Habari za kazi mheshimiwa Michuzi,
nilipitia hapa kwenye blog yako nikakuta bwana Chumaka wa Korogwe akiomba msaada wa namna ya kutatua tatizo lake la kukoroma ambalo linamnyima mkewe usingizi.Majibu mengine niliyoyasoma yalikua ya ajabu na pia hayakuweza kumsaidia bwana Chumaka.
Na vifaa vingi vilivozungumzwa kwa mtu aliyopo Korogwe sidhani angevipata kwa urahisi. Kwakua kulikua na comments zaidi ya 35 nikahisi nikiweka na yangu pale wengi hawataiona,naomba uiweke peke yake ili iweze kusaidia watu kama mimi ilivyonisaidia.
Niliwahi kusafiri na mzee wa kijapani kwenda mikoani kikazi na katika safari zetu kuna siku ilibidi tulale kwenye mji mdogo ambao tulikosa vyumba na kupata kimoja tu ambacho kilikua na vitanda viwili.Watu wengi walishaniambia kuwa nakoroma sana nilalapo usiku.Siku ya pili tulipokua tunapata kifungua kinywa yule mzee akaniambia nina tatizo la kukoroma na atanifundisha namna ya kulitatua bila kutumia dawa,mbinu ambayo wanaitumia kwao.
Fungua mdomo wako mpaka mwisho, toa ulimi na usukume nje mpaka mwisho,rudisha ulimi ndani mpaka mwisho-rudia mara 20.
Ukimaliza utahisi kuna misuli nyuma na pembeni ya koo umeifanyisha kazi,sasa misuli hii ikilegea ndio inayosababisha kukoroma.Fanya zoezi hili mara 2 mpaka 3 kwa siku na tatizo hili litaisha baada ya siku 10-20 kutegemea mtu hadi mtu.
Mzee huyu aliniambia mtu anaekoroma mwili wake haupati mapumziko ya kutosha na mara nyingi huamka huku bado akihisi uchovu na husababisha watu wengine kunenepa sana na wengine kukonda ikitegemea mwili wa muhusika na homoni zake.
Tatizo langu liliisha kabisa baada ya wiki 2 lakini naendelea na mazoezi hata mara mbili kwa wiki ili misuli isilegee tena.Kwakua naishi peke yangu ilibidi nimchukue waifu wa siku 2-3 anihakikishie sikoromi kabisa.Nikiamka siku hizi sihisi uchovu ule wa zamani.
Mdau Ibrahim,D'salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hii safi nitajaribu maana tunaokoroma tuko wengi

    ReplyDelete
  2. Hii ni kweli,mie sipati usingizi wa kutosha na nimeambiwa ni mkoromaji mzuri sana.I'll try this one.Thank u.

    ReplyDelete
  3. Duh! Na ili kuleta maana zaidi, ukifanya hilo zoezi na mazoezi kwa ujumla utakuwa unaondoa tatizo la kukoroma, kisukari, presha kupanda, presha kushuka n.k. Mazoezi muhimu, usiishie kutoa ulimi nje hadi mwisho na kurudisha ulimi ndani hadi mwisho tu.

    Na ili kutathmini kama 'zoezi la kijapani' limefanya kazi kwa wale wasio na wenzao wa kulala nao nashauri watumie kidubwana kama kile alichowekewa Dr. Slaa na mwenzake kule hotelini Dodoma. Hii ni kuzingatia ukweli kwamba itakuwa vigumu kwa akina dada/mama wa aina hiyo kuwapata waume wa siku 2-3 na ni hatari pia.

    Asante Ibrahimu kwa zoezi la ulimi la kijapani.

    ReplyDelete
  4. kukoroma ni moja ya mnogezo wa kulala, wengine bila ya kukoroma usingizi haunogagi,sawa na akina mama kufanya mapenzi bila kunogeza zile kelele zao zinazofahamika na wengi,

    ReplyDelete
  5. soln imeenda shule hii

    mdau netherlands

    ReplyDelete
  6. Anon wa feb 15, 6:23 Si lazima kila linaloongelewa ujibu kama huna cha msingi jaribu kunyamaa mwanakwetu huna soni.Ama kweli limjazalo mtu ndilo limtokalo.

    ReplyDelete
  7. Toa ulimi mpaka mwisho, unautoaje mpaka mwisho, well labda kuutoa wote nje kadri ya urefu wa ulimi wako.
    Halafu rudisha ndani wote, mmmh,ni kama kawaida, kwani ulimi kuurudisha ndani unaweza ukarudisha nusu?.
    Ninachojaribu hapa na kuelewa vipi unafanya.
    Kwa kifupi basi, ni kutoa na kurudisha ulimi (kwa nguvu) huku umefungua mdomo, au sio?
    M3

    ReplyDelete
  8. Ibrahim Mwenyezi Mungu akubariki umetuokoa wengi sana ... zoezi linaanza mara moja si kutwa mara mbili au tatu ni kila wakati Inshallah
    Huyu asie na kusema basi kweli aache haisaidii mtu kusoma upuuzi wako. Technologia ni kwa watu wastaarabu

    ReplyDelete
  9. Hii itanisaidia mana ninakotoma ile mbaya mpka najiogopa mi mwenyewe jamani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...