waombolezaji wakiwasili kwenye makaburi ya kisutu jioni hii na mwili wa gwiji wa siku nyingi katika fani ya habari, Mzee Abdullah Ahmed Riyami, aliyefariki mchana kwa kusumbuliwa na maralia kali na upungufu wa damu. Mzee Riyami, ambaye amefariki akiwa na umri wa miaka 87, alikuwa mkurugenzi wa mwanzo wa Idara ya habari ya Tanganyika (sasa Maelezo), baada ya kupigana katika vita ya pili ya dunia. pia alikuwa mhazini wa chama cha waandishi wa habari (TAJA) kwa muda mrefu. amecha watoto 10, wajukuu 18 na vilembwe 10. --------------------------------------
GLOBU YA JAMII INATOA POLE KWA WAFIWA KWA MSIBA HUU MZITO WA BABA YETU AMBAYE WENGI AMETUFUNDISHA KAZI NA KUTUASA MIIKO NA MAADILI YA KAZI NA FAIDA YAKE TUNAIONA HADI DAKIKA HII.
POLE SANA MDAU KHADIJA RIYAMI WA VOA NA FAMILIA NZIMA YA MZEE RIYAMI KWA MSIBA HUU WA BABA.
MOLA AILAZE PEMA ROHO YA MAREHEMU PEPONI
AMIN
ANGALIA VIDEO YA MAZISHI
BOFYA HAPA


Namkumbuka sana, alikuwa na busara sana na pia alipenda sana uandishi wa habari. Pole sana Dada Khadija. Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu.
ReplyDeleteRest in Peace Mzee Riyami. Amen.
R.I.P Mzee Riyami, pole sana Khadija Riyami, mdau U.S, khadija i worked with u @ TSN pole sana
ReplyDeleteRIP
ReplyDeleteInnalilahi wainna illahi rajiuun!
Rest In Peace Mzee Riyami.Nawapa pole wafiwa wote mungu awape mioyo ya ujasiri ktk wakati huu mgumu, AMEN
ReplyDelete