasa ni lazima i-partner na sekta binafsi katika sekta hizi maalumu ili kuweza kutoa 'protection' kwa viwanda nyeti. I mean joint ownership of major corporations (sio natinalisation!). Hii pia itasaidia katika kufanya tathmini na kutoa guarantees kwa mikopo mikumbwa endapo itahitajika kurahisisha utekelezaji.

    Tano, tusiishie kwenya ng'ombe na matunda peke yake. Ili kupata economic 'take off' tunahitaji serious and TARGETTED upgrade ya miundombinu. Tukumbuke, misaada minge imefika TZ lakini uzalishaji mbovu yaani under utilisation na low productivity kwenye viwanda
    vyetu ndio imekuwa ikitu let down. Fedha peke yake haitoshi. Technology transfer agreements na local work ethic za wafanyakazi viwandani pia ninahitaji kuangaliwa upya.

    Pia, tujaribu kuboresha uwezo wa wachimbaji wazalendo. Enhancing technologies for local mining capacity is key ili tuchimbe dhahabu yetu wenyewe na pesa zetu zote zikae nyumbani,na sio asilimia tatu tu. Wenzetu kule Amerika ya kusini na Asia ndivyo wanavyofanya siku hizi. Brazil wana Brazil Petroleum corporation yao wenyewe. Na sisi tunataka Tanzania Mining Corporation yetu wenyewe na siyo kutegemea wageni wachimbe, wachukue kila kitu na mwishowe ndio watuachie chenji tu. Tu-invest kwenye training of local mining expertise.

    Sita, ndiyo, saruji muhimu. Lakini kama wakandarati watajenga majumba yanayobomoka ovyo haitasaidia. Inabidi tuangalie process nzima na siyo saruji pake yake. Ukaguzi wa majengo kabla, during na baada ya kumalizika ujenzi ni muhimu. vile vile wawekezaji kwenye ujenzi wanatishika kama umeme ni wa kubahatisha. Tuzingatie possibility ya projects za solar powered towns. Hii wala si ngumu. mali ghafi zote tunazo. Wenzetu kule Japan na Indonesia wana technologia za ujenzi nyumba bora kwa bei ya chini sana. Tuwasiliane nao ili wasaidie kufundisha watanzania. Tukishajua tutafanya wenyewe.

    Saba, swali, je serikali ina aim kwa 'labour intensive' development (LID)(ili watu wapate ajira) au 'capital intensive project' kufix BOP deficit? Ya kwanza (LID) inasaidia survivalna kupunguza uhalifu nchini kwani watu watapata ajira. Lakini kama tunataka export driven economy, ni lazima tuangalie pia 'capital intensive', katika sekta kama product recycling/ overhauling (kwa kuuza nchi jirani). Joint owbership na wawekezaji toka nje inawezekana kwa hii ku-take off. Pia, wataalamu wetu katika vyuo vikuu vilivyopo hapa nyumbani wanaweza toa mchango mkubwa katika hili. It's also cost effective ikiwa tuta-focus kwenye transfer of older technologies.

    Nane, Tusisahau kuwa aggressive marketing ya products zetu nchi za nje ni muhimu sana. Serikali ifanye mikakati maalum ya kuimarket 'Tanzania' nje ya nchi ili kuonyesha ni vipi hii Tanzania mpya inatofautiana na 'image' ya Tanzania ya zamani. Ili products zetu zishindane na zile takutoka India au China katika soko la dunia, country image is central. Angalia jinsi wenzetu wa Asia wanavyo-market nchi zao katika CNN, BBC, n.k. Inasaidia utalii pia.

    Tisa, tusisahau teknologia ya umwagiliaji. Ngo'mbe hawanenepi kama majani hayakuota vizuri. Hapo hapo, msaada maalumu kwa veterinaries. Hatutaweza jenga a strong agricultural base kama skilled manpower itasahaulika. Human resource development, na Science and technology is key to capacity building. Bila ya kusahau a serious revision ya salary scales. Je serikali iko tayari?

    Kumi, tusiwache kuwahamisisha wanachi ili sote pamoja tuchangie kwa hili. Rushwa, uzembe na ufisadi vipigwe vita. Mungu ibariki Tanzania.

    Asante Michuzi kwa hizi posting zako. Nimeiona leo na nikaamua kuandika haya kwa sasa. Lakini kama nikipata idea zingine zaidi nitatuma.

    ReplyDelete
  6. Mimi binafsi muhtasari huo wa maazimio baina ya Rais Kikwete na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Viwanda bado umenitia woga sana kwamba bado hatujui nini tunachopaswa kufanya katika sekta ya viwanda kwa sasa na kwa malengo ya muda mrefu.Maazimio hayo yameshindwa kutoa "Situation Analysis" ya sekta ya viwanda nchini.Yameshindwa kuja na "Identification of Basic Domestic Needs" mahitaji ya msingi ya nchi kwa sasa na kwa wakati ujao!Ni kutokana na ubainishaji wa maeneo hayo mawili muhimu kwamba utaweza kutambua ni mwelekeo gani wa uwekezaji katika viwanda utahitajika na ni aina gani ya viwanda vitakavyo hitaji kutiliwa mkazo na kupewa kipau mbele!Sikusikia popote likizungumzwa suala la "gharama kubwa za uzalishaji viwandani" kama kikwazo kikubwa kinacho wakimbiza wawekezaji hapa nchini.Sikusikia popote suala la mfumo mbaya wa kodi nchini,wa kutoza kodi hadi malighafi,na namna gani serikali itakavyo lishughulikia.Pamezungumzwa Unenepeshaji wa Ng'ombe kwa ajili viwanda vya kusindika nyama.Lakini sikusikia popote pale likizungumziwa suala la Viwanda vya Usindikaji wa Maziwa ya Ng'ombe na bidhaa zake.Viwanda vingi vya maziwa vimekufa hivi karibuni kwa kukosa support ya serikali against unfair competition na repressive taxation!Papo hapo serikali inawahamasisha wawekezaji wajitokeze zaidi kuwekeza katika viwanda hivyo.It beats all stretches of imagination.Kwa jinsi ninafahamu mimi,wizara ya viwanda per se is just too weak resource wise to bring about any meaningfull change in the country.Serikali imechezea sana Wasomi wake na Wataalamu wake kwa kuwapa maslahi duni kabisa na mishahara mibovu,ambayo haitaisaidia serikali wala wale waliokuwa wakipitisha maamuzi hayo.Watanzania wetu hawa hawa tuliowasomesha tunawadhihaki,nchi hii itakuja kujengwa na nani?Hakuna hata Mkoa mmoja wenye Integrated Industrial Plan yake yenyewe!Check me out!How do you talk of industries in this country?Labda kama mikutano hii ni Routine Exercise ya kutimiza mradi siku ziende!Hapo sawa.

    ReplyDelete
  7. URASIMU WA WATENDAJI UNAKUJA KWA SABABU YA KU-CREATE LOOP HOLE YA RUSHWA, CHA MSINGI NI KUPIGA VITA RUSHWA KWA SILAHA ZA AINA ZOTE IKIWEZEKANA HATA MABOMO YATUMIKA, AU MABOMO YA KUJILIPUA / YA KUJITOA MHANGA KAMA IRAQ

    ReplyDelete
  8. Kwenu Wadau,

    Nimetafakari kwa kina kuhusu mikutano hii ya Raisi na watendaji wakuu wa Wizara mbalimbali na maazimio yake baada ya kushindwa kuelewa mantiki yake mwisho na mimi nimefikia majumuisho yangu binafsi kuwa:

    1. Raisi amesahau kazi yake
    2. Hivi vikao havina nafasi
    yeyote katika utaratibu mzima
    wa utendaji wa Serikalini.
    3. Hakuna muelekeo wowote kuwa
    nani anawajibika kutekeleza
    maazimio ya vikao hivi, Muda wa
    kutekeleza, nani au utaratibu
    wa kupima matokeo na nini
    kitafanyika ikiwa utekelezaji
    utakuwa hauridhishi.
    4. Raisi anapoanza kufuatilia
    risiti ni hatari maana wakaguzi
    wa mkaguzi wa hesabu wafukuzwe?!

    Kwa elimu yangu ndogo naelewa kwamba kazi ya Rais ni kuweka sera bora, kuzisimamia, kupima matokeo yake. Na Kikao kikubwa kabisa cha Kiserikali kinachopaswa kusimamia utekelezaji wa Sera za Serikali ni Baraza la Mawaziri na ambacho Raisi ndio mwenyekiti wake.

    Sasa bila kurudi katika utaratibu wa serikali na kuhakikisha kuwa mfumo mzima wa serikali unaifanya kazi yake kikamilifu, kuweka sera mathubuti na kusisimamia tutaendelea tu kukutana, kuongea, kupiga porojo, kusemana halafu kila mtu anaenda nyumbani bila mafanikio yeyote.

    Huu ni mwaka wa nne wa serikali hii na hakuna sera bayana kuhusu Elimu, Afya, Viwanda, nk

    Ushauri wangu kwa Raisi wetu ni kurudi kwenye utaratibu wa kiserikali, kuhakikisha serikali yake inafanya kazi. Na pale ambapo kuna wanaozembea basi aweke utaratibu wa hao watu wajulikane na waondolewe. Kusemana, Kukaripiana hakutakuwa ni jawabu na vikao vya kuwekana sera sio badala ya Sera.

    Mungu Ibariki Tanzania,
    Mungu Iokoe Tanzania,
    Mzawa.

    ReplyDelete
  9. Ukweli ni kwamba Wizara zetu zote zitahitaji kusukwa upya kimuundo na kimfumo ili zikidhi matakwa na mahitaji ya nchi.Na watako weza kuifanya kazi hiyo ni wale waliokwisha pitia katika wizara hizo za serikali na baadaye kuhamia katika sekta binafsi ambako walijishughulisha na Utendaji kwa Vitendo na kubaini mapungufu yaliyopo wizarani na udhaifu wa sekta binafsi katika kuzitafsiri na kuzitekeleza sera za serikali.Kuna "Miingiliano" mingi sana baina ya wizara na wizara na baina ya idara na idara katika mfumo wa sasa.Kutambua "Mipaka ya Mamlaka na ya Utendaji" baina ya Serikali Kuu na Serikali za Mitaa bado ni tatizo kubwa sana linalokwaza maendeleo ya nchi na watu wake.Muundo wa Mamlaka ya Ukusanyaji wa Mapato ya Serikali,ya Ndani na Nje,bado ni kikwazo kikubwa sana.Bado hatuna "Mamlaka ya Usimamizi wa Matumizi ya Mapato ya Serikali",ingawa kazi hiyo imekuwa ikifanywa na Wizara ya Fedha.Kwa maoni yangu,Wizara ya Fedha ingepewa jukumu la kusimamia na kuzidhibiti hizo Mamlaka Mbili iwapo zote zingekuwapo.Na jambo hilo lingefanyika kwa ufanisi zaidi kuliko ilivyo sasa.Yote hayo ili yakamilike,itabidi marekebisho yafanyike katika baadhi ya vifungu fulani vya sheria.Haya ni baadhi tu ya mapendekezo yangu,ambayo nafikiri Rais Kikwete angeyawekea mkazo na kipau mbele katika Ratiba yake.----papperazzi antonnio----

    ReplyDelete
  10. Issa habari za siku!Naomba unipatie nakala ya habari hii katika lugha ya Kiingereza ili niwaonyeshe wawekezaji ambao walikuja Tanzania wiki mbili zilizopita lakini wakalalamikia urasimu walioupata.Wanawekeza kwa ubia na kampuni yetu na naamini wakiiona itawafariji sana

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...